Rafiki mjane Bibi John aliyekosa msaada, nasikitika sikumzika

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
875
2,427
Salam ziwafikie JF members.

Ni mwanamke aliyebarikiwa kupata watoto 5, wakike 2 na wakiume 3. Tuliishi katika Kijiji kimoja huko katika ardhi ya Mtemi Milambo mkoa unaosifika kwa zao la tumbaku. Rafiki yangu alikua ni mtu wa karibu sana na mama yangu mzazi. Aliachwa na mumewe Toka miaka ya 90 na alisimama kama mama kuhakikisha anawalea watoto wake. Alishinda msituni kutafuta kuni na kuziuza kwa watu ili apate pesa ya kujikimu yeye na watoto wake. KIFUPI MJANE BIBI JOHN NI MFANO WA KUIGWA KWANI HAKUWATELEKEZA WATOTO ILA ALIHAKIKISHA ANAWAHUDUMIA MPAKA WALIPOFIKIA UMRI WA KUJITEGEMEA.

Siku miezi na miaka ilipita pasipo kuonana na rafiki yangu kwani kwanzia mwaka 2010 nilikuwa bize na elimu na nilikuwa nasomea mbali na kijijini kwetu. Nilikuwa napata habari zake kupitia mama yangu. Mwaka 2011 BIBI JOHN alipata ajali akiwa porini aliangukiwa na mti lakini alikuja kupona baada ya wanakijiji kumchangia pesa za matibabu. Mwaka 2013 BIBI JOHN aliangukia katika moto kwasababu alikua na kifafa, alipata majeraha mkononi na kupelekea mkono wa kushoto kushindwa kunyooka yani nyama za ngozi zilishikana. Hayo ni machache kati ya mengi alopitia BIBI JOHN.

Mwaka 2020 baada ya kumaliza chuo nilirudi nyumbani kijijini kusalimia. Jioni Moja nilienda kumtembelea rafiki yangu BIBI JOHN nyumbani kwake. BIBI JOHN aliponiona alitokwa na machozi sana namim nilishindwa kujizuia nilimkumbatia hku natokwa na machozi japo sikuwa najua nini hasa kilimfanya alie baada ya kuniona.

Rafiki yangu alinipa kiti kifupi cha mbao kilichovunjika vunjika na kuungwa kwa kamba. Tulisalimiana na akaanza kunipasha habari juu ya tabia ya watoto wake hasa wa kiume walio naye pamoja pale kijijini. Habari zile zilinisikitisha sana kwani watoto wake wa3 wakiume wote walikua pale kijijini lakini hawakuwa karibu na mama yao, walimtelekeza, hawakumpa msaada alipokuwa akipata changamoto hasa za chakula na kuugua. Hata siku Ile nilipofika kwake nilimkuta anakunywa uji ambao haukuwa na sukari. Aliniambia kwamba pale alipo ni mgonjwa na alichokipata kama msaada kutoka kwa watoto ni Panadol za mia5 nazo zililetwa na kutupwa chino pembeni ya alipokuwa amelala na kisha mtu akaondoka. Alinihadithia mengi mengi sana na kifupi nililia kwasabb kwa jinsi yule mama alivyowapambania watoto wake mpka wakafika umri ule basi hawakuwa na hata chembe ya sababu ya kumfanyie vile mama yao.

Niliingia mfukoni nikatoa kiasi flani cha pesa nikampa, asee hapa nilijikuta nalia tena maana rafiki yangu alinishukuru kwa zaidi ya dakika 10 huku anatoa machozi.

Aliniambia maneno haya..........

"MUNGU AKUBARIKI UISHI MAISHA MAREFU UWATUNZE WAZAZI NA FAMILIA YAKO, UPATE MKE MWEMA NA UZAO MWEMA, LAANA NA MIPANGO MIOVU VISIKUPATE, NAKUOMBA USINISAHAU UKISHAONDOKA NA NIKIFA UJE UNIZIKE MWANANGU"

Nisiwe muongo baada ya yale maneno ya BIBI JOHN nilijihisi mwepesi na nimezaliwa upya, nilihisi furaha sana.

BIBI JOHN nilipomuaga aliniomba niende nyumbani nichukue mfuko wa debe moja, halafu nirudi kwake. Niliporudi aliuchukua mfuko na kuingia nao ndani na kutoka na kiasi cha mpunga nilimsihi sana asifanye vile lakini alikataa na kusema niende nikoboe halafu nile wali. Niniupokea na nikafikiria kwamba BIBI JOHN anashida ya chakula si vizuri kuondoka na akiba ya chakula alichokua nacho, nikapiga hesabu nikapata jibu kuwa kile kiasi cha mpunga kina range 10k-15k basi nikazama tena mfukoni nikampa misimbazi mi3 nikamwambia hiyo ni kwa ajili ya maziwa yani awekw bili ya maziwa maana maziwa ni kitu muhimu sana kwa wazee au watu wenye umri mkubwa. Basi nikamuaga na alinisisitizia kwamba NISIMSAHAU NA AKIFA NIRUDI KUMZIKA.

Ilikuwa kwa 2022 katikati nilipata taarifa kwamba rafiki yangu BIBI JOHN amefariki dunia. Huu msiba kwangu ilikuwa mzito kwasabb nilijihisi mwenye kukosa bahati kwani nilipanga mengi makubwa kumfanyie BIBI JOHN lakini wakati uliamua. Nilishindwa kwenda KUMZIKA rafiki yangu BIBI JOHN kwasababu nilikuwa mbali sana na nilikosa ruhusa kazini na huo ndo ukawa mwisho wa BIBI JOHN rafiki yangu.

NIPENDE KUTOA USHAURI KIDOGO, PLZ TUSIWASAHAU WAZAZI WETU. HAWA WATU NI MBEGU ILOTULETA SISI DUNIANI. NO MATTER WHAT MZAZ HANINUWI NA HAKOSEI TUOMBE SANA MUNGU WAZAZI WETU WAONDOKE DUNIANI WAKIWA NA FURAHA NA RADHI NA SISI AU TUONDOKE DUNIANI TUKIWA TUKO SAWA NA WAZAZI WETU.
 
mkuu umenikumbusha mbali sana nimetokwa na machozi mie mwenyew
ilinitokea mwaka 2018 sikumzika mama mdogo wangu alinipenda sana nilikuwa mbali kikazi
 
Safi sana Mkuu,namkumbuka rafiki yangu ma kishori sijui kama mzima yule.
Mara ya mwisho nimekutana na Mwanae akaniambia Mama anakulilia,anajua uko mjini ila hujaja kumuona.
Mama alinilea yule maskini mi nilikua mpangaji tu pale kwake,ila akanigeuza mwanae.
Wanae walikua vibaka tu ni kuja kula wanaondoka kwenda kukaba.
hawana habari kabisa na mama yao
sasa sijui hela wanazoiba zinapelekwa wapi?
Ntaenda kumtafuta
 
Fanya ukamuone mkuu
 
Back
Top Bottom