Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Hakika kuna nyakati ngumu! Nasikia utu wangu wa ndani ukilia sana; Mungu awatie nguvu wazazi wake, ndg, jamaa, viongozi wa cdm; na watz wote.
Mungu tunaomba umpumzishe kwa amani, ameni
 
Hii gari ni balaa,haifai kabisa kujifundishia hasa huku mkono mmoja unapost kwenye JF.Baadhi ya kampuni za bima wanakwepa kuziwekea bima kwa vile uwezekano wa ajali ni mkubwa.
Hata hivyo nasema InnaLILLAAH WA INNA ILAIHI RAAJIUUN.

nani aliyekuambia mkono mmoja ulikuwa unapost JF?
 
Naona dady unaanza kuwa Tomaso...Pole na msiba.

Ahsante mama pole nawe pia.

Si mambo ya utomaso, nimetumia uzoefu tu wa barabarani baada ya kuona hiyo picha ya gari iliyopata ajali, ndipo nikajiridhisha kwamba haikuwa ajali ya kugongana na gari nyingine, inaonekana ilipinduka.
 
Nami naomba kuungana na wana JF wote kutoa pole kwetu sote tulioguswa na kifo hiki ch ghafla cha kamanda wetu Mh. Regia Mtema (RIP) Kweli imenisikitisha sana sana,
 
Kwahiyo wasabato hawafi siku ya sabato? Acha masihala bwana. Mungu agenda zake hapangi na binadamu wa aina yoyote. Anapanga jinsi inavyompendeza.

Masihara Gani! wacha kuniwekea maneno mdomoni au hujaelewa Kilichoandikwa? hapo
 
RIP Regia Mtema
Pumzika kwa amani ndilo naweza kusema kwa sasa .
 
nashndwa hata nitamke neno gan kuonesha my sympathy...nwey, RIP beloved one. May the almighty rest ur beautful soul in eternal life. WE LOVED N U CCTA.
 
Sikuwahi kumjua Regia binafsi, sikuwahi kukutana naye, na wala sikuwahi kuongea naye, lakini nilipenda uwezo wake wa kujenga hoja, nilipenda alivyokuwa na nia ya dhati kuwatetea wanyonge wa nchi hii, nilipenda mtizamo wake kwenye mambo ya taifa letu. She has gone too soon, but she lived her life well; A life well lived is a life to be treasured; we mourn your death since you have gone too soon, but we also celebrate your life Regia, we will remember you... May your soul rest in eternal peace Regia.

Kiranga upo?
 
Nalia nalia nalia...umeniachia deni kubwa sana!!!! Kuna kitu uliniuliza hapa ofisini ili nikupe data kamili bt nilikuwa nakuzungusha kila siku! Regia pumzika kwa amani!
Kama hicho kitu kinahusu maslahi ya taifa unaweza kulitua hilo deni kwa kupeleka hizo data kamili kwa mmojawapo wa hawa; Lissu, Zitto, Lema, Mnyika, Mbowe au Dr. Slaa.... Be brave and do it now before its too late.
 
she didnt live to see true independence,but regia,i tell you this,.come 2015 you will be smiling from heaven,we will make you proud,.in ash we came in ash we shall return,ashes to ashes dust to dust,i hope you hear us now in god we trust.

umenitia huzuni mkuu,maneno yako yana ujumbe na hisia kali sana,Regia amesikia bila shaka.
 
The news has been so painful to me! I can not explain how sad this day has ended. Rest n Peace beloved Regia.We will miss u terribly in Tanzanian Politics
 
Rip regia,the legacy you have left behind will never be forgotten.
 
RIP- Regia

Nina hakika kabisa kuwa ajali za barabarani zinaweza kuzuilika kwa 70% kama tutasimamia sheria za barabarani kuanzia katika ujenzi mpaka kwenye ku-approve madereva. Tumuenzi Regia kwa kuzingatia sheria za barabarani kwani second moja tu yaweza kuokoa uhai au kuutoa ukiwa barabarani.

Funga mkanda, hakikisha haulifuatishi gari linavyotaka maana hizi automatic unaweza kuwa unakanyaga unaona kama hauendi kumbe upo kwenye 120mph.

Sitaki kusema kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa barabarani hasa kwenye masafa marefu maana sijui ameanza lini kuendesha gari na amejifunzia wapi.

Ila kwa wale wenye kumbukumbu wakati wa Rais Mwinyi aliwahi kutoa mikopo ya magari kwa maafisa wa jeshi (Hyundai-zilizokuwa na namba za TZJ...) maafisa wengi walipoteza maisha kwa ajali za barabarani

Kama tunaingia barabarani kwa mara ya kwanza kama madereva ningeshauri tujizuie na hizi route za mkoa kwa mkoa kwani kuna challenges nyingi sana barabani ambazo huhitaji maamuzi ya haraka sana na kama ni 'Pass driver' huwezi kuzishinda mpaka ukae kwa muda mrefu barabarani. Tujaribu kujiweka wenyewe katika standard za udereva kwa kuendesha at least miaka mitatu mijini tu kabla ya kuamua kusafiri wenyewe kwenda mikoani. Tutumie madereva wazoefu kwa safari hizi. Japo ni polisi ndiyo watakuwa na right information lakini mimi kwa kuangalia picha hii ya gari Looks like a 'Driving error' ndiyo iliyotufanya tumkose dada yetu kipenzi.

395649_281918401868137_100001499385296_761545_2120467546_n.jpg
 
Regia hakuumwa,ni asubuhi tu aliamka na huenda alikuwa na mipango yake ya kukamilisha kwa siku ya leo, lakini kufumba na kufumbua hatunaye tena! Tukio hili linatufundisha kuwa Maisha ya mwanadamu ni mafupi sana, tena yamejaa taabu na shida, laiti tungelijua kuwa kila dakika tunayoipitisha tukiwa hai ni muujiza wa Mungu tungeliomba msamaha wa dhambi zetu kila dakika na kuwa na amani na watu wote.........!!Mungu utuwezeshe kuzihesabu siku zetu, ili siku la kutufika likitufika tufe tukiwa mikononi mwako!!

Nawaombea ndugu wote, watanzania wote na chadema wote wawe na subira na Mungu awapatie wepesi katika kuomboleza msiba huu mzito wa dada yetu Regia.

Mbele yetu ni wewe, nyuma yako ni sisi, Mungu ametwaa kiumbe chake, kazi yake haina makosa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom