IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Ooh my God, RIP REGIA,
Mhe Regia alikuwa na dada ambae alimsaidia kazi zake ndogondogo,ambae walikuwa wote nae amefariki mida hii,yeye alihamishiwa Muhimbili,idadi ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali imefikia wawili sasa.baada ya taarifa hiyo hapa nyumbani palipo na msiba watuwote walijawa na simanzi.
Regina amegusa jamii zake karibia zote ikiwa ni pamoja na Familia yake, Kanisa lake, Kijiji chake, JF, CDM, Kilombero (jimbo lake), Bunge la JMT, Tanzania... Mimi pia amenigusa kama vile ni jamaa yngu wa karibu. Hii ni kutokana na maisha yake mafupi aliyoishi kwa kuipenda jamii yake na kuitumikia kwa bidii, nguvu na maarifa yake. Bwana alitowa na Bwana ametwaa, jina la Bwana na libarikiwe.
Onyo:
(1) Maisha yetu ni mafupi
(2) Kifo hakibishi hodi
(3) Kifo hakina wakati mwafaka kwa mtu
Hivyo tuishi kwa kutegemea ulinzi kutoka kwa Mungu na mapenzi yake siku zote. Sisi pia tunaweza kuishi kwa tahadhari kadiri ya vile tunavyoweza...
Kweli ww ni mgeni wetu!
Kwani gari mpya haipati ajali? Salome Mbatia alikufa kwa ajali ya gari used? Ondoa upumbavu wako hapa, tupo kwenye majonzi. Nyinyi ndio wale mnaocheka cheka hata kwenye misiba! Lol!
Hapana mkuu alipo kuwa ana overtake alikosea timingn ghafla akaona gari mbele yake ikabidi ahame barabarani na kusababisha gari kupinduka