Tundu Lissu na wenzake waachiwa kwa dhamana

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,022
144,379
Habari hii ni kwa mujibu wa Martin Maranja Masese kupitia mtandao wa X.

-
Lissu.jpg

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limempatia dhamama Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama hicho waliokamatwa muda huu saa 2 usiku jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure amesema viongozi hao wametakiwa kesho saa tatu asubuhi kuripoti polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo iliyotolewa leo Jumapili Septemba 10, 2023 ilisema kuwa Lissu na wenzake watatu walishikiliwa kwa tuhuma za kufanya mikusanyiko isiyo halali na kuzuia polisi kufanya kazi zao.

Mwandishi wa Habari kutoka Jambo TV, Oscar Kasubi aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo naye ameachiwa usiku huu.

 
Polisi ni kama hospital wanafanya kaxi masaa 24/ 7. Mambo mengine ni kukomoana tu kwa kuishi bila hofu ya Mungu na roho mbaya za polisi wengi kuwa na vinasaba na familia maskini na uchawi.
Imebidi nishangae maana sio kawaida aisee
 
Back
Top Bottom