Regia Mtema is No More!

Regia Mtema is No More!

Status
Not open for further replies.
Inaumiza sana!Kazi ya mungu haina makosa,,,,niliahidi kumpatia vielelezo vya kero alizotuomba tumpatie katika kikao kijacho cha bunge!!!!Wakati naviandaa napata msg ya kifo!Nimeumia sana sana!Nakuombea pumziko jema huko ulikotangulia mpendwa.
 
Bwana alitoa, bwana ametwaa. Jina lake liabudiwe na ailaze mahala pema peponi roho yake regia.
 
Rest in Peace Regia. Wengi tutakukumbuka sasa.

2623635.jpg
 
Habari hii imenishitua sana na nimeiona kwa post za Mh. Heche kule facebook...Inauma sana coz I spoke with her majuzi kama sikosei na ilikuwa nionane...Lol...R.I.P Hon Mtema...
maana ya RED

RIP REGIA MTEMA
 
Rest in peace Regia. We will always remember you. You have been an inspiration to majority of people in Tanzania but i think God loved you than us. I know God has a plan on you and us and thats why he has called you to his kingdom. Its so sad but we will always live in hope....:disapointed:
 
Nilishtuka sana wakati naona habari hii kupitia TBC 1 saa 10 jioni kwakweli machozi yalinitoka. sijawahi kumfahamu huyu dada binafsi lakini kupitia JF namfeel sana.R I P Regia. Pole kwa familia
 
RIP Regia,Sikukufahamu kwa kuonana nawe lakini nilifahamu busara na hekima zako kupitia JF,hasa ulipokua ukichangia na kuanzisha maada zenye mashiko na zilizoonyesha juhudi zako katika kulikomboa taifa hili.Machozi yananitoka nionapo picha yako.
 
Wana JF wenzangu, nimestushwa na kufadhaishwa sana na kifo cha mwana wa nchi mwenzetu, mzalendo mwenzetu. Nimefahamu msiba huu wakati niko mapokezi guest hse huku Manyoni kwenye habari ITV, sikuamini!
Wapendwa, tupeane pole na tujipe moyo shujaa katangulia, sisi tutafuata.
Somo alotuachia ni hili: ingawa alikuwa nasi kipindi kifupi lkn alitumika vema kwa nchi yake na watu wake.
Sisi, tutaifanyiani na kuiachiani?
Mshumaa umezimika, giza limeingia, nuru ilioangaza, sasa imetoweka. KWAHERI REGIA MTEMA
 
Yes,
Katika siku nilizotaabika sana ni leo.

USHUHUDA:
Kwa ufupi, Regia amekuwa rafiki yangu tokea mwaka 2009, JF ikiwa ndiyo chanzo cha kufahamiana.
Ilikuwa kila akija Arusha alitutaarifu, na alisababisha sisi marafiki wa JF tukutanike pamoja naye jioni hiyo na kukaa hadi usiku tukichatt naye kwa furaha na bashasha za aina yeke...tunalikumbuka sana hilo, na ni sababu ya sisi kuomboleza kwa machungu.

Lakini sura ya mwisho akiwa hai nilikuwa Dodoma kiofisi, na yeye alikuwa Bungeni, ilikuwa tarehe 17/11/2011!
Nilimpigia nikimjulisha kuwa nipo Dom, alifurahi sana kusikia, akaniomba tuonane jioni Dodoma Hotel, ambapo katika muda tuliokubaliana nilikuta ameshafika, akiwa na Godbless Lema, na mke wa Lema...

Tuliongea mambo mengi sana, ya kisiasa, kijamii na kirafiki...tukapata kinywaji na mlo pamoja, na baadaye tuliagana pale nje ya hoteli, wao wakaingia kwenye gari iliyokuwa inaendeshwa na Lema,wakatokomea...sijamwona tena hata dakika hii!

Appreciation:
Namshukuru Mungu kuwa niliongea naye, mtu ambaye anapendwa na jamii na kuheshimika sana kwa misimamo yake na moyo usiokata tamaa!
Kwa mtizamo wangu, kazi aliyofanya inatosha kabisa, alistahili kupokewa, na nahisi alikuwa anachoka sana!...Acha apumzike.
Kama hatujaiga na kujifunza toka kwake, basi sisi ni wapumbavu!


RIP REGIA-MAXIMUM RESPECT!
 
Rest In Peace Dada Regia. Nami nilimjua pitia JF,kweli tutakukumbuka kwa ushirikiano wake kwetu sisi na alikuwa mwepesi kutujuza yale tusiyoyajua mathalan mambo ya bunge.
 
Never known this lovely lady zaidi ya hapa JF...bado siukubali ukweli kwamba she is gone.

Hapa ndipo binadamu huwa hatumwelewi Mungu.... Regia umeondoka so soon!
 
Wakuu JF hasa Mods naomba hii iwe kwenye sticky. Pili naomba mtafute utaratibu mzuri wa kuweza kutufahamisha jinsi ya kushiriki ktk huu msiba ikiwa ni pamoja na rambirambi na kumuaga huyu ahujaa wa CDM, JF na Watanzania kwa ujumla. Inakuwa vigumu kusoma post kwenye hii thread kwa kuwa inaenda kasi mno
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom