Nimekuwa nikisikia mijadala mingi mtaani na hata mitandaoni kuhusu Yesu na Nabii Isa. Wengine wanasema ni mtu mmoja kwa majina tofauti, wengine wanadai kuna tofauti kubwa sana.
Katika Ukristo, Yesu anatajwa kama Mwana wa Mungu, alizaliwa na Bikira Maria, alifanya miujiza mingi, alisulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za wanadamu, akafa, akafufuka na kupaa mbinguni. Ana nafasi ya kipekee kama Mwokozi wa ulimwengu.
Kwa upande wa Uislamu, Nabii Isa bin Mariam naye alizaliwa kwa muujiza bila baba, pia alifanya miujiza mingi (kama kuponya wagonjwa na kufufua wafu), lakini haaminiki kama Mwana wa Mungu bali Nabii wa Mwenyezi Mungu. Waislamu huamini hakuuliwa msalabani bali alinyakuliwa na Mungu, na atarudi tena kabla ya Siku ya Kiyama.
Swali langu kwa wana Jamii Forums:
Hivi tunaposema Yesu na Nabii Isa ni mtu mmoja, ni sahihi kihistoria na kiimani?
Je, tofauti hizi za kiimani zinaathiri vipi maelewano ya kidini?
Na kwa wale wanaopenda kuchimba zaidi, kuna maandiko yanayofanana kwenye Biblia na Qur’an kuhusu maisha yake?
Naomba tujadili kwa heshima, kueleweshana, siyo mihemko