TEMESA wakubaliana na Azam Marine kuvusha abiria Kigamboni (Ferry)

Bado nawaza kuhusu yale mawimbi ya saa nne saa tano hivi yanayopelekea Kivuko kubadili root zake na hata kuamua kugeuza kilipotoka je hizi za AZAM zitaweza kuhimili yale mawimbi kweli?
 
Dar es Salaam. Ili kuendelea kuwapa wananchi huduma huduma ya uhakika, kwenye safari za Magogoni na Kigamboni Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Tamesa) imefikia makubaliano na kampuni ya Azam marine ya kuvusha abiria.

Siku za hivi karibuni wananchi wanaokaa Kigamboni na vitongoji vyake, walipata adha ya usafiri baada ya kivuko cha Mv Magogoni kuharibika na kushindwa kufanya safari zake kama ilivyo kawaida.

Hali hiyo ilisababisha kivuko cha MV Kigamboni kuelemewa na abiria walikuwa wakivuka kutoka upande mmoja kwenda upande wa pili, huku wakijazana, ambapo magari yakizuiliwa kuvuka kutokana na kivuko hicho kuwa kidogo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Juni 13, 2022 na kitengo cha masoko na uhusiano Tamesa imeeleza kuwa, imefikia makubaliano na kampuni hiyo wakati wakiendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake.

Aidha katika taarifa hiyo Tamesa imewashauri wananchi kuacha kutumia mitumbwi ili kulinda usalama wao.

Source: Mwananchi
 
Jamaa wanataengeneza mazingira ya kupiga pesa vizuri hapo
 
Back
Top Bottom