Jerry Silaa: Watu wote wanaozungumza kwa kufoka kwenye suala la Mkataba wa DP World wamenunuliwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa anazungumza na waandishi wa habari Muda huu kuhusu sakata la Bandari na uwekezaji wa DP World.

===

Kuna watu wanatumika kwa maslahi yao binafsi kumuondoa kwenye reli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye utendaji wake wa kazi.

Sitajadili watu, nitajadili mawazo yao. Nasikitishwa na hoja za kisheria ambapo baadhi ya wanasheria wanajadili kwa namna tofauti. Mkataba huu ni mkataba wa kimataifa chini ya Vienna convetion.

IGA kati ya JMT na Dubai ni Mkataba ama makubaliano yanayolenga kujenga msingi wa makubaliano, ni hatua ya kwanza ambapo hatua zingine zitafuata. Wapotoshaji wamejikita kwenye eneo hili tu, hawataji mbele kitaendelea nini.

Dubai ni mojawapo ya sehemu za falme za Kiarabu na Sheria yao inaruhusu kuingia makubaliano na nchi zingine kama Tanzania. Mkataba huu upo kisheria, umeingiwa kwa kurejea Vienna Convention.

Ubinafsishaji wa benki ya NMB ulikumbwa na changamoto nyingi kama ilivyo sasa kwenye bandari ya Dar es Salaam, hata hivyo, bandari hii haibinafsishwi. Hii ni mikataba ya uendeshaji au ukoshadishaji.

Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam unamilikiwa na Serikali, lakini Swisport na washirika wengine wanaendesha uwanja huo. Je, pale masuala ya ulinzi na usalama yanasimamiwa na nani? ni serikali. Vivyo hivyo kwa ushuru wa forodha, kuna TRA pale. Uwekezaji wa DP World utakuwa hivyo pia.

IGA kwenye ibara ya 5 inaelezea kuwa huyu bwana (DP World) akitaka kufanya jambo lolote ni lazima alete mapendekezo Serikalini. Ikitokea wameelewana watasaini concesion agreement, suala la usalama linahusu mamlaka za Nchi.

Kwanini serikali imeamua kutafuta operator mwenye uwezo?
Bado ufanisi ni mdogo, meli zinazubiri hadi siku 5 kuweka nanga na kushusha shehena. Kila siku moja ya kusubiri n kati ya milioni 60-90 ambayo analipa msafirishaji, inaongeza gharama ya bidhaa kwa wanunuzi. Kama ni transit, gharama za usafirishaji zitakuwa kubwa.

Kushusha kontena siku 3, kuondosha mzigo utatumia masaa 12, clearance ya kawaida ni zaidi ya siku 7. Mifumo ya TEHAMA haijaboreshwa vya kutosha.

Watu wote wanaozungumza kwa kufoka wamenunuliwa. Watu wengi hawafurahi kuona Rais Samia anataka kuifanya bandari hii kuwa na ufanisi mkubwa kuliko bandari nyingi duniani.

Wako maafisa forodha waaminifu, lakini wapo wanaonufaika na ule urasimu, hawawezi kufurahia mabadiliko haya. Wapo pia washindani wa bandari yetu na corridor zingine za kibiashara, wote hawa hawawezi kufurahia.

Kuna mambo mengine mazuri yanaendelea mbona hayajadiliwi? Watu wameshika jambo moja tu, yawezekana kuna nguvu nyuma ya hao wanaopiga kelele.

Wanaopinga hawatanyamaza leo, wataendelea kusema. Mfano, baadhi ya wanasheria wameenda mahakamani kutafuta tafsiri, lakini bado wanaongelea suala hili. Wengine ni watu wazima, wakati mwingine utu uzima usipojipanga unaweza kukujia vibaya, ukiangalia sura na siha zao unaona kidogo pengine njaa imeingia.

Wito kwa Serikali ni kwenda kasi kwenye kutekeleza ili watanzania waone manufaa. Tuone tani zinaongezeka, siku 5 za kusubiri nangani ifikie hadi siku 1, kushusha kontena iwe siku 1, kushusha mzigo kichere iwe maximum siku 2 hadi 3 na release iwe hadi saa 1.

