Shauri dhidi ya Mbunge Gekul lasikilizwa Mahakamani, Wakili Madeleka asema DPP hakuwa na Mamlaka ya kufuta kesi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imesikiliza shauri la Jinai namba 577/2024 mbele ya Jaji Devotha Kamuzora, linalomhusu Hashim Ally ambaye ni Mrufani dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ambaye ni Mrufaniwa.

Katika rufaa hiyo, Ally anapinga maamuzi yaliyofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati mnamo Desemba 27, 2023 ya kuiondoa kesi hiyo Mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Gekul alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Ally Novemba 11, 2023 kinyume cha Kifungu cha 41 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya 2022.

Mmoja wa Mawakili wa Mrufani, Peter Madeleka anaelezea kilichotokea kwa kusema “Shauri limesikilizwa lakini jana Machi 20, 2024 Mrufaniwa Pauline Gekul alisajili pingamizi la awali kwa kuweka mapingamizi matatu Mahakamani akipinga rufaa hii kusikilizwa.

“Mahakama ilianza kusikiliza mapingamizi ya Mrufaniwa na baada ya kusikiliza ikaendelea kusikiliza rufaa yenyewe iliyowasilishwa na Hashim Ally.

“Mahakama imepanga kutoa uamuzi Aprili 15, 2024, katika hoja za pingamizi zilizowasilishwa na Mrufaniwa, anadai Mahakama haikuwa na uwezo wa kusikiliza rufaa hii kwa kuwa sababu ya kwanza na ya pili ilihusisha hoja ya katika na hii si Mahakama ya Kikatiba.

“Pili anasema rufaa hii imekuja mapema mno, imejichanganya na haina maana yoyote, tatu anasema rufaa hii inapaswa kutozingatiwa kwa ujumla.

“Mrufani (Hashim Ally) kupitia Mawakili wake Peter Madeleka, Thadei Lista na Joseph Masanja katika kupinga mapingamizi hayo tulisema hayana mashiko kwa kuwa Mahakama hii ina uwezo wa kisheria chini ya Kifungu cha 300 (59) na 300 (61) kupokea rufaa zote zinazotokana na maamuzi ya Mahakama za chini.”

Upande wa Wakili Ephraim Kisanga ambaye ni Wakiliwa Mahakama Kuu aliyekuwa akimuwakilisha Pauline Gekul amesema:

“Shauri lilipangwa kusikilizwa, limesikilizwa na Mahakama Kuu, kabla ya hapo siku moja kabla tuliwasilisha mapingamizi matatu.

“Mapingamizi yote matatu yamesikilizwa na rufaa pia imesikilizwa, Mahakama imesema Aprili 15, 2024 itatoa uamuzi mdogo wa mapingamizi na kama yatakuwa hayana mashiko, siku hiyohiyo tutarejea kwa ajili ya hukumu ya rufaa iliyowasilishwa.”

Pia soma

Naibu Waziri na Mbunge Pauline Gekul adaiwa kumfanyia Ukatili wa Kimwili Mtoto

Breaking News: - Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana

Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

CCM Manyara yakutana kumjadili Pauline Gekul, kutoa tamko Novemba 27, 2023

Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

Mbunge Pauline Gekul akamatwa na Jeshi la Polisi akijaribu kutoroka nchini kuelekea nchini Kenya

Mbunge Pauline Gekul ahojiwa Polisi na kupewa dhamana, karudi nyumbani kwake

Peter Madeleka kusikiliza kesi ya Gekul mahakama ya Wilaya kwa tuhuma alizonazo dhidi ya Hamis

Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake

Nani anamlinda Gekul? DPP asema hana mpango wa kuendelea na kesi

Ya Gekul hayajaisha, Wakili Madeleka kukata rufaa

DPP: Hakukuwa na nia ya kufungua kesi ya Jinai dhidi ya Pauline Gekul

Rufaa ya Pauline Gekul (Mbunge Babati Mjini) yapigwa kalenda
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imesikiliza shauri la Jinai namba 577/2024 mbele ya Jaji Devotha Kamuzora, linalomhusu Hashim Ally ambaye ni Mrufani dhidi ya Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul ambaye ni Mrufaniwa.

