Sakata la Jerry Silaa kuvunja majumba ya watu nchi nzima: Johnson Mahululu aidai serikali ya Tanzania bilioni 20

Kuishitaki serikali ama kumshitaki waziri wa ardhi kwenye kesi ya umiliki wa ardhi ni kama unatwanga maji kwenye kinu.

Tambua kwenye katiba yetu ya nchi Rais ndie ana custody ya ardhi yote iliyo ndani ya Tanzania. Yeye ndie ana mamlaka ya kufuta hati ya ardhi yoyote iliyo ndani ya Tanzania.

Rais haitaji hukumu ya mahakama. Ili kufuta hati ya mtu.

Jerry silaa ametumwa na rais ndio maana juzi kapewa sifa nyingi na rais kwamba ndie waziri ambae anafanya kazi nzuri
ardhi ni mali ya uma trusted to the president,ni kweli.lakini kuna watu wana interest juu yake, kama vile wanaojenga au kufanya shughuli juu yake. kufanya chochote kinachoathiri maslahi haya ya watu kunatakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria. hata rais hayupo juu ya sheria, hawezi kufanya chochote hata kama kinakuathiri ati kwasababu yeye ni rais.

Ndio maana sheria zimewekwa. AG alishatoa pendekezo sheria zitungwe kuwafanya hawa viongozi wanaotia hasara watu na kusababisha serikali kushtakiwa, wawe responsible kwa matendo yao binafsi. hata hivyo, sidhani kama waziri ana kinga hiyo ya kutoshtakiwa akikiuka sheria, hayupo juu ya sheria, decision yeyote inayoathiri maslahi ya mtu lazima itolewe sababu ya kufanya hivyo na chombo kilichowekwa na sheria kutoa maamuzi/haki. dunia yote ipo hivyo hata nchi yako ya tz ina katiba yake inayoongea hivyo.

shida ni kwamba halmashauri imejaa wanasheria ambao ni weak kwenye practice, na wanawashauri vibaya sana mawazili na viongozi wengine, jerry mwenyewe ni mwanasheria ambaye sina uhakika kama aliwahi kukanyaga mahakamani kama wakili. hao wanasheria wanaowashauri hawa wawe wanapikwa vizuri ili wawashauri vyema wasisababishe hasara kwa wananchi na kwa serikali, pia ili kulinda utawala wa sheria. pasipokuwepo nautawala wa sheria kila mtu atachukua sheria mkononi na patachafuka. kwa mwenye akilia takuwa amenielewa.
 
Fedha zipi zimelipwa?
Au na wewe unakupuka na kuongezea mafuta bila kwanza kuujua uhalisia.
Huyu mleta mada kaandika tu bila kutoa source yake ya habari.
Huyo Tapeli mwenyewe alisafirishwa toka Mafichoni Dodoma!
Alikokimbilia na kuletwa Dar ili ajibu mashtaka ya kuendesha genge la utakatishaji ardhi.
Sasa huyu chiembe hatuelezi kwenye huu uzi wake!
Kwamba ametumia hukumu ya mahakama gani ili kumpa ushindi Huyo Mahululu anaye Mhululu!
Ni hulka ya Chadema kutetea wezi na mafisadi wanaowadhulumu wananchi

Hata Mbowe amewadhurumu waandishi kumi wa Lililokuwa gazeti lake la "Tanzania Daima".
Hapa chadema iweke pembeni, wote tumeona viashiria vya utapeli unaosaidiwa na mahakama kudhulumu haki za wanyonge,tuunganishe nguvu kupambana na udhalimu huu wa akina mahululu ambao wapo ccm wapo chadema,mwenye haki na aipate haki yake,na siyo tu aipate ila wote tuone ameipata.
 
Jerry Silaa anashinikiza ifunguliwe kesi ya criminal trespass wakati msimamo wa Mahakama za Tanzania ni kwamba hiyo ni civil case, kama kuna dispute ya umiliki ni lazima kwanza mahakama ya madai ithibitishe nani mmiliki ndipo ujue nani kafanya criminal trespass.

Pengine Mwendesha Mashtaka wa Mkoa kawagomea kupeleka jalada Mahakamani kwa sababu hiyo

Anajua hiyo bili ya bilioni 20 lazima aitolee maelezo Baraza la Mawaziri, au kabla,kwa Waziri Mkuu
Na kiwanja amesha kigawa.
Uki fuatilia vizuri una weza kuta huyu dada ana uhusiano na Waziri.
Huwezi vunja nyumba ya mtu bila notisi wala kumsikiliza.
 
kufanya chochote kinachoathiri maslahi haya ya watu kunatakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria. hata rais hayupo juu ya sheria,
Mkuu hoja yako iko kinadharia zaidi kuliko uhalisia. Kwa katiba yetu rais yuko juu ya sheria. Ndiyo maana hahojiwi wala kishitakiwa na mtu ama chombo chochote hata kama akipora ardhi ama kuwaua watu wa wilaya yako wote.

