The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Hatimaye mbuyu wa "vijisenti" umepigwa shoka moja na kuanguka.
 
Kikwete hata kama ni msafi kweli lakini akumbuke kuna msemo kwamba:

"The birds of the same feathers fly in one flock"

AU mwingine unaosema:

"Tell me your friends and I can tell you what kind of a person you are"

Hata hivyo JK bado hajachelewa sana. Anatakiwa kuamka kwa kasi na kutimiza matakwa ya walio wengi.

Inatia huzuni sana kusikia kwamba eti hawa mafisadi ni hatari na wana nguvu sana hata kuiyumbisha serikali. Kwa kweli hii kauli inatudhalilisha sana watanzania wote hadi rais wake.

Siwezi kukubali kuwa Serikali yangu na Rais wake ni dhaifu kiasi cha vyombo vyetu vikuu vya usalama kukiri hadharani kwamba wamezidiwa nguvu na kundi dogo la mafisadi. Huu ni unyonge na udhalilishwaji unaotia kichefu chefu kabisa. Naona hata aibu kuitwa Mtanzania kwa hali kama hii! Bora udikteta kabisa, ili tujue moja.
 
Mods mnaweza kuinganisha hii thread na ile ya chenge kujiuzulu maana lengo limetimia ama mnaweza kuifunga pia
 
Yaani hawa viongozi wetu wa serikalini si mchezo

The money trail..... unbelievable

Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25

Amchotea kigogo bilioni moja
Amwashia indiketa Ben Mkapa

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.

Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.

Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.

Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.

Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.

Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.

Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.-08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).

Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.

Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.

Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.

Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.

Kampuni hiyo, ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, tarehe 29 Desemba 2005 dola 13,340,168.37 na 30 Desemba 2005 ilichota kiasi kama hicho.

Siku hiyohiyo, 30 Desemba, kampuni ilihamisha dola 13,340,168.37 na kuzipeleka mahali ambapo hapajafahamika.

Hii ni siku ambayo Rais Kikwete alizindua Bunge jipya mjini Dodoma baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na kabla ya kuunda baraza lake la kwanza la mawaziri.

Katika uteuzi wake wa mawaziri, Chenge alipewa uwaziri wa Afrika Mashariki kabla ya mabadiliko yaliyompeleka kuwa Waziri wa Miundombinu na kurejea kwenye nafasi hiyo rais alipounda baraza jipya baada ya kulivunja kufuatia kashfa ya Richmond.

Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo MwanaHALISI, TANGOLD ilipokea kutoka kampuni tata ya Deep Green Finance Limited Sh. 39,761,397.98 hapo 8 Oktoba 2005 wakati tarehe 10 Desemba 2005 TANGOLD ililipa Deep Green Sh. 100,940,489.-71.

Wakati wa kuchezesha malipo hayo, kulikuwa na uchaguzi mkuu ambapo inadaiwa kuwa fedha hizo huenda ziliingizwa kwenye uchaguzi huo.

Kampuni ya Deep Green ndiyo ilisajiliwa na kampuni ya uwakili ya IMMA ya Dar es Salaam, ambako mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete na mtoto wa Rais Amani Karume, Fatma wanafanya kazi.

Ni kampuni hii mashuhuri ambayo mmoja wa waanzilishi wake ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na mmoja wa mawakili waanzilishi, Protas Mujulizi aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu.

Kampuni ya Deep Green ndiyo imetia fora kwa viroja kwa kuonyesha kuwa ilifungua akaunti yake benki siku ya Mei Mosi wakati siyo siku ya kazi.

Tarehe 23 Novemba 2005 TANGOLD iliichotea Meremeta Sh. 555,300,040 ambazo haijulikani ni kwa kazi ipi.

Siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, hapo 12 Desemba, TANGOLD iliichotea tena Meremeta Sh. 551,060,000 ambazo haijafahamika zilikuwa kwa shughuli ipi.

Kinachozidisha utata ni kwamba tangu Februari 2006 baada ya kuundwa baraza la mawaziri, akaunti ya TANGOLD ya fedha za kigeni haijalipa wala kupokea fedha yoyote hadi tarehe 31 Machi 2008 huku ikiwa na akiba ya dola 12,997,950.84 (sawa na zaidi ya bilioni 15 za Tanzania).

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye akaunti ya nje, akaunti ya ndani ya TANGOLD imefanya malipo yamwisho 6 Juni 2006 ya Sh. 220,980,370. Hadi 31 Machi mwaka huu ilikuwa na akiba ya Sh. 1, 379,359,367.-39.

Kiasi cha fedha kilicholimbikizwa kwenye akaunti za TANGOLD ambako wakurugenzi ni pamoja na Chenge na watumishi wengine wa serikali, zinalingana na kiasi ambacho serikali inapigia magoti kutoka kwa wafadhili.

Hivi sasa Chenge anachunguzwa na makachero wa Uingereza na Tanzania kuhusiana na uwezekano kuwa alipokea hongo katika biashara ya kununua rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

Alipoulizwa kuhusu hali hii ya uchotaji fedha na ulimbikizaji nje, Dk.

Willibrod Slaa, mbunge wa Karatu amesema, "kama hizi fedha ni za serikali kwa nini serikali igeuke ombaomba wakati zimelala benki?"

Kwa nini umma usiamini kuwa fedha hizo zimo mikononi mwa mtandao wa kifisadi, anahoji Dk. Slaa na kuongeza, "Kigugumizi cha serikali kinatoka wapi hapa wakati fedha hizi zinatosha kujenga madarasa 400 ya sekondari au wastani wa shule moja kwa kila mkoa."

HAYA PATENI NA HII SIJUI KAMA IMESHAWEKWA HUMU.
 
Kuupata usafi wa JK ndni ya mafisadi wanaomzunguka ni kazi kubwa na tukiacha unafiki, anayetembea na mwizi naye ni mwizi na wala hakuna sababu ya kuumauma maneno kwani kila kitu kipo wazi kama jiko la maskini.

USAFI HAUONWA KWA JICHO LA TATU
 
Kina nani hawa....

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

baadhi ya majibu yaliyopo kwenye thread ya Chenge atua na kulonga

HAWA NI VIONGOZI WA CCM AMBAO WALIPEWA HELA WAKATI WA UCHAGUZI KWA AJILI YA KUGAWIA WAJUMBE POSHO. HAZIKUWA ZAO.

MARY CHATANDA NI KATIBU WA CHAMA WA MKOA NA WAKATI WA UCHAGUZI NDIO ALIKUWA AKIZUNGUKA NA MAMA JK MIKOANI, NI MTU MWADILIFU SANA...

KALUMUNA NI KATIBU WA VIJANA WA WILAYA MBEYA.

SHEHA NI KATIBU WA VIJANA MKOA WA MOROGORO.

Sokomoko said:
Livingstone Ruhere = mwandishi wa habari wakati ule alikuwa Habari Cooparation haijulikani sasa yupo wapi.

Kuna wengine hapo hatuwajui bado, nani mwenye taarifa atusaidie kwa hilo!
 
Unashangaa braza kufa! Umesahau naye alijidai ni ajent wa zirail akatoa roho ya suka! Tena bora amefia gesti kwani stahili ya jahiri ni kifo cha kunyongwa tena pale Isanga

MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI
 
Pinda: Waacheni JK, Chenge wamalizane

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kuamua juu ya hatma ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuhusu tuhuma zinazomkabili hivi sasa za kukutwa na zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake nje ya nchi.

Alitoa kauli hiyo jana baada ya kufungua mkutano wa tano wa wanahisa wa Benki ya Wananchi Mbinga, uliofanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.

Pinda ambaye alikuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo na hatua za serikali dhidi ya Chenge, alisema wawaache Rais Kikwete na Chenge wamalizane kwa sababu Chenge ni mteuliwa wa rais.

"Tungoje, Chenge ni mteuliwa wa rais na rais amesharudi, tusubiri aamue mwenyewe kitakachofaa, hakuna kitakachoharibika," alisema Pinda.

Aidha, waandishi walipotaka kujua kama kiongozi huyo ameorodhesha mali zake kwenye fomu ya Tume ya Maadili kama ambavyo sheria inaelekeza, Pinda alisema fomu za kiongozi kuorodhesha mali ni suala binafsi, hivyo si rahisi yeye (Waziri Mkuu) kufahamu kiasi cha mali alizonazo ama alichoorodhesha.

Na kuhusu kauli ya Waziri Chenge kusema mabilioni yaliyokutwa kwenye akaunti yake ni vijisenti, alisema kuwa kauli ya msingi ni ile ya Chenge kuomba radhi.

"Nimeona kwenye magazeti jana (juzi) Chenge ameomba radhi, na hiyo ndiyo kauli ya msingi," alisema Pinda ambaye alikuwa akizungumza kwa ufupi bila kupindisha maneno.