Katika rufaa hiyo, Ally anapinga maamuzi yaliyofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati mnamo Desemba 27, 2023 ya kuiondoa kesi hiyo Mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Gekul alidaiwa kumshambulia na kumdhuru Ally Novemba 11, 2023 kinyume cha Kifungu cha 41 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 ya 2022.

Mmoja wa Mawakili wa Mrufani, Peter Madeleka anaelezea kilichotokea kwa kusema “Shauri limesikilizwa lakini jana Machi 20, 2024 Mrufaniwa Pauline Gekul alisajili pingamizi la awali kwa kuweka mapingamizi matatu Mahakamani akipinga rufaa hii kusikilizwa.

“Mahakama ilianza kusikiliza mapingamizi ya Mrufaniwa na baada ya kusikiliza ikaendelea kusikiliza rufaa yenyewe iliyowasilishwa na Hashim Ally.

“Mahakama imepanga kutoa uamuzi Aprili 15, 2024, katika hoja za pingamizi zilizowasilishwa na Mrufaniwa, anadai Mahakama haikuwa na uwezo wa kusikiliza rufaa hii kwa kuwa sababu ya kwanza na ya pili ilihusisha hoja ya katika na hii si Mahakama ya Kikatiba.

“Pili anasema rufaa hii imekuja mapema mno, imejichanganya na haina maana yoyote, tatu anasema rufaa hii inapaswa kutozingatiwa kwa ujumla.

“Mrufani (Hashim Ally) kupitia Mawakili wake Peter Madeleka, Thadei Lista na Joseph Masanja katika kupinga mapingamizi hayo tulisema hayana mashiko kwa kuwa Mahakama hii ina uwezo wa kisheria chini ya Kifungu cha 300 (59) na 300 (61) kupokea rufaa zote zinazotokana na maamuzi ya Mahakama za chini.”

Upande wa Wakili Ephraim Kisanga ambaye ni Wakiliwa Mahakama Kuu aliyekuwa akimuwakilisha Pauline Gekul amesema:

“Shauri lilipangwa kusikilizwa, limesikilizwa na Mahakama Kuu, kabla ya hapo siku moja kabla tuliwasilisha mapingamizi matatu.

“Mapingamizi yote matatu yamesikilizwa na rufaa pia imesikilizwa, Mahakama imesema Aprili 15, 2024 itatoa uamuzi mdogo wa mapingamizi na kama yatakuwa hayana mashiko, siku hiyohiyo tutarejea kwa ajili ya hukumu ya rufaa iliyowasilishwa.”

Pia soma
- Audio: Emmanuel Gekul akitoa vitisho vya kutaka kumdhuru anayedaiwa kusambaza Video ya kijana aliyefanyiwa ukatili na Pauline Gekul

- Rufaa ya Pauline Gekul (Mbunge Babati Mjini) yapigwa kalenda

- Mbunge Pauline Gekul atakiwa kufika Mahakamani Disemba 27, 2023 kujibu tuhuma dhidi yake
Huu ni mtihani kwa kile wanaita utawala wa sheria wakati wananchi wanachotaka ni utawala wa haki. Utasikia vigogo serikali na mabwanyenye wakisema wanataka utawala wa sheria huku wakijua wanaweza kununua haki kutoka wanasheria na vyombo vya kusimamia sheria. Huyu gekul ni mfano kabisa wa kigogo kununua haki na kumdhulumu mwananchi mnyonge. Wametumia vibaya kifungu chenye kumruhusu DPP kufuta kesi bila kulazimika kutoa sababu kumdhulumu raia wa kawaida kupata haki yake. Rais alifanya vizuri kumtema gekul kwa uzito wa shutuma tu ila mchezo wa DPP ndio unauza haki. Kesi hii lazima isikilizwe.
 
Hawa wanatusumbua tu vichwa vyetu,
Hawa kwenye mahakama za duniani wanafukuzwa kortini.maana wanaongea upuuzi tu,na utasikia wanajiita mawakili wasomi
Kuna wakili hajasoma?
 
Back
Top Bottom