The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

...hivi tukianza siasa za kuchafuana mnadhani nani atabaki humu ndani...

Haya ya Chenge tumeshayasikia, next!!


Chenge achukuliwe hatua.Na wewe ni mmoja wao nini, the next might be you so watch your steps.
 
"...hivi tukianza siasa za kuchafuana mnadhani nani atabaki humu ndani..."

Haya ya Chenge tumeshayasikia, next!!

Duh, siasa za kuchafuana!!!!!

Kama vile huoni kilichotendeka, mpaka useme kuchafuana???? Nadhani kuna watu watanzania kama wewe, nao ni viongozi wa serikali, wakiongozwa na JK mwenyewe ambao wataliona hili kama wewe unavyoliona.

Kwa hivyo unataka watu baada ya sentensi mbili wakae kimya iwe imekwisha?? Huo mchezo hatuna tena. Mtu ambaye yupo kwenye payroll ya serikali tunayoilipia kwa kodi zetu, halafu anajifanya kuwa na kiburi kama vile yeye ni Mungu mtu, na sisi tuliowachagua ni wapumbuvu, hakuna muda tena wa kumsitiri na kumwogopa. Hivi kama mtu unapoliona hili ukaona ni kawaida na hata halikuumizi, basi wewe mwenyewe ni tatizo, na naweza kusema ni mmoja wao.
 
Kwanini asiseme tu kuwa ali win Lottery?

Mi sijasema ni fisadi, najiuliza tu amewezaje kusave hizo hela?. Labda tumpe nchi inaonekana anauwezo mkubwa mno kwenye kutafuta hela!

Just thinking aloud
 
"...hivi tukianza siasa za kuchafuana mnadhani nani atabaki humu ndani..."

Haya ya Chenge tumeshayasikia, next!!

I beg to differ mzee! Hakuna kuchafuana hapa. Let him come clean then. Kama kachafuliwa anaweza kujisafisha na watanzania tukaamini kweli alichafuliwa.

Vinginevyo ni fisadi tu. Uingereza imemchafua eh? Teteeni tu, ila fisadi ni fisadi tu, hata ukimwosha kwa JIK haondoki madoadoa yake.
 
Nasikia Chenge aliuza Ngombe 2500 huko kwao Bariadi kila ngombe aliuza kwa shs 400.000 *2500
=1.000.000.0000!!!
 
LoooooooooooooooooooooooooooL!

Very gud one! basi kumbe ni msafi
 
Jana katika hafla fulani nilikutana na afisa mmoja mkubwa mstaafu. Tukagusia suala la hela za Chenge na yeye akasema huyu fisadi alikuwa akilamba si chini ya dola laki mbili kwa kila mradi uliokuwa unapitia ofisini kwake. Kwa hiyo sikushangaa Waingereza kugundua dola milioni moja katika akaunti yake nje ya nchi. Lakini kujiuzulu tu haitoshi. Tungekuwa na serikali makini huyu alipaswa kuswekwa lupango na mali zake zote kutaifishwa.
 
Hapa hakuna kuachia ngazi, Chenge atapashwa kuwajibishwa kwa ufisadi wake huo na ashitakiwe, sisi watz tunasikitisha sana kuona vyombo vya habari Uingereza ndizo zinalipua hizi issue wakati hapa kwetu tumesinzia usingizi wa pono pia mheshimiwa JK analake jambo kwani baada ya kuvunja baraza lake la mawaziri ni kipi kilichomsukuma kumteua tena chenge aendelee na wizara yake????
Jamani maandamano ya nchi nzima na kuzomewa chenge kila atakakopita pamoja na familia yake yote tuitenge ndilo litakuwa suluhisho la mwisho.
 
Hili neno siasa sikuhizi limepoteza maana yake kabisa...sio tena ku serve,ni kuji serve.Lakini hii inadhihirisha wazi hii nchi ilifika katika hali mbaya sana,na watu walikuwa wanajichotea pesa kimashindano.sasa huyu Chenge wakati wa uchaguzi wa wa NEC kuna taarifa kuwa 'alisahau' pesa nyingi sana kwenye treni za kuwahonga wajumbe,na alipofika Dodoma ali withdraw milioni 400 nyingine za kuhonga.

