Akitajwa mwanamke lazima nimzungumzie mwanaume kwasababu tunajadili “uhusiano “ two way lane…. Kimoja kinasababisha kingine.
Hii ni jamii ambayo inafanya interaction, tabia ya kundi A inaathiri tabia ya kundi B na kinyume chake.
Sijui kuhusu whataboutism (would like to learn about it)
Kuhusu trauma dumping ningekupa mfano wa trauma dumping wanayofanya wanaume, but again utaniambia nafanya whataboutism! 😀
Niambie ni kwa namna gani katika mada tajwa mezani, naweza wajadili wanawake tu bila kutaja wanaume? Kila aliyefanya mjadala ambao una balance huko juu amefanya same thing, umeelewa nini kwenye hili..?
Sasa kwenye uhusiano wa wanawake na wanaume, wanawake hawawezi kupanga, wao wanapangiwa na wanaume tu? Wanawake ni dhaifu hivyo?
Whataboutism ni goal shifting. Hii ni mbinu mbaya sana ya kuepuka mada. Au pengine ni ujinga tu si mbinu mahsusi kuepuka mada.
Basically kwenye masuala haya mara nyingi huishia kuleta gender war badala ya ku address issues.
Mada imeletwa. Wanawake wa Tanzania ni ombaomba sana. Hii ndiyo mada.
Tuna nafasi ya kuangalia matatizo ya kiutamaduni, mfano, mwanamke anayeambiwa analipiwa mahari ili aolewe, na anakuta utamaduni huu tangu anazaliwa, naturally atajiona yeye ni kama commodity anapatikana kwa kulipiwa mahari, na psychologically ataona kuomba pesa ili atoe mbunye ni sawa. Ndiyo maana hata kwenye kuolewa analipiwa mahari. Kwa hiyo hapa kuna nafasi ya kubadili utamaduni wa kulipa mahari kwa mwanamke ili kuondoa hii dhana kwamba mwanamke ni bidhaa inayonunuliwa. Hiki ni tatizo la kijamii, si la mwanamke wala mwanamme. In fact linaumiza wanaume wengi wanaotaka kuoa lakini hawana mahari. In fact linaumiza wanawake wengi wanaoolewa na kuonekana kama bidhaa iliyonunukiwa kwa sababu wamelipiwa mahari. In fact kuna wanawake wapo katika ndoa zao kwa sababu wakitoka watatakiwa kurudisha mahari ambayo hawana tena ishatumika na familia zao.
Badala ya kuichambua mada, kidhahania, kifalsafa, wanawake wa Tanzania ni ombaomba sana, mnarukia kusema "What about wanaume, wanaume ni malaya wanahonga sana na wao ndio wanasababisha hili".
Lakini hiyo si mada. Inaonekana hilo la wanaume nalo ni kweli, lakini, hilo linaweza kuwa na mjadala tofauti. In fact ukikimbilia hilo la wanaune katika mada ya wanawake, kimsingi ni kama unawaondolea wanawake agency, unawafanya wanawake kuwa ni kama watoto wanapangiwa maisha na wanume tu, hawana usemi wao wenyewe, hawana maamuzi yao wenyewe, ni viumbe dhaifu.
Sasa, wanawake ni viumbe dhaifu hivyo?
On trauma dumping.
Kiutamaduni Tanzania wanaume hawaruhusiwi kufanya trauma dumping kwa sababu utamaduni wetu ni wa machismo. Mwanamme anatakiwa kuwa mtu imara anayepigana na dunia bila kulia wala kuonesha udhaifu. Anayelinda mwanamke wake na famikia.
Huyu mwanamme haruhusiwi kulialia, kuombaomba na kuonesha udhaifu kwa mwanamke wake. Na hii dhana ndiyo imejenga dhana ya kwamba mwanamme anatakiwa kutoa pesa kwa mwanamke na si mwanamke kwa mwanamme.
You are right ukiniambia wanamme pia wanafanya trauma dumping kwa wanawake nitakuambia ni whataboutism. Tena hiyo wala si whataboutism tu, hiyo ni disproportionate dichotomy, unalinganisha mlima Kilimanjaro na kichuguu kwa sababu vyote vina shape sawa bila kujali ukubwa.
Unaweza kutaja wanawake bila wanaume kwa sababu wanawake si kivuli cha wanaume. Si lazima kumtaja mwanamme ili kumzungumzia mwanamke.
Mfano, tukianzisha mada, "Je wanawake wanaweza kujitegemea? Unapoanza kumtaja mwanamme tu, unaondoka kwenye ku affirm maana hata mada kuiongelea bila kumtaja mwanamme umeshindwa.
Kwamba kila mtu hapo juu kataja mwanamme inawezekana ni udhaifu wa kufanya hoja za kidhahania (abstract thinking) katika jamii yetu. Na udhaifu unaweza kufanywa na wengi, hususan ukiwa ni wa kijamii au kiutamaduni. Tanzania tuna tatizo kwenye kufanya abstract thinking, tuna tatizo kwenye kupinga premise iliyowekwa tayari (mtu akianzisha kitu, kusema tofauti tunaona ni kumkosea heshima tunatafuta namna ya kukubaliana naye. Ndiyo maana hatabkwenye kura watu wanaambiwa wapige vipi.)
Tuna tatizo la kufanya argument from popularity logical fallacy, kuona kwamba kitu kikisemwa au kufanywa na wengi, basi ni lazima kitakuwa sawa tu. This is what you are doing.
No, kitu kinaweza kufanywa na wengi na pia kikawa cha kijinga, simply because jamii ina wajinga wengi.