Japan yapuuza maslahi ya nchi nyingine kwa mpango wake wa kutupa maji machafu ya nyuklia baharini

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111393657916.jpg
Kampuni ya Umeme ya Tokyo ya Japan hivi karibuni imeanza kazi ya majaribio ya mitambo ya kupeleka maji machafu ya nyuklia baharini. Baada ya kumalizika kwa majaribio hayo, Japan inatarajia kuanza rasmi mpango wake wa kutupa maji machafu ya nyukilia kwenye bahari ya Pasifiki.

Mwaka 2011, tetemeko kubwa la ardhi na tsunami iliyotokana na tetemiko hilo vilisababisha uvujaji wa nyuklia kwenye Kiwanda cha Umeme cha Nyuklia cha Fukushima nchini Japana. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ambayo inamiliki kiwanda hicho, imehifadhi mamilioni ya tani za maji yenye mionzi yanayotumiwa kupoza mitambo ya nyukilia. Mwaka 2021, serikali ya Japan ilitangaza kwamba itamwaga maji hayo baharini, ikidai kuwa maji hayo hayataleta athari kwa baharini. Hata hivyo, hadi sasa Japan imeshindwa kuthibitisha kuwa maji hayo ni salama kwa mazingira ya bahari.

Tangu kutokea kwa ajali ya kuvuja kwa nyuklia katika Kiwanda cha Umeme cha Fukushima, athari za uchafuzi wa nyuklia zimezidi kuonekana. Viumbe wengi waliobadilika wamegunduliwa nchini Japani, wakiwemo pweza wenye mikia tisa, sungura wasio na masikio, na vipepeo wa kijivu wenye mabawa yaliyobadilika. Hivi majuzi, samaki wa baharini waliovuliwa katika bandari karibu na kinu cha nyuklia cha kiwanda hicho walipatikana kuwa na Cesium yenye mionzi ambayo kiwango chake ni mara 180 kuliko kile cha kawaida.

Kutupa uchafuzi wa nyuklia baharini bila shaka kutaeneza mionzi kwa dunia yote. Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Ujerumani ilisema kwamba, pwani ya Fukushima ina mikondo ya bahari yenye nguvu zaidi duniani. Ndani ya siku 57 baada ya kutupa maji machafu ya kinyukilia baharini, mionzi itaenea katika sehemu kubwa ya Bahari ya Pasifiki, na miaka 10 baadaye, itaenea katika bahari zote duniani. Wataalamu wa nyuklia wa Greenpeace walisema kwamba, kaboni iliyo katika maji machafu ya nyuklia ya Japan ina hatari itakayoendelea kwa maelfu ya miaka, na inaweza kusababisha uharibifu wa jeni ya viumbe.

Mpango huu wa Japan kwanza umepingwa na nchi jirani zake. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, kutupa maji machafu ya nyuklia baharini kutaharibu mazingira ya bahari duniani na afya ya watu wa nchi nyingine. Korea Kusini iko karibu sana na Japan. Baada ya Japan kuanza majaribio ya utupaji wa maji taka ya nyuklia, watu wa Korea Kusini wamenunua chumvi nyingi, wakiwa na wasiwasi mkubwa kwamba, maji machafu ya nyuklia ya Japan yatasababisha upungufu wa chumi. Kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia cha Korea Kusini Lee Jae-myung, alitaja mpango huo wa Japan ni “kitendo cha ugaidi wa mionzi”, na kusisitiza kwamba asilimia 85 ya Wakorea Kusini wanapinga Japani kufanya hivyo.

Mpango wa Japan pia umepingwa vikali na nchi za visiwa vya Pasifiki. Katibu Mkuu wa Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki Henry Puna anaamini kwamba mpango huo wa Japana “utafungua sanduku la Pandora”, na haipaswi kusubiri miongo kadhaa kuelewa athari za mpango huo kwa Pasifiki. Kulingana na takwimu, nusu ya samaki aina ya tuna duniani huzalishwa na nchi za visiwa vya Pasifiki. Utupaji wa maji machafu ya nyuklia unaweza kuwa na athari mbaya kwa uvuvi ambao unategemewa sana kwa uchumi wa nchi hizo. Aidha, kitu kibaya zaidi ni kwamba, uhai wa binadamu, wanyama na mimea katika nchi za visiwa vya Pasifiki unategemea sana ikolojia ya baharini. Ikiwa maji machafu ya nyuklia yataharibu mazingira ya bahari ya Pasifiki na kusababisha majanga ya kiikolojia, wakazi wa nchi hizo watalazimishwa kuondoka majumbani mwao.

Kutupa taka chafu za nyuklia baharini sio chaguo pekee kwa Japan. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ilikuwa na mipango mingine, ikiwemo kuweka matangi zaidi ya kuhifadhi maji machafu, kuanzisha maeneo mengine ya kuhifadhi maji hayo, na kuingiza maji hayo ardhini. Lakini ikilinganishwa njia nyingine, gharama za kutupa maji hayo baharini moja kwa moja ni ndogo zaidi. Japan, ikiwa nchi ya tatu kwa uchumi duniani, kitendo hiki ni cha kibinafsi na kutowajibika.
 
Niliona kwenye taariofa za habari za vyombo vya nnje hawaja jamaa walionyesha walivyo yatibu hayo maji na watu wa mazingira ya Baharini na Nchi kavu walikuwa wanafwatilia mchakato mzima wakati wa usafishaji wa maji hayo, sasa sijajua nao hawakujuwa au wana funika kombe haslafu kesho waje na Miradi ya kusafisha bahari?
 
