Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Unaruka mkojo unakanyaga mavi huyo anayesema hapo kwenye Mathayo ni nani ?? Mkorinto??

Tunarudi kulekule Mkorinto ndiye anayesema

Tumieni akili, nyinyi viumbe , hizo biblia zimechakachuliwa vibaya sana
Unayo ambayo haijachakachuliwa???
 
Unayo ambayo haijachakachuliwa???

Wazee wa kanisa hao wasikilize maneno yao

There is nothing so easy as by sheer volubility to deceive a common crowd or an uneducated congregation.’

– St. Jerome (Epistle to Nepotian, Lii, 8.)​
 
Wazee wa kanisa hao wasikilize maneno yao

There is nothing so easy as by sheer volubility to deceive a common crowd or an uneducated congregation.’

– St. Jerome (Epistle to Nepotian, Lii, 8.)​
Si ndio maana Muhammad alifanikiwa.
 
Sijasema mimi , hivi akili yako ipo ??, hao wanaosema hivyo ni hao wataalamu wenu wanaokutafsiria biblia ??
sio wewe uliyesema biblia imechakachuliwa!!!au unakataa madai yako mara hii??
 
sio wewe uliyesema biblia imechakachuliwa!!!au unakataa madai yako mara hii??

Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek la October 31, 1988, p. 44., lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?' kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".

Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.

Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.

Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.

Dr. J.K. Elliott, wa kitengo cha Thiolojia na Tafiti za Kidini wa Chuo Kikuu cha Leeds, ameandika makala iliyochapishwa katika jarida la The Times, London (10 Septemba, 1987) yenye kichwa "Kutazama mizizi ya Biblia".

Ndani ya makala yake, ameeleza kuwa: "Zaidi ya miswada 5,000 inayojumuisha Agano Jipya lote au sehemu yake iliyo katika lugha ya asili. Miswada hii imepangika katika madaraja ya kuanzia karne ya pili hadi kuvumbuliwa kwa uchapaji.

Imekisiwa kuwa hakuna hata watu wawili wanaoafikiana kwa kila kitu.

Bila shaka, maandishi yote ya mkono yanastahili kuwa na makosa ya bahati mbaya wakati wa kunukuu. Hata hivyo, katika kazi za kitiolojia si jambo la kushangaza kuwa mabadiliko ya kufikirika sana yaliingizwa ili kuondosha au kubadili maelezo ambayo waandishi wanayaona kuwa hayapendezi. Pia kulikuwa na mwelekeo wa wanukuzi wa kuongeza ufafanuzi au fasiri.

Mabadiliko ya hadhari yanadhaniwa kuwa yameingizwa katika zama za mwanzo kabla ya kuanzishwa hali ya kanisa ya Agano Jipya.
 
Si ndio maana Muhammad alifanikiwa.

Mwandishi aliendelea kufafanua kuwa "hakuna hata mswada mmoja wenye matini isiyobadilishwa kutoka katika uasilia wa ukamilifu wake, na kwa hiyo, "hakuna awezae kuchagua mswada wowote miongoni mwa miswada hiyo na kuuamini kwa imani ya pekee eti mswada huo ndio wenye ukiritimba wa kuwa ndio maneno asilia ya watunzi."

Aliendelea kusema zaidi:

"Kama mtu ataendelea kupinga na kudai kuwa maandiko asilia yamenusurika pahala fulani kwenye maelfu ya miswada iliyopo, basi mtu huyo atalazimika asome miswada yote hiyo, hatua kwa hatua, ili kukusanya tofauti miongoni mwa miswada hiyo, kisha atathimini, lahaja kwa lahaja, ili ajue ni mswada upi wenye [matini] asilia na upi ndio wa matini ya nafasi ya pili.

Matarajio kama hayo yaliwakatisha tamaa10F11 wasomi wengi wa Biblia walioaminia yaliyomo katika matini zilizochapwa za zama za mwanzo, wasomi hao walichukua ushahidi wa miswada waliyoiona kuwa ni bora.

Hata matoleo ya Agano Jipya kwa Kigiriki yaliyochapwa kisasa, vilevile mafafanuzi ya kisasa yametegemea chapa hizo za zama za mwanzo; kwa kawaida hufuata utaratibu huu wa kujenga matini zao kwa kutumia msingi finyu ambao hauonekani kuwa ni wa asili kikamilifu."
 
Ndio ukubali kwamba Yesu ambaye ni Mungu ni tofauti na Yesu ambaye si Mungu.
Halafu ni muhimu kufahamu kuwa jina Yesu ni jina la kawaida kabisa huko Israel. Hivyo, ukitaka kufahamu ni Yesu huyu aliye mwokozi lazima Umwite Yesu Kristo. Kwa hiyo kuna mayest wengi tu. Hata kwenye Biblia kuna anayeitwa Yesu Yusto.
 
ukristo haukuja baada ya Yesu kuondoka,sema umetajwa baada ya Yesu kuondoka,nikikwambia uislam umekuja na Muhammad unakataa,kwa sababu unasema uislam ni tafsiri ya neno kujinyeyekeza kwa Alla.

Nawewe kwanini ulazimishe kuwa ndiye huyo huyo,tunaokataa ni sisi,sisi tuna Yesu nyie mna issah kwanini hamjiamini naye??

Aliyekusudiwa hapa kuwa mmoja tunalinganisba taarifa za msingi kuwahusu,miaka 400 ijayo,akija mtu akasema Mtume Muhammad alikufa aliuawa kwa kuliwa na simba,atakuwa anamjua Muhammad mnayemjua kweli??

HAwawezi kupinga hilo sababu lina walakini pia hata ktk vichwa vyao.

ukristo haukuja baada ya Yesu kuondoka,sema umetajwa baada ya Yesu kuondoka,nikikwambia uislam umekuja na Muhammad unakataa,kwa sababu unasema uislam ni tafsiri ya neno kujinyeyekeza kwa Alla.

Nawewe kwanini ulazimishe kuwa ndiye huyo huyo,tunaokataa ni sisi,sisi tuna Yesu nyie mna issah kwanini hamjiamini naye??

Aliyekusudiwa hapa kuwa mmoja tunalinganisba taarifa za msingi kuwahusu,miaka 400 ijayo,akija mtu akasema Mtume Muhammad alikufa aliuawa kwa kuliwa na simba,atakuwa anamjua Muhammad mnayemjua kweli??

HAwawezi kupinga hilo sababu lina walakini pia hata ktk vichwa vyao.
Kwahiyo wakristo nao wanalazimisha kwamba majini waliyotajwa kwenye Qur'an ndio wawe malaika waovu waliyotajwa kwenye biblia?
 
Soma kuran na biblia
Biblia imemzungumzia mtu mwenye kuitwa Yesu na Qur'an ikaja ikamzungumzia huyo huyo na imeeleza kabisa wazi nani inamkusudia, sasa wewe ukisema hao ni watu wawili tofauti ndio labda uonyeshe wapi hapo palipoeleza hivyo?
 
Kwahiyo wakristo nao wanalazimisha kwamba majini waliyotajwa kwenye Qur'an ndio wawe malaika waovu waliyotajwa kwenye biblia?
Hakuna anayelazimisha,infact mnaamini ni waumini wenzenu kwa Allah,tutaanzaje kuwanathibisha na waliotajwa katika Biblia??
 
Biblia imemzungumzia mtu mwenye kuitwa Yesu na Qur'an ikaja ikamzungumzia huyo huyo na imeeleza kabisa wazi nani inamkusudia, sasa wewe ukisema hao ni watu wawili tofauti ndio labda uonyeshe wapi hapo palipoeleza hivyo?
Kipi kinatofautisha simba dangote na simba wa serengeti??
 
Nimekuwa nikisikia mijadala mingi mtaani na hata mitandaoni kuhusu Yesu na Nabii Isa. Wengine wanasema ni mtu mmoja kwa majina tofauti, wengine wanadai kuna tofauti kubwa sana.

Katika Ukristo, Yesu anatajwa kama Mwana wa Mungu, alizaliwa na Bikira Maria, alifanya miujiza mingi, alisulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu, akafa, akafufuka na kupaa mbinguni. Ana nafasi ya kipekee kama Mwokozi wa ulimwengu.

Kwa upande wa Uislamu, Nabii Isa bin Mariam naye alizaliwa kwa muujiza bila baba, pia alifanya miujiza mingi (kama kuponya wagonjwa na kufufua wafu), lakini haaminiki kama Mwana wa Mungu bali Nabii wa Mwenyezi Mungu. Waislamu huamini hakuuliwa msalabani bali alinyakuliwa na Mungu, na atarudi tena kabla ya Siku ya Kiyama.

Swali langu kwa wana Jamii Forums:

Hivi tunaposema Yesu na Nabii Isa ni mtu mmoja, ni sahihi kihistoria na kiimani?

Je, tofauti hizi za kiimani zinaathiri vipi maelewano ya kidini?

Na kwa wale wanaopenda kuchimba zaidi, kuna maandiko yanayofanana kwenye Biblia na Qur’an kuhusu maisha yake?


Naomba tujadili kwa heshima, kueleweshana, siyo mihemko

Quran 3:37
Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariya awe mlezi wake. Kila mara Zakariya alipo ingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryamu! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.
Quran 3:38
Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi.
Quran 3:39
Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.

USHAHIDI WA KIHISTORIA

1) Quran inasema Mariam mama yake Yesu alilelewa na mzee Zakaria
JE ! Bibilia inasemaje?

2) Quran inasema mzee Zakaria alikuwa akiingia chumbani Kwa Mariam anakuta vyakula kibao akamuuliza unapata wapi vyakula hivi Mariam akasema vinatoka mbinguni
JE! Bibilia inasemaje?

3) Mzee Zakaria alivyoona miujiza ya Mungu anayoifanya Kwa Mariam kama hiyo ya vyakula na Yeye akamuomba Mungu ampe mtoto mwema
JE ! Bibilia inasemaje?

3) Mungu akapokea maombi ya mzee Zakaria na akapewa mtoto nabii anaitwa Yahaya au Yohana mbatizaji
JE ! Bibilia inasemaje?

1) Kwa mujibu wa Quran umri wa Yohana mbatizaji na Yesu haujapishana sana
JE ! Bibilia inasemaje?

Hiyo ndio Quran mpaka Maneno aliyokuwa anayesema bibi yake Yesu wakati akiwa anebeba Mimba ya Mariam tumboni kwake yapo
 
Biblia imemzungumzia mtu mwenye kuitwa Yesu na Qur'an ikaja ikamzungumzia huyo huyo na imeeleza kabisa wazi nani inamkusudia, sasa wewe ukisema hao ni watu wawili tofauti ndio labda uonyeshe wapi hapo palipoeleza hivyo?
Kwenye Biblia imesemaje kuhusu kuzaliwa kwake, na kwenye kuran imesemaje kuhusu kuzaliwa kwake?
 
Back
Top Bottom