Aprili 12, mwaka huu, Gazeti la The Guardian la Uingereza, liliandika kuwa katika uchunguzi wa Taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai ya nchini humo (SFO) iligundulika kuwa akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.

Akizungumzia tuhuma hizo kwa mara ya kwanza akitokea nchini China, Chenge aliwataka Watanzania kusubiri uchunguzi dhidi yake huku akiziita fedha hizo ni vijisenti.

Kauli yake ya kuyaita mabilioni ya shilingi vijisenti ilitafsiriwa na wananchi kuwa ni dharau, hali iliyomlazimu Chenge kuwaomba radhi wananchi.

Awali, Waziri Mkuu akifungua mkutano wa wanahisa wa Benki ya Wananchi wa Mbinga jana, alizitaka halmashauri na Serikali za Mitaa kuhakikisha benki za wananchi kama hiyo zinaanzishwa kutoa huduma kote nchini.

Pinda alisema anashangaa kuona mpaka sasa halmashauri hazijaweza kupokea wito huo, ambao ni muhimu kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Halmashauri kaeni, zungumzeni kuanzisha benki za wananchi kama hii, kwani mchango wake ni mkubwa katika kupambana na umaskini," alisema Pinda.

]
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 16 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Mimi namuona huyu jamaa kama msanii vile, haya Chenge kutokana na pesa yake mpaka waziri mkuu anashindwa kusema lolote, wakati Chenge anaripoti kwa waziri mkuu!!!!!

Hawa wasanii viongozi sijui wataisha lini,angalau Sofia simba na kujiumauma kwake aliongea kitu.

PINDA KAKA ULICHAGULIWA KWA AJALI YA LOWASSA, SASA NA WEWE UNAONEKANA BADO NI AJALI ZILE ZILE.

na Imani, USA, - 21.04.08 @ 09:04 | #7621

ebo pindisha mizengwe anatwambia kua hajui km chenge aliorodhesha hiyo bilioni 1 kwenye fomu zao,sasa hizo fomu zinajazwa tu ili kuridhisha wananchi ama vipi,na anaekagua km kilichoandikwa ni ukwelini nani,bongo watu wanajiita wasomi ila mambo wanayofanya ni vituko na ajabu hata unashindwa kuelewa ni nini hasa,hawa watawala hawatufai jamani watoeni 2010

na mstari wa mbele, calif/usa, - 21.04.08 @ 09:15 | #7625

HAKUNA JIPYA WALEWALE!MLITEGEMEA ATASEMA NINI?HUYU WAZIRI MKUU TANGU AMEANZA SIJAONA POINTI HATA MOJA MARA MAFISADI WA EPA HAWAWEZEKANI MARA ACHA WAMALIZANE WENYEWE.USHAURI WA BURE NAMUOMBA AWE ANANYAMAZA STAILI YAKE YA KUZUNGUMZIA MAMBO YANAYOKERA WANANCHI INATIA KICHEFUCHEFU

na mishi daud, tz, - 21.04.08 @ 09:54 | #7639

HAYA MIZENGWE PINDISHA TUMESHAKUJUA KUWA HUNA LOLOTE NI USANII ULE ULE, SASA MJUE DAWA YENU IKO JIKONI INACHEMSHWA. MNAZIDI KUTUCHEFUA WATANZANIA. INJI HII SI YENU PEKE YENU, NI YETU SOTE, MTAONA....

na Hashim, Canada, - 21.04.08 @ 10:09 | #7644

tumewafukuza wakoloni na kuwachagua wakoloni wengine watutawale ,ni heri kuwa na utawala wa kijeshi sasa ,Kikwete ,Pinda na maswahiba wenu hatuna imani na nyie .Kila mtu anatucheka. Wizi wa BOT , Richmond maamuzi yenu yanatia wasi wasi .Vipi leo mtu aibe pesa za umma halafu aanze kuzirudisha kimya kimya bila mkulima kumfahamu

na radhim m, bongo, - 21.04.08 @ 10:55 | #7710

pindisha unawaogopa mafisadi acha uoga fanya kazi.

