Somanga: Rais Magufuli asikitishwa na uzembe wa Wizara ya Ujenzi kutokarabati barabara Somanga. Azawadiwa jogoo

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,077
4,115


Ilibidi niende Dar es Salaam kwa kutumia Ndege kutokea Mtwara lakini nimepita hii Barabara (Mtwara- DSM) makusudi nione hali yake, hii Barabara imeharibika, 90 KM zote zimeharibika. magari yenye uzito mkubwa yameharibu hii Barabara

Barabara hii ya Mtwara - Lindi-Dar es Salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange vizuri utunzaji sio mzuri.

Mmeniudhi Wizara ya Ujenzi, sijafurahia. Nimetoka na machungu kwa kumzika Mzee Mkapa, lakini hapa Somanga napo nimepata machungu kwa kukuta barabara hii haijatengenezwa”

Barabara hii ya Mtwara-Lindi-Dar es salaam imeharibika sana, Waziri wa Ujenzi atafute utatuzi wa hii Barabara, ajipange, utunzaji sio mzuri.Hii barabara imeharibika, huwezi ukaamini kama tuna Waziri wa Ujenzi. Kilometa 90 zote nilikuwa nahesabu zimeharibika -
Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 4.9 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Msingi Somanga baada ya mwanafunzi wa shule hiyo Rehema Mikidadi Ngenje kumwambia Changamoto za Shule hiyo. Pia Rais amemzawadia mwanafunzi huyo Tsh 100,000.Naichangia Shule ya Msingi Somanga TZS Milioni 5. OCD wa hapa hakikisha hizi fedha zinaenda benki na zinapelekwa katika hiyo shule, mkazitumie kweli nitakuja nifuatilie lakini TZS 100,000 ibaki kwa huyu mtoto - Rais MagufuliRais Magufuli pia amezawadiwa Jogoo na mzee mmoja ambaye pia Rais Magufuli amemzawadia Tsh.100,000 na kutania kwamba analichukua jogoo lakini asije akafika nalo nyumbani likageuka kuwa radi.

"Nisikilize Mzee wangu, baba yangu ameshatangulia mbele ya haki,umetoa jogoo,siku ukienda chato nitakukabidhi mama yangu na wewe uwe baba,haya kamlete huyo jogoo" - Rais Magufuli
 
Dkt MagufuliJP noma katoka msibani kasimama somanga kapewa kuku na mzee mmoja.

Pia akatoa million 5 za ujenzi wa shule ya msingi somanga, Kuna mtoto kaongea nae kampa laki moja.

Pia mzee alitoa Zawadi ya kuku nae kapewa laki, unalala masikini unaamka tajiri
IMG-20200730-WA0254.jpg
 
Mlioko Somanga nitafutieni namba ya huyo OCS wenu hapo kituoni mniwekee kwenye PM!
 
Back
Top Bottom