TANROADS inaendelea na kazi ya kurejesha mawasiliano Barabara ya Somanga

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Timu ya wataalamu kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) wanaendelelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja hilo linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa.

Akitoa taarifa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa jitihada kubwa zinaendelea za kurudisha mawasiliano ya barabara eneo la Somangafungu, Lindi.

“Timu za TANROADS kutoka Mikoa ya Lindi na Pwani zimeungana kuongeza nguvu ili kabla ya mchana safari ziweze kuendelea. Tunawapa pole wasafiri wote kwa changamoto iliyojitokeza”, ameeleza Waziri Bashungwa.

Pia soma > Daraja la Somanga limekatika
 
Haohao waliosimamia miundombinu mibovu ndio haohao wanaopewa kazi ya kurekebisha. Bora lipewe jeshi la wananchi
 
Back
Top Bottom