Nafikiri kinachowagharimu wanawake wengi wa bongo wa mjini ni kutaka kuishi juu zaidi ya uwezo wao binafsi wa kifedha. Unakuta mtu hana hata pesa ya nauli kutoka Mbezi kwenda Sinza kwa boyfriend au kujinunulia pedi ila anataka kusuka nywele za elfu 30, awe na pochi kali, mafuta ya elfu 20, wigi la elfu 50, anywe sijui Hennessy, Bruto na upuuzi mwingine, hapo sasa ndipo vizinga na kazi ya omba omba inapoanza.
Halafu kwa uombaomba wa hivi hata apewe milioni hawezi kufanya kitu cha maana kuanza kujiondoa katika hali hiyo.
Anakuwa ombaomba tegemezi.
Ni kitu kimoja kumsaidia mwanamke anayeweza kujipanga na kusimama mwenyewe.
Huyu hata bila kutaka kumdinya unaweza kumuonea huruma ukamsaidia ayapate maisha hata kama kiroho safi tu umemuona mwananchi mwenzako ana potential ya kufanya vizuri. Labda na wewe ulipitia au kujua matatizo, unajua everybody deserves support. Unaweza kumsaidia hata pale huna nia ya kumdinya. Wanaume huwa tunasaidia hivyo pia. Wengine hatuwezi kutaka kumdinya kila mwanamke tunayekutana naye. Kwanza si kila mwanamke atakuvutia hivyo, wengine wana ukurutu.
Wengine tumewasaidia hata hapa JF bila ya kuwaona tukijua hatutawaona maisha haya wako Africa na mtu kama mimi sijarudi Africa mwaka wa 14 huu na sina mpango wa kurudi mpaka afe mtu wa karibu kabisa. So tumesaidia hata bila ya nia ya ngono, kutoka mbali.
So unamuona mtu analialia njaa huko Africa, unaona pesa anayohitaji ni dola elfu chache tu ambazo kwako unamaliza kwenye anasa ya siku chache, ila yeye inaweza kumuanzishia biashara ya kubadilisha maisha yake, unampa bila hata kufikiria kuwa kuna siku mtaonana, kiroho nzuri tu. Mimi nishafanya hilo. Unajinyima anasa ndogo tu, mtu anapata nafasi ya kubadilisha maisha.
Mimi mara nyingine nakuwa na huruma sana kwa wanawake. Naona shida za Tanzania. Ingawa mimi si tajiri, nafikiria sana kuwa sina shida kama zile. So, I try to give back.
Ila sasa, ukifanya hivyo kumuanzishia biashara asimame mwenyewe, yeye anaona wewe ndiyo danga lake sasa.
Unashindwa kabisa kuelewa hii mentality.
So, ni kitu kimoja kumsaidia mwanamke anayeweza kujiongeza mwenyewe.
Ni kitu tofauti kabisa kumpa pesa mwanamke zombie ambaye hajui kufanya lolote zaidi ya kuomba pesa tu.
Na wanawake wa Tanzania wengi ni wa kundi hili la pili.