The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Hii regime ya Mr. Kikwete is by far the most INCOMPETENT administration ever. Haijawahi kutokea. Kwa serikali ya kawaida ile scandal moja ya Radar tu ilikuwa inatosha kuleta mapinduzi (kusafisha) ya nguvu ndani ya serikali. Lakini tunaendelea kuona series ya ubadhirifu na scandals one after the other. Iko wapi ile motto yako ya "Ari mpya nguvu mpya", ziko wapi zile ahadi "tam tam" za kuinua maisha ya watanzania? Kutokana na mambo yaliyojiri siku za karibuni kama vile kutoweka na kutotafutwa kwa governor wa zamani wa BOT, kudanganywa kwamba mamilioni ya EPA yameanza kurudishwa bila kutajwa majina ya wahusika, Richmond gate, na ma uvundo mengine kama hili la A. Chenge nimeamua ku conclude kuwa serikali ya Mh. Kikwete inakumbatia mafisadi kwa kila njia. Na ninafikiri sitakuwa na makosa nikisema kuwa sina imani na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alikuwa sahihi kama angetoka na slogan "BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA
 
Haya wan JF mfungulieni kesi Chenge Mahamakani siju katika hati ya kiapo tutaapa kwa majina gani!!Natamani siku hiyo nimuone Mwanakijiji kisutu akiwa ana file kesi ya Chenge!!
 
It is foolish to turn off the hitter while the water start to boil.
 
Kuna wakati mtu unajisikia kushika silaha na kuwatandika baadhi ya watu haki ya nani. Mama na baba zetu wanakufa vijijini kwa sababu ya kukosa pesa za matibabu ambayo wanastahili kwa sababu wanalipa kodi, lakini unakuta kuna mjinga mmoja anajilimbikizia pesa zote hizo ambazo hata muda huu akifa ataziacha hapa hapa.
Hivi wanasali kweli watu kama hawa? Na kama wanasali, sala zao zinafika kwa Mungu kweli?

Kwa wakristu, wengi wao ni wazee wa kanisa!
 
Haya wan JF mfungulieni kesi Chenge Mahamakani siju katika hati ya kiapo tutaapa kwa majina gani!!Natamani siku hiyo nimuone Mwanakijiji kisutu akiwa ana file kesi ya Chenge!!
hilo wala lisikupe wasi mkuu tutaapa kwa jina lako.
 
Mkapa alipoingia madarakani ali-institutionalize usalama wa taifa on paper, na kabla ya hapo ofisi hii ilikuwa inaelea tu bila kuratibiwa na kuhasibiwa kwa sababu katika karatasi ilikuwa haipo, sana sana walipokuwa na haja ya kuhalalisha vitu fulani au kwenye resumes za wazee walikuwa wanaweka "ofisi ya rais".Mkapa alivyoipitisha kisheria nikaona Mr. Clean tunaye hataki vitu vya kificho.

Fast forward now mambo ya ufisadi wa EPA na ujinga wote huu yameibuka kwa kupitia usalama wa taifa naelewa nia halisi ya Mkapa ilikuwa nini.

Remove immunity and try Mkapa and his goons now.
 
Ajira ya mtoto wa Mkapa yazua utata

na Happiness Katabazi
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI taasisi za dola zikiwa zimeshaanza kuifanyia uchunguzi Kampuni ya Tanpower Resources inayohusishwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa, utata umeibuka kuhusu ajira ya mtoto wake mmoja ambaye ameajiriwa katika ofisi moja nyeti serikalini.

Utata huo ambao tayari umeanza kuwatia wasiwasi watendaji, unatokana na ukweli kwamba, mtoto huyo ambaye naye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, hivi karibuni aliajiriwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Maofisa wa juu wa serikali waliozungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa majina yao, wanasema kwamba, mtoto huyo wa Mkapa aitwaye, Nicholaus Merinyo (39), Januari mwaka huu aliajiriwa kama mwanasheria wa serikali.

Uchunguzi wa Tanzania Daima, umedhihirisha kuwa kijana huyo ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliajiriwa Januari mwaka huu na tayari ameshapangiwa kituo cha kazi kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Kanda ya Dar es Salaam.

Ofisa mmoja wa juu serikalini alilieleza gazeti hili kwamba, tayari baadhi ya watendaji ambao ndio waliopewa dhamana ya kufanya uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo ya Tanpower inayolalamikiwa kumilikishwa isivyo halali mgodi wa makaa ya mawe ya Kiwira uliopo mkoani Mbeya, wameielezea hatua hiyo ya kumuajiri Nicholaus kuwa inayolenga kuingilia uchunguzi huo.

Mbali ya Nicholaus, wanahisa wengine wa Tanpower Resources, Anna Mkapa ambaye ni mke wa rais huyo mstaafu, aliyekuwa waziri katika serikali ya Mkapa, Daniel Yona, Joseph Mbuna, ambaye ni mkwewe Mkapa na Evans Mapundi.

Kampuni ya TanPower Resources inayomiliki asilimia 85 ya hisa katika Kampuni ya Kiwira Coal and Power Limited (KCML) imekuwa ikituhumiwa kwa muda sasa, kwa kununua mgodi huo uliokuwa ukimilikiwa na serikali kwa bei ya sh milioni 700 katika mazingira ya kutia shaka.

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya ubinafsishaji na uthamanishaji wanasema kwamba, bei halisi ya mgodi huo ambao umeme wake unatarajiwa kusaidia taifa kukabiliana na tatizo sugu la kukatikakatika kwa umeme ni shilingi bilioni nne na si sh milioni 700.

Ofisa mmoja wa juu katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aliliambia gazeti hili kwamba, uchunguzi wa kina dhidi ya kampuni hiyo inayuhusishwa na Mkapa, uliidhinishwa kuanza mwishoni mwa mwaka jana.

“Tunakuhakikishia vyombo vya dola ikiwemo ofisi yetu vinaendelea kuchunguza mkataba huo na uchunguzi unafanyika kwa siri na tulianza kazi hiyo mwishoni mwa mwaka jana,” alisema ofisa huyo huku akiionyesha Tanzania Daima baadhi ya nakala zinazohusiana na uchunguzi huo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, ajira ya Nicholas katika ofisi ambayo tayari inamchunguza mwajiriwa ni jambo lisilofungamana na kanuni za utawala bora, kwa vile unavunja kanuni inayopinga mgongano wa masilahi.

Tanzania Daima ilipowasiliana na DPP, Eliezer Feleshi, kwa njia ya simu kuhusu tuhuma hizo, alimtaka mwandishi kuwasiliana naye atakapokuwa amerejea ofisini kutoka nje ya nchi alikokuwa amekwenda kwa shughuli za kikazi.

Hata hivyo mwanasheria mwingine wa serikali alilieleza Tanzania Daima kwamba, ajira hiyo ya Nicholaus inaweza kwa namna moja au nyingine kuingilia uchunguzi ambao tayari umeanza.

“Hakuna sababu ya wananchi kuamini kuwa uchunguzi unaofanywa dhidi ya TanPower Resources utafanywa kwa umakini na haki kwa kuwa tayari suala la kulinda watoto wa wakubwa linaweza kupewa kipaumbele,” alisema wakili mmoja wa serikali ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria, Katiba na Utawala wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Edmund Sengondo Mvungi, alipohojiwa kuhusu ajira hiyo, alisema kuwa ajira ya umma inatakiwa ifungamane na katiba na sheria za nchi.

“Si tu kwamba ni kinyume cha sheria kuajiri mtu ambaye ajira yake italeta mgongano wa kimasilahi lakini nafasi ya wakili wa serikali inampa mwajiriwa fursa ya kutekeleza mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kwa mujibu wa Ibara ya 59 (3) ya Katiba ni mshauri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo ya sheria. Tukiamua kuajiri hovyo hovyo tutakuwa tunajenga misingi ya ufisadi ndani ya serikali,” alisema Dk. Mvungi.

Suala hilo linakuja wakati kukiwa na taarifa zinazowatuhumu Mkapa na Yona ambao walikuwa viongozi wa juu serikalini kujiuzia mradi huo wa Kiwira wakati ukiwa mali ya umma chini ya Shirika la Taifa na Maendeleo (NDC) katika mazingira yanayotia shaka.

