TANROADS Inaendelea na Kazi ya Kurejesha Mawasiliano ya Barabara ya Somanga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

TANROADS INAENDELEA NA KAZI YA KUREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA SOMANGA.

Timu ya wataalamu kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) wanaendelelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja hilo linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa.

Akitoa taarifa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara eneo la Somangafungu, Lindi.

“Timu za TANROADS kutoka Mikoa ya Lindi na Pwani zimeungana kuongeza nguvu ili kabla ya mchana safari ziweze kuendelea. Tunawapa pole wasafiri wote kwa changamoto iliyojitokeza”, ameeleza Waziri Bashungwa.
 

Attachments

  • WhatsApp Video 2024-03-25 at 10.07.11.mp4
    19.3 MB
Back
Top Bottom