Ndio zinaweza lakini ni lazima upate/ununue/uazime/ukodi printer yenyewe. Kama unanunua printer zinaanza laki mbili
Tanzania nchi ya kijima sana. TRA ndiyo wanatakiwa kuwa na hiyo program na iwe bure kwa kila mfanya biashara. Badala wavutie watu kulipa kodi wanazidi kuwakamua. Kwa nini wasitengeneze program na kutoa bure ili watu wavutike kulipa kodi badala ya kuachia vishoka wakamue watu laki tatu?
 
Acha wivu, Subiri uletewe na TRA Bure au kaombe kuwa kishoka na wewe basi upige pesa...

Umekosea bei lakini mimi nachaji laki ya kukusetia halafu elfu hamsini kwa mwaka.
 
Sambamba na EFD za kawaida sasa wafanyabiashara wanaweza pia kutumia kompyuta, Point ya Uuzaji (POS), SIMU na mashine yoyote inayofaa inayoweza kuunganisha kwenye mfumo wa EFDMS kwa kusudi la kutuma taarifa za kodi bila kupata EFD mpya.
Bwana Elya hongera sana.

Nakukubali tokea tukiwa shule hukuwa mtu wa kukubali kufeli pambania hapo hapo.
 
Amina sana kaka... Nashukuru sana.. Mapambo lazima yaendelee shule haijawahi kuisha.

Sasa wale Wapuuzi wameongeza gharama za bando, pumbavu kweli! Sijui nani katuroga

Ni kweli ila ukiacha tozo, mabando ya simu nchi zote huwa yanakua juu ni vizuri kutafuta internet za waya au fiber kama zinapatikana uweki wifi nyumbani au ofisini

Kwa sababu hio na nyingine naona TRA wameruhusu iweze kutoa risiti bila kutegemea mtandao... Yani sio lazima uwe na internet ili utoe risiti.
 
Tanzania nchi ya kijima sana. TRA ndiyo wanatakiwa kuwa na hiyo program na iwe bure kwa kila mfanya biashara. Badala wavutie watu kulipa kodi wanazidi kuwakamua. Kwa nini wasitengeneze program na kutoa bure ili watu wavutike kulipa kodi badala ya kuachia vishoka wakamue watu laki tatu?
TRA wamejazana makada wa ccm ubunifu ni zero! Wao wanacho jua ni kukamua kodi tu na kuunza vikosi vya kuvamia maduka ya watu
 
Sambamba na EFD za kawaida sasa wafanyabiashara wanaweza pia kutumia kompyuta, Point ya Uuzaji (POS), SIMU na mashine yoyote inayofaa inayoweza kuunganisha kwenye mfumo wa EFDMS kwa kusudi la kutuma taarifa za kodi bila kupata EFD mpya.
Safii sanaaaaaaa, ndio vijana mnahitajika Taifa hili. Weka No yako
 
Tanzania nchi ya kijima sana. TRA ndiyo wanatakiwa kuwa na hiyo program na iwe bure kwa kila mfanya biashara. Badala wavutie watu kulipa kodi wanazidi kuwakamua. Kwa nini wasitengeneze program na kutoa bure ili watu wavutike kulipa kodi badala ya kuachia vishoka wakamue watu laki tatu?
Dah! Sasa kosa la TRA ni nini hapo?

TRA wamefungua mlango kwa wote wanaopenda kutoa huduma hii watoe.

Ningefurahi kuona unafanya au una fund project ya kutoa VFD bure. Kwa TRA walitakiwa kuishia hapo kwenye kufungua API. Wakienda mbali ya hapo maana yake inabidi watengeneze programu ya kurekodi mauzo yako. Hapo watakuwa wanakusanya kodi bado kweli?

TRA wanajaribu kutoa alternative kwa EFD machines ambazo zina limitations zake. Hili tumelisema sana hata humu JF. Tuwapongeze wamefanya jambo la maana. Sio uungwana kumkosoa mtu hata pale anapofanya jambo jema!
 
Dah! Sasa kosa la TRA ni nini hapo?
TRA wamefungua mlango kwa wote wanaopenda kutoa huduma hii watoe.
Ningefurahi kuona unafanya au una fund project ya kutoa VFD bure. Kwa TRA walitakiwa kuishia hapo kwenye kufungua API. Wakienda mbali ya hapo maana yakeinabidi watengeneze programu ya kurekodi mauzo yako. Hapo watakuwa wanakusanya kodi bado kweli?

TRA wanajaribu kutoa alternative kwa EFD machines ambazo zina limitations zake. Hili tumelisema sana hata humu JF. Tuwapongeze wamefanya jambo la maana. Sio uungwana kumkosoa mtu hata pale anapofanya jambo jema!
Hapana. Hapana. Hapana. TRA walitakiwa watengeneze program ambayo itatumika bure na walipa kodi. Hili linge-motivate zaidi walipa kodi na pia lingeondoa loopholes za upigaji. Hili la kusema ''inabidi watengeneze program ya kurekodi mauzo yako'' ni tishia nyau unayoweza kuitumia kwa watu ambao hawana uelewe na field ya IT. Narudia tena: hili wanalofanya sasa hivi ni jambo litakaloleta loopholes nyingi kwa wapigaji. Muda utasema.
 
Vipi wewe unaelewaje utaratibu unaotumika sasahivi?
 
