ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,076
- 49,774
Waziri wa Ardhi na Nyumba ameagiza Nchi nzima ipimwe.
Moja ya shida kubwa kabisa ya Tanzania ni ujenzi holela na Nchi inakuwa kama dampo Kwa kujaaa ma slums na mabanda Kila sehemu.
My Take:
Peleka Kwenye Balaza la Mawaziri pendekezo la kuunda Mamlaka au Wakala wa Mipango Miji na Matumizi Bora ya Ardhi (Urban planning & Land administration Agency).
Wakala huyo ndio atafaulu kupima Nchi nzima dizaini ya Luwasa, Tarura nk.
=========
Waziri mpya wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga Jerry Silaa amemtaka Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kuja na mpango wa kuipima Nchi nzima ya Tanzania pamoja na kuwasilisha ‘case study’ ya Nchi zilizofanikiwa kwenye eneo hilo.
Waziri Silaa ameyasema haya leo kwenye siku yake ya kwanza Wizarani hapo wakati akiweka wazi Vipaumbele vyake 12 atakavyovifanyia kazi kama Waziri mwenye dhamana (video nzima ya tukio hili ipo kwenye Youtube ya millardayo ).
“Mara ya mwisho sheria za ardhi zimefanyiwa marekebisho mwaka 2019 na leo ni 2023 hakuna jinsi kwa miaka hii minne hizi sheria zipo ‘valid’ kwa asilimia 100 lazima kuna mambo yamejitokeza hapa katikati kwahiyo sheria zote zikiwemo sheria za nyumba ambazo zinakwamisha, tukikutana tuzungumze tutengeneze mchakato wa kurekebisha sheria, Bunge lipo.
”Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani tukikutana uje na mpango wa kupima hii Nchi, hii Nchi nzima ipimwe na uje na ‘case study’ ya Nchi zilizofanikiwa, ukishapima ukawa na mfumo madhubuti wa ki-digitali tukija hapa miaka mitano baadae kuna baadhi ya idara zitafungwa na neno mgogoro litakuwa halipo tena”