The Radar Scandal: Investigation & Progress

Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, anayetuhumiwa kwa ufisadi, amewasili na kusema hawezi kuzungumza kwa kuwa anachunguzwa!!!

Nilisema ajieleze kwa misingi gani? Hawezi kuongea mpaka uchunguzi wa SFO uishe. Baada ya hapo hawezi kuongea mpaka uchunguzi wa PCCB uishe. PCCB wakimaliza aidha ana kesi ya kujibu - kwa hiyo hawezi kuongea kwa sababu ana kesi -, au hana kesi ya kujibu - kwa hiyo hana la kuongea, ni msafi, na mambo yalienda safi kama walivyosema dili la EPA. Angalia mchezo utakavyo enda.

Kesi yetu isiwe kumtaka ajieleze. Hana mzigo wa kujieleza. Na hatutaki maelezo. Kesi ni kumtaka ajiuzulu kwa historia ya harufu ya rushwa (appearance of corruption) na kwa kukosa uzalendo kwa kusweka hela nje. Vinginevyo tunapotea stepu.
 
Chenge alitishia waandishi wa habari mwaka jana na kwa muda mrefu baadhi ya magazeti yalishindwa kumgusa kabisa. Na kwa kiburi wakati imetangazwa ile orodha ya aibu yeye alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kujitokeza na kutamba kuwa yeye ni mkurugenzi na hana mpango wa kushtaki mtu yeyote.
 
Moja ya sifa kubwa ya kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ni kuhakikiksha kwamba serikali haijikwai katika kila jambo ilifanzalo, liwe la kidharimu au kimaadili.

Yeye ni kama "caretaker" wa shughuli zote hizo na huweza kupona suluba yoyote ile endapo kuna matatizo ya kisheria kwani huwa anafahamu "avenues" zote za ku-"circumvent" mambo yote yatokeayo sasa hivi Tanzania.

Maana ya Circumvent:

Kwanza ni kitenzi halafu,maana halisi kwa kiingereza nanukuu;

avoid or try to avoid fulfilling, answering, or performing (duties, questions, or issues); "He dodged the issue"; "He skirted the problem"; "They tend to evade their responsibilities"; "he evaded the questions skillfully"- mwisho wa kunukuu.

Ufafanuzi:

"He" tunaweza tukasema ni Chenge

"They" tunaweza kusema ni Serikali

Kwa hio Chenge ni master na Prince wa Darkness.

Wananchi tunaweza kumshitaki huyu bwana bila wasiwasi. Na baadae (2010) kubadilisha mawazo.

NB:

Kama Chenge unasoma hii utanielewa.
 
Mimi nauhakika Muungwana anatumia staili kama EL alivyoondoka Chenge atajitundika kamba yeye mwenyewe clock is ticking
 
Kwa hakika huyu nadhani ni mtu mzito sana kuliko hata alivyokuwa gavana wa benki kuu!!!

Aliyekuwa mwanasheria mkuu wa nchi kama kweli akijulikana bila shaka ametuibia... Then kama taifa tuna tatizo kubwa... maana kama ni ethics, kufuata sheria mwanasheria mkuu wa serikali ndiye angekuwa mtu wa kwanza kwa usafi immediate after head of the state... sasa kama yeye kweli atajulikana ametuibia... du kazi ipo...
 
Someni wenyewe

Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25 Amchotea kigogo bilioni moja
Amwashia indiketa Ben Mkapa

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.

Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.

Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.

Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.

Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.

Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.

Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).

Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.

Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.

Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.

Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.

Kampuni hiyo, ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, tarehe 29 Desemba 2005 dola 13,340,168.37 na 30 Desemba 2005 ilichota kiasi kama hicho.

Siku hiyohiyo, 30 Desemba, kampuni ilihamisha dola 13,340,168.37 na kuzipeleka mahali ambapo hapajafahamika.

Hii ni siku ambayo Rais Kikwete alizindua Bunge jipya mjini Dodoma baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na kabla ya kuunda baraza lake la kwanza la mawaziri.

Katika uteuzi wake wa mawaziri, Chenge alipewa uwaziri wa Afrika Mashariki kabla ya mabadiliko yaliyompeleka kuwa Waziri wa Miundombinu na kurejea kwenye nafasi hiyo rais alipounda baraza jipya baada ya kulivunja kufuatia kashfa ya Richmond.

Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo MwanaHALISI, TANGOLD ilipokea kutoka kampuni tata ya Deep Green Finance Limited Sh. 39,761,397.98 hapo 8 Oktoba 2005 wakati tarehe 10 Desemba 2005 TANGOLD ililipa Deep Green Sh. 100,940,489.71.

Wakati wa kuchezesha malipo hayo, kulikuwa na uchaguzi mkuu ambapo inadaiwa kuwa fedha hizo huenda ziliingizwa kwenye uchaguzi huo.

Kampuni ya Deep Green ndiyo ilisajiliwa na kampuni ya uwakili ya IMMA ya Dar es Salaam, ambako mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete na mtoto wa Rais Amani Karume, Fatma wanafanya kazi.

Ni kampuni hii mashuhuri ambayo mmoja wa waanzilishi wake ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na mmoja wa mawakili waanzilishi, Protas Mujulizi aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu.

Kampuni ya Deep Green ndiyo imetia fora kwa viroja kwa kuonyesha kuwa ilifungua akaunti yake benki siku ya Mei Mosi wakati siyo siku ya kazi.

Tarehe 23 Novemba 2005 TANGOLD iliichotea Meremeta Sh. 555,300,040 ambazo haijulikani ni kwa kazi ipi.

Siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, hapo 12 Desemba, TANGOLD iliichotea tena Meremeta Sh. 551,060,000 ambazo haijafahamika zilikuwa kwa shughuli ipi.

Kinachozidisha utata ni kwamba tangu Februari 2006 baada ya kuundwa baraza la mawaziri, akaunti ya TANGOLD ya fedha za kigeni haijalipa wala kupokea fedha yoyote hadi tarehe 31 Machi 2008 huku ikiwa na akiba ya dola 12,997,950.84 (sawa na zaidi ya bilioni 15 za Tanzania).

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye akaunti ya nje, akaunti ya ndani ya TANGOLD imefanya malipo yamwisho 6 Juni 2006 ya Sh. 220,980,370. Hadi 31 Machi mwaka huu ilikuwa na akiba ya Sh. 1, 379,359,367.39.

Kiasi cha fedha kilicholimbikizwa kwenye akaunti za TANGOLD ambako wakurugenzi ni pamoja na Chenge na watumishi wengine wa serikali, zinalingana na kiasi ambacho serikali inapigia magoti kutoka kwa wafadhili.

Hivi sasa Chenge anachunguzwa na makachero wa Uingereza na Tanzania kuhusiana na uwezekano kuwa alipokea hongo katika biashara ya kununua rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

Alipoulizwa kuhusu hali hii ya uchotaji fedha na ulimbikizaji nje, Dk. Willibrod Slaa, mbunge wa Karatu amesema, "kama hizi fedha ni za serikali kwa nini serikali igeuke ombaomba wakati zimelala benki?"

Kwa nini umma usiamini kuwa fedha hizo zimo mikononi mwa mtandao wa kifisadi, anahoji Dk. Slaa na kuongeza, "Kigugumizi cha serikali kinatoka wapi hapa wakati fedha hizi zinatosha kujenga madarasa 400 ya sekondari au wastani wa shule moja kwa kila mkoa."
 
Inaelekea hawa Ngosha haka kamchezo ka ufisadi wamejifunza ukubwani walipokuja mjini! Kwanza tulimwona Balozi Mahalu akiburuzwa mahakamani na sasa huyu Chenge!

Sijui wanakula kisha wanasahau kunawa au wakishiba vyombo wanasahau kusafisha ???!!!

Tumeona mafisadi wengi lakini tunaambiwa ushahidi wa "kimazingira" hata mahakamani hawapelekwi; lakini hawa watani zangu wasubiri kutolewa kama mbuzi wa kafara - hapa ndiyo tutasikia serikali ikisifiwa kwa kupambana na ufisadi!
 
Chenge alitishia waandishi wa habari mwaka jana na kwa muda mrefu baadhi ya magazeti yalishindwa kumgusa kabisa. Na kwa kiburi wakati imetangazwa ile orodha ya aibu yeye alikuwa ni miongoni mwa watu wa kwanza kujitokeza na kutamba kuwa yeye ni mkurugenzi na hana mpango wa kushtaki mtu yeyote.

Yaani acha tu,

miye nilikuwa namuangalia majigambo yake na nikaanza kumhesabia siku ...... tik tak tik tak tik tak
 
Kujiuzxulu kumemfika sasa hana jinsi ya kukwepa.

JK asipomfungulia mbwa wamng'ate basi ajue kuwa anazidi kujiharibia kukubalika kwake.

Chenge apende asipende kipindi hiki kakamatwa pabaya.
 
