Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
15,806
28,470
Serikali ya Rwanda imetia saini hapo jana makubaliano na shirika kutoka mataifa ya Canada na Ujerumani, ili kuanzisha ujenzi wa kinu cha nyuklia ambacho kitakuwa tayari kwa majaribio ifikapo mwaka 2026.

1694583439761.png

Ujenzi wa Kinu cha Nyuklia mjini Kurchatov, Urusi:02.11.2022

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya "Dual Fluid Energy", Goetz Ruprecht amewaambia waandishi wa habari mjini Kigali kuwa " aina mpya ya vinu hivyo, vinaweza kutumiwa kuzalisha umeme, haidrojeni na mafuta yaliyosindikwa kwa gharama ndogo kuliko mafuta ya visukuku.

Waziri wa miundombinu wa Rwanda Ernest Nsabimana amesema matumizi ya nishati ya nyuklia yatatoa chanzo thabiti na cha kuaminika cha umeme, kupunguza utegemezi wa mafuta na kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya nishati.

Nsabimana amendelea kuwa kujumuisha nyuklia katika jumla ya vyanzo vya nishati kutapelekea kuwa na aina mbalimbali za vyanzo vya nishati, kuimarisha usalama wa nishati na kupunguza hatari ya uhaba wa usambazaji.

Awali mnamo mwaka 2019, Rwanda ilitia saini mkataba wa kuanzisha vinu vya nyuklia kwa ushirikiano na wakala wa nyuklia wa Urusi "Rosatom", jambo lililozusha upinzani mkali hasa kuhusu hatari zinazohusiana na masuala ya kiusalama.

1694583713391.png

Rais wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha "Democratic Green Party of Rwanda", Frank Habineza, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa makubaliano kati ya serikali na Kampuni ya "Dual Fluid Energy" ni hatari na kwamba hayana tofauti kubwa na makubaliano ya mwaka 2019 kati ya serikali ya Kigali na wakala wa nyuklia kutoka Urusi.

Habineza amesisitiza : " Hakuna utafiti unaoweza kunishawishi kuwa kuna mahali katika nchi hii (Rwanda) ambapo kinu cha nyuklia kinaweza kujengwa bila kuyaweka maisha ya watu hatarini.

Bodi ya Nishati ya Atomiki ya Rwanda ikishirikiana na Kampuni hiyo wamebaini kuwa miradi yao ni salama na wala si tishio kwa watu au mazingira. Katika taarifa yao ya pamoja wameeleza: " Kinu chetu cha majaribio ni kifaa kidogo chenye chembechembe ndogo za mionzi. Kwa sababu hii, maradi huu si tishio kwa mazingira."

Taarifa hiyo imeendelea kwa kusema: " Kwa mfano, hata ikitokea mripuko kwenye kinu hicho au kwenye jengo lenyewe, basi ni kiwango kidogo mno cha mionzi ndicho kitakachotawanyika."

Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyo na mpango wa nyuklia wa kiraia, na vinu vyake viwili vimekuwa vikifanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 na kuzalisha megawati 1,860 za umeme, ikiwa ni sawa na karibu 4% ya nishati yote inayozalishwa nchini humo.
 
Rwanda yatia saini makataba na kampuni ya Kanada-Ujerumani kujenga kinu cha cha umeme wa nyuklia.

Rwanda itaunda kinu cha majaribio ya nyuklia kwa kutumia teknolojia mpya chini ya makubaliano kati ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kampuni ya Kanada na Ujerumani iitwayo Dual Fluid Energy Inc.

Kinu hicho kitatumia mbinu iliyobuniwa na kampuni mpya kwa kutumia mafuta ya kioevu na kipozezi cha lead, na hivyo kuzalisha uchafu mdogo wa mionzi.

Kinu icho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo 2026 na majaribio ya baadaye ya teknolojia ya Dual Fluid yatakamilika ifikapo 2028.

Awamu ya majaribio itagharimu euro milioni 70, zitakazofadhiliwa na kampuni iyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Dual Fluid alisema.
 
