Vivuko vya Azam pale feri Dar es salaam kuna dalili za Ufisadi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,106
Nimepita maeneo ya feri Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kwenda upande wa Kigamboni. Nilichokiona pale kwa kweli kimenifikirisha na kunitafakarisha sana na kunifanya niwaze sana juu ya mustakbali wa nchi hii.

1. Kuna dalili kampuni ya Azam imepewa dili kinyemela kufanya kazi ya kuvusha watu feri

Mwanzoni, walitupiga changa la macho eti kuna tatizo la hali ya hewa, na hivyo kivuko cha Azam kimeletwa ili kusaidiasaidia. Cha ajabu mpaka leo hii hivyo vivuko vinaendelea kufanya kazi, wakati vile vivuko vya MV Kigamboni na MV Magogoni ni vizima.

2. Vivuko vya MV Magogoni na MV vipo na vinaendeshwa polepole Makusudi ili kuvipa nafasi vivuko vya Azam
Inaelekea kuna mpango mkakati wa kuwafanya watu wavizoee vivuko vya Azam pale feri. Nilichokishuhudia, Pale kuna vivuko vinne, Viwili ni vya Azam na viwili ni vya serikali(MV Magogoni na MV Kigamboni), Cha ajabu, Vivuko vya serikali vinaendeshwa polepole kuliko ilivyokuwa zamani.

Yaani nimeshuhudia MV Kigamboni ikikaa upande wa feri kwa takriban dakika 40, bila kuondoka huku Kivuko cha Azam kikiwa kimepiga trip mbili kwenda na kurudi kigamboni. Hii kama siyo hujuma kwa Vivuko vya serikali ni nini?.

3. Maisha ya wananchi yanawekwa hatarini kwa jinsi wanavyotolewa ndani ya sehemu ya kusubiria vivuko na kupangwa nje karibu na ukingo wa maji kusubiri vivuko vya Azam

Kikawaida watu huwekwa ndani ya hall la kusubiria kivuko, kikishafika geti linafunguliwa na kivuko kikishashusha watu na Magari ndo geti linafunguliwa na watu kuruhusiwa kuingia. Cha ajabu nilichokishuhudia leo, kwa kuwa vivuko vya Azam ni vidogo basi askari anawatoa watu nje ya hall ya kusubiria watu mapema kabisa kabla watu wanaoshuka hawajaisha. Maana yake ni iwamba Ujio wa kivuko cha Azam umeondoa hata kusudio la yale mahall ya kusubirisha abiria. Na hata usalama wa Abiria.

4. Ninachokiona
Huenda Kampuni ya Azam, inapewa dili na wakubwa wachache serikalini ili itoe huduma ya kuvusha watu licha ya kuwa vivuko vya serikali vipo pale.
Kampuni ya Azam kupewa kandarasi ya kutoa huduma siyo tatizo iwapo

1. Tenda inatangazwa kwa uwazi
2. Usalama wa wanajchi unazingatiwa ipasavyo
3. Serikali inapata faida

Kilicho dhahiri inaelekea Azam ya Mzee Bakhressa inapigiwa pande kinyemela ktk hii ishu, ambayo dhahiri shahiri kuna harufu za watu kuwa na 10% zao pale.

Hapa Chini ni picha ambayo wananchi wametolewa kwenye hall ya kusubiria kivuko, wamepangwa nje foleni wakisubirie kwa nje. Hii ni hatari sana, na ni very local
IMG_20230103_161435_513.jpg

Hapa Chini, Kivuko cha MV kigamboni kimekalishwa zaidi ya dakika 40, huku kikiwa na watu ndani na magari huku Kivuko cha Azam kikipiga trip tu kwenda na kurudi, Sijui hawa Azam wanalipwa kwa idadi ya Trips wanazopiga?

IMG_20230103_160237_290.jpg
 
Nina wasiwasi na ulichoandika hapo.