Sambamba na EFD za kawaida sasa wafanyabiashara wanaweza pia kutumia kompyuta, Point ya Uuzaji (POS), SIMU na mashine yoyote inayofaa inayoweza kuunganisha kwenye mfumo wa EFDMS kwa kusudi la kutuma taarifa za kodi bila kupata EFD mpya.

Setup nayopendekeza kama tayari una smartphone ni hii... Inaghalimu laki tatu tu na unaweza lipa baada ya kupewa huduma uzuri ni mteja hawezi to fautisha risiti zake na za mashine na risiti zake zinatambulika na TRA

SOMA ZAIDI: Simu Janja kama Mashine ya EFD - Nafuu kubwa kwa wajasiliamali na wafanya biashara.
Nina mashine nilinunua maximalipo,je inaweza kutumika
 
Hapana. Hapana. Hapana. TRA walitakiwa watengeneze program ambayo itatumika bure na walipa kodi. Hili linge-motivate zaidi walipa kodi na pia lingeondoa loopholes za upigaji. Hili la kusema ''inabidi watengeneze program ya kurekodi mauzo yako'' ni tishia nyau unayoweza kuitumia kwa watu ambao hawana uelewe na field ya IT. Narudia tena: hili wanalofanya sasa hivi ni jambo litakaloleta loopholes nyingi kwa wapigaji. Muda utasema.
Okay, sawa hiyo programu ilipaswa kufanya nini na nini? Ukiisha kujibu then tuonyeshe inahusiana vipi na kazi za kukusanya kodi?

Swali la pili ni kwa nini mamlaka za mapato, sio Tanzania tu, hazihusiki na biashara ya hizi EFD machines?
 
Nina mashine...
Hizo mashine za EFD unazosema zimefungwa kutopokea mfumo toka sehemu nyingine isipokua kwa mtu aliyekuuzia... hata hivyo naona wengi kwa maelekezo ya TRA walitoa update ya bure ili kuziwezesha nazo zitoe risiti za kisasa zenye qr-code kama tulizokua tunatoa sisi. Kama ulifanya hiyo update basi mashine yako haina shida na unaweza endelea kutumia.

Kama utapenda kutumia mfumo wetu kama nyongeza ya hiyo sababu TRA wanaruhusu uwe na mashine zaidi ya moja karibu tupigine kwenye namba zilizo chini ya picha.

Stefano Mtangoo Nashukuru kwa kunasiadia... Naona macho_mdiliko hajui vizuri kinachoendelea wala technologia inavyofanya kazi anadhani huu mfumo ni kama maembe tunachukua tra na kuwauzia watu mtaani, na kwamba vitu vya bure serekarini vinatokana na kodi zetu wenyewe na pengine vinatekelezwa kwa upigaji mkubwa na/au usimamizi mbovu.
 
Maelezo yake hayajani-convince hata kidogo. Pia wewe hujaweza. Mimi naona ni ule ule mtindo wa kibongo-bongo wa kuzunguka kwa kufanya jambo rahisi liwe na kona kona ili ulaji uwepo. Muda utaongea!
 
Maelezo yake hayajani-convince hata kidogo....

Sina cha kufanya kama upeo wako ni mdogo. Na mda wote unahisi unaibiwa tu.

Sikatai kuhusu TRA kuja kutoa bure wakiamua au huenda wanatoa bure ila bado hawajapita dukani kwako kukupa, lakini kuwa mwerevu kua hapa sio mahala pake, nilifungua huu uzi kwaa ajili ya watu wanotaka huduma leo hii, wewe ungetumia busara kufungua uzi wako na kuomba vyote unavyotaka ufanyiwe bure na TRA huko. Hizo konakona unazoongelea kwangu hazipo lasivyo wateja wangu ambao ni wana JF wangerudi kulalamika humu.

Labda useme muda utaongea nini? Maana umeshindwa kuelewa hii huduma rahisi unaishia kusema muda utaongea bila kufafanua... Mimi sio TRA kama una tatizo nao au kuna vitu vya bure unataka unajua kwa kuwapata.
 
Maelezo yake hayajani-convince hata kidogo. Pia wewe hujaweza. Mimi naona ni ule ule mtindo wa kibongo-bongo wa kuzunguka kwa kufanya jambo rahisi liwe na kona kona ili ulaji uwepo. Muda utaongea!
Sikuandika ili nikushawishi, unfortunately. So hakuna shida kama hujashawishika.

Nimeandika pure fact. TRA wanaweza kutengeneza mfumo unaoutaka na wakatoa bure. Haya ni maamuzi ya CG na timu yake.
Nilichosema ni kuwa TRA wako sahihi kuishia kwenye API kwa sababu lengo lao ni kukusanya kodi na sio kukusaidia wewe kutunza kumbukumbu zako.

Kwa wale wanaotumia manual work au Excel, EFD machines zipo kwa ajili ya kodi. Na wale ambao wanatumia mifumo ku automate kazi yao, TRA wametoa API ya ku connect na kuepuka EFD Machine.

Kiufupi TRA wamefanya kazi yao vizuri na hata wakiishia hapo hakuna atakayelalamika.

Huu ndio ukweli na uhalisia hata kama hutaki kuukubali!
 
Chanamoto jamaa hajui maana Kabisa ya API... Na hata ikitokea hivyo bado angesema ni wapigaji wamnunulie na simu. Inaaikitisha sana sababu kuna watu wanasoma wanadhani anaelewa anachoandika.
 
Back
Top Bottom