Uchaguzi 2020 Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yamtangaza Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya pili

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dkt. John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 28. Pia imemtangaza Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais Mteule.

Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali) akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye amepata kura 1,933,271 (sawa na 13.04% ya kura halali)

Dkt. Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania amepata ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili kama Marais waliotangulia.

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195 huku kura 261,755 zikiwa zimeharibika.

Safiii
 
Uchaguzi wa 2020 mungu ndo ajua,ipo siku mungu ataoneshesha uwezo wake,ujumbe mahalum elekea 2021, mungu anawataka WOTE wakatubu,vinginevyo vilio lahana vitatawala kuu yao ,mmoja Bahada ya mwingine, sio ujumbe wangu bali asema bwana,elekea 2021 ,so hutaki acha,full stop
Duuh mkuu uliona mbali sana
 
Kumbe tekinolojia ya Tz ilikuwa juu toka kitambo! Tume ya Tz ilihesabu kura milioni 15 kwa siku mbili tu (Uchaguzi tarehe 28 Coctober, matokeo tarehe 30 October), lakini tume ya Kenya imehesabu kura milioni 14 kwa wiki nzima (uchaguzi tarehe 9 August, matokeo tarehe 15 August)
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Dkt. John Magufuli, aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kuwa mshindi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 28. Pia imemtangaza Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais Mteule.

Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali) akifuatiwa na aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia CHADEMA, Tundu Lissu ambaye amepata kura 1,933,271 (sawa na 13.04% ya kura halali)

Dkt. Magufuli ambaye pia ni Rais wa Tanzania amepata ridhaa ya kuongoza kwa muhula wa pili kama Marais waliotangulia.

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195 huku kura 261,755 zikiwa zimeharibika.

Rubbish
 
Back
Top Bottom