Nachokumbuka vivuko vya Azam vilipewa kazi baada ya vivuko vingine kuwa matengenezoni, hivyo pakawa na uhaba wa vyombo vya usafiri, ukawepo usumbufu kwa abiria, ndipo Azam wakaombwa kutoa hiyo huduma.

Kama kwa sasa pametokea hali isiyo ya kawaida, sioni kama hilo litakuwa ni tatizo la Azam, huo ni uzembe tu wa wasimamizi wa mamlaka ya usafiri huko bandarini.

Walichotakiwa kufanya kama vivuko vingine vilishapona, ni kusitisha mkataba na Azam, lakini kuwaacha Azam waendelee ni sawa na kukaribisha vurugu, japo pia, uwepo wa Azam unasaidia kuondoa adha ya usafiri inayokuwepo eneo hilo mara kwa mara.
 
Vivuko vya serikali kwa sasa ni vizima, na vinafanya kazi, isipokuwa inaonekana vinahujumiwa ili Watu waizoee na waipende Azam. I see mpango mbeleni ni kumpa Azam tenda ya hapo
 
Vivuko vyetu vinakalishwa sana tena makusudi huku Abiria wakipakiwa kwenye vile vya Azam. Sijui Azam wanalipwa kwa idadi ya trips wanazofanya?
Wanalipwa kila trip Suma anaandika kikijaa full anaandika 250+ anaandika departing time na arriving time
Btw na mimi nilijua sheikh azam katoa msaada mpaka nilipokuja kujua kumbe wanahesabu na wao
 
Mbona mie naona wako sawa tu. Vinapishana vizuri tu, halafu vya Azam havipakii magari...
Vya serikali vimefanywa kuwa slow makusudi. Kwa kuwa ni vikubwa, Vinakuwa vinagawana watu na vile vya Azam.

Kwa kuwa vya Azam ni vidogo, kwa hiyo vinapiga trip hata tatu kwenda na kurudi huku cha serikali kikisubirishwa kijae.

Laiti vivuko vya Azam visingekuwepo wale abiria wote wanaingia ktk vivuko vya serikali, vinajaa haraka na kuondoka haraka.

Ila sasa hivi vimefanywa viwe vinachelewa, na kwa sababu hiyo raia kukimbilia Azam. Hii ni kama hujuma fulani hivi kwa vivuko vya serikali!
 
Nina wasiwasi na ulichoandika hapo.

Nachokumbuka vivuko vya Azam vilipewa kazi baada ya vivuko vingine kuwa matengenezoni, hivyo pakawa na uhaba wa vyombo vya usafiri, ukawepo usumbufu kwa abiria, ndipo Azam wakaombwa kutoa hiyo huduma.

Kama kwa sasa pametokea hali isiyo ya kawaida, sioni kama hilo litakuwa ni tatizo la Azam, huo ni uzembe tu wa wasimamizi wa mamlaka ya usafiri huko bandarini.

Walichotakiwa kufanya kama vivuko vingine vilishapona, ni kusitisha mkataba na Azam, lakini kuwaacha Azam waendelee ni sawa na kukaribisha vurugu, japo pia, uwepo wa Azam unasaidia kuondoa adha ya usafiri inayokuwepo eneo hilo mara kwa mara.
Mkuu unachopinga ni kipi sasa, vivuko vimepona na Azam ipo tu
 
Wanalipwa kila trip Suma anaandika kikijaa full anaandika 250+ anaandika departing time na arriving time
Btw na mimi nilijua sheikh azam katoa msaada mpaka nlipokuja kujua kumbe wanahesabu na wao
Umeona eh!

Azam kapewa dili kimyakimya bila tenda kutangazwa. Ni Upigaji mwingine katika serikali ya awamu ya Sita.

Hiki chanzo cha Mapato kilikuwa ni chanzo cha uhakika cha mapato ya serikali, Leo wahuni, Mafisadi na Wapigaji inaelekea wameweka 10% yao kupitia hii kitu.