Taarifa zilizopata kuandikwa na gazeti moja la kila siku (siyo Tanzania Daima) mwishoni mwa mwezi uliopita, zilikariri nyaraka ambazo zilikuwa zikionyesha kuwa Mkapa na Yona walisajili kampuni hiyo Desemba 29, 2004, mwaka mmoja tu kabla rais huyo mstaafu hajamaliza kipindi chake cha pili na cha mwisho cha uongozi na kisha Machi mwaka 2005 kampuni hiyo ikanunua mgodi huo wa makaa ya mawe wa Kiwira.

Mgodi huo ulioko mkoani Mbeya hivi sasa unakamilisha mradi wenye thamani ya dola za Marekani milioni 27.8 (takriban bilioni 340) wa kuzalisha umeme utakaokuwa ukiuzwa Shirika la Taifa la Ugavi wa Umeme (Tanesco).

Kikubwa ambacho kimekuwa kikizusha maswali kuhusu hilo ni ukweli kwamba, kampuni hiyo ya TanPower iliyokuwa imesajiliwa katika kipindi kisichozidi miezi mitatu tu, tena ikiwa na wanahisa wazito ndiyo iliyoshinda zabuni wa ununuzi wa mgodi huo, kwa bei ambayo imeacha maswali mengi.

Nyaraka zaidi zinaonyesha kwamba mkakati wa kupata mradi huo zilianzishwa na Yona ambaye Machi 24, aliandika barua wakati huo akiwa Waziri wa Nishati na Madini kwenda kwa Evans Mapundi aliyekuja kuwa mkurugenzi katika kampuni hiyo ya TanPower Resources (T) Ltd.

Katika barua yake hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza Yona alisema; “I am glad to inform you that the government has agreed to go into joint venture partnership with TanPower Resources (T) Ltd in managing and operating Kiwira Coal Mines Ltd, as outlined in your writen proposal.” Tafsiri yake: “Nina furaha kukuarifu kwamba Serikali imekubali kuwa na ubia na TanPower Resources (T) Ltd. Katika kumeneji na kuendesha kampuni ya Mgodi wa Kiwira.”

Katika barua hiyo, Yona alisema serikali imeteua timu ya kufanya majadiliano na TanPower Resources jinsi ya kuendesha mchakato huo kwa haraka kisheria na kitaalamu.

Katika barua yake hiyo, Yona anataja majina ya maofisa wa serikali walioteuliwa katika timu ya majadiliano kuwa ni: Ms A. Bukuku (Mwenyekiti), Kaimu Kamishna wa Madini, Omari Chambo, Mtaalamu wa Ushauri wa Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma- PSRC, J.J. Ngelime na wakili wa Serikali, B. Sahel.

Aidha, kumbukumbu zinaonyesha kuwa, nakala za barua hiyo zilisambazwa kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Waziri wa Mipango na Ubinafsishaji, Dk. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Andrew Chenge, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Marten Lumbanga, aliyekuwa Mwenyekiti wa PSRC, John Rubambe na aliyekuwa Mwenyekiti wa KCML, Rumisha Kimambo.


Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 9 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
dhamana.na heshima kubwa waliokupa malofa na makabwela wa tz asante yao ni kuwaibia unafikili utaishi milele duniani yukowapi napolean utamjibu nini mungu wako kesho kwa dhuluma uliowatendea raia wako mkapa na mafisadi wenzako muogopeni mungu

na peter, arusha, - 16.04.08 @ 12:31 | #6848

Simtetei Nicholaus lakini mwaka jana nilifanya naye 'Internship' katika ofisi hiyo na kumuacha akiendelea kama mwanasheria mwanafunzi. Nilimuona kama mwanasheria mwenye uwezo wa kufnya kazi na kujituma. Kama taratibu za ajira zilifuatwa na watanzania wengine wakahojiwa tumpe nafasi, vinginevyo watoto wa wakubwa watakasa pa kufanya kazi wakati wana sifa walizosomea.
Kama upelelezi ulianza mwishoni mwa mwaka jana, Nicholaus nilimmkuta tangu mwanzoni mwa mwaka jana kwa ajili ya mazoezi kwa vitendo. Cha msingi apangiwe kazi ingine ambayo hatahusika na upelelezi wa kampuni hiyo maana ofisi ya mwanasheria ni kubwa na pana sana.

na T.MUZUMA, Narita-Japan, - 16.04.08 @ 12:51 | #6859


Mambo kama haya yanaonyesha jinsi viongozi wetu wanavyowadharau wananchi wa nchi hii tukufu. Haiwezekani wakacheza michezo ya kitoto namna hii kama kweli wanatuheshimu.