Kinu cha nyuklia sio kuchoma mkaa kiongozi! Angalia vinu vyote vya nyuklia
Mazingira vilipojengwa! Ni karibu na bahari au open space kubwa kiwezesha mfumo wa upoozeshaji na kukabiliana na majanga! Nchi masikini na yenye uhaba wa ardhi kama Rwanda technically impossible! Ni kujimwambafai na kujitutumua
 
Much big up, tutabaki na kelele za bandari, katiba, bila faida yoyote, watanzania tu sometime tunaupofu kabisa, kila kiumbe bandari, ngorongoro😁😁😁
Kwanza mi ningekuwa rais, TEC nimeshafuta siku nyingi mana wapo kutetea maslahi Yao tu na kuwapa waumini mizigo ya bahasha za mtoto yesu tu wao wanakula mayai daily. Unyonyoji tu
 
Huwezi kufuta Taasisi ya Vatican

Kanisa Moja Takatifu la Mitume 😀
 
Huwezi kufuta Taasisi ya Vatican

Kanisa Moja Takatifu la Mitume 😀
Kanisa moja la kishetani. Kanisa Gani la matabaka wakati Mungu anasema watu wote ni sawa. Mapadre au maaskofu ni kama mungu kanisani ndo mana waumini wanakamuliwa tu wao kazi Yao ni kula na kuhonga na kiwajengea vimada wao tu. Dini ni uislamu ambao hakuna matabaka ya kinyonyaji hata shekhe anaambiwa awe na kazi yake ya kumuingizia kipato ndo awe shehe
 
Kwanza mi ningekuwa rais, TEC nimeshafuta siku nyingi mana wapo kutetea maslahi Yao tu na kuwapa waumini mizigo ya bahasha za mtoto yesu tu wao wanakula mayai daily. Unyonyoji tu
Unazani ni jambo rahisi hivyo unaongea tu kama mtu wa elimu ya darasa la saba na kazi yako kuchunga ng'ombe huna unalolijua zaidi ya kuendeshwa na mihemko
 
Rwanda yatia saini makataba na kampuni ya Kanada-Ujerumani kujenga kinu cha cha umeme wa nyuklia.

Rwanda itaunda kinu cha majaribio ya nyuklia kwa kutumia teknolojia mpya chini ya makubaliano kati ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki na kampuni ya Kanada na Ujerumani iitwayo Dual Fluid Energy Inc.

Kinu hicho kitatumia mbinu iliyobuniwa na kampuni mpya kwa kutumia mafuta ya kioevu na kipozezi cha lead, na hivyo kuzalisha uchafu mdogo wa mionzi.

Kinu icho kinatarajiwa kuanza kufanya kazi ifikapo 2026 na majaribio ya baadaye ya teknolojia ya Dual Fluid yatakamilika ifikapo 2028.

Awamu ya majaribio itagharimu euro milioni 70, zitakazofadhiliwa na kampuni iyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Dual Fluid alisema.

Megawatts ngapi?
 
Kila mara nikisikia Kabobo za Bi Tozo nachoka kabisa. Rwanda ni nchi ndogo sana na haina Rasilimali za kutosha kuishinda Tanzania 🇹🇿. Lakini kimaendeleo inaonekana Rwanda inapiga hatua kubwa sana kila kukicha. Hata majirani zetu Kenya japo kila siku wanagombana (civil war 2007), kuandamana mixture ukabila na kutokuwa na rasilimali kutushinda bado hatuwafikii au kuwapita.