JK kama kawaida yake anataka Chenge ajifunge kamba shingoni yeye mwenyewe kama Lowasa. I said it last time wakati magazeti mengi nyumbani yalikuwa bado yanaogopa kuandika habari za Chenge kuwa JF itapelekea mwisho wa chenge na baadhi ya watu wakanibeza hapa kama kawaida yao.

Sasa angalia story ya Chenge ilikoanzia, kwenye the Guardian la UK na kuanguka kwenye magazeti ya Tanzania kama sunami. I love jamboforums so much!

Mimi nawashauri mafisadi waendeleze dharau zao dhidi ya hii forum kwani kadri wanavyotudharau kama Lowasa ndivyo yanavyowakuta mmoja baada ya mwingine!

Hana ubavu wa kumfukuza mtu, yuko pale Ikulu kama picha tu ndio maana hata mafisadi huwa wanakuwa na kiburi cha kutamka sijiuzulu ng'o kama alivyotamka Balalli.
 
Huyu awajibike kwanza na kwa kuwa yeye ni mwanasheria ni matumani yangu kwamba anaelewa umuhimu wa kuwajibika ili kupisha uchunguzi huru na wa haki

Mbona hakutumia u-anasheria wake kuhakikisha hashiriki kuiuza nchi kifisadi? Kwa kutumia hii reference, do you think anaweza tumia common sense na kuamua kujiuzuru at this juncture? Nope!
 
Nukuu "WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua".

please give me break, mapigo ya moyo yamesita kufanya kazi kwa muda.
 
Karudi....karudi kutoka wapi?

Ngabu,

Karudi toka kwenye msafara muhimu sana aliokuwa afanye kwa niaba yake na "serikali ya Tanzania". Mambo yamemfika shingoni hadi sasa anaogopa hata kwenda UK maana anasubiriwa kwa hamu na media ya huko.

Chenge alikuwa hajui nguvu ya mtandao wa watanzania uliotanda dunia nzima. Bado namuhesabia siku ... tik tak tik tak tik ...
 
Jamani, mimi hizi tuhuma za ufisadi wa watu zimeshanichosha! Hivi ni wapi duniani zaidi ya Afrika ambapo serikali inakuwa na mafisadi na maskendo kibao halafu hakuna hatua zozote za maana zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa? Hii haingii akilini kabisa hata kwa mimi mwenye akili ya wastani.

Hivi ni wapi duniani penye demokrasia ya kweli ambapo watu watakichagua chama kilichopo madarakani kuendelea kutawala huku viongozi wa serikali yake wakiendelea kuiba (allegedly) na kuitafuna nchi huku wananchi wake wengi wakiishi maisha ya kifukara? Hivi ni watu gani duniani wanaoweza kuwachagua viongozi ambao ni mafisadi na wasiotetea maslahi yao?

Nina mengi ya kusema na nimechoka kusikia watu wakituhumiwa kwa ufisadi na nimechoka kuona watu wakiendelea kuwapigia makofi na vigelegele mafisadi ambao hata hawawajali.

Aaaagh...nimechoka hata kuandika...
 
Someni wenyewe

Chenge kufuru tupu, amiliki bilioni 25 Amchotea kigogo bilioni moja
Amwashia indiketa Ben Mkapa

WAZIRI wa Miundombinu, Andrew Chenge anaogelea katika utajiri wa zaidi ya Sh. 25 bilioni zenye utata huku Rais Jakaya Kikwete akiendelea kumkumbatia, MwanaHALISI limegundua.

Chenge amekuwa mfanyakazi serikalini kwa karibu miaka 30 na hafahamiki kuwa mfanyabiashara.

Kiwango kinachotajwa ni pamoja na fedha zilizogunduliwa na makachero wa Uingereza katika akaunti zake za nchi za nje.

Fedha zilizoko kwenye akaunti yake ya nchini, Na. 011101006950 katika benki ya NBC Limited, ni Sh. 25,794,805.89 za Tanzania hadi Ijumaa iliyopita, tarehe 11 Aprili 2008.

Katika akaunti yake ya Uswisi, ambako ana akaunti ya fedha za kigeni, Chenge amehamishia dola za Marekani 467,000, sawa na zaidi ya nusu bilioni kwa fedha za Tanzania.

Fedha za Uswisi zimelimbikizwa katika akaunti Na. 030105000364. Zilihamishwa kutoka akaunti Na. 011105011782 ya kampuni ya TANGOLD Limited, tangu 22 Februari 2006 kupitia NBC Limited.

Taarifa za kuaminika ambazo MwanaHALISI imezipata zinasema Chenge ni Mkurugenzi wa kampuni ya TANGOLD Limited ambayo ina dola 12,997,950.84 sawa na Sh. 15 bilioni za Tanzania katika NBC Limited tawi la Makao Makuu.

