The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

pinda hawezi kutuambi tumuache JK alimalize hili kwa kuwa yeye ndo alomteua! its totally bollocks!
basi mawaziri wote na wafanye madudu watakayo, kisha tumsubiri JK manake ndo alowachagua!
hivi hawa viongozi huwa wanafikiri saa zote kuwa wao wanaongea na watoto wadogo au?
 
Huyu Mataka ni takataka...mpaka leo website ya ATC ni kichekesho kitupu! HAMNA KITU!
Anang'ang'ania udhamini halafu mpaka leo hamna kitu kwenye website. By now tulitakiwa tuwe tunanunua tickets online.

Hebu linganisha hii,
http://www.airtanzania.com/

dhidi ya,
http://www.precisionairtz.com/

Ni kama mtu anayekusanya stock halafu hana jinsi ya kuziuza.

Bado tuko na watendaji wasioelewa faida za internet katika kuadvertise, kumarket na kuuza. Kama kuna mtu wa ATC hapa afikishe kwa huyu mkuu wa tongotongo kwani nilishawaandikia mara nyingi kutokea wakati ya issue ya logo lakini wameamua kukaa kimya.

Again ni suala la accountability. At the end of the day anajua tutapiga kelele na hatuna meno. How do we hold such kind of leaders accountable?
 
labda huyo lawyer wa Marekani hamlipi anamfanyia kazi bure:d
 
Kama JK ni msafi kama ninavyomfikiria visenti vitarudi tu!

Sina uhakika kama Kikwete atafanya chochote katika hili kwa sababu na yeye ni mmoja wa watajwa katika ile orodha ya akina Slaa.
Unasemaje mpaka hapo?
 
Bunge lilishawahi kupitisha sheria kuhusu Anti-laundering. Kama pana mtu anayo atupatie.
 
Gazeti jongo. Limeandika habari za kuotea otea tu. Chenge kasema hasemi lolote, kashaingia katika hali ya kujitetea, sio kujiuzulu. Nchi za watu ukiandika kama hivi gazeti lako ndio mwisho wake.

Vyombo vya habari Tanzania ndio kiungo dhaifu kuliko vyote kwenye mnyororo wa kuvuta gurudumu la maendeleo.

Si yametimia lakini?????????????????????????
 
Pinda ambaye alikuwa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliotaka kujua msimamo na hatua za serikali dhidi ya Chenge, alisema wawaache Rais Kikwete na Chenge wamalizane kwa sababu Chenge ni mteuliwa wa rais.

"Tungoje, Chenge ni mteuliwa wa rais na rais amesharudi, tusubiri aamue mwenyewe kitakachofaa, hakuna kitakachoharibika," alisema Pinda.

Nilivyomuelewa mwandishi hiyo ya kumalizana ni uelewa wake ya yale aliyoyasema Pinda. Quotation ya Pinda ni hiyo niliyoibold kwa rangi nyekundu. Bado ni vitu viwili tofauti. Mwandishi amemwekea maneno Pinda kinywani. Na zaidi ya hayo maneno aliyoyasema Pinda sijui wenzangu mlitaka aseme nini? Tukitilia maanani yeye akiwa ni waziri mkuu katika serikali hii! Sidhani kama ushauri wa kumng'oa au kutokumng'oa Chenge anaweza kuutoa hadharani kabla ya bosi wake kutoa tamko. Anafuata utaratibu wa kufanya kazi na si kumkingia mtu kifua. Hawezi kuamka mbele ya kadamnasi na kusema kuwa nimemshauri Rais amtimue kazi mara moja hata kama alifanya hivyo. Ni lazima uamuzi kama huu uonekane umetoka kwa aliyemteua na si mwingineyo katika uongozi.Ndivyo ilivyo.
 
pinda hawezi kutuambi tumuache JK alimalize hili kwa kuwa yeye ndo alomteua! its totally bollocks!
basi mawaziri wote na wafanye madudu watakayo, kisha tumsubiri JK manake ndo alowachagua!
hivi hawa viongozi huwa wanafikiri saa zote kuwa wao wanaongea na watoto wadogo au?

Mkuu, kwa heshima na taadhima, zaidi ya kuandika humu ungeweza kumchukulia hatua gani Chenge? Pinda hakutuziba midomo wala kukataza kuongelea suala hili. lakini ukweli usiopindika in kuwa mtu pekee aliyekuwa na uwezo wa kuchukua hatua ni yule aliyemteua. huyu alikuwa na uwezo wa hataka kumkatalia kuachia ngazi. Sisi wengine njia pekee tuliyonayo ni kuhakikisha kuwa siku ya siku ikifika hatutayumbishwa na masinia ya pilau na kutowarudisha wale wote tunaowaona hawafai bungeni.
 
Kwa kweli kama kuna watu siwaelewi ni pamoja ma huyu Mattaka, ana wrong decisions nyingi sana mbovu, na still hawamuachi lazima wampe vitengo sensitive!
Sijui naye ni Fi***i?
 
pinda anapinda pinda maneno yake!!!! fanya kazi waziri mkuu wetu,jiamini wewe,watanzania tumechoka na maneno,tunataka vitendo.
 
Mwashangaa Bw. Vijisenti kutokutoa uamuzi wa kuguarantee ukodishaji wa Air Bus? Angetoaje wakati alikuwa hajapewa pay in slip inayothibitisha kuwa mgawo wake umewekwa kwenye akaunti yake ya nje? Mie sishangai bcose that is our leaders stile of maaking decision. Jambo litapelekwa supidi iwapo watu wameshalamba chao.
 
Ni vijisenti mapesa yako kwa Mkapa na Mramba.

Mapetha mengine yako kwa Grey Mgonja mi thijui kwanini bado yupo madarakani, huyu jamaa anahuthika na ufithadi wote unaofanyika hapa Tanzania. Thiku atakapotoka madarakani nitawaarika wana JF kushereheka nyumbani kwangu
 
Jamani ina maana hakijapatikana kitu cha kumburuta Chenge Cents mahakamani mpaka dk hii???
 
Wa kwanza kwenda chini alikuwa ni Mamvi Lowassa akafuatia Karamagi sasa Chenge.

Katika List yetu ya Mafisadi 11, watatu wametutoka.

Kwa speed hii tunayokwenda wote watamalizika hivi karibuni, wa mwisho atakuwa MH sana Jakaya Mrisho Kikwete.
MH Kikwete endelea kushindwa na moto huo huo mpaka zamu yako ifike.

Mmeamua kututia kilema cha uchumi kwa makusudi kabisa, endeleeni siku yenu inakuja, tutavunja vunja misingi ya ubabe wenu na kuwatieni pingu ili mkafie jela kwa uhaini wenu.

Ulaji huu hauwezi kwisha kamwe kama CCM bado inasimama kifua mbele nchini Tanzania.
CCM ni lazima ikatwe Kende zake ili Watanzania walio wengi wasiangamie.

Hata sisi watanzania tungekuwa kondoo wapole sana walau tungetoa mlio wa mee meee kwa mahasidi wetu kuwaonyesha kwamba hatukubali dhurma.

Watanzania walo wengi wako kimya wakisubiri wakati wa uchaguzi wale Wali na Nyama na kupata hotuba za Nyama ya ulimi.

Mafisadi 8 waliobaki wanatakiwa kuanzan kupiga kura ya kumchagua Fisadi namba 4 katika kuumbuka kwa mara ya pili, ni suala la muda tu hata Mzee wa kuachwa apumzike naye atatueleza kama Mwalimu Nyerere alimwachia usia wa kuchota mapesa na kufanya biashara Ikulu. Ikumbukwe kwamba MH Mkapa ni chaguo la MWalimu Nyerere kwa kisingizio kwamba Mkapa ni mtu safi si mla Rushwa.

Historia imedhihirisha wazi kwamba katika shughuli za Rushwa Domo la Mkapa ni kubwa kuzidi lile la Chewa, akila anakula na mikono yote miwili tena bila kunawa.
 
Kwa Kifupi Ni Hasara Ya Kama Billioni 6 Mpaka Sasa Wasiojua Billion Ni 6,000,000,000.hatujajenga Uwanja Wa Pinda International Airport,,,,,,,,mi Nafikiri Sasa Hivi Undwe Kamati Za Kuchunguza Malipo Na Matumizi Ya Mashirika Ya Umma Kutoka Bungeni Hapo Ndipo Tutakapojua Ufisadi Halisi Wacha Uko Epa,,,
Bwana Awe Nanyi.....

Hii ingetoka na kwenye magazeti jamani ili watz wengi zaidi wajue serikali yao inavyowatafuna wazimawazima! Hiyo pesa haitoshi kununua ndege nyingine used kweli? Hebu wataalamu wa eneo hili watufumbue macho wadanganyika!
 
sitaacha kulia na hii namba mpaka kieleweke


GRAY S. MGONJA



Bwana Gray Mgonja ni Katibu Mkuu wa siku nyingi wa Wizara ya Fedha. Vile vile ni Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania na anashikilia nafasi ya ukurugenzi katika kampuni ya kigeni ya Tangold Limited ambayo maelezo yake tumeyatoa kuhusiana na ufisadi unaomhusu Gavana Balali na Andrew Chenge. Kwa kuzingatia nafasi yake kama Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mkurugenzi katika Benki Kuu na vile vile Mkurugenzi katika Tangold Ltd. iliyolipwa mabilioni ya fedha za umma katika mazingira yenye utata mkubwa, ni wazi kwamba kumekuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi unaomhusu Bwana Mgonja.
 
If money makes You fool- no dought!! You will be fool with other things!!

Tanzania Ni masikini kwasababu Inaongozwa na viongozi masikini kwa muda mrefu!!! Mtu akikwambia wewe ni masikini hakuna tofauti na kuku tukana...neno Masikini ni tusi!! tena ni tusi zaidi ya matusi mengine...Na shangaa hatukasiriki Tuki ambiwa sisi ni masikini* kwasababu ni kweli...!! Kiongozi Kama Chenge amesha simama mara nagapi aki sema nchi yangu ni masikini!! ...Nime fikiria sana - nini maana ya neneo Masikini...!!

Chenge Ni masikini..kwasababu umasikini ni Ujinga No dought Chenge ni Mjinga...

Na chama Chake vile vile Ni masikini na wajinga!!!......
 
MARY CHATANDA NI KATIBU WA CHAMA WA MKOA NA WAKATI WA UCHAGUZI NDIO ALIKUWA AKIZUNGUKA NA MAMA JK MIKOANI, NI MTU MWADILIFU SANA...DIKTETA

Dikteta tema mate chini na umrudie mungu, huyu mama ndiye aliyetumwa na wenye nguvu ndani ya CCM kumteketeza Dr.Ngasongwa morogoro,ndiye mhandisi wa kashfa za kumpakazia Ngasongwa morogoro-Ulanga akishirikiana na mkuu wa mkoa huo,wakuu wa wilaya za Ulanga na morogoro, huyu ndie aliyesimama kidete kukanusha madai ya rushwa yaliyoibuliwa ktk mkutano wa CCM mkoa morogoro,huyu ndie alikuwa PCCB,Mwana habari na mkuu wa Chama morogoro,kama unataka ushahidi nenda PCCB morogoro waulize nini alifanya Aziz Abood na kwa baraka za nani chini usimamizi wa nani?
Huyu mama ni kumuua kama joka la kike lenye rangi nzuri lakini limejaa sumu kali.
Sishangai kuona kuwa naye alikuwa kwenye payrol ya Chenge maana kiburi na nguvu zilizo juu ya kanuni za CCM alichoonyesha 2007 ktk chaguzi zao CCM wilaya mpaka mkoani ilikuwa ni zaidi ya hatari. Nawamkumbusha kuwa ktk jina hili kuna Colonel mwisongo,Makamba ,Anna Makinda na Jaka Mwambi ambao waliongoza kampeni ya uchi ya kumuangamiza kada mwenzao Ngasongwa; hatufahamu kisa nini ni cha kumuangamiza huyu bwana tena kwa kutumia hela nyingi na mambo mengi ya giza!!! Waliapa kuwa watamtoa ktk baraza la mawaziri na wamefanikiwa sasa wamebakisha nadhiri moja nayo ni ubunge wake,tunawasubiri watufuate na nyumbani kwetu hapo ndipo watafahamu uzito wa kuvuka mto kilombero,kuhusu huyu mama na Makamba hayo tutayaona 2012,tutakuja kuchukua chama chetu
 
Back
Top Bottom