Mkapa uliyoyafanya yanatosha kuizika nchi hii, bado unaendelea na dharau ileile!! Mungu si Athmani, itafika siku zako arobaini zitatimia na tutakukaanga kwa mafuta yako mwenyewe. Wanaokulinda hawatadumu milele.

Hivi wewe unajisikiaje kama Mkristu unapolalamikiwa na taifa zima? Hivi hizo mali ulizojilimbikizia utazitumia wapi na kwa namna gani? Hivi una habari kwamba utakufa sawasawa na sisi unaotudhulumu? Hivi una habari nawe vilevile utazikwa kaburini na wala sio mbinguni au hata angani? Yaangalie sana maneno haya, ni madogo lakini makubwa.

Sala ya kila Mtanzania sasa hivi ni Mungu atusaidie tuweze kukuweka mbaroni na kukutaka ujibu kwetu sisi na kwa Mungu wako. Ikitokea ukafariki kabla ya kutimiza hili tutakuwa tumepata hasara isiyo kifani!!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu watokomeze mafisadi.

na Amk, Dar, - 16.04.08 @ 12:53 | #6860

unajua kuna mambo mengine mtu unaweza fanya ukamkufuru Mungu....kwa mfano, naomba tukiamka kesho viongozi wote wa CCM wafe...huu ni ushenzi,tena uliokithiri....hausemekeki!!


na mdau, tz, - 16.04.08 @ 13:05 | #6867

Hivi mtu kweli na akili zako unamtetea Nicholaus??Au ni wewe mwenyewe Nic unajisafisha....??At nifanya naye internship mwaka jana aibu tupu ina maana jamaa amemaliza bachelor yake mwaka jana,u see jinsi alivyotapeli kama baba yake fisadi mkubwa, MUDA SI MREFU TUTAANZA KUPIGA NAO KWA MAPANGA...TUMECHOKA NA KUNYONYWA NA VITA LAZIMA. YEYE NA BABA YAKE NA MAMA WOTE WEZI WAKUBWA HAWASTAILI KUISHI DUNIANI

na ATANASI MSAKI, dar, - 16.04.08 @ 13:11 | #6869

ndg yangu T.MUZUMA, Narita-Japan, - 16.04.08 @ 12:51 | #6859

usichokijua ni kwamba kwanini mkapa na kundi lake lilishiriki kwenye ubadhirifu mkubwa wa rasilimali za taifa hili(KIWIRA,ANABEN,EPA,UUZAJI WA NBC,BOTMIKATABA MIBOVU YA MADINI,NET GROUP SOLUTION etc)wanataka nico merinyo(ambaye naye ni mtuhumiwa kashfa ya kiwira)afanye kazi katika ofisi ya mwanasheria mkuu(kituo cha Ofisi ya Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Kanda ya Dar es Salaam)

huu ni mkakarti mahususi wa kuhakikisha kwamba ikitokea wakashitakiwa basi anakuwepo mtu pale wa kuvuruga ushahidi kwani katika hili hawa mabwana wenyewe wanajua kwamba hali si shwari na waliyoyafanya kwa taifa hili ni uovu mkubwa!

hivyo basi kijana huyu(nico merinyo) kuajiriwa katika
ofisi ambayo inamchunguza yeye na familia yake juu ya ufisadi ni mgongano wa maslahi wenye lengo la kuvuga upelelezi dhidi ya tuhuma zinazowakabili!
hivyo aondoke au aondolewe mara moja!

