Serikali kuendelea na uwekezaji wa Bandari na DP World kama ilivyopangwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,115
49,829
Licha ya Makelele ya TEC na Chadema ila Msemaji wa Serikali bwana Msingwa amesema Serikali itaendelea na uwekezaji na DP World kama ilivyopangwa ila itazingatia maoni ya wadau.

=======

SERIKALI KUENDELEA NA MCHAKATO WA UWEKEZAJI BANDARI NA DP WORLD

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kila hatua na kadri majadiliano yatakavyokuwa yanaendelea ikiwemo kuafikiana au kukubaliana pande zote kati ya Serikali ya Tanzania na mwekezaji kwenye uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam , umma wa Watanzania tumehakikishiwa kuwa utajulishwa.

Hayo yamesemwa Agosti 26, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna mkataba wowote wa utekelezaji kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa bandari ambao umeshasainiwa.

Msigwa amesema, baada ya hatua ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai hatua itakayofuata ni mikataba ya utekelezaji.

Kuhusu mikataba hiyo ya utekelezaji, Msigwa amesema

"Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani"

Msigwa ameendelea kwa kusema kuwa, hatua itakayofuata ni uandaaji wa nyaraka na katika hatua hii ndipo miradi ya utekelezaji itaandaliwa huku akiendelea kusisitiza kuwa hakuna bandari iliyouzwa.

======

My Take
Msemo wa Waswahili: Kelele za mlango hazimtoshi mwenye nyumba.

Waraka ni makaratasi tuu kama makaratasi mengine.

Wapinzani na TEC mtakuja na move ipi baada ya Serikali kukataa kufuta mkataba na DP World?
Screenshot_20230828-095109.jpg
 
Msemaji wa Serikali bwana Msingwa amesema Serikali itaendelea na uwekezaji na DP World kama ilivyopangwa ila itazingatia maoni ya wadau.

=======

SERIKALI KUENDELEA NA MCHAKATO WA UWEKEZAJI BANDARI NA DP WORLD

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kila hatua na kadri majadiliano yatakavyokuwa yanaendelea ikiwemo kuafikiana au kukubaliana pande zote kati ya Serikali ya Tanzania na mwekezaji kwenye uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam , umma wa Watanzania tumehakikishiwa kuwa utajulishwa.

Hayo yamesemwa Agosti 26, 2023 na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa hadi sasa hakuna mkataba wowote wa utekelezaji kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa bandari ambao umeshasainiwa.

Msigwa amesema, baada ya hatua ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai hatua itakayofuata ni mikataba ya utekelezaji.

Kuhusu mikataba hiyo ya utekelezaji, Msigwa amesema

"Baada ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kinachofuata sasa ni mikataba ya utekelezaji, katika mikataba hiyo ya utekelezaji ndio itasema sasa miradi itakuwa ni ya muda gani"

Msigwa ameendelea kwa kusema kuwa, hatua itakayofuata ni uandaaji wa nyaraka na katika hatua hii ndipo miradi ya utekelezaji itaandaliwa huku akiendelea kusisitiza kuwa hakuna bandari iliyouzwa.

======

My Take
Wapinzani na TEC mtakuja na move ipi baada ya Serikali kukataa kufuta mkataba na DP World?
Bora serikali imeamua kusimamia masilahi ya taifa. Hizi kelele za wanufaika wa mfumo mbovu wa bandari zimeturudisha nyuma miaka nenda miaka rudi.

Wanaonufaika na upitishaji wa mizigo yao bila kulipa kodi wala ushuru pale bandarini watafute kazi zingine za kufanya.
 
Maadamu Wabunge wanaenda Vatican kutubu kwa baba mtakatifu anayeketi Kitini pake Petro Mtume inatosha

Msamaha wa Dhambi tuliupata Calvary
Kwani Serikali ni Msigwa au Rais? Serikali inawekwa na wananchi. Msigwa anasema haya ni "Makubaliano" Mahakama inasema ni "Mkataba". Huu ni mkataba wa kibiashara. Wananchi kuelezwa kila hatua itakayofuata siyo suluhu; la muhimu ni kama uhuru wa wananchi na faida kwa Tanzania ni kubwa kuliko ambavyo ingepatikana vinginevyo. Hiyo ndiyo kamali au bet iliyopo mezani. Mwishoni wananchi ndiyo wanaosema, siyo msemaji wa Serikali wala serikali; mradi kura kwenye chaguzi zijazo zisiibiwe.
 
Ni jambo jema iwapo serikali imeona kuna tija na faida nalo ijapokuwa kuna vipengele vya mkataba vina utata.

Ila ni vema zikaondolewa kinga za viongozi kushtakiwa ili wawe na uhakika na mikataba wanayoingia.

Ikibainika kuna magumashi basi viongozi husika wapelekwe mahakamani kusomewa mashtaka na ikibainika walitupiga changa la macho wafilisiwe na watumikie adhabu kali.

Katiba mpya ianze na hilo jambo. Pia mahakama na bunge viwe vyombo huru na vyenye nguvu sio kuwa puppet (chawa) wa serikali.
 
Back
Top Bottom