Tuone mizigo ya TEHAMA inaweza kumfanya mtu aone maendeleo na kama kuna ukadiriaji wa kodi yaweze kufanyika kwa uwazi pia gharama za usafirishaji ipungue.

Mambo haya yatatamanisha na kuvutia nchi zingine zisizo na bandari zikimbilie hapa, tuone pia mapato ya forodha yanaongezeka.

Natoa wito kwa watanzania waendelee kuwasikiliza (wanaopinga) kwa masikio matatu. Kamati za bunge hadi kufikia hatua ya kutoa maoni bungeni ilikuwa imepokea maoni mengi kutoka kwa wananchi, na maoni yao yatazingatiwa.

===

MASWALI NA MAJIBU

1. IGA ina matobo?
Ameulizwa kama IGA ina matobo kwa kuwa baadhi ya vipengele vyake vinaitaka Tanzania kuipa taarifa Dubai juu ya fursa zilizopo Bandarini.

Amejibu: IGA haina matobo. Kuhusu Tanzania kuipa taarifa Dubai kwenye masuala na fursa mbalimbali za Bandari, Kwenye sheria neno likiandikwa "WILL" inakuwa sio lazima, lakini kwa nia njema Tanzania inaweza kuitarifu Dubai kuhusu fursa zilizopo Bandarini ili Dubai walete mapendekezo yao Serikalini yajadiliwe ambapo yanaweza kukubaliwa au kukataliwa.

2. Mikataba ya HGA itakuwa siri?
Ameulizwa, watu wanapigia kelele IGA sababu baadae hawataweza kujua kilichomo kwenye HGA maana inasemekana itakuwa ni siri.

Amejibu: Hata kura ni siri, kila jambo na taratibu zake. Hata nyumbani kuna baadhi ya mambo yanafanyika kwa siri.

===

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
 
Sijui anazungumzia nini, akiwa upande upi.

Lakini kwa kuanzia tu, Wakati huo mkataba ukipitishwa hapo Bungeni, Jerry Slaa alikuwa wapi?
Kama alikuwepo bungeni, kwanini hakuupinga?
Kama aliuunga mkono basi kwa sasa akae zaidi kimya (maana jukumu lake alishalimaliza), jukumu la kuupinga tumebakia nalo sisi wananchi huku mtaani.
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa anazungumza na waandishi wa habari Muda huu kuhusu sakata la Bandari na uwekezaji wa DP World.

===

Kuna watu wanatumika kwa maslahi yao binafsi kumuondoa kwenye reli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye utendaji wake wa kazi.

Sitajadili watu, nitajadili mawazo yao. Nasikitishwa na hoja za kisheria ambapo baadhi ya wanasheria wanajadili kwa namna tofauti. Mkataba huu ni mkataba wa kimataifa chini ya Vienna convetion.

IGA kati ya JMT na Dubai ni Mkataba ama makubaliano yanayolenga kujenga msingi wa makubaliano, ni hatua ya kwanza ambapo hatua zingine zitafuata. Wapotoshaji wamejikita kwenye eneo hili tu, hawataji mbele kitaendelea nini.

Dubai ni mojawapo ya sehemu za falme za Kiarabu na Sheria yao inaruhusu kuingia makubaliano na nchi zingine kama Tanzania. Mkataba huu upo kisheria, umeingiwa kwa sheria za Vienna Convention.
CCM watu wameisha kabisa Yaani ! huyu ndio wa kujibu jambo hili kweli ?
 
Ubinafsishaji wa benki ya NMB ulikumbwa na changamoto nyingi kama ilivyo sasa kwenye bandari ya Dar es Salaam, hata hivyo, bandari hii haibinafsishwi. Hii ni mikataba ya uendeshaji au ukoshaji.

Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam unamilikiwa na Serikali, lakini Swisport na washirika wengine wanaendesha uwanja huo. Je, pale masuala ya ulinzi na usalama yanasimamiwa na nani? ni serikali. Vivyo hivyo kwa ushuru wa forodha, kuna TRA pale.

Washughulikieni acheni kucheka nao,Bora utoke kwenye reli ulinde maslahi Yao kuliko kuwaacha wanapotosha..

Huyu ndio anafaa Sasa nafasi ya Waziri wa Sheria na Katiba
 
Hebu tufafanulie please.
Kwa mujibu wa Katiba ya UAE ibara ya 123; Emirates zinaruhusiwa kuingia mikataba na serikali za jirani na UAE (UAE's neighbouring states), au za Kanda jirani na UAE (UAE's neighbouring regions).

Sisi siyo nchi mojawapo ya Kanda jirani na UAE, kwa kifupi tupo nao mbali sana. Dubai hakupaswa kuingia mkataba nasi kwa kuwa hawana hadhi ya nchi kama tulivyo.

Kwa kuwa UAE ni nchi, ilipaswa iingie mkataba nasi; kwa kuwa wana hadhi sawa ya nchi kama tulivyo.

Kwa kifupi; Dubai siyo nchi, ni emirate tu. Nchi ni UAE.
 
Mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa anazungumza na waandishi wa habari Muda huu kuhusu sakata la Bandari na uwekezaji wa DP World.

===

Kuna watu wanatumika kwa maslahi yao binafsi kumuondoa kwenye reli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwenye utendaji wake wa kazi.

Sitajadili watu, nitajadili mawazo yao. Nasikitishwa na hoja za kisheria ambapo baadhi ya wanasheria wanajadili kwa namna tofauti. Mkataba huu ni mkataba wa kimataifa chini ya Vienna convetion.

IGA kati ya JMT na Dubai ni Mkataba ama makubaliano yanayolenga kujenga msingi wa makubaliano, ni hatua ya kwanza ambapo hatua zingine zitafuata. Wapotoshaji wamejikita kwenye eneo hili tu, hawataji mbele kitaendelea nini.

Dubai ni mojawapo ya sehemu za falme za Kiarabu na Sheria yao inaruhusu kuingia makubaliano na nchi zingine kama Tanzania. Mkataba huu upo kisheria, umeingiwa kwa kurejea Vienna Convention.

Ubinafsishaji wa benki ya NMB ulikumbwa na changamoto nyingi kama ilivyo sasa kwenye bandari ya Dar es Salaam, hata hivyo, bandari hii haibinafsishwi. Hii ni mikataba ya uendeshaji au ukoshaji.

Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam unamilikiwa na Serikali, lakini Swisport na washirika wengine wanaendesha uwanja huo. Je, pale masuala ya ulinzi na usalama yanasimamiwa na nani? ni serikali. Vivyo hivyo kwa ushuru wa forodha, kuna TRA pale. Uwekezaji wa DP World utakuwa hivyo pia.

IGA kwenye ibara ya 5 inaelezea kuwa huyu bwana (DP World) akitaka kufanya jambo lolote ni lazima alete mapendekezo Serikalini. Ikitokea wameelewana watasaini concesion agreement, suala la usalama linahusu mamlaka za Nchi.

Kwanini serikali imeamua kutafuta operator mwenye uwezo?
Bado ufanisi ni mdogo, meli zinazubiri hadi siku 5 kuweka nanga na kushusha shehena. Kila siku moja ya kusubiri n kati ya milioni 60-90 ambayo analipa msafirishaji, inaongeza gharama ya bidhaa kwa wanunuzi. Kama ni transit, gharama za usafirishaji zitakuwa kubwa.

Kushusha kontena siku 3, kuondosha mzigo utatumia masaa 12, clearance ya kawaida ni zaidi ya siku 7. Mifumo ya TEHAMA haijaboreshwa vya kutosha.

Watu wote wanaozungumza kwa kufoka wamenunuliwa.

Nafikiri hakuna kuheshimu elimu tena. Kama Prof wa sheria ameshaongea,mwanafunzi unaongea nini tena?
 
Back
Top Bottom