TEMESA wakubaliana na Azam Marine kuvusha abiria Kigamboni (Ferry)

Inashangaza kusikia mambo kama haya. Tena Habari yake yaweza kukusababishia kicheko ukapaliwa na mashudu anayosema msemaji wao " eti tumemkodisha kwa muda" . Hivi kweli hamna mtu wa planning, manyumbu hawajui preventive maintenance!
 
Kipindi cha JK alitusaidia sana huyu bwana kulipa mishahara wafanyakazi wa Serikali baada ya sisi Serikali kuchemsha. Kwa sasa anatusaidia tena kutubebea wananchi baada ya sisi serikali kazi kutushinda.

Mishahara ikitushinda tena kulipa tutamrudishia hili jukumu huyu bwana Bakhresa.
 
CCM huu mradi mdogo wa hapo Ferry unawashinda, siamini kama mna akili za kutengeneza mazingira ya raia milioni 65 waweze kujikomboa kwenye umasikini, mpeni azam moja kwa moja ausimamie muone jinsi watu wenye akili timamu watakavyo toa huduma. Nyinyi ni wehu hamko timamu
Chukua serengeti lite apo Kisuma bar umwagilie moyo nakuja kulipa
 
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) unapenda kuujulisha umma kuwa umefikia makubaliano na kampuni ya Azam marine kutoa huduma ya kuvusha abiria baina ya Magogoni na Kigamboni ili kuendelea kuwapa wananchi huduma ya uhakika wakati huu Wakala ukiendelea kufanyia matengenezo vivuko vyake.

Aidha Wananchi wanashauriwa kuacha kutumia mitumbwi ili kulinda usalama wao.

View attachment 2259522


PICHA: Boti za Azam Marine zikiwa zimeanza kazi ya kuvusha abiria
View attachment 2259723View attachment 2259724


Deal Done wanasemaga waarabu
 
Kipindi cha JK alitusaidia sana huyu bwana kulipa mishahara wafanyakazi wa serikali baada ya sisi serikali kuchemsha. Kwa sasa anatusaidia tena kutubebea wananchi baada ya sisi serikali kazi kutushinda.

Mishahara ikitushinda tena kulipa tutamrudishia hili jukumu huyu bwana bakhresa.
Natamani aje mtu waserikali akanushe hii comment.
 
Back
Top Bottom