Ngaliwe

Senior Member
Dec 30, 2015
161
364
Mnamo mwaka 2020 Wakili Peter Madeleka alikamatwa na kufunguliwa kesi ya Uhujumu Uchumi no. 40 (Economic case no 40/2020) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Arusha. Katika kesi hiyo alishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kughushi (forgery) kinyume na Sheria ya Mwenendo wa Adhabu (Penal Code) kifungu cha 337 cha sheria hiyo.

Pia alishtakiwa chini ya kifungu cha 12 cha Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumu (Anti Money Laundering Act).

Wakati shauri lake linaendelea aliomba kufanya makubaliano na Serikali (Pre Bargaining) na taratibu zote za kufanya makubaliano zilifuatwa na ndipo aliachiwa huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii Wakili Madeleka aliendelea kuchapisha habari kuwa alilazimishwa kukiri kosa na aliekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

Baadaye alifungua kesi katika Mahakama Kuu akipinga taratibu hizo lakini maombi hayo madogo yalitupwa nje kwa kuwa Mahakama haikuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Ndipo alifungua shauri hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kupinga maamuzi hayo lakini Mahakama ilitoa maamuzi kuwa taratibu zote za makubaliano (Plea Bargaining) zilifanyika sawa.

Baada ya maamuzi hayo alikata rufaa tena na kuja na sababu tofauti ambapo Mahakama ilisikiliza hoja zake na kutoa amri kuwa taratibu za makubaliano hazikuzingatiwa hivyo kuamuru status ya kesi yake kurudi kama ilivyokuwa awali.

Baada ya maamuzi hayo Wakili Madeleka alikamatwa tena ili kuweza kuendelea na kesi yake ya msingi na kwa kuwa makosa anayoshtakiwa nayo hayana dhamana.

UPOTOSHAJI:

Jamii inapotoshwa na kuaminishwa kuwa mshtakiwa ameshikwa kutokana na kutoa maoni yake juu ya Mkataba wa DP world na Serikali ya JMT jambo ambalo si sahihi.

Ikumbukwe watu mbalimbali wametoa mawazo yao na hakuna yoyote alieshikwa. Hata katika kesi iliyofunguliwa na mawakili yeye si miongoni Mwao.

Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba Mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.

Pia soma Wakili Peter Madeleka akamatwa na polisi baada ya Mahakama Kuu kufuta Plea Bargain aliyoingia na DPP
 
Ukweli mchungu tunaishi in a pithole country, nchi ambayo mihimili ya judiciary na Bunge ipo mifukoni mwa mhimili wa magogoni, katiba mpya ndio nchi inahitaji, kesi hii taasisi mbili huru zingeihusu, Human rights commission na PP, haki ya mlalamikaji ingepatilkana kihalali, na jeshi letu la police livunjwe na tuanze upya, all above 40yrs waondolewe maana wapo corrupted na systems, tuajiri young graduates, watuwekee msingi mpya na bora, mfano tuchukue 1000 tuwapeleke pale Botswana wakajifunze kuwa traffic officer's bora na kuona wenzetu wamefanikiwa vipi kuwa na zero corruption kwenye utendaji wake hasa barabarani.
 
Acha upuuzi huu, read to understand, nchi hii ina middle class wa ajabu, tatizo hapo lipo wapi?,kila msomaji wa mada hii imetambua nini lilikua lengo la aliyeandika mada hii, generation iliyojaa vihiyo wasiojua how to read to the meaning
Nimeelewa kakusudia nini ndiyo maana nikamrekebisha, mimi siyo poyoyo mwenzako, hakuna neno "Pre" kwenye hiyo sheria.

Uzi wa kisheria huu siyo nyuzi ulizozowea za kijingajinga.
 
Hizo taratibu zote za kesi mahakamani kama kweli zilikuwepo, iweje mkamvizie akiwa kwenye chumba cha mahakama mnamsubiri akitoka nje ndio mumkamate?

Kwani hampafahamu nyumbani au ofisini kwake? mliwahi kumtaka ajisalimishe kituo cha polisi kwa hayo mashtaka akakataa kutii wito?

Huu utetezi uliouleta hapa ni ujinga mtupu, kimsingi mmemkamata Adv. Madeleka kwa sababu ya msimamo wake kuhusu utoaji bure wa bandari zetu zote Tanganyika, lakini sio kwa hizo sababu nyepesi ulizotuandikia hapo.
 
Hivyo ifahamike na itambulike mshtakiwa ameshikwa kwa makosa yake aliyoyafanya huko nyuma ambapo yeye mwenyewe alikiri na sasa ameomba mahakama ifute maamuzi hayo hivyo kesi yake ya msingi inaendelea.
Sasa kama alikiri kutenda kosa, kesi yake ya msingi inaendelea kwa muktadha upi?
 
Hizo taratibu zote za kesi mahakamani kama kweli zilikuwepo, iweje mkamvizie akiwa kwenye chumba cha mahakama mnasubiri akitoka nje ndio mumkamate?

Kwani hampafahamu nyumbani au ofisini kwake? mliwahi kumtaka ajisalimishe kituo cha polisi kwa hayo mashtaka akakataa kutii wito?
sasa ulitaka akamatwe wapi?

Si mkamuwekee dhamana?
 
Back
Top Bottom