chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,003
- 20,681
Leo katika taarifa ya habari ya ITV nimemuona Jerry Silaa akisimamia kubomoa ghorofa, na bila shaka kwa kujifanya yeye ni hakimu au Jaji mwenye uamuzi wa mwisho, kwa nini asishauri watu wafuate mlolongo wa mahakama ambao unasikiliza pande zote na kutoa haki ya rufaa ya ngazi tofauti? Kwa nini asiache tafsiri ya mwisho ya haki ifanywe na mahakama kabla ya mtu yoyote kuingizwa kwenye hasara?
Hofu kubwa ni kwamba haya mambo anayafanya Dar es salaam kwa kusaidia watu ambao mi marafiki zake, au marafiki wa familia yake. Ukikutana na family friend wa Silaa, na kimsingi wanamzonga sana pale ofisini watumie fursa kabla hajatenguliwa, ujue lazima atavuruga kila kitu ili kwemye vikao vya ukoo au harusi akasifiwe. Imagine Waziri mzima anatembea mpaka kwako na mmoja wa watu waliolalamika, yule anayelalamikiwa yuko na nani? Na ameshamumini anayekulalamikia, kamkodia mpaka greda, sijui kwa hela za serikali au kamshawishi akodi! utamwambia nini akuelewe?
Ajiepusha kuiweka serikali mbele katika kila tukio, aache sheria ichukue mkondo, akiwa waziri wa ardhi, miaka kumi serikali italipa fidia za trilioni na zaidi.
Nina imani haya mambo ya hovyo anayafanya bila kuhusisha ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, angewahusisha wangemkatalia maana wao ndio wanajua vita ya mahakamani ikoje, yeye atafanya upuuzi wake, atatenguliwa, na anatuachia hasara kubwa ya kulipa fidia.
Mawaziri wapya watoto watoto wasipewe wizara nzito kama ardhi. Waziri badala ya kushughulikia sera za kitaifa, anazurura mitaani ambako tayari ana maafisa ardhi. Mchi hii ina mitaa mingapi? Kama sera ina shida kutatua migogoro ya ngazi hizo, yeye kama waziri kaliambia nini Bunge limtungie sheria kutengeneza mfumo imara wa watu wa ardhi kuwa na mawasiliano na wateja wao? Atafika lini Chankende kutatua mgogoro?
Wazara yake inatoa hati, baadae inaikataa hati moja,inaikubali nyingine, halafu yuleyule waliyempa hati na kibali cha ujenzi, wao wenyewe wanaenda kumvujia walichomruhusu ajenge!