View attachment 2661937Kampuni ya Umeme ya Tokyo ya Japan hivi karibuni imeanza kazi ya majaribio ya mitambo ya kupeleka maji machafu ya nyuklia baharini. Baada ya kumalizika kwa majaribio hayo, Japan inatarajia kuanza rasmi mpango wake wa kutupa maji machafu ya nyukilia kwenye bahari ya Pasifiki.

Mwaka 2011, tetemeko kubwa la ardhi na tsunami iliyotokana na tetemiko hilo vilisababisha uvujaji wa nyuklia kwenye Kiwanda cha Umeme cha Nyuklia cha Fukushima nchini Japana. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ambayo inamiliki kiwanda hicho, imehifadhi mamilioni ya tani za maji yenye mionzi yanayotumiwa kupoza mitambo ya nyukilia. Mwaka 2021, serikali ya Japan ilitangaza kwamba itamwaga maji hayo baharini, ikidai kuwa maji hayo hayataleta athari kwa baharini. Hata hivyo, hadi sasa Japan imeshindwa kuthibitisha kuwa maji hayo ni salama kwa mazingira ya bahari.

Tangu kutokea kwa ajali ya kuvuja kwa nyuklia katika Kiwanda cha Umeme cha Fukushima, athari za uchafuzi wa nyuklia zimezidi kuonekana. Viumbe wengi waliobadilika wamegunduliwa nchini Japani, wakiwemo pweza wenye mikia tisa, sungura wasio na masikio, na vipepeo wa kijivu wenye mabawa yaliyobadilika. Hivi majuzi, samaki wa baharini waliovuliwa katika bandari karibu na kinu cha nyuklia cha kiwanda hicho walipatikana kuwa na Cesium yenye mionzi ambayo kiwango chake ni mara 180 kuliko kile cha kawaida.

Kutupa uchafuzi wa nyuklia baharini bila shaka kutaeneza mionzi kwa dunia yote. Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Ujerumani ilisema kwamba, pwani ya Fukushima ina mikondo ya bahari yenye nguvu zaidi duniani. Ndani ya siku 57 baada ya kutupa maji machafu ya kinyukilia baharini, mionzi itaenea katika sehemu kubwa ya Bahari ya Pasifiki, na miaka 10 baadaye, itaenea katika bahari zote duniani. Wataalamu wa nyuklia wa Greenpeace walisema kwamba, kaboni iliyo katika maji machafu ya nyuklia ya Japan ina hatari itakayoendelea kwa maelfu ya miaka, na inaweza kusababisha uharibifu wa jeni ya viumbe.

Mpango huu wa Japan kwanza umepingwa na nchi jirani zake. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema, kutupa maji machafu ya nyuklia baharini kutaharibu mazingira ya bahari duniani na afya ya watu wa nchi nyingine. Korea Kusini iko karibu sana na Japan. Baada ya Japan kuanza majaribio ya utupaji wa maji taka ya nyuklia, watu wa Korea Kusini wamenunua chumvi nyingi, wakiwa na wasiwasi mkubwa kwamba, maji machafu ya nyuklia ya Japan yatasababisha upungufu wa chumi. Kiongozi wa Chama cha Kidemokrasia cha Korea Kusini Lee Jae-myung, alitaja mpango huo wa Japan ni “kitendo cha ugaidi wa mionzi”, na kusisitiza kwamba asilimia 85 ya Wakorea Kusini wanapinga Japani kufanya hivyo.

Mpango wa Japan pia umepingwa vikali na nchi za visiwa vya Pasifiki. Katibu Mkuu wa Jukwaa la Visiwa vya Pasifiki Henry Puna anaamini kwamba mpango huo wa Japana “utafungua sanduku la Pandora”, na haipaswi kusubiri miongo kadhaa kuelewa athari za mpango huo kwa Pasifiki. Kulingana na takwimu, nusu ya samaki aina ya tuna duniani huzalishwa na nchi za visiwa vya Pasifiki. Utupaji wa maji machafu ya nyuklia unaweza kuwa na athari mbaya kwa uvuvi ambao unategemewa sana kwa uchumi wa nchi hizo. Aidha, kitu kibaya zaidi ni kwamba, uhai wa binadamu, wanyama na mimea katika nchi za visiwa vya Pasifiki unategemea sana ikolojia ya baharini. Ikiwa maji machafu ya nyuklia yataharibu mazingira ya bahari ya Pasifiki na kusababisha majanga ya kiikolojia, wakazi wa nchi hizo watalazimishwa kuondoka majumbani mwao.

Kutupa taka chafu za nyuklia baharini sio chaguo pekee kwa Japan. Kampuni ya Umeme ya Tokyo ilikuwa na mipango mingine, ikiwemo kuweka matangi zaidi ya kuhifadhi maji machafu, kuanzisha maeneo mengine ya kuhifadhi maji hayo, na kuingiza maji hayo ardhini. Lakini ikilinganishwa njia nyingine, gharama za kutupa maji hayo baharini moja kwa moja ni ndogo zaidi. Japan, ikiwa nchi ya tatu kwa uchumi duniani, kitendo hiki ni cha kibinafsi na kutowajibika.

Hizi nazo ni Propaganda
 
Back
Top Bottom