Jamani mawaziri kama subordinates wa fisadi Mkapa waliona Kingunge yuko busy kukusanya utajiri kwa kila hali, na wao wakaingia kazini.
Chenge amponza Mkapa
na Asha Bani
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
TUHUMA za kujilimbikizia mamilioni ya fedha nchi za nje zinazomwandama Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, zimemgusa Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye sasa ametajwa kuwa chanzo cha viongozi kutumia madaraka yao kujilimbikizia mali.
Mkapa, ambaye kwa kipindi kirefu sasa amekuwa akidaiwa kutumia vibaya madaraka ya urais katika kipindi cha miaka kumi alichokuwa rais, anakabiliwa na shinikizo la kutangaza mali alizochuma katika kipindi chake chote cha uongozi.
Shinikizo hilo limetolewa jana na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) wakati akiwahutubia mamia ya wafuasi wa vyama vya upinzani katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha maandamano ya kukishinikiza Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza makubaliano ya kuanzishwa kwa Serikali ya mseto Zanzibar yaliyofikiwa na vyama hivyo mwishoni mwa mwezi uliopita, uliofanyikia viwanja vya Ilala Garden, Buguruni, Dar es Salaam.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya Tanzania Labour na CHADEMA, Prof. Lipumba alisema viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali za ufujaji wa fedha za umma na kutumia madaraka yao kujilimbikizia mali, walishirikiana kufanya vitendo hivyo na Mkapa.
Alisema kushindwa kwa Mkapa kutangaza mali alizoondoka nazo madarakani ni ushahidi kwamba anahusika pia katika tuhuma zinazowaandama baadhi ya waliokuwa wasaidizi wake wakati akiwa madarakani.
Huku akishangiliwa na umati wa waandamanaji, Prof. Lipumba alimtuhumu moja kwa moja Mkapa kuwa ndiye chanzo cha ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupitia akauti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) na Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, kwa kile alichodai kuwa, alitumia madaraka yake kuwalinda viongozi waliokuwa wamepewa dhamana ya kusimamia maeneo hayo.
Mkapa alishindwa kusimamia vizuri rasilimali za wananchi wake katika kipindi chake cha miaka kumi ya urais. Ni katika kipindi hicho alianzisha asasi yake ya ANBEN.
Tunajua kuwa ANBEN ilianzishwa baada ya kufariki Baba wa Taifa, hizi ni dalili kwamba walikuwa wanamuogopa kwa sababu alikuwa akikemea rushwa na ufisadi waziwazi, hivyo hawakuthubutu kufanya hivyo alipokuwapo, alisema Prof. Lipumba.
Alisema tuhuma zinazomkabili Waziri Chenge pamoja na viongozi wengine walio ndani na nje ya madaraka, ni lazima zichunguzwe kwa umakini na Tume ya Maadili yenye mamlaka yote kisheria.
Tunaelewa kwamba hapo awali viongozi walitakiwa kuorodhesha mali zao katika fomu za maadili, sasa tunataka kuziona ili kubaini kila mmoja ana mali kiasi gani, alisema Lipumba.
Alisema kesho (Jumatatu) atakuwa mmoja wa viongozi wa upinzani wanaokusudia kwenda katika ofisi za Tume ya Maadili ya Viongozi kuomba fomu za viongozi mbalimbali akiwemo Chenge, Mkapa na Dk. Daudi Balali, kuona wana mali kiasi gani.
Kwamba wamekubaliana katika kambi ya upinzani kuchukua hatua hiyo ili kutambua mali zinazomilikiwa na viongozi wastaafu na walioko madarakani wanaotuhumiwa kuwanyonya Watanzania.
Dalili za Chenge na Mkapa kulindana zilianza siku nyingi kwani Mkapa alipotakiwa kutaja mali zake, Chenge alidai haruhusiwi wakati huo. Baadaye tunasikia baadhi ya viongozi walianzisha benki wakiwa madarakani, lakini kwa unyonge wa Watanzania hatukugundua, alisema Lipumba.