Wizi mtupu!
 
Nimepita maeneo ya feri Dar es Salaam kwa ajili ya kuvuka kwenda upande wa Kigamboni. Nilichokiona pale kwa kweli kimenifikirisha na kunitafakarisha sana na kunifanya

1. Kuna dalili kampuni ya Azam imepewa dili kinyemela kufanya kazi ya kuvusha watu feri

Mwanzoni, walitupiga changa la macho eti kuna tatizo la hali ya hewa, na hivyo kivuko cha Azam kimeletwa ili kusaidiasaidia. Cha ajabu mpaka leo hii hivyo vivuko vinaendelea kufanya kazi, wakati vile vivuko vya MV Kigamboni na MV Magogoni ni vizima.

2. Vivuko vya MV Magogoni na MV vipo na vinaendeshwa polepole Makusudi ili kuvipa nafasi vivuko vya Azam
Inaelekea kuna mpango mkakati wa kuwafanya watu wavizoee vivuko vya Azam pale feri. Nilichokishuhudia, Pale kuna vivuko vinne, Viwili ni vya Azam na viwili ni vya serikali(MV Magogoni na MV Kigamboni), Cha ajabu, Vivuko vya serikali vinaendeshwa polepole kuliko ilivyokuwa zamani.

Yaani nimeshuhudia MV Kigamboni ikikaa upande wa feri kwa takriban dakika 40, bila kuondoka huku Kivuko cha Azam kikiwa kimepiga trip mbili kwenda na kurudi kigamboni. Hii kama siyo hujuma kwa Vivuko vya serikali ni nini?.

3. Maisha ya wananchi yanawekwa hatarini kwa jinsi wanavyotolewa ndani ya sehemu ya kusubiria vivuko na kupangwa nje karibu na ukingo wa maji kusubiri vivuko vya Azam

Kikawaida watu huwekwa ndani ya hall la kusubiria kivuko, kikishafika geti linafunguliwa na kivuko kikishashusha watu na Magari ndo geti linafunguliwa na watu kuruhusiwa kuingia. Cha ajabu nilichokishuhudia leo, kwa kuwa vivuko vya Azam ni vidogo basi askari anawatoa watu nje ya hall ya kusubiria watu mapema kabisa kabla watu wanaoshuka hawajaisha. Maana yake ni iwamba Ujio wa kivuko cha Azam umeondoa hata kusudio la yale mahall ya kusubirisha abiria. Na hata usalama wa Abiria.

4. Ninachokiona
Huenda Kampuni ya Azam, inapeea dili wakubwa wachache serikalini ili itoe huduma ya kuvusha watu licha ya kuwa vivuko vya serikali vipo pale.
Kampuni ya Azam kupewa kandarasi ya kutoa huduma siyo tatizo iwapo

1. Tenda inatangazwa kwa uwazi
2. Usalama wa wanajchi unazingatiwa ipasavyo
3. Serikali inapata faida

Kilicho dhahiri inaelekea Azam ya Mzee Bakhressa inapigiwa pande kinyemela ktk hii ishu, ambayo dhahiri shahiri kuna harufu za watu kuwa na 10% zao pale.

Hapa Chini ni picha ambayo wananchi wametolewa kwenye hall ya kusubiria kivuko, wamepangwa nje foleni wakisubirie kwa nje. Hii ni hatari sana, na ni very localView attachment 2468085

Hapa Chini, Kivuko cha MV kigamboni kimekalishwa zaidi ya dakika 40, huku kikiwa na watu ndani na magari huku Kivuko cha Azam kikipiga trip tu kwenda na kurudi, Sijui hawa Azam wanalipwa kwa idadi ya Trips wanazopiga?

View attachment 2468089
Karibu pia Mwanza ujionee, kivuko cha Busisi Kigongo, ni heri hayo ya Musa, huku kuna firauni.
 
Back
Top Bottom