na sheila, mivinjeni, - 21.04.08 @ 08:36 | #7721

hakikaka hata mie naungana na waliotangulia kusema kuwa huyu PM ni mwoga na hakika sijui kama ataimudu vyema post hii, na kwa ujumla JK naye ni msaniia ambaye watanzania hatumhitaji tena , amalize awamu yake tu, ndani ya miaka 2 na ushee, uongozi wake umeshindwa kulerta faraja ya kweli kwa wananchi, wao wanajilimbikizia, wananchi wanateseka, ebu angalia leo bei za vyakula zimepanda maradufu, JK kushindwa kuchukua hatua zinazostahili ni dhahiri ameshindwa kazi, na maana hiyo hatufai, kwa mtazamo wangu ndani ya CCM angalau spika wa sasa ana afadhali, waliobaki ni WEZI tu wa mali za umma, wananchi wa tz wakati wa BWANA ni huu, amka, tafakari na chukua hatua unayoona inafaa katika ujenzi wa tz huru na mpya, nitarudi.

na geofrey, tz, - 21.04.08 @ 08:49 | #7728

Halafu la kushangaza kwa usanii huu, nasikia wale akina RICHMOND/DOWANS bado wanalipwa kila siku/mwezi kwa umeme hewa hadi leo hii. Hivi jamani watu hawa vipi akina Pindisha Mizengwe na Msanii mwenziwe JK? mbona wanatufanya watoto wadogo watanzania?
Nyie....Kikwete na Mizengwe muachie ngazi pia

na Chande, Germany, - 21.04.08 @ 09:02 | #7732

Ukurasa huu ni mzuri sana, kwani unawapa wananchi nafasi ya kutoa maoni yao. Naomba maoni haya muwe munayatoa kwenye magazeti ya siku inayofuata ili kuwapa fursa wananchi ambao hawana uwezo wa kuaccess internet nao kupata mawazo ya wananchi wenzao. Keep it up

na Noel Sawe, Serengeti - Mara, - 21.04.08 @ 09:20 | #7744

Pinda!
Shushushu wa zamani mwenye mrengo wa wa Kirusi acha uoga! Wewe ndiye Kingunge mwanangu au hujui hilo? Hata wale watoto wa Ze Comedy akina Masanja Mkandamizaji wa Mbeya ya Shinyanga si umewacheki wakikunyali kukupiga mangumi wakati wa mpira wa Dobo?
Poti acha kuzuga chukua hatua, Tunataka fedha zetu wazirejeshe! Upo msururu mrefu mno wa mafisadi tena wengine wanasubiri wakati nchi iko kwenye matatizo ya giza la kutisha! Hata hawa jamaa waliochezea mali wakati nchi inataka kujilinda dhidi ya adui walejeshe, tena na riba na tuwatengenezee kaadhabu ka kuwaning'iza kwenye kamba live!

na LCD, Taipei Taiwan, - 21.04.08 @ 09:40 | #7755

Pinda kama Waziri Mkuu, unawasimamia mawaziri, unapaswa kujua mawaziri wako wana nini na tabia zao. Hebu tuambie, nani anapaswa kuziona fomu za hawa mawaziri kama si wewe na rais. Habari ya kufichiana siri imetufikisaha hapa ambapo viongozi wanajilimbikizia mabilioni halafu mnajifanya kushangaa!

na Stephen Mariki, Nairobi, Kenya, - 21.04.08 @ 09:52 | #7760

Ayaaaaaaaaaaaaaa! Mtoto wa mkulima!!!!

Naunga mkono hoja ya Bw.Noel Sawe, sidhani kama hawa akina Lowasa, Chenge, Rostam, Pinda na msanii mkuu JK wanasoma haya, hebu angalieni uwezekano wa kuyapatia haya yanayosemwa nafasi katika magazeti ili watu wengine wasome na wanaoandikiwa pia.

Mawazo yafanyiwe uhariri na yanayoweza kusomeka yawekwe juu. Kwani inaweza kuwa nasi tunafanya mchezo wa kitoto wa kupika mchanga na kuuita ubwabwa!!

na Christopher, Dar - Tz, - 21.04.08 @ 10:47 | #7781

huyu pindisha mizengwe(andunje)naona hata hajui alisemalo masikini....kiwete amemchagua ili aweze kumburuza atakavyo.mie nasema yy na huyu msanii mkubwa kiwete wote mafisadi tu

na kifo, afghanistan, - 21.04.08 @ 12:00 | #7805

jamani huyu waziri mkuu gani huyu aliyekuwa hana maamuzi ?mimi baada tu ya kuchaguliwa nilijuwa hapa ndio kawapa point mafisa hana uwezo wa kupambana na ufisadi huyu sidhani kuwa anauwezo wa kuongoza hata kuwa mkuu wa wiliya achiliambali waziri mkuu tupate waziri mkuu kama marehem sokoine au hata mzee mandevu hawa mafisadi wote wangalikuwa wakinyea ndoo mida hii

na king, tz, - 21.04.08 @ 12:17 | #7810

Kwani aliyeibiwa hela ni Kikwete ama sisi wananchi? kwa nini JK ndio aamue hatma yake ya mwisho, kuna tofauti gani kati ya hii na udikteta?

na Hassan - 21.04.08 @ 12:33 | #7815

PINDA BORA HATA YA LOWASSA NAE ATAKUWA KAZI YAKE KWENDA MISIBANI, KUKARIBISHA MABALOZI, LABDA KAMA KUNA MAAFA YAMETOKEA KAMA MWENZAKE SHEIN, KIKWETE NAE KUSAFIRI NA HIVI WAMEMPA AU WE ACHA 2 KAMA AMECHAGULIWA NA AU VILE AKISKIA KASHFA 2 KAKIMBIA MARA MAREKANI, MARA CHINA, MBONA NCHI AINA MWENYEWE.

na john - 21.04.08 @ 12:52 | #7822
 
Pinda bado anafikiri style atakayoingia nayo ktk utendaji wake, bado anafikiri haya mafisadi atayakwepaje yasije yakamchafua
 
mtoto wa kulima anafuja....
tuwaache JK na Chenge wamalizane kwani hili ni personal beef kwao?
hapa ni pesa za wananchi, na wananchi wana haki ya kujua huyu mtu atafanywa nini na kwa misingi ya sheria ipi, sio amalizane na JK kama kama wamechukuliana warembo mtaani!!
 
Mizengwe kaianza, pita, pinda. Isipopinda yenyewe inapindishwa. Tutapinda sana mwaka huu! Hadi awamu hii iishe tutageuka upinde bila mshale. Twapindwa na kupindiwa huku tukipindishiwa na kupindishwa!
 
Haya mambo ya sijui ajiuzulu ,yaani akijiuzulu kwenye Uwaziri anashuka kwenye ngazi ya Ubunge napo ajiuzulu ,naona kama hapa kuna zimwi na hili litatula sana tu. Na kujiuzulu nako kuna mizengwe yake mtu anapeleka mafeza huko alikotoka anawakusanya wateja na kuwanunulia masanduku ya pombe na kuwaangushia pilau ya ng'ombe mia ,akiludi anatandikiwa zulia jekundu jamaa wanasema hapa bado anatufaa na ni shujaa wetu kutoka Munduli no sorry kutoka baliadi.
Nasema hiki ni kiini macho kinachochezwa na CCM au na majinamizi haya ya ufisadi yalioielemea Tanzania ,hapa jamani hakuna kujiuzulu hapa ni kukamatwa mtu kwenda kukaa segerea mpaka uchunguzi umalizike mambo haya ya kungoja mtu ajiuzulu sijui uwazili ,sijui ubunge mbona yanakwamisha juhudi za Muheshimiwa Kikwete kama Raisi wa Nchi na badala yake zinazidi kumponza ,Ikiwa Waziri mkuu anaogopa anasema mpaka Kikwete ,kukamatwa haiwezekani kwani ni mbunge ,hivi Usalama wa Taifa upo wapi hapa kama kuna mizunguko mingi kuna sheria ya kutoa WARANTY wa kukamatwa popote alipo na akiwa na cheo chochote kile , au ndio mnamgoja Kikwete basi hakuna atakae kamatwa wala kuhukumiwa na mambo yataishia hivi hivi tu watu wakisubiri mafisadi wajiuzulu ,mwisho CCM watapata cha kusema na kutuambia tusubiri wajiuzulu ndio Upinzani ukamate Nchi...mpo !!!
 
Mizengwe kaianza, pita, pinda. Isipopinda yenyewe inapindishwa. Tutapinda sana mwaka huu! Hadi awamu hii iishe tutageuka upinde bila mshale. Twapindwa na kupindiwa huku tukipindishiwa na kupindishwa!

Jamani kweli majina yana reflect personality!? Pinda anapindisha....
 
Huyu Pinda mimi nilianza kumsema hapa the first day tu amepewa uongozi kuwa na nikashambuliwa kama ...... Muda si mrefu yeye mwenyewe akaanza kulikoroga bungeni na kusema kuwa yaliyopita si ndwele.

Just wait uone kazi yake!
 
Now that is Mizengo Pinda doing what he does best: kupindisha mizengwe.

Toka ameteuliwa kuwa PM amekuwa akitoa visingizio visivyokwisha kutetea mafisadi badala ya kufanya wajibu wake. Someone remind this joker of his job description, unless there is none, which could very well be the case!
 
Pinda: Waacheni JK, Chenge wamalizane

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema Rais Jakaya Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kuamua juu ya hatma ya Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge kuhusu tuhuma zinazomkabili hivi sasa za kukutwa na zaidi ya dola milioni moja za Marekani katika akaunti yake nje ya nchi.

Alitoa kauli hiyo jana baada ya kufungua mkutano wa tano wa wanahisa wa Benki ya Wananchi Mbinga, uliofanyika katika Ukumbi wa Msimbazi Center, Dar es Salaam.

Pinda ambaye alikuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo na hatua za serikali dhidi ya Chenge, alisema wawaache Rais Kikwete na Chenge wamalizane kwa sababu Chenge ni mteuliwa wa rais.

"Tungoje, Chenge ni mteuliwa wa rais na rais amesharudi, tusubiri aamue mwenyewe kitakachofaa, hakuna kitakachoharibika," alisema Pinda.

Aidha, waandishi walipotaka kujua kama kiongozi huyo ameorodhesha mali zake kwenye fomu ya Tume ya Maadili kama ambavyo sheria inaelekeza, Pinda alisema fomu za kiongozi kuorodhesha mali ni suala binafsi, hivyo si rahisi yeye (Waziri Mkuu) kufahamu kiasi cha mali alizonazo ama alichoorodhesha.

Na kuhusu kauli ya Waziri Chenge kusema mabilioni yaliyokutwa kwenye akaunti yake ni vijisenti, alisema kuwa kauli ya msingi ni ile ya Chenge kuomba radhi.

"Nimeona kwenye magazeti jana (juzi) Chenge ameomba radhi, na hiyo ndiyo kauli ya msingi," alisema Pinda ambaye alikuwa akizungumza kwa ufupi bila kupindisha maneno.

Aprili 12, mwaka huu, Gazeti la The Guardian la Uingereza, liliandika kuwa katika uchunguzi wa Taasisi ya kuchunguza makosa makubwa ya jinai ya nchini humo (SFO) iligundulika kuwa akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.

Akizungumzia tuhuma hizo kwa mara ya kwanza akitokea nchini China, Chenge aliwataka Watanzania kusubiri uchunguzi dhidi yake huku akiziita fedha hizo ni vijisenti.

Kauli yake ya kuyaita mabilioni ya shilingi vijisenti ilitafsiriwa na wananchi kuwa ni dharau, hali iliyomlazimu Chenge kuwaomba radhi wananchi.

Awali, Waziri Mkuu akifungua mkutano wa wanahisa wa Benki ya Wananchi wa Mbinga jana, alizitaka halmashauri na Serikali za Mitaa kuhakikisha benki za wananchi kama hiyo zinaanzishwa kutoa huduma kote nchini.

Pinda alisema anashangaa kuona mpaka sasa halmashauri hazijaweza kupokea wito huo, ambao ni muhimu kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

"Halmashauri kaeni, zungumzeni kuanzisha benki za wananchi kama hii, kwani mchango wake ni mkubwa katika kupambana na umaskini," alisema Pinda.

]
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 16 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Mimi namuona huyu jamaa kama msanii vile, haya Chenge kutokana na pesa yake mpaka waziri mkuu anashindwa kusema lolote, wakati Chenge anaripoti kwa waziri mkuu!!!!!

Hawa wasanii viongozi sijui wataisha lini,angalau Sofia simba na kujiumauma kwake aliongea kitu.

PINDA KAKA ULICHAGULIWA KWA AJALI YA LOWASSA, SASA NA WEWE UNAONEKANA BADO NI AJALI ZILE ZILE.

na Imani, USA, - 21.04.08 @ 09:04 | #7621

ebo pindisha mizengwe anatwambia kua hajui km chenge aliorodhesha hiyo bilioni 1 kwenye fomu zao,sasa hizo fomu zinajazwa tu ili kuridhisha wananchi ama vipi,na anaekagua km kilichoandikwa ni ukwelini nani,bongo watu wanajiita wasomi ila mambo wanayofanya ni vituko na ajabu hata unashindwa kuelewa ni nini hasa,hawa watawala hawatufai jamani watoeni 2010

na mstari wa mbele, calif/usa, - 21.04.08 @ 09:15 | #7625

HAKUNA JIPYA WALEWALE!MLITEGEMEA ATASEMA NINI?HUYU WAZIRI MKUU TANGU AMEANZA SIJAONA POINTI HATA MOJA MARA MAFISADI WA EPA HAWAWEZEKANI MARA ACHA WAMALIZANE WENYEWE.USHAURI WA BURE NAMUOMBA AWE ANANYAMAZA STAILI YAKE YA KUZUNGUMZIA MAMBO YANAYOKERA WANANCHI INATIA KICHEFUCHEFU

na mishi daud, tz, - 21.04.08 @ 09:54 | #7639

HAYA MIZENGWE PINDISHA TUMESHAKUJUA KUWA HUNA LOLOTE NI USANII ULE ULE, SASA MJUE DAWA YENU IKO JIKONI INACHEMSHWA. MNAZIDI KUTUCHEFUA WATANZANIA. INJI HII SI YENU PEKE YENU, NI YETU SOTE, MTAONA....

na Hashim, Canada, - 21.04.08 @ 10:09 | #7644

tumewafukuza wakoloni na kuwachagua wakoloni wengine watutawale ,ni heri kuwa na utawala wa kijeshi sasa ,Kikwete ,Pinda na maswahiba wenu hatuna imani na nyie .Kila mtu anatucheka. Wizi wa BOT , Richmond maamuzi yenu yanatia wasi wasi .Vipi leo mtu aibe pesa za umma halafu aanze kuzirudisha kimya kimya bila mkulima kumfahamu

na radhim m, bongo, - 21.04.08 @ 10:55 | #7710

pindisha unawaogopa mafisadi acha uoga fanya kazi.

na sheila, mivinjeni, - 21.04.08 @ 08:36 | #7721

hakikaka hata mie naungana na waliotangulia kusema kuwa huyu PM ni mwoga na hakika sijui kama ataimudu vyema post hii, na kwa ujumla JK naye ni msaniia ambaye watanzania hatumhitaji tena , amalize awamu yake tu, ndani ya miaka 2 na ushee, uongozi wake umeshindwa kulerta faraja ya kweli kwa wananchi, wao wanajilimbikizia, wananchi wanateseka, ebu angalia leo bei za vyakula zimepanda maradufu, JK kushindwa kuchukua hatua zinazostahili ni dhahiri ameshindwa kazi, na maana hiyo hatufai, kwa mtazamo wangu ndani ya CCM angalau spika wa sasa ana afadhali, waliobaki ni WEZI tu wa mali za umma, wananchi wa tz wakati wa BWANA ni huu, amka, tafakari na chukua hatua unayoona inafaa katika ujenzi wa tz huru na mpya, nitarudi.

na geofrey, tz, - 21.04.08 @ 08:49 | #7728

Halafu la kushangaza kwa usanii huu, nasikia wale akina RICHMOND/DOWANS bado wanalipwa kila siku/mwezi kwa umeme hewa hadi leo hii. Hivi jamani watu hawa vipi akina Pindisha Mizengwe na Msanii mwenziwe JK? mbona wanatufanya watoto wadogo watanzania?
Nyie....Kikwete na Mizengwe muachie ngazi pia

na Chande, Germany, - 21.04.08 @ 09:02 | #7732

Ukurasa huu ni mzuri sana, kwani unawapa wananchi nafasi ya kutoa maoni yao. Naomba maoni haya muwe munayatoa kwenye magazeti ya siku inayofuata ili kuwapa fursa wananchi ambao hawana uwezo wa kuaccess internet nao kupata mawazo ya wananchi wenzao. Keep it up

na Noel Sawe, Serengeti - Mara, - 21.04.08 @ 09:20 | #7744

Pinda!
Shushushu wa zamani mwenye mrengo wa wa Kirusi acha uoga! Wewe ndiye Kingunge mwanangu au hujui hilo? Hata wale watoto wa Ze Comedy akina Masanja Mkandamizaji wa Mbeya ya Shinyanga si umewacheki wakikunyali kukupiga mangumi wakati wa mpira wa Dobo?
Poti acha kuzuga chukua hatua, Tunataka fedha zetu wazirejeshe! Upo msururu mrefu mno wa mafisadi tena wengine wanasubiri wakati nchi iko kwenye matatizo ya giza la kutisha! Hata hawa jamaa waliochezea mali wakati nchi inataka kujilinda dhidi ya adui walejeshe, tena na riba na tuwatengenezee kaadhabu ka kuwaning'iza kwenye kamba live!

