Ziara za viongozi CCM, zigusie uwekezaji wa DP World unaendeleaje

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,155
22,655
Salaam, Shalom,

Itakumbukwa kuwa, uteuzi wa Katibu Mwenezi wa CCM, ulifanyika siku ya utiaji Saini kati ya Serikali na Kampuni ya DP World, hatujasahau Bado!!!

Hivi sasa tunaona ziara na misururu mirefu ya magari yakiambatana maeneo mbalimbali nchini, viongozi wa chama,akiwamo Katibu Mwenezi, wanapita wakisema wanatatua kero za wananchi.

Tatizo la mfumuko wa Bei za bidhaa nchini, una mahusiano ya moja kwa Moja na Bandari yetu ya Dar es Salaam maana shehena zinapita pale kwenda Kwa wananchi Nchi nzima.

Tuliambiwa Kwa mbwembwe kuwa, ujio wa DP World utasaidia uharaka wa upakuaji wa mizigo bandarini na kupunguza mfumuko wa Bei za bidhaa nchini.

Nchi yetu inakabiliwa na upungufu wa Sukari na simenti na bidhaa zingine muhimu nchini, tungetegemea uwepo wa kampuni hii, ungewezesha wafanyabiashara ufaulishaji wa mizigo Kwa haraka kuliko mwanzo.

Mizigo imezidi kuchelewa , na siku za Kutoa mizigo bandarini zimeongezeka Badala ya kupungua ilhali kampuni hii tayari imepewa mkataba wa utendaji.

Viongozi Walio katika ziara mbalimbali, watueleze hatua zinazoendelea kufanywa na kampuni hii kuongeza ufanisi wa Bandari yetu kupunguza Bei za bidhaa nchini Kwa kusaidia mizigo ya wafanyabiashara Kutoka haraka bandarini.

Ikiwa wapo wanaoona harakati zozote za kampuni hii hapo bandarini Kwa sasa watujuze.

Karibuni🙏
 
Meli zilizoingia nchni tarehe 9/01/2024 mpaka leo bado hazijashusha mizigo, maanake ni kwamba bidhaa madukani zinazidi kupanda bei.
 
Mbona hakuna kiongozi anayegusia uwekezaji wa kampuni hii kubwa tuliambiwa itafadhili budget Kwa kiasi kikubwa?

Mbona hawasemi lini tutaanza kuona matunda ya uwekezaji wao nchini?
 
Meli zilizoingia nchni tarehe 9/01/2024 mpaka leo bado hazijashusha mizigo, maanake ni kwamba bidhaa madukani zinazidi kupanda bei.
Na ndicho kitovu Cha tatizo la mfumuko wa Bei za bidhaa nchini.

Maana mfanyabiashara akitozwa gharama kubwa Kutoa Mzigo sababu za ucheleweshwaji wa makusudi,

Lazima ataongeza Bei Ili kufidia HASARA.
 
Na ndicho kitovu Cha tatizo la mfumuko wa Bei za bidhaa nchini.

Maana mfanyabiashara akitozwa gharama kubwa Kutoa Mzigo sababu za ucheleweshwaji wa makusudi,

Lazima ataongeza Bei Ili kufidia HASARA.
Ndivyo ilivyo mkuu, mfano mdogo tu, tafta karatasi/ream zimeadimika kisa meli hazijashusha mzigo siku ya 20 sasa.
 
Ndivyo ilivyo mkuu, mfano mdogo tu, tafta karatasi/ream zimeadimika kisa meli hazijashusha mzigo siku ya 20 sasa.
Halafu tunaambiwa wanatatua kero za Wanachi Kwa kuongeza matumizi ya Serikali kugharamia magari ya Serikali katika ziara ya chama.
 
Salaam, Shalom,

Itakumbukwa kuwa, uteuzi wa Katibu Mwenezi wa CCM, ulifanyika siku ya utiaji Saini kati ya Serikali na Kampuni ya DP World, hatujasahau Bado!!!

Karibuni🙏
Tena tuliambiwa kuna dubwasha, mfumo wa kielektroniki(monitoring sysytem) ofisini mwa Mwenyekiti wa CCM anaona kila kitu!

Na teknolojia ilivyo, Makonda anaweza pata hizi live kwenye simu yake janja. Watujuze kwa kweli.
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom