mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Ilibidi niende Dar es Salaam kwa kutumia Ndege kutokea Mtwara lakini nimepita hii Barabara (Mtwara- DSM) makusudi nione hali yake, hii Barabara imeharibika, 90 KM zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii Barabara
Barabara hii ya Mtwara - Lindi-Dar es Salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri.
Mmeniudhi Wizara ya Ujenzi, sijafurahia. Nimetoka na machungu kwa kumzika Mzee Mkapa, lakini hapa Somanga napo nimepata machungu kwa kukuta barabara hii haijatengenezwa”
Barabara hii ya Mtwara-Lindi-Dar es salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange, utunzaji sio mzuri.Hii barabara imeharibika, huwezi ukaamini kama tuna Waziri wa Ujenzi. Kilometa 90 zote nilikuwa nahesabu zimeharibika - Rais Magufuli
Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Somanga baada ya mwanafunzi wa shule hiyo Rehema Mikidadi Ngenje kumwambia Changamoto za Shule hiyo. Pia Rais amemzawadia mwanafunzi huyo Tsh 100,000.
Naichangia Shule ya Msingi Somanga TZS Milioni 5. OCD wa hapa hakikisha hizi fedha zinaenda benki na zinapelekwa katika hiyo shule, mkazitumie kweli nitakuja nifuatilie lakini TZS 100,000 ibaki kwa huyu mtoto - Rais Magufuli
Rais Magufuli pia amezawadiwa Jogoo na mzee mmoja ambaye pia Rais Magufuli amemzawadia Tsh.100,000 na kutania kwamba analichukua jogoo lakini asije akafika nalo nyumbani likageuka kuwa radi.
"Nisikilize Mzee wangu, baba yangu ameshatangulia mbele ya haki,umetoa jogoo,siku ukienda chato nitakukabidhi mama yangu na wewe uwe baba,haya kamlete huyo jogoo" - Rais Magufuli