na LCD, Taipei Taiwan, - 21.04.08 @ 09:40 | #7755

Pinda kama Waziri Mkuu, unawasimamia mawaziri, unapaswa kujua mawaziri wako wana nini na tabia zao. Hebu tuambie, nani anapaswa kuziona fomu za hawa mawaziri kama si wewe na rais. Habari ya kufichiana siri imetufikisaha hapa ambapo viongozi wanajilimbikizia mabilioni halafu mnajifanya kushangaa!

na Stephen Mariki, Nairobi, Kenya, - 21.04.08 @ 09:52 | #7760

Ayaaaaaaaaaaaaaa! Mtoto wa mkulima!!!!

Naunga mkono hoja ya Bw.Noel Sawe, sidhani kama hawa akina Lowasa, Chenge, Rostam, Pinda na msanii mkuu JK wanasoma haya, hebu angalieni uwezekano wa kuyapatia haya yanayosemwa nafasi katika magazeti ili watu wengine wasome na wanaoandikiwa pia.

Mawazo yafanyiwe uhariri na yanayoweza kusomeka yawekwe juu. Kwani inaweza kuwa nasi tunafanya mchezo wa kitoto wa kupika mchanga na kuuita ubwabwa!!

na Christopher, Dar - Tz, - 21.04.08 @ 10:47 | #7781

huyu pindisha mizengwe(andunje)naona hata hajui alisemalo masikini....kiwete amemchagua ili aweze kumburuza atakavyo.mie nasema yy na huyu msanii mkubwa kiwete wote mafisadi tu

na kifo, afghanistan, - 21.04.08 @ 12:00 | #7805

jamani huyu waziri mkuu gani huyu aliyekuwa hana maamuzi ?mimi baada tu ya kuchaguliwa nilijuwa hapa ndio kawapa point mafisa hana uwezo wa kupambana na ufisadi huyu sidhani kuwa anauwezo wa kuongoza hata kuwa mkuu wa wiliya achiliambali waziri mkuu tupate waziri mkuu kama marehem sokoine au hata mzee mandevu hawa mafisadi wote wangalikuwa wakinyea ndoo mida hii

na king, tz, - 21.04.08 @ 12:17 | #7810

Kwani aliyeibiwa hela ni Kikwete ama sisi wananchi? kwa nini JK ndio aamue hatma yake ya mwisho, kuna tofauti gani kati ya hii na udikteta?

na Hassan - 21.04.08 @ 12:33 | #7815

PINDA BORA HATA YA LOWASSA NAE ATAKUWA KAZI YAKE KWENDA MISIBANI, KUKARIBISHA MABALOZI, LABDA KAMA KUNA MAAFA YAMETOKEA KAMA MWENZAKE SHEIN, KIKWETE NAE KUSAFIRI NA HIVI WAMEMPA AU WE ACHA 2 KAMA AMECHAGULIWA NA AU VILE AKISKIA KASHFA 2 KAKIMBIA MARA MAREKANI, MARA CHINA, MBONA NCHI AINA MWENYEWE.

na john - 21.04.08 @ 12:52 | #7822
Nilisema toka mwanzo kuwa Pinda amewekwa kuja kupindisha haki!Kuna watu walipingana na mimi..sasa they see!Vijikoti vya kijamaa vyenye symbol ya unafiki vilimficha kidogo..but the world/country has clearly changed..nashangaa kwa nini wasijiandae tu kuyapokea mabadilko haya!There's no way around zaid ya acountability na mabadiliko ya kweli!Eti Kikwete aachiwe!aachiwe na nani?Alishaachiwa akamrudisha madarakani!Kauli ya Mh Pinda inatia kichefu chefu!Rais ana mamlaka makubwa ya kuweza kusimamia mapinduzi haya otherwise historia itamuumbua!
 
Huyu Pinda mimi nilianza kumsema hapa the first day tu amepewa uongozi kuwa na nikashambuliwa kama ...... Muda si mrefu yeye mwenyewe akaanza kulikoroga bungeni na kusema kuwa yaliyopita si ndwele.

Just wait uone kazi yake!

Kuna mtu alisemaga eti Pinda anaonekana ni mzungumzaji "mzuri"....
 
Back
Top Bottom