View: https://www.instagram.com/p/CxIWgTarVGu/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Wiki hii Nchi ya Rwanda imetia Saini ya kuanza kutengeneza Vinu vya Nyuklia (Jamaa mmoja akanidokeza eti vya kuwapigia Utopolo wakifika Rwanda), utani tu. Bongo bado tuko kwenye Vichambo vya wanasiasa kwamba hatujui kusoma katiba. Ni bora Magufuli angebaki uenda tungeona maendeleo ya maana kuliko hawa walioingia na kelele za mama kafungua Nchi, nchi gani mafuta yanakosekana, Dollar imekimbia kurudi kwao, maji na umeme wa mgao. Filamu ya Royal Tour imeleta athara tu, ingekuwa imeleta faida tungeona wazungu plus Dollars zikimiminika, tunazidiwa na Rwanda ambayo juzi kati Wameazimisha sherehe za kuwapa Sokwe majina ambayo imehudhuriwa na kina Kelvin Heart, Idris Elba na watu wengi mashuhuri wa Duniani, bado tunaona Visit Rwanda kwenye matangazo ya timu kubwa za mpira Duniani.

Bongo Nyoooosoooo
 
Serikali ya Rwanda imetia saini hapo jana makubaliano na shirika kutoka mataifa ya Canada na Ujerumani, ili kuanzisha ujenzi wa kinu cha nyuklia ambacho kitakuwa tayari kwa majaribio ifikapo mwaka 2026.

View attachment 2747498
Ujenzi wa Kinu cha Nyuklia mjini Kurchatov, Urusi:02.11.2022

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya "Dual Fluid Energy", Goetz Ruprecht amewaambia waandishi wa habari mjini Kigali kuwa " aina mpya ya vinu hivyo, vinaweza kutumiwa kuzalisha umeme, haidrojeni na mafuta yaliyosindikwa kwa gharama ndogo kuliko mafuta ya visukuku.

Waziri wa miundombinu wa Rwanda Ernest Nsabimana amesema matumizi ya nishati ya nyuklia yatatoa chanzo thabiti na cha kuaminika cha umeme, kupunguza utegemezi wa mafuta na kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya nishati.

Nsabimana amendelea kuwa kujumuisha nyuklia katika jumla ya vyanzo vya nishati kutapelekea kuwa na aina mbalimbali za vyanzo vya nishati, kuimarisha usalama wa nishati na kupunguza hatari ya uhaba wa usambazaji.

Awali mnamo mwaka 2019, Rwanda ilitia saini mkataba wa kuanzisha vinu vya nyuklia kwa ushirikiano na wakala wa nyuklia wa Urusi "Rosatom", jambo lililozusha upinzani mkali hasa kuhusu hatari zinazohusiana na masuala ya kiusalama.

View attachment 2747502

Rais wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha "Democratic Green Party of Rwanda", Frank Habineza, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa makubaliano kati ya serikali na Kampuni ya "Dual Fluid Energy" ni hatari na kwamba hayana tofauti kubwa na makubaliano ya mwaka 2019 kati ya serikali ya Kigali na wakala wa nyuklia kutoka Urusi.

Habineza amesisitiza : " Hakuna utafiti unaoweza kunishawishi kuwa kuna mahali katika nchi hii (Rwanda) ambapo kinu cha nyuklia kinaweza kujengwa bila kuyaweka maisha ya watu hatarini.

Bodi ya Nishati ya Atomiki ya Rwanda ikishirikiana na Kampuni hiyo wamebaini kuwa miradi yao ni salama na wala si tishio kwa watu au mazingira. Katika taarifa yao ya pamoja wameeleza: " Kinu chetu cha majaribio ni kifaa kidogo chenye chembechembe ndogo za mionzi. Kwa sababu hii, maradi huu si tishio kwa mazingira."

Taarifa hiyo imeendelea kwa kusema: " Kwa mfano, hata ikitokea mripuko kwenye kinu hicho au kwenye jengo lenyewe, basi ni kiwango kidogo mno cha mionzi ndicho kitakachotawanyika."

Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyo na mpango wa nyuklia wa kiraia, na vinu vyake viwili vimekuwa vikifanya kazi kwa zaidi ya miaka 30 na kuzalisha megawati 1,860 za umeme, ikiwa ni sawa na karibu 4% ya nishati yote inayozalishwa nchini humo.
Haya ndo maneno ya kibabe
 
Back
Top Bottom