Alidai kushangazwa na hatua ya Mkapa kushindwa kutangaza mali zake wakati akiondoka madarakani, lakini alipokuwa akiingia Ikulu alitaja mali alizokuwa nazo kuwa ni pamoja na nyumba mbili, moja ikiwa Masasi mkoani Mtwara na Dar es Salaam, pamoja na shamba lenye mikorosho 100.
Kauli hii ya Prof. Lipumba imekuja baada ya Chenge kudaiwa kujilimbikizia kiasi cha zaidi ya sh bilioni moja katika benki moja iliyoko katika visiwa vya Jersey, nchini Uingereza.
Prof. Lipumba pia alitumia sehemu ya muda wa hotuba yake kumshangaa Rais Kikwete kwa kukataa kumaliza mtafaruku wa kisiasa Zanzibar, wakati aliweza kufanya hivyo nchini Kenya baada ya kushiriki kuwapatanisha Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga.
Alisema kuwa Rais Kikwete ni sawa na msanii, kwa vile ni mtu anayependa starehe za kutembea katika nchi za watu na kujizolea sifa zisizo na kichwa wala miguu, huku kwake kukiwa na matatizo ambayo hayahitaji hata nguvu kutatua, lakini anafanya mzaha na kuwadharau Watanzania wanaodai haki.
Alisema anachokitaka Kikwete sasa ni ule usemi wa vijana wa jino kwa jino na ndicho kinachofuata, kwa kuwa ameshindwa kulinda demokrasia ya Watanzania na kuwachezea.
Nafahamu Tanzania ni nchi ya demokrasia, lakini viongozi wake hawapendi demokrasia, wanajilimbikizia mali na kushindwa kuwahudumia Watanzania walio wengi, ambao ni maskini na ndio wapiga kura wao.
Kwa kushindwa kumaliza suala hili na kulifanya liwe la mzunguko, mimi namwita Kikwete kama msanii, alisema Prof. Lipumba.
Naye Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad, aliwaambia waandamanaji hao kuwa Katibu wa CCM, Yusuph Makamba, hana kitu cha maana anachokifanya katika chama hicho, kwa sababu anashindwa hata kuaminiwa na wenzake waliomtuma kukaa katika meza ya muafaka, kwa kudharau maamuzi aliyoshiriki kuyakifikia katika meza hiyo.
Na rais akumbuke kuwa haiwezekani kukaa meza moja na Makamba, kwa kuwa Makamba ni kama mtu asiye aminika katika chama chake, yuko hapo kwa ajili ya kula na kuchuma fedha za walalahoi, alisema Maalim Seif.
Alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais kikwete ya kutaka kuwepo kura ya maoni ya kuamua uanzishwaji wa serikali ya mseto wakati mambo yalishamalizika na kubaki utiaji saini kwa makubaliano yaliyofikiwa.
CUF haiwezi kupoteza muda na kuzungumzia suala kama hilo ambalo Rais Kikwete analifanya kama ni la usanii na mzaha, alisisitiza Maalim Seif.
Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema kwa upande wake alisema Rais Kikwete ana sura tatu zisizofanana.
Naye alimlaumu kwa kushindwa kumaliza mgogoro wa Zanzibar na kufanikiwa kutatua ule wa Kenya.
Mkurugenzi wa Vijana Taifa wa CHADEMA, John Mnyika, ambaye alimwakilisha Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, alisema suala la kutaka kuundwa kwa serikali ya mseto Zanzibar ni suala la wote bila kujali itikadi.
Watanzania si wajinga, ila CCM inajifanya kama imeweka ganzi katika mishipa ya fahamu na kufumbia macho matakwa ya wananchi, lakini hiyo ganzi itakwisha siku moja, alisema Mnyika.
