Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,606
- 29,755
Julai 17 2023 Mahakama ya Rufaa ilitoa maamuzi ya rufani iliyowasilishwa na Wakili Msomi Peter Madeleka dhidi ya plea bargain iliyoingiwa kati yake na DPP. Tangu siku hiyo ya hukumu Wakili Mzalendo, Msomi Peter Madeleka yupo rumande akisubiri mchakato wa kesi yake ya msingi uanze.
Mahakama kuonesha uchungu na maumivu makubwa ya serikali kuhusu hoja za mrufani zilizoiangusha iliamua kusimama upande wa serikali ambapo ilitoa uamuzi tata wa kuamuru kesi ya msingi ianze kusikilizwa.
Maamuzi hayo yalikuja baada mrufani kuonesha ujasiri wa kuhoji na kukosoa dhamira ya mkuu wa nchi kuingia mkataba tata baina ya serikali na DP World kwa mlango wa Dubai. Jambo hilo liliwaudhi wakuu wa serikali na ndani ya Chama Tawala hivyo kwa mwenendo wa kesi hiyo ya rufaa iliamua kuhitimishwa kwa kuhakikisha Wakili Msomi Peter Madeleka ananyamazishwa kwani kesi yake ya msingi haina dhamana.
Serikali ya awamu ya sita imejipambanua wazi namna isivyoweza kulinda rasilimali zetu kwa kuamua kuzikabidhi kwa wawekezaji milele huku mikataba inayoiingia ikiwapa ulinzi na haki za kipekee wawekezJi hao.
Mara baada ya kukamatwa Peter Madeleka, jamii ya wapenda haki imepigwa na mstuko na kuamua kukaa kimya bila kupaza sauti wala kufuatilia hatima ya wakili msomi mzalendo Peter Madeleka.
NINI KIFANYIKE
- Kuiburuza serikali kwenye mahakama za kikanda na kimataifa dhidi ya sheria zinazokiuka haki za binadamu ikiwemo sheria ya makosa ya mtandao na uhujumu uchumi ambayo inawanyima watuhumiwa haki ya dhamana ambayo ni ya Kikatiba
- Kuiomba jamii yq kimataifa kukemea mwenendo wa serikali yetu kudhibiti, kukamata na kuwatesa wakosoaji wake mbalimbali.
- Wakili msomi Mwabukusi naye anatafutwa kwenye mawanda ya kisheria na soon anaweza kupewa kesi ya uhaini. Dalili zipo wazi na maandalizi yanaelekea kukamilika
- Wanasheria wazalendo wafungue kesi (PIL) Mahakama Kuu ili sheria ya kinga kwa Spika na maafisa wa usalama wa taifa ifutwe kwa sababu haiendani na Utawala Bora, Uwajibikaji na Utii kwa Katiba na Sheria za nchi.