nzahaksm

Member
Dec 2, 2018
11
11
Leo wakati navuka kutokea Kigamboni nimekutana na suala la kustaajabisha sana.

Viti na mapambo yamewekwa eneo la mbele kidogo ukishuka kwenye kivuko kutoka Kigamboni. Kulikuwa na kivuko chetu kimesimama kutoa huduma na leo ndio kuna sherehe ya kutia saini ili ukarabati uanze mara moja.

Kuna cameran man wa kutosha mpaka waendesha drones wapo standby kwa ajili kuchukua matukio ya utiaji saini huo.

Hivi ni kweli swala hili linahitaji hafla au lingeweza kumalizwa na watu wawili ofisini?

Nani mratibu wa shughuli hii anayekosa ata huruma na Watanzania?

Wananchi wote wanapita wanapigwa na butwaa.

Mungu atusaidie sana kama taifa.

=====

Serikali yasaini mkataba ujenzi wa MV Magogoni

SERIKALI imesaini mkataba wa ukarabati wa kivuko cha MV Magogoni wenye thamani ya Sh bilioni 7.5 ambazo ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Akizungumza katika viwanja vya kivukoni jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema, ukarabati wa kivuko hicho ni juhudi na mikakati ya serikali katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji.

Profesa Mbarawa amesema kuwa miradi mitano ya ujenzi wa vivuko vingine vipya na miradi 16 ya ukarabati wa vivuko unaendela baada ya kusainiwa kwa mikataba yake ambayo hadi kukamilika kwa miradi hiyo itagharimu Sh bilioni 60.7.

Ametoa wito kwa watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kusimamia vema ukarabati wa kivuko hicho utakaofanyika Mombasa nchini Kenya chini ya kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd kwa muda wa miezi mitano.

Kivuko cha MV Magogoni kilijengwa mwaka 2008, kina uwezo wa kubeba abiria elfu mbili na tani 500 za mizigo yakiwemo magari madogo 60 kwa wakati mmoja.
 
Fedha zipo tutazitumiaje?

Andaa hafla na iende mubashara ili wananchi nao waone kwamba serikali inafanya kazi!

Okay:
Perdeim, tents, lunch, mc, drinks, usafiri, mafuta, matangazo: huko kote kata 10/%.

Wizarani tutaandika Ni matumizi mengine, HUKU WATOTO WETU WANAKAA CHINI NA WANAOARIFU MUBASHARA WANAKAMATWA
 
Huo ujinga kwa jpm haukuwepo, kama taifa,tunayo safari ndefu,na tatizo kubwa wapiga firimbi wameungana na wezi,sijui nani atapaaza sauti kulisemea taifa,

Vyama vya upinzani ni zaidi ya bunge,ndio wanatakiwa kuiamsha serikali na kuwapigia kelele watawala,cha ajabu paka na panya wameweka makubaliano,

Twaaaafaaaaaa,
 
Watengeneze kivuko Mv Magogoni Kisha kikirudi kazini wasibanie mafuta kwa kuwasha injini moja tu na kuchelewesha abiria kama mda mwingine wanavyofanya Mv Kigamboni yani wanaboa kinoma! Laana ziwashukie wale wote watesao masikini bongo. Amin
 
Leo wakati navuka kutokea Kigamboni nimekutana na swala la kustaajabisha sana.

Viti na mapambo yamewekwa eneo la mbele kidogo ukishuka kwenye kivuko kutoka Kigamboni. Kulikuwa na kivuko chetu kimesimama kutoa huduma na leo ndio kuna sherehe ya kutia saini ili ukarabati uanze mara moja...
Hataki kuambiwa hakuna walichofanya
 
Inasikitisha sana kuona jambo dogo la utiaji saini kwa ajili ya kwenda kwenye matengenezo ya Mv Magogoni ukifanyiwa sherehe kitu ambacho hakikufanyika kwa Mv Kazi japokuwa ilitengeneza hapa hapa na mzawa Songoro marine.

Leo pale kivukoni wamezuia magari na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi ili uweza kufanya hiyo hafla ya utiaji saini,ukiliangalia hili jambo kiundani utakuja kugundua inaonyesha wazi wazi jinsi viongozi wetu wa zama hizi wasivyokuwa serious na kazi, kivuko cha Mv Magogoni ni cha muda mrefu kidogo na kilipaswa kupelekwa mapema sana kwenye matengenezo bila kuchelewa kwa sababu ni kikubwa na ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Kigamboni sasa kimeegeshwa ni wiki ya 3 sasa na leo ndio inafanyika hiyo hafla kwanza kabla ya kupelekwa Mombasa kwa matengenezo.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni malalamiko na minongono mingi ya wananchi mbalimbali waliokuwa wanavuka hakika wameshangazwa sana na hilo jambo wamebaki wakijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu.

Tunaomba serikali ijaribu kuwa inaangalia umuhimu wa jambo kabla halijafanyika kwa maslahi mapana ya Taifa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Hii tabia ya kutafuta attention kwenye kila jambo ni dalili ya uoga na kutojiamini kwa serikali yetu, na watendaji wake.

Nchi imegeuka ya "hafla" kila siku, hapo naamini budget iliandaliwa wajanja wameshajipigia chao, maisha yanaendelea, kesho tena wanapanga waandae "hafla" ya nini kingine wajipigie pesa za wajinga.
 
Hii tabia ya kutafuta attention kwenye kila jambo ni dalili ya uoga na kutojiamini kwa serikali yetu, na watendaji wake.

Nchi imegeuka ya "hafla" kila siku, hapo naamini budget iliandaliwa wajanja wameshajipigia chao, maisha yanaendelea, kesho tena wanapanga waandae "hafla" ya nini kingine wajipigie pesa za wajinga.
kweli kabisa.....inasikitisha sana
 
Inasikitisha sana kuona jambo dogo la utiaji saini kwa ajili ya kwenda kwenye matengenezo ya Mv Magogoni ukifanyiwa sherehe kitu ambacho hakikufanyika kwa Mv kazi japokuwa ilitengeneza hapa hapa na mzawa Songoro marine...
Kuna theory moja sijui hii ni ya ukweli iko hivi; ikitoka awamu ya kiongozi imara, mchapa kazi na asiyetaka mchezo kwenye kazi basi awamu inayofuata itakuwa goigoi na yenye kuchezewa na wapiga deal hadi wananchi washangae!!

Sijui upo ukweli?
 
Azam terminal itajengwa palipo na kituo cha Posta ya zamani BRT tutawahama temesa tuvuke kwa Azam kwa 500
 
Back
Top Bottom