Lakini chanzo cha yote haya ni umaskini...umaskini wa chama tawala,kwamba una encourage wizi
 
KATIBA YA JAMHURI 57 (2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-

(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi Kwa sababu nyingine yoyote

Asante Kuhani Mkuu,
Nilitaka kusoma katiba kifungu 57(2)(e) ila nimetoka nduki baada ya kukutana na maneno haya mwanzo '(Toleo hili la Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya Mwaka 1977, .... tangu ilipotungwa mwaka 1977 hadi tarehe 30 Aprili, 2000.
Dar es Salaam, A.J. CHENGE 1 Novemba, 2000 Mwanasheria Mkuu'

All in all, Chenge should not resign, rather he should be sacked and tried!
 
They will never sack him....believe me.

Mkuu FD nakuamini....100%! Sio mara ya kwanza wala haitakua ya mwisho katika siasa za bongo. Unakumbuka ya Moniza Mbega na kupeleka ndugu zake Ureno? BWM akampongeza kwa kujiuzulu ili akasome..
 
They will never sack him....believe me.

Mama meghji nae alisema hivyo hivyo sasa yuko wapi???

Kuna sababu ya kuomba International community imuwekee pressure ikiwa ni pamoja na kumnyima visa ya kuingia chi zote za Ulaya na Marekani.

Pili wananchi waanze kumzomea popote pale aendapo mpaka kieleweke
 
Nasikia Chenge aliuza Ngombe 2500 huko kwao Bariadi kila ngombe aliuza kwa shs 400.000 *2500
=1.000.000.0000!!!

Maneno haya yalisemwa na mmoja wa vigogo serikalini kwamba kulingana na maslahi yake yaani mshahara wake hawezi kuwa na kiasi hicho labda awe aliuza ng'ombe. Kwa yeye kama Chenge ng'ombe wenyewe ni RADA, NDEGE, MIKATABA YA MADINI NA KIWIRA SPECIFICALLY NK NK.
 
Heshima Mbele wanabodi,

Chenge ataondoka hivi karibuni,na kwa taarifa yenu tu tunajipanga kuweza kumuangamiza kupita kule kule alikotokea Lowassa,

Hoja zilishapangwa,Madokezo yapo tayari na Msemaji tulishmpata na atakuwa mwanaharakati mmoja ambaye kwa sasa jina lake ni siri ila anatoka chama cha mapinduzi,Ni mbunge shupavu asiye na woga.

pindi ushahidi ukikamilika nitaleta Ripoti kamili hapa Jf kabla Motion haijapanda hewani,kaeni mkao wa kula tu...kama sio katika kikao hiki basi kinachokuja cha Bajeti,na mie nilipendekeza iwe kipindi cha bajeti coz ufisadi huu unahusiana sana na pesa ya Bajeti yetu.

tuwe wavumilivu wakti tukijipanga kupunguza mafisadi.
 
ayyyaaaaaaaaa,kwa mtindo huu,nchi hii haitoendelea ng'o,maana mwenye kisu ndio anaye kula nyama
 
NI kweli anapaswa kujiuzulu. Ana kufulu ya kufa mtu huyu jamaa. Kuna wakati akiwa Lakairo Hotel Mwanza alimuuliza mmiliki kuwa, gharama ya annex ya jengo la Hotel yake alilofanya ili kuboresha huduma amejenga kwa kiasi gani, alipoambiwa akasema kumbe unaweza kujenga tuhotel twa namna hiyo kumi kwa mkupuo, na ukachuma sana.

Pia katika uchaguzi wa Ubunge katika jimbo lake wilayani Bariadi alimwaga pesa nyingi na kununua magari mapya mapya yakiendeshwa na jamaa zake. Na aliwahi kusikika kuwa kwenye uchaguzi ametumia pesa nyingi na anatafuta deal kusudi arejeshe, hapa ananukuriwa na kijana mfanyabiashara, mdogo wake na waziri mmoja wa zamani.

end
 
Back
Top Bottom