gstar
JF-Expert Member
- Jun 19, 2011
- 759
- 1,250
Hivi karibuni nchi ya Rwanda imesaini mkataba wakuiwezesha kuunda kinu cha kufua nguvu za nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme. Ikumbukwe kwamba kinu cha nyuklia cha kuzalisha umeme pia kinaweza kutumika kuzalisha silaha hatari za kivita za nyuklia.
Hii ni hatari kwa nchi zinayoizunguka ikiwemo Tanzania ambazo zinaweza kuingia kwenye tatizo la kiusalama kwa siku zijazo. Viongozi wa Umoja wa Afrika Mashariki ni vyema wakakutana ili kuliweka sawa jambo hilo, hata hivyo sioni kwamba ni busara kukaa kimya.
Inafaa maelezo ya kina kutolewa kutoka serikali ya Rwanda ukiachilia kwamba nchi hii imesha wahi kushutumiwa kufadhili uasi kwenye nchi ya Kongo, hivyo wasije kutumia mbinu hiyo ili kujiimarisha kiulinzi kwa kuzalisha mabomu ya nyuklia.
Taarifa ya Reuters kwenye komenti ya kwanza.