na jingo - 16.04.08 @ 13:13 | #6871

Tukuwaanbia Mkapa hana busara wala chochote zaidi ya kuendeshwa na mkewe mama mpenda pesa/ Sasa angalia kila uchafu yupo.
Ama kweli Nyerere alikula hasara kumbeba nuda asijue atawamaliza watu wake.
Mkapa,mkewe, mwanae, Sumaye, Yona na mafisadi wengine wanapaswa kuvamiwa na wananchi kama vibaka na kupewa displine

na Mpayukaji Msemahovyo, Siri, - 16.04.08 @ 13:16 | #6874

ndugu Mhariri, naoma nitumie nafasi hii kutoa pendekezo jingine. Nashauri pawepo mahali pengine ambapo tutakuwa tukitoa maoni yetu mengine, yasiyofungamana na habari hizi unazoziandaa.iwe kama vile maoni ya wasomaji kwenye magazeti

na David, Dar es Salaam, - 16.04.08 @ 13:19 | #6875

Haya sasa angalia,watu ni wale wale;kama si Mramba ni Yona ni Kigoda ni Chenge ni Karamagi ni Mkapa ni Lowasa ni Sumaye ni Balali na Maafisa wa Madini/Nishadi ambao,yumkini,hutumika ka chambo tu.Rada,ndege ya Rais,BoT/EPA,nk, majina hayo hayakosi,inakuwaje? Yaani Wa-Tz milioni 37 wanatapeliwa na kikundi cha watu wachache.Leo hii ktk Afrika Tz ndo inaongoza kupata misaada toka nchi zilizoendelea,Benki ya dunia imeifutia Tz madeni kibao,pia inazidiwa madini na A.Kusini na Kongo (Zaire) tu,ni pekee duniani kuzalisha Tanzanite,inachuana na A.Kusini kwa mbuga za wanyama duniani,ktk Afrika ni ya pili kwa mifugo mingi baada ya Ethiopia,nk,nk.Je,Mungu angetupa nini ili tumshukuru? Mh Kikwete ktk ziara zake Ulaya amewahi kuulizwa nini sababu ya umasikini wa Tz akawajibu kuwa hata yeye anashangaa na hajui.Kwa miaka mingi wa-Tz tunatafuta kiini cha umasikini wetu hatupati jibu.Ktk hatuba zake Mkapa alikuwa akitugombeza wananchi kuwa eti sisi ni wavivu,hatujitumi.Kumbe jibu ni hili 'tunaporwa na maafisa wa serikali'.

na Matiku, Dar,Tz, - 16.04.08 @ 13:32 | #6884
 
Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, anayetuhumiwa kwa ufisadi, amewasili na kusema hawezi kuzungumza kwa kuwa anachunguzwa!!!
 
SASA WANA JF NAWEKA BAYANA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA KWA MJIBU WA KATIBA YETU YA JAMHURI YA MUUGANO WA TANZANIA.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, Sura ya 2 ya Sheria za Tanzania imeweka ‘Malengo Muhimu na Misingi ya Mwelekeo wa Shughuli za Serikali' kuwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
(1) Kwamba "wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi….";

(2) Kwamba "lengo kuu la Serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi"; na

(3) Kwamba "Serikali itawajibika kwa wananchi…."


Katika kutekeleza malengo na misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali iliyotajwa, "… Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:
(a) …
(b) Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) Kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine;

(d) Kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;
(h) Kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) Kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

(j) Kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;

Ibara ya 7(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano imeamuru kuwa "… Serikali, vyombo vyake vyote na watu wote na mamlaka yoyote yenye kutekeleza madaraka ya utawala, madaraka ya kutunga sheria au madaraka ya utoaji haki, watakuwa na jukumu na wajibu wa kuzingatia, kutia maanani na kutekeleza masharti yote ya Sehemu hii …" ya Katiba. Katiba pia imewapa viongozi wa umma "… wajibu wa kufuata na kuitii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano." Aidha, viongozi wa umma wamepewa "… wajibu wa kulinda mali asilia ya Jamhuri ya Muungano, mali ya Mamlaka ya Nchi na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…." Vile vile viongozi wote wa umma "watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya Mamlaka ya Nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhirifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao."