Jiwe alinyang'anya ekari 33 za mhe. Sumaye alizokuwa anamiliki kihalali kule Mabwepande na ekari 200 za kule Mvomero kukiwa na ng'ombe zaidi ya 500. Jiwe hakufanyowa chochote.

Jiwe alikataza mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani iliyowekwa kikatiba hakufanyowa chochote.

Jiwe alimuondoa prof. Asad ktk nafasi ya CAG wakati katiba imemzuia kufanya hivyo lkn hakufanyowa chochote.

Samia amemuondoa spika Ndugai kiihuni na hajafanywa chochote.

Mifano hii yote inathibitisha kuwa rais wa Tanzania yuko juu ya sheria.
 
Suluhu siyo kutumia ubabe wa kiongozi. Mahakama ndiyo chombo cha kutoa haki.
Mahakama sasa hivi wanatakuwa kujithamini hii trend ya wananchi kukimbilia kutafuta suluhu kwa wanasiasa mihimili miwili inatakiwa ijitathimini kama iko relevant kwenye nchi mihimili hiyo ni ya serikali wale wafanyakazi wa .kudumu walioko maofisini maofisa ardhi na Mahakama

Ikifika mahali wananchi wanawaamini zaidi wanasiasa kuliko wasomi waajiriwa serikalini na mahakimu na majaji jua kuna shida kubwa kwenye nchi ya hiyo Mihimili na wananchi walio wengi hawana imani nao

Wao ndio wajitadhimini

Kifupi serikali performance appraisal ya mfanyakazi ofisa ardhi ihusishe kipimo.cha je kazalisha migogoro ya ardhi ? Kama ndiyo atimuliwe kazi bila kulipwa hata mia na Hakimu au jaji anayesababisha wananchi walio wengi wakose imani na mhimili wa Mahakama watafute namna ya kumtoa kuhukumu kesi awekwe hata kuwa mkuu wa kitengo cha mapokezi au cha kutia photocopy ya karatasi za kesi
Ule mrundikano wa watu kujazana kwa wanasiasa awe makonda au Slaa au waziri mkuu Majaliwa inaonyesha wazi watendaji wa serikali kuna maeneo wamepwaya na mahakama zimepwaya

Hilo ni hatari kwa usalama wa nchi serikali na mahakama zichukue hatua na mahakama ichukue hatua kurudisha confidence za wananchi kwa mahakama confidence ambayo kwa sasa wananchi wengi hawana confidence na mahakama
 
Watanzania wameonewa saana, wamezulumiwa saana Viwanja vyao, ngoja matapeli wa viwanja pia wajue maumivu Waliyokuwa wanapitia Watanzania wanyonge.
 
Watanzania wameonewa saana, wamezulumiwa saana Viwanja vyao, ngoja matapeli wa viwanja pia wajue maumivu Waliyokuwa wanapitia Watanzania wanyonge.
Sahihi hizo mali zao za dhuluma wacha mighorofa yao ipigwe chini na magreda hadi waumwe visukari na na kupata stroke, na pressure ziwapabde juu wafe wapuuzi wakubwa matapeli hao hawana faida kwa dunia wafe tu dunia na Tanzania matapeli wapungue
 
Source: Youtube-wakiliTv, taarifa ya Wakili Dickson Matata

Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.

Sasa watanzania wataingia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha kumuita tapeli wakati hana hukumu ya mahakama iliyompata na hatia ya utapeli, na kumharibia jina na biashara zake.

Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.

Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.

Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.

Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa.

Kuhusu nyumba kuvunjwa, soma Aliyevamia Kiwanja cha mwingine kwa miaka 20 Mbezi Africana avunjiwa ghorofa

Pia soma Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!
huyo tapeli anataka kushindan na dola ataiweza?
 
Mtoa mada nadhani hujui ukubwa wa tatizo la migogoro ya ardhi,na mara nyingi masikini ndo wanaoonewa sababu hawana uwezo wa kushindana na wenye pesa na connection.
 
Source: Youtube-wakiliTv, taarifa ya Wakili Dickson Matata

Nilisema kwamba haya mambo ya kujifanya mwendesha mashitaka na hakimu anayofanya Jerry Silaa yasipoangaliwa, ataitia nchi hasara kubwa sana.

Sasa watanzania wataingia hasara ya bilioni 20 ili kumlipa Johnson Mahululu baada ya Jerry Silaa kuvunja ghorofa lake, kumdhalilisha kumuita tapeli wakati hana hukumu ya mahakama iliyompata na hatia ya utapeli, na kumharibia jina na biashara zake.

Niliwahi kuonya humu kwamba wizara kubwa na nzito wasipewe watoto, hawa watoto waanzie wizara ya michezo, utamaduni na kwingine.

Nimefuatilia kule Mwanza, anatangatanga na Polisi kwemye mikutano, na wale ambao hawajaelewa maelezo yake, anatoa amri wakamatwe na Polisi. Kimsingi, analeta chaos kubwa sana.

Ameenda kuonana na RPC na kutoa amri (udikteta ambao samia hataki) kwamba Johnson Mahululu anyimwe dhamana, ana siku tano hajatoka.

Tunajua weekend iliyoisha ilibidi awahi kikao mahali akutane na bosi wake mkubwa., tunaipa angalizo serikali dhidi ya Jerry Silaa.

Kuhusu nyumba kuvunjwa, soma Aliyevamia Kiwanja cha mwingine kwa miaka 20 Mbezi Africana avunjiwa ghorofa

Pia soma Serikali impe angalizo Jerry Silaa, namuona anaiingiza Serikali katika mgogoro mkubwa wa kulipa fidia!
Acha kutisha watu kijana, sheria zifuate mkondo wake "Nani mmiliki halali wa eneo husika" nani mvamizi, docs zilipatikana kihalali?, hakuna aliyezulumiwa? Historia ya eneo ipoje?, mkale wa eneo alikuwa ni nani?, Yapo mambo ya msingi ya kufuata, docs pekee siku hizi hazitoshelezi, physical witness inasemaje?, majirani wanasemaje? Mtu wa awali kuanza kununua anasemaje juu ya historia ya eneo?, naandika hapa nikiwa na hasira sana ya kudhulumiwa eneo langu, Mbezi beach, goigy plot no. 471,block A.
 
ardhi ni mali ya uma trusted to the president,ni kweli.lakini kuna watu wana interest juu yake, kama vile wanaojenga au kufanya shughuli juu yake. kufanya chochote kinachoathiri maslahi haya ya watu kunatakiwa kufanyika kwa mujibu wa sheria. hata rais hayupo juu ya sheria, hawezi kufanya chochote hata kama kinakuathiri ati kwasababu yeye ni rais. ndio maana sheria zimewekwa. AG alishatoa pendekezo sheria zitungwe kuwafanya hawa viongozi wanaotia hasara watu na kusababisha serikali kushtakiwa, wawe responsible kwa matendo yao binafsi. hata hivyo, sidhani kama waziri ana kinga hiyo ya kutoshtakiwa akikiuka sheria, hayupo juu ya sheria, decision yeyote inayoathiri maslahi ya mtu lazima itolewe sababu ya kufanya hivyo na chombo kilichowekwa na sheria kutoa maamuzi/haki. dunia yote ipo hivyo hata nchi yako ya tz ina katiba yake inayoongea hivyo.

shida ni kwamba halmashauri imejaa wanasheria ambao ni weak kwenye practice, na wanawashauri vibaya sana mawazili na viongozi wengine, jerry mwenyewe ni mwanasheria ambaye sina uhakika kama aliwahi kukanyaga mahakamani kama wakili. hao wanasheria wanaowashauri hawa wawe wanapikwa vizuri ili wawashauri vyema wasisababishe hasara kwa wananchi na kwa serikali, pia ili kulinda utawala wa sheria. pasipokuwepo nautawala wa sheria kila mtu atachukua sheria mkononi na patachafuka. kwa mwenye akilia takuwa amenielewa.

Katiba inampa mamlaka Rais kufanya jambo ambalo haliwezi kuhojiwa mahakamani.. waziri ametumwa na president hivyo anavunja kwa Presidential power.
 
Tulidhani mzee wa Isimani Kaka Lukuvi aliimudu Sana hii wizara, kumbe aliacha migogoro kibao. Alichoweza Ni kutulipisha Kodi ya 1500 kila mwezi regardless ya thamani ya kiwanja.
 
Acha kutisha watu kijana, sheria zifuate mkondo wake "Nani mmiliki halali wa eneo husika" nani mvamizi, docs zilipatikana kihalali?, hakuna aliyezulumiwa? Historia ya eneo ipoje?, mkale wa eneo alikuwa ni nani?, Yapo mambo ya msingi ya kufuata, docs pekee siku hizi hazitoshelezi, physical witness inasemaje?, majirani wanasemaje? Mtu wa awali kuanza kununua anasemaje juu ya historia ya eneo?, naandika hapa nikiwa na hasira sana ya kudhulumiwa eneo langu, Mbezi beach, goigy plot no. 471,block A.
Umeshaacha kunywa pombe za kienyeji.....mataputapu,naona machicha yanaturukia huku
 
Back
Top Bottom