Maharage wa TANESCO atimuliwa kwenye kikao cha Waziri Mkuu Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Biteko. Apewa siku tatu

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake. Siku tatu zinamtosha kweli au ndo wanamkomoa baba wa watu?
Screenshot_20230920-153410.png

Na Biteko akija kujua dili za Luku atamla kichwa mazima.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table ametabasamu na furaha zote amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Tarehe 25 Septemba 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO akichukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka

Kutokana na Mgao Mkubwa wa Umeme unaoendelea Nchini, Maharage anadai hakuna Mgao bali ni Upungufu wa umeme.

Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Maharage Chande aliwaomba Wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho kuna Upungufu wa Umeme unaosababisha baadhi ya Maeneo kuwa na Umeme na mengine kukosa Huduma hiyo

Maharage alisema "Katika Mtandao wa Umeme hitilafu huwa zinatokea mara kwa mara na pale zinapotokea Wateja wetu huwa tunawataarifu. Tunapopata upungufu sio Nchi nzima inakuwa haina Umeme ila ni kwa baadhi ya maeneo na huwa tunatoa taarifa"

Sasa baada ya kwambiwa aende kushughulikia umeme, nilijua ataenda site. Cha ajabu yupo Ofisini kwake Ubungo kakaa huku tai ameilegeza, inaonekana ana mawazo sana.

Tumuombee presha yake isipande.

Baadhi ya Watanzania wamesema mgao wa umeme umekuwa ukisababisha hasara katika biashara zao mara kwa mara. Na wamelitaka shirika la umeme (TANESCO), kutoa taarifa rasmi ya jinsi mgao huo unavyoendeshwa. Je, kwa sasa Tanesco inazalisha kiwango gani cha umeme? Ni upungufu wa aslimia ngapi?
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
🤣🤣Jamaa anakaa high table afu umeme aka electricity hauko mtaani
Ila anajiamini
Ningekuwa Mimi ningeanzia site hata kinyerezi kuzuga tu🤣🤣
 
Boss wa TANESCO atimuliwa kikaoni. Sioni nyota njema kwake.

Kaambiwa nenda kashughulikie Umeme. Alikuwa high Table amekaa kwenye Maonesho yanayoendelea ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
Nani anaemteua? Halafu kwani Maharage Chande ndio kaleta ukame? Maharage ndio mtoa pesa za kuanzisha vyanzo vipya? Upuuzi.

Ila Sasa Kwa Afrika Jamaa wanaodhalilisha hivi na kuongea ndio huonekana Viongozi Sasa 😁😁
 
Back
Top Bottom