Licha ya masharti ya kikatiba yaliyotajwa hapo juu, Andrew Chenge kama kiongozi wa umma bado anabanwa na masharti ya sheria nyingine za nchi yetu kama ifuatavyo:
SHERIA YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA, 1995


Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inamtaka Rais kuhakikisha kwamba taratibu zinatengenezwa zitakazojenga maadili na kuongeza imani ya wananchi kwa uadilifu wa viongozi wa umma na katika taratibu za utoaji maamuzi ndani ya Serikali na katika sekta ya umma. Katika kutekeleza wajibu wake, Rais anatakiwa kuweka taratibu thabiti za maadili katika utumishi wa umma ambazo:

(a) Zitahakikisha kwamba kiongozi wa umma hatajiweka katika hali ambayo maslahi yake binafsi yatagongana na wajibu wake kama kiongozi wa umma;

(b) Zitaweka taratibu za wazi za maadili kuhusu migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa;

(c) Zitapunguza uwezekano wa migongano inayotokana na maslahi binafsi kuingiliana na shughuli za umma za viongozi wa umma na kuweka taratibu za utatuzi wa migongano hiyo inapotokea.

Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma vile vile imeweka kanuni zinazotakiwa kuongoza utendaji wa viongozi wa umma:

(a) kwamba wanapokuwa madarakani, viongozi wa umma watakuwa waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali;

(b) kuhusiana na uwazi kwa wananchi, viongozi wa umma watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi na umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu;

(c) kuhusiana na utoaji wa maamuzi, viongozi wa umma watatekeleza wajibu wao kufuatana na sheria na kwa maslahi ya umma;

(d) kuhusiana na maslahi binafsi, viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya;

(e) kuhusiana na maslahi ya umma, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, viongozi wa umma watapanga masuala yao kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma;

(f) kuhusiana na zawadi, viongozi wa umma hawatadai au kupokea manufaa ya kiuchumi zaidi ya zawadi ndogo ndogo, ukarimu wa jadi/takrima au manufaa mengine yenye thamani ishara, isipokuwa tu kama manufaa hayo yatatokana na mkataba au mali ya kiongozi wa umma;

(g) kuhusiana na upendeleo, viongozi wa umma hawatatumia vyeo vyao rasmi katika kusaidia taasisi au watu binafsi katika mahusiano yao na serikali iwapo kufanya hivyo kutasababisha upendeleo kwa mtu yeyote;

(h) Kuhusiana na mali ya serikali ambayo viongozi wa umma hawatatumia ama moja kwa moja ama kisiri siri, au kuruhusu kutumiwa kwa mali ya serikali ya aina yoyote, ikiwa ni pamoja na mali ya serikali iliyokodishwa kwa ajili ya kumnufaisha kiongozi wa umma;

(i) Kuhusiana na ajira baada ya utumishi wa umma, viongozi wa umma hawatafanya vitendo vitakavyoshusha hadhi na heshima ya utumishi wa umma baada ya kuondoka katika utumishi ili kupunguza uwezekano wa matarajio ya ajira kuleta migongano ya maslahi kwa viongozi wa umma wanapokuwa katika utumishi wa umma; kupata upendeleo baada ya kuondoka katika utumishi wa umma; kutumia taarifa zinazopatikana kutokana na utumishi wa umma kwa maslahi binafsi; na kutumia utumishi wa umma kwa ajili ya kupatia nafasi za ajira nje ya utumishi wa umma
 
Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, anayetuhumiwa kwa ufisadi, amewasili na kusema hawezi kuzungumza kwa kuwa anachunguzwa!!!

Ndio mwanzo huu wa mwisho wa Chenge tuliyemjua miaka yote hii kwa kibri na dharau kubwa dhidi ya wenzake. Hureee JF, alitishia media za nyumbani lakini JF ikaendeleza vita na mambo yameanza tartibu kufit kwenye the whole plan ya kumtokomeza huyu fisadi hatari kabisa kwa nchi yetu!
 
Kwa kweli anaonekana mpole na mnyenyekevu kuliko ilivyo kawaida yake
 
Chenge anasema hawezi kujiuzulu, kwa kuwa hayo mambo yanachunguzwa
 
Ndio mwanzo huu wa mwisho wa Chenge tuliyemjua miaka yote hii kwa kibri na dharau kubwa dhidi ya wenzake. Hureee JF, alitishia media za nyumbani lakini JF ikaendeleza vita na mambo yameanza tartibu kufit kwenye the whole plan ya kumtokomeza huyu fisadi hatari kabisa kwa nchi yetu!

