Rais Samia, tuondolee huyu RC Amos Makalla mkoa wa Dar es Salaam

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, amesema wahalifu wanaodaiwa kuwa Panyarodi waliovamia maeneo ya Bunju sio wakazi wa mkoa huo, kwani kazi ya kuwashughulikia wahalifu hao ilishaimaliza.

Wahalifu hao wakiwa kundi la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanane, walifika kwenye mtaa makazi katika eneo la Bunju B Mtaa wa Idara ya Maji saa 8 usiku wa kuamkia jana Februari 10, 2023 na kujeruhi watu kwa mapanga.

Akizungumza leo Jumamosi Februari 11, 2023 alipokutana na uongozi wa Wamachinga na Bodaboda kupokea taarifa ya ziara yao nchini Rwanda, Makalla amesema wahalifu hao sio wakazi wa Dar es Salaam bali ni wa Mapinga mkoani Pwani.

Chanzo:
mwananchi_official

=======

Yaani RC wa Dar es Salaam Amos Makalla anakimbilia kusema hawa Panya Road si wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwakuwa tu huko nyuma aliendesha Oparesheni ya Zimamoto kisha akaja Ikulu Kwako Kukudanganya kuwa ameshawamaliza (Panya Road) wote hivyo leo anasema hawatoki Mkoani hapa Dar es Salaam ili usije Ukakasirika na Kumtumbua.

RC mwenye Akili timamu angesema kuwa kama Mkoa bado tunaendelea Kupambana kukabiliana na Panya Road na si Kukurupuka na kukimbilia kusema hawatoki Mkoani Dar es Salaam na Kusingizia Mikoa mingine ambayo ina Wakuu wa Mikoa very Intelligent and Committed kuliko Yeye.

Rais Samia Binafsi kama MINOCYCLINE ukimuondoa huyu Amos Makalla kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nitakushukuru mno kwani hakufai, hana uwezo, muongo muongo na hajui anachokifanya na sijui ni kwanini Mama (Mheshimiwa) na Wewe ulikosea na ukamteua tena kwa Mkoa wenye 'Changanyikeni Brain' kama huu wa Dar es Salaam.

Nyumba uliyozaliwa tu na Kuishi (Kukulia) uliyoachiwa na Marehemu Baba yako iliyoko Kawe Ukwamani (Nyuma ya Hotel ya Victoria) inayotizama na Ghorofa Jipya la Tajiri wa Kiha Muyama One hadi Leo (miaka nenda rudi) umeshindwa Kuiboresha Kiujenzi mpaka inatia Aibu na Kukuaibisha ndiyo utauweza Mkoa wa Dar es Salaam na Kuuendeleza Kimaendeleo?

Hovyo kabisa!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla, amesema wahalifu wanaodaiwa kuwa Panyarodi waliovamia maeneo ya Bunju sio wakazi wa mkoa huo, kwani kazi ya kuwashughulikia wahalifu hao ilishaimaliza.

Wahalifu hao wakiwa kundi la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanane, walifika kwenye mtaa makazi katika eneo la
Mkoa ulimfaa Makonda hawa wengine hakuna aloupatia
 
Kwa kosa moja tu hilo au kuna makosa mengine?
Masikini wengi wamezulumiwa sana ardhi na wengine nyumba zimevunjwa huko Mabwepande na maeneo ya jirani kama Kinondo, Mji Mpya, Mbopo, n.k. kipindi hiki akiwa yeye kiongozi pamoja na mkurugenzi wa Kinondoni na mwenzao Gondwe ambaye ameshahamishwa. Badala ya kutatua migogoro ya ardhi wao tangu wameingia ndio wameiongeza imekuwa balaa.

Wakaazi wa huko wanajiuliza mbona wakuu wote wa mikoa waliopita mpaka wa mwisho Kunenge hali haikuwa hivyo imeanza tu baada ya Makala na Gondwe kuja wakishirikiana na mshirika wao mkurugenzi wa Kinondoni? Yaani amebaki tu Gwajima peke yake ndie anaetetea wakaaazi wa huko wasivunjiwe au wasinyangánywe ardhi/viwanja vyao.

Huu mkoa mama atafanya la maana kama ataenda kumuomba mstaafu Mecky Sadiki (kama bado yupo) arudi kwa muda aurekebishe kwa muda halafu apewe mtu mwingine au mama ajilipue kabisa amlete Mtaka toka Njombe.
 
Kwenye mboga mboga wote wapo kama yeye waongo waongo, wanafki, wezi, majungu, uuwaji ndio tabia zao
 
Huo inatokea sana Wakazi wa sehemu nyingine kuja kufanya uharifu sehemu ambayo hawajulikani.
 
Rais Samia Binafsi kama MINOCYCLINE ukimuondoa huyu Amos Makalla kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nitakushukuru mno kwani hakufai, hana uwezo, muongo muongo na hajui anachokifanya na sijui ni kwanini Mama ( Mheshimiwa ) na Wewe ulikosea na ukamteua tena kwa Mkoa wenye 'Changanyikeni Brain' kama huu wa Dar es Salaam
Jifunze kuonge na wakubwa;
Normally unapo-present challenge kwa watoa maamuzi jitahidi sana ku ainisha na mitigations za kutatua changamoto hiyo, binafsi nilidhani ungeainisha kuwa mbadala wa Makala kwa mkoa kama wa Dar ni nani angalau watatu...sasa yeye kwa kutumia vyombo vyake angefanya vetting na ku come up na conclusion. Au hata useme Makala anafaa wapi kwa kuwa Dar hafai....
 
Na kwelii alishawashughulikia
Nenda ukaulize huko vingunguti kilichowapata
 
Huyu mhe. Mm namuona kama dalali sijui ilikuwaje akajikuta mwanasiasa ila anakipaji cha udalali asilimia 100%
 
Wakuu wa MIKOA na WILIYA hawana kazi yoyote zaidi ya POROJO tu huo ndio ukweli kuna yule mwingine aliye vuma sana hadi mawaziri walikuwa wanamuogopa AKA BASHITE yule mwamba alikuwa bigwa wa POROJO nakumbuka kuna mwaka 2017 Alianzisha mradi mmoja unaitwa AUTOMOBILE ZONE ambao ulitakiwa uwe Kigamboni YARD ZOTE za magari zinatakiwa ziwe KIGAMBONI tena alitoa hadi dead line lkn hadi anaondoka ikabaki kuwa POROJO case kama hizi za RC na DC za porojo porojo zipo nyinge na sifa moja ya kuwa RC au DC lazima uwe unaogea sn.
 
Back
Top Bottom