Somanga: Rais Magufuli asikitishwa na uzembe wa Wizara ya Ujenzi kutokarabati barabara Somanga. Azawadiwa jogoo

Rais Dkt John Magufuli amepokea zawadi ya jogoo kutoka kwa mkazi mmoja wa Somanga mkoani Lindi ambayo amempatia zawadi hiyo ili akampe mama yake mzazi.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo Rais Magufuli alimpatia shs laki moja ”Umenipa zawadi ya kuku na mimi nakupa zawadi ya Tsh. Laki moja”

Rais amepatiwa zawadi hiyo akiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam akitokea Lupaso, Masasi mkoani Mtwara alikokwenda kwenye msiba wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa.

Jpm for 2020-2025View attachment 1521685
Huyu Rais wa ajabu kweli, yani kabadilishana huyo jogoo na mama yake mzazi! Yani jamaa kaambiwa kuwa kwa sasa ni ruksa kumrithi Mama Magufuli! Sema ndo ashazeeka itakuwa unachukua tu mzigo wa kuulea!
 
Lofa anamzawadia mwenye uwezo? Inaingia akilini.
IMG_20200730_200222.jpg
 
Rais Dkt John Magufuli amepokea zawadi ya jogoo kutoka kwa mkazi mmoja wa Somanga mkoani Lindi ambayo amempatia zawadi hiyo ili akampe mama yake mzazi.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo Rais Magufuli alimpatia shs laki moja ”Umenipa zawadi ya kuku na mimi nakupa zawadi ya Tsh. Laki moja”

Rais amepatiwa zawadi hiyo akiwa njiani kuelekea jijini Dar es Salaam akitokea Lupaso, Masasi mkoani Mtwara alikokwenda kwenye msiba wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamin Mkapa.

Jpm for 2020-2025View attachment 1521685
Mbona Membe sikumuona hata ule moshi wa siku ile? Magufuli alipokua ziarani?
 
Huyu Rais wa ajabu kweli, yani kabadilishana huyo jogoo na mama yake mzazi! Yani jamaa kaambiwa kuwa kwa sasa ni ruksa kumrithi Mama Magufuli! Sema ndo ashazeeka itakuwa unachukua tu mzigo wa kuulea!
wale ni watani wake kimakabila,usiwe fala muda wote
 
Barabara hii ya Mtwara - Lindi-Dar es Salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri.

Serikali iweke mazingira mazuri kuvutia wawekezaji ktk usafiri wa baharini wapatikane ili meli kubwa za watanzania zibebe mizigo mizito
Barabara hii ya Mtwara-Lindi-Dar es salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange, utunzaji sio mzuri.Hii barabara imeharibika, huwezi ukaamini kama tuna Waziri wa Ujenzi. Kilometa 90 zote nilikuwa nahesabu zimeharibika - Rais Magufuli

Hakuna namna lazima kuwepo mchanganyiko wa usafiri wa reli na wa bahari kwenda Dsm, Tanga, Bagamoyo, Pangani, Zanzibar, Kilwa, Rushungi, Lindi na Mtwara n.k ili kunusuru barabara zetu na kufanya gharama za kusafirisha gypsum, makaa ya mawe, chuma na mizigo mingi mizito kwa bei nafuu.
 
Ukiangalia mazingira ambayo Rais Magufuli alikuwa akihutubia huko Kilwa utaona nyumba za makuti tu, ambayo ni dalili ya namna umasikini ulivyo ndani ya jamii yatu!

Malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa vyoo, na madarasa ya kusomea watoto ni magofu! Malipo ya korosho nayo mpaka leo hakuna!
Screenshot_2020-07-31-15-55-21.png

Mtoa zawadi ya jogoo kwa Rais naye ukimwangalia, utaona kwa namna gani wananchi walivyochoka na maisha magumu!

Nashawishika kusema, zawadi ya jogoo aliyopewa Rais, si ya wana Kilwa, ni ulaghai wa kutapeli akili za watu!

Vinginevyo wana Kilwa na Kanda ya Kusini mtuambie, Magufuli na CCM yake amewafanyia maendeleo gani hadi mumtunuku jogoo?
 
Huyu jogoo wa kizungu ametoka Mbagala asubuhi hata maji ya uso hakunawa.

Ni baada ya nyomi iliyompokea Lissu Airport na wengine walipanga kuonyesha jamii wanavyokubalika.

Yule mzee anafahamu maendeleo ya flyover na ununuzi wa na ununuzi wa ndege.
Usizidishe Hali ya kuwa opposite Kila Jambo, Ni bora ujadili hoja ya mleta mada ambayo kiukweli inahitaji mjadala mpana, ukiangalia Ni kweli watu wako katika maisha magumu Sana!
 
We huoni mtu katoa Jogoo nae kapewa zawadi mbili???

Laki moja
Na ile ahadi nyingine??😄😄

Hicho ndo alivhowafanyia hadi kupewa zawadi ya Jogoo( You scratch my back I scratch yours)
 
Huu ni uthibitisho kuwa watu wote sasa wadogo kwa wakubwa wanajua kwamba mzee anapenda kiki.
Ukiangalia mazingira ambayo Rais Magufuli alikuwa akihutubia huko Kilwa utaona nyumba za makuti tu, ambayo ni dalili ya namna umasikini ulivyo ndani ya jamii yatu!

Malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa vyoo, na madarasa ya kusomea watoto ni magofu! Malipo ya korosho nayo mpaka leo hakuna!View attachment 1522693

Mtoa zawadi ya jogoo kwa Rais naye ukimwamgalia, utaona kwa namna gani wananchi walivyochoka na maisha magumu!

Nashawishika kusema, Zawadi ya jogoo aliyopewa rais, si ya wana Kilwa, ni ulaghai wa kutapeli akili za watu!

Vinginevyo wana Kilwa na kanda ya kusini mtuambie, Magufuli na CCM yake amewafanyia maendeleo gani hadi mumtuku jogoo!?

Back
Top Bottom