Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wadau nawasabahi.

Nikiwa mlipa kodi pamoja na tozo mbalimbali najisikia uchungu sana kusikia kuwa Serikali inataka kukarabati kivuko cha Mv Magogoni kwa bil.7. wakati bei ya kuunda kivuko kipya ni kati ya bil.8.5 -9

Najiuliza kwanini ufanyike ukarabati?

Kwanini kisinunuliwe kivuko kipya?

Hata kama kununua ni gharama lakini tofauti yake ni ndogo sana. Hebu watendaji wa serikali tuwe na uchungu na kodi za masikini wananchi wananchi wana maisha magumu sana hata kama mnatuamulia mtakavyo lakini tunaumia tunapohisi mnatuibia.

Juzi juzi mmetoka kutuibia kwenye ukarabati wa mv hapa kazi mlikikarabati kwa bil.4.5 wakati kivuko kipya ni bil 7.5 kumbukeni watanzania sio wajinga kihivyo

======

Serikali yasaini mkataba ujenzi wa MV Magogoni

SERIKALI imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni wenye thamani ya Sh bilioni 7.5 ambazo ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Akizungumza katika viwanja vya kivukoni jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema, ukarabati wa kivuko hicho ni juhudi na mikakati ya serikali katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji.

Profesa Mbarawa amesema kuwa miradi mitano ya ujenzi wa vivuko vingine vipya na miradi 16 ya ukarabati wa vivuko unaendela baada ya kusainiwa kwa mikataba yake ambayo hadi kukamilika kwa miradi hiyo itagharimu Sh bilioni 60.7.

Ametoa wito kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia vema ukarabati wa kivuko hicho utakaofanyika Mombasa nchini Kenya chini ya kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd kwa muda wa miezi mitano.

Kivuko cha MV Magogoni kilijengwa mwaka 2008, kina uwezo wa kubeba abiria elfu mbili na tani 500 za mizigo yakiwemo magari madogo 60 kwa wakati mmoja.
 
Ndani ya nchi zipo kampuni zingefanikisha ukarabati kwa bei ya kawaida.

Huu ni upigaji tu.

Screenshot_20230216-194509.jpg
 
Hicho cha billion 8 ni kikubwa sana na itakuwa wastage ya pesa kukinunua maana eneo la kigamboni ni fupi sana kuhitaji kivuko kikubwa.

But kuna vivuko vya watu 70, 120, 150 etc ambavyo vinauzwa kwa,$250,000, $350,000, $400,000 hadi $ 500,000. Ambayo ukileta hela ya Tanzania haifiki hata one billion.

So hapo vivuko viwili vipya havikutakiwa kula hata 4 bilioni.

Ila kwasababu majizi yamerudi kazini shughuli imeanza.
 
Hiki hapa ni kivuko kipya kilijengwa na Songoro Marine kikapelekwa Mafia- Nyamisati!, Kilijengwa kwa Billion 5.8 kipya sio ukarabati! Sasa sijui wanapeleka tender Kenya kufanya nini wakati miaka mingi Songoro Mirine amekuwa mjenzi na mkarabati wa hivi vivuko vyetu kwakushirikia lna na TEMESA
Screenshot_2023-02-16-17-45-50-05_0b2fce7a16bf2b728d6ffa28c8d60efb.jpg
 
Wezi sana hawa. Halafu wanajidai kufanya sherehe kutiliana sahihi mkataba hadharani. Wanafikiri wananchi ni wajinga. Hizo bei hawapendi kutujulisha ili tusijue ufisadi wao.
 
Hiki hapa ni kivuko kipya kilijengwa na Songoro Marine kikapelekwa Mafia- Nyamisati!, Kilijengwa kwa Billion 5.8 kipya sio ukarabati! Sasa sijui wanapeleka tender Kenya kufanya nini wakati miaka mingi Songoro Mirine amekuwa mjenzi na mkarabati wa hivi vivuko vyetu kwakushirikia lna na TEMESAView attachment 2519632
Sasa watu 200 unaleta hapa?? We jamaa una akili kichwani kweli?
Hiko kivuko kinachoenda kukarabatiwa unajua Capacity yake.
We jamaa maku kweli.
 
Ni mambo ya Ajabu ,yalojaa wizi , Roho mbaya Kwa Watanzania , matumizi mabaya ya Fedha zetu, na kutuona Watanzania ni wajinga sana .


Lakini haya yote ni matokeo ya kuongozwa na Kiongozi mwepesi mwepesi, asiyemjuzi na mdadisi, ambaye yeye akiletewa jambo ni kutia wino tu!.


Bahati mbaya sana, Unakuta Hizi Pesa, watu wa TAKUKURU wanafungu lao, Usalama Wana lao, Vyombo vyetu vya Ulinzi ma Usalama nao wa lao, Viongozi wa Dini Wana lao, Wapinzani njaaz Wana lao , Kiongozi Mkuu naye ana lake '.


Tumejengewa madaraja ya mbao Kwa mamilion, tumejengewa vibanda Kwa ma milion, watu wameonba Trillion 11, watu wameingia mikatana na wahindi, wr mikatana ya kumonitor hali ya umeme nchini..


Mambo ya ovyo ovyo ovyooo..


Hivi Kwa akili ya haraka haraka, Kivuko kiloungwa Kwa Billion 8, Leo kinakarabatiwa Kwa Bilion 7??.


RAIS KWELI ??
 
Back
Top Bottom