Umenikumbusha siku aliyorudi barazani watu walipinga sana,Jamaa yako JK kama angesikila wana JF sidhani kama angepata hii aibu anayo pata sana, namshauri aanze kufanyia kazi kelele za JF kuepuka aibu.
 
Chenge achukuliwe hatua.Na wewe ni mmoja wao nini, the next might be you so watch your steps.

Duh, siasa za kuchafuana!!!!!

Kama vile huoni kilichotendeka, mpaka useme kuchafuana???? Nadhani kuna watu watanzania kama wewe, nao ni viongozi wa serikali, wakiongozwa na JK mwenyewe ambao wataliona hili kama wewe unavyoliona.

Kwa hivyo unataka watu baada ya sentensi mbili wakae kimya iwe imekwisha?? Huo mchezo hatuna tena. Mtu ambaye yupo kwenye payroll ya serikali tunayoilipia kwa kodi zetu, halafu anajifanya kuwa na kiburi kama vile yeye ni Mungu mtu, na sisi tuliowachagua ni wapumbuvu, hakuna muda tena wa kumsitiri na kumwogopa. Hivi kama mtu unapoliona hili ukaona ni kawaida na hata halikuumizi, basi wewe mwenyewe ni tatizo, na naweza kusema ni mmoja wao.

I beg to differ mzee! Hakuna kuchafuana hapa. Let him come clean then. Kama kachafuliwa anaweza kujisafisha na watanzania tukaamini kweli alichafuliwa.

Vinginevyo ni fisadi tu. Uingereza imemchafua eh? Teteeni tu, ila fisadi ni fisadi tu, hata ukimwosha kwa JIK haondoki madoadoa yake.

Mbona ndugu zangu mmekuwa wepesi wa kusahau kiasi hiki, hayo si maneno yangu au mmemsahau Mzee Ngoyai kwamba ndiye aliyesema?
 
Chenge anasema hawezi kujiuzulu, kwa kuwa hayo mambo yanachunguzwa

hapo alipo sio yeye anaeongea ngoja yapite masaa ma2 kila kitu kikae vzr kwny damu yake, moto uwake.... apende asipende mwisho umemfika
 
Umenikumbusha siku aliyorudi barazani watu walipinga sana,Jamaa yako JK kama angesikila wana JF sidhani kama angepata hii aibu anayo pata sana, namshauri aanze kufanyia kazi kelele za JF kuepuka aibu.

JK kama kawaida yake anataka Chenge ajifunge kamba shingoni yeye mwenyewe kama Lowasa. I said it last time wakati magazeti mengi nyumbani yalikuwa bado yanaogopa kuandika habari za Chenge kuwa JF itapelekea mwisho wa chenge na baadhi ya watu wakanibeza hapa kama kawaida yao.

Sasa angalia story ya Chenge ilikoanzia, kwenye the Guardian la UK na kuanguka kwenye magazeti ya Tanzania kama sunami. I love jamboforums so much!

Mimi nawashauri mafisadi waendeleze dharau zao dhidi ya hii forum kwani kadri wanavyotudharau kama Lowasa ndivyo yanavyowakuta mmoja baada ya mwingine!
 
Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, anayetuhumiwa kwa ufisadi, amewasili na kusema hawezi kuzungumza kwa kuwa anachunguzwa!!!


Kwa vile anachunguzwa ingekuwa vizuri zaidi ajiuzulu ili apishe uchunguzi huru. Kwani kuna ulazima gani wa yeye kuendelea na uwaziri!!!??? mwambieni asing'ang'nie madaraka, watu hawamtaki na hawampendi. Nasikia eti kijiwe chake ni kwenye bar moja maarufu ndani ya Movenpick.
 
This is my country, a peacefull country, but!!!Hebu sisi wataz nani katutia uoga huu, nani katunywesha uji wa mgonjwa? Hapana haiwezekani!!haiwezekani, mijitu michache ijitajilishe huku sisi tukiendelea kuchoka,iko dawa moja ni kugawana yalivyonavyo kama yale mashamba ya Balali.
 
Huyu awajibike kwanza na kwa kuwa yeye ni mwanasheria ni matumani yangu kwamba anaelewa umuhimu wa kuwajibika ili kupisha uchunguzi huru na wa haki
 
Back
Top Bottom