Katika maandamano hayo, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe wa aina mbalimbali, kumtaka Rais Kikwete kukubaliana na majadiliano yaliyofikiwa baina ya CUF na CCM.
Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 5 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Kisukuma hela alizonazo Chenge ni mashitabalwa yaani uncountables, tusende ni lugha ya dharau sana kwamba nothing nothing.Halafu nyie wadanganyika wenzangu Sielewi kwa nini hamkumbuki mwanzilishi wa yote haya. Huyu aliwaita mafisadi wenzake huko Zanzibar wakasema azimio la Arusha linatunyima usingizi hatuwezi hata kutajirika yahe futilia mbali hilo azimio kuanzia sasa kila kitu ruksa! Sasa waliotumia vizuri hiyo ruksa mnawalaumu kwa nini? Mbaya ni nani ndugu yako aliyeacha mlango wazi baada ya kupanga na ma******* au ******* aliyefunguliwa na ndugu yako akatwaa bila mlio wa bunduki?
Kwa nini hamkumbuki Mrema alipolalamika nji hii nimekamata sahabu sa vigogo airport? Zilikuwa kilo ngapi? Ni za thamani ya visenti trillion ngapi? Kama Mwinyi alidiriki kukubali hata kuitwa shemeji na watoto wa shule kwenye uporaji alikuwa kinara kiasi gani? Kwa nini mnahangaikia matawi badala ya kuchimba mzizi? Sasa hivi Hussein Mwinyi anaandaliwa kuwa raisi wa Zanzibar ili akafiche siri huu ufisadi hamuuoni?
na Ntemi, Mwanza, TZ, - 20.04.08 @ 14:05 | #7529
Ukweli Tanzania ilishaanza kuharibika enzi za Mwinyi ingawa watu hawataki kuliona hilo.
na *****, Tz, - 20.04.08 @ 14:14 | #7531
Sijui ni nani atakuwa safi Tanzania! Ifikie mahali tuachane na itikadi za Vyama! Nilipokuwa China Juzi watu mafisadi walikuwa wakinyongwa hadi Wakuu wa haki za Binadamu walipiga makelele. Nilimwona Rais wangu Kikwete alikuwapo nchini humo na anajua Mafisadi walikuwa wakinyongwa wakati yeye alikuwa akifanya ziara nchini humo! Kwa bahati nilitembelea sehemu alipokuwapo Rais wangu huyo! Pembeni yake, katika mkutano mmojawapo alikaa CHENGE, mwanasiasa ***** na mwenye dharau anayeita mapesa vijisenti kwanini tusianze naye wakati Rais alikuwa akiona wenzake?
na LCD, Taipei Taiwan, - 20.04.08 @ 14:16 | #7532
Rais kikwete ameshapoteza mwelekeo na sasa hana la maana analofanya zaidi ya usanii.Sasa watz tuamke tudai haki zetu kwa umoja,tuhakikishe mkapa na mafisadi wenzake wanarudisha mali zote walizopora ili zihudumie wananchi wote wa tanzania.
na RUME, DSM, - 20.04.08 @ 14:19 | #7533
Kazi ya kupapambana na mafisadi tuianze sasa. List inazidi kuongezeka ilikuwa JK eleven sasa ni zaidi, tuwang'oe wote kwa nguvu ya umma.
Na huu ni wakati wa kum confront JK na maswali kutoka kwa waandishi wa habari-ambao ni mdomo wa wananchi: Aulizwe na waandishi wa habari kwa nini anakumbatia mafisadi? Kwa nini rafiki zake wa karibu ni mafisadi?. Of course waandishi wamuulize siku ya Jumanne, kwa sababu JK leo na kesho anaomboleza kifo cha Ditopile Mzuzuri ambaye amefia Hotel ya Hilux Morogoro leo asubuhi. Ikumbukwe alimuua dereva wa daladala kwa risasi barabarani
na Kawamala, Ubelgiji, - 20.04.08 @ 14:52 | #7538