nyboma

JF-Expert Member
Aug 29, 2021
2,220
6,972
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
IMG_3142.jpeg

KUHUSU MAKALLA
20230516_063252.jpg

Makalla alishawahi kushika nafasi ya katibu wa uchumi na fedha wa CCM na aliwahi kukaimu nafasi ya katibu wa umoja wa vijana wa CCM ( UVCCM).

Pia. Amewahi kuwa mbunge wa Mvomero kwa vipindi tofauti na mara ya mwisho alikuwa mbunge mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Makalla pia, amewahi kuwa naibu waziri wa habari enzi za utawala wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Aliwahi kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kisha kuhamishiwa Mkoa wa Mbeya kabla ya kuhamishiwa Mkoa wa Katavi.

Mei 14, 2019 Hayati John Magufuli alitengua uteuzi wake akiwa mkoani Katavi.

Mei 15, 2021, Rais Samia alimteua Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam

Pia, soma: Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam

KUHUSU CHALAMILA
20230516_001300.jpg

Chalamila aliteuliwa Rais Samia kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mei 15, 2021 akitokea Mbeya alikodumu kwa takribani miaka minne tangu Julai 29, 2018 alipoteuliwa na Hayati Dk John Magufuli.

Baadaye uteuzi wake wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ulitenguliwa na raia Samia na kukaa nje kwa siku 412 hadi Julai 28, 2022 alipoteuliwa tena na rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kabla ya hapo Chalamila alikuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, wadhifa alioupata Desemba 5, 2017 baada ya kushinda katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho.

Kabla ya kuibukia katika siasa, Chalamila alikuwa mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini) mkoani Iringa na amewahi kuwa mwalimu katika shule mbalimbali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa baadhi ya Wakuu wa Mikoa kama ifuatavyo:

  1. Bw. Amos Gabriel Makalla amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
  2. Bw. Adam Kighoma Malima amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
  3. Bi Fatma Abubakar Mwassa amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
  4. Bw. Albert John Chalamila amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Uhamisho huu wa Wakuu wa Mikoa unaanza mara moja.
AAEB0FC1-3EE6-45A4-A0FB-B04D4F069033.jpeg
 
Last edited:
Back
Top Bottom