Aidha, kampuni hiyo inahifadhi Sh. 1,379, 359,367.39 katika akaunti Na. 011103024852 tawi hilohilo la NBC Limited.

Habari tulizopata wakati tukienda mitamboni, zinasema kwamba makachero wa Uingereza wanafuatilia uhalali wa Euro 3 milioni (sawa na zaidi ya Sh. 8 bilioni za Tanzania) zinazodaiwa kuwa Chenge alizipeleka kwenye akaunti zake nje ya nchi.

Taarifa nyingine ambazo hatukuweza kuzithibitisha haraka, zinasema Chenge alihamisha kwa mkupuo dola 600,000 za Marekani kwenda kwenye akaunti ya ofisa mwandamizi mmoja aliyekuwa Benki Kuu miaka kadhaa iliyopita, na ambaye kwa sasa anaongoza shirika la umma nchini.

TANGOLD ni kampuni ambayo inadaiwa kumilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na ambayo inadaiwa pia kuwa ndiyo imerithi mali na madeni ya kampuni ya Meremeta Limited iliyokuwa ikijihusisha na uchimbaji madini, Buhemba, mkoani Mara.

Hata hivyo, kuna utata juu ya lini kampuni hiyo ilianzishwa nchini. Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi aliuambia Mkutano wa Tisa wa Bunge kuwa TANGOLD iliundwa mwaka 2006 kupitia Task Force maalum ya serikali, kumbukumbu zinaonyesha kuwa kampuni ilianzishwa mapema 2000 au kabla.

Hiyo inathibitishwa na ukweli kwamba tarehe 1 Januari 2000 walikuwa na akaunti ambayo haikuwa hata na senti moja katika akaunti zake mbili hadi 29 Desemba 2005 zilipoingizwa dola 13,340,168.37.

Fedha hizo zilikuwa zinatoka Hazina kupitia Benki Kuu (BoT).

Kwa akaunti ya fedha za Tanzania, tarehe 1 Agosti 2005, TANGOLD Limited ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, Sh. 4,703,221,229.08 kwa hundi Na. 241741 na kufanyiwa uhamisho wa haraka (special clearance).

Chenge, akiwa mkurugenzi, anahusika na uhamishaji, ulimbikizaji na ulipaji wa fedha kutoka akaunti za TANGOLD.

Wakurugenzi na waidhinishaji malipo wengine wa kampuni hiyo ni, Daudi Ballali, Gray Mgonja, Vincent Mrisho na Patrick Rutabanzibwa.

Ballali alikuwa gavana wa BoT, Mgonja akiwa Katibu Mkuu Hazina, Mrisho akiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Rutabanzibwa akiwa Katibu Mkuu Maji na Umwagiliaji.

Matumizi ya fedha kutoka akaunti hizi ambako kuna mkono wa Chenge ndiyo yanaongeza utata.

Kutoka kwenye akaunti ya binafsi ya Chenge, mamilioni ya shilingi yamelipwa kwa watu mbalimbali wakiwa ni pamoja na Janet Mashale, Mary Nchimbi, Mary Chitanda na Livingstone Ruhere.

Wengine ni Getrude Mtiga, Hawa Kiama, Leocardia Kalumuna, Athumani Sheha na David Sanga.

Miongoni mwa waliolipwa ni viongozi wa CCM, waandishi wa habari na wengine ambao hawakuweza kutambulika. Muhimu ni kwamba karibu fedha hizo zote zililipwa wakati uchaguzi wa CCM mwaka jana ambapo Chenge aliwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC). Alishinda kwa kura nyingi.

Akaunti ya TANGOLD inaonyesha kutoingiza kiasi chochote cha fedha kwa miaka mitano, kati ya Januari 2000 na Desemba 2005.

Kampuni hiyo, ilichota kutoka Hazina kupitia BoT, tarehe 29 Desemba 2005 dola 13,340,168.37 na 30 Desemba 2005 ilichota kiasi kama hicho.

Siku hiyohiyo, 30 Desemba, kampuni ilihamisha dola 13,340,168.37 na kuzipeleka mahali ambapo hapajafahamika.

Hii ni siku ambayo Rais Kikwete alizindua Bunge jipya mjini Dodoma baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na kabla ya kuunda baraza lake la kwanza la mawaziri.

Katika uteuzi wake wa mawaziri, Chenge alipewa uwaziri wa Afrika Mashariki kabla ya mabadiliko yaliyompeleka kuwa Waziri wa Miundombinu na kurejea kwenye nafasi hiyo rais alipounda baraza jipya baada ya kulivunja kufuatia kashfa ya Richmond.

Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo MwanaHALISI, TANGOLD ilipokea kutoka kampuni tata ya Deep Green Finance Limited Sh. 39,761,397.98 hapo 8 Oktoba 2005 wakati tarehe 10 Desemba 2005 TANGOLD ililipa Deep Green Sh. 100,940,489.71.

Wakati wa kuchezesha malipo hayo, kulikuwa na uchaguzi mkuu ambapo inadaiwa kuwa fedha hizo huenda ziliingizwa kwenye uchaguzi huo.

Kampuni ya Deep Green ndiyo ilisajiliwa na kampuni ya uwakili ya IMMA ya Dar es Salaam, ambako mtoto wa rais, Ridhiwani Kikwete na mtoto wa Rais Amani Karume, Fatma wanafanya kazi.

Ni kampuni hii mashuhuri ambayo mmoja wa waanzilishi wake ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na mmoja wa mawakili waanzilishi, Protas Mujulizi aliteuliwa kuwa jaji wa mahakama kuu.

Kampuni ya Deep Green ndiyo imetia fora kwa viroja kwa kuonyesha kuwa ilifungua akaunti yake benki siku ya Mei Mosi wakati siyo siku ya kazi.

Tarehe 23 Novemba 2005 TANGOLD iliichotea Meremeta Sh. 555,300,040 ambazo haijulikani ni kwa kazi ipi.

Siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2005, hapo 12 Desemba, TANGOLD iliichotea tena Meremeta Sh. 551,060,000 ambazo haijafahamika zilikuwa kwa shughuli ipi.

Kinachozidisha utata ni kwamba tangu Februari 2006 baada ya kuundwa baraza la mawaziri, akaunti ya TANGOLD ya fedha za kigeni haijalipa wala kupokea fedha yoyote hadi tarehe 31 Machi 2008 huku ikiwa na akiba ya dola 12,997,950.84 (sawa na zaidi ya bilioni 15 za Tanzania).

Wakati hali ikiwa hivyo kwenye akaunti ya nje, akaunti ya ndani ya TANGOLD imefanya malipo yamwisho 6 Juni 2006 ya Sh. 220,980,370. Hadi 31 Machi mwaka huu ilikuwa na akiba ya Sh. 1, 379,359,367.39.

Kiasi cha fedha kilicholimbikizwa kwenye akaunti za TANGOLD ambako wakurugenzi ni pamoja na Chenge na watumishi wengine wa serikali, zinalingana na kiasi ambacho serikali inapigia magoti kutoka kwa wafadhili.

Hivi sasa Chenge anachunguzwa na makachero wa Uingereza na Tanzania kuhusiana na uwezekano kuwa alipokea hongo katika biashara ya kununua rada ya kijeshi kutoka kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

Alipoulizwa kuhusu hali hii ya uchotaji fedha na ulimbikizaji nje, Dk. Willibrod Slaa, mbunge wa Karatu amesema, "kama hizi fedha ni za serikali kwa nini serikali igeuke ombaomba wakati zimelala benki?"

Kwa nini umma usiamini kuwa fedha hizo zimo mikononi mwa mtandao wa kifisadi, anahoji Dk. Slaa na kuongeza, "Kigugumizi cha serikali kinatoka wapi hapa wakati fedha hizi zinatosha kujenga madarasa 400 ya sekondari au wastani wa shule moja kwa kila mkoa."

Hawa watu wana-deserve kunyongwa... Huu ni uhujumu wa uchumi wa hali ya juu. Hawapaswi kusimama majukwaani na kutuhutubia tena. Enough is enough.. Wote ni majizi. Wana-deserve kuwa executed kwa kudungwa "Lethal Injection" ama kupigwa shoti kwenye "Electric Chair". Kama Tanzania hakuna "Electric Chair" niko tayari kuanzisha kampeni ya kutafuta watakaochangia ununuaji wa hiki kiti. Huu ni uhujumu wa uchumi at its best!!!

Pamoja na data hizi zote je watanzania tunahitaji nini zaidi ku-prove hawa jamaa wanatuzidishia umaskini? Are we really serious?
 
bado zile Paundi milioni 5...

Mwanakijiji,

Fafanua maana nimetoka kapa hapo.

Naona Wazungu wamekosea, hizo milioni ni shilingi sio pounds au dola
kwi kwi kwi!!!!!

Si ajabu Chenge alikuwa analundika tu, alisahau ni dola na akadhani ni pesa za madafu.
 
Back
Top Bottom