mzenjiboy
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 907
- 387
Shekhe hapa kidogo umepitikiwa siku hiyo ya Laylatil Qadir imebarikiwa kuliko miezi 1000 moja na sio siku 1000 moja.
Umeni quote mie?Shekhe hapa kidogo umepitikiwa siku hiyo ya Laylatil Qadir imebarikiwa kuliko miezi 1000 moja na sio siku 1000 moja.
Ramadhaan MubaarakRamadhan Kareem
Umeni quote mie?
Tuzidi kukumbushana mema na kukatazana mabaya.
Masaa matatu kwa siku katika mwezi wa Ramadhani yasikupite kwa thamani yoyote ile ukiyahifadhi, nayo ni masaa matatu kwa idadi ya siku za Ramadhani yanakua kwa Jumla masaa (90) nayo ni kama yafuatavyo:
Saa moja wakati wa kufuturu hakika andaa futari yako mapema na ujipe faragha kwa ajili ya dua, kwasababu mwenye kufunga wakati wa kufungua kwake ana Dua ambayo hairudi patupu, jiombee mwenyewe na vipenzi vyako na waombee maiti wa kiislamu kwasababu wanahitaji kutoka kwako Dua.
Ama jisaa la pili: Ni mwisho wa usiku jipe faragha uwe pamoja na Allah kwasababu yeye ana ita akisema nani anaomba nimpe nani anayaka msamaha nimsamehe, na uzidishe katika usiku huo kwa kumuomba Allah msamaha.
Ama jisaa la tatu: Ni kukaa kwako baada ya swala ya Alfajiri katika mahali uliposwali ukifanya adhkar mpaka jua likachomoza kwasababu ni sawa na umra na hijja iliyo kamilika.
Haya ni masaa tisaini, na kua na pupa na wakati mwengine uliobaki wote kwa kumtaja Allah, na ujiepushe na usengenyaji kwasababu unamaliza thawabu zako, na weka azma isikupite swala ya faradhi na uchukue fursa ya kutekeleza Swala za sunna, kwasababu ni siku thalathini, na niharaka iliyoje tukijipata tukisema imeisha, Allahul Mustaan!
Hata ukinuwia kueneza maneno hqta nuwia kwa ajili ya kheir, huenda Allah akakufariji kwa mazito katika mazito ya Dunia na Akhera
Na kumbuka: fanya kheir hata ukaiona ndogo vipi kwasababu hujui jema gani litakuingiza peponi
RAMADHAN MUBAARAK

Allaah akuhifadhi na akuongoze kwenye kheri zaidi.Najivunia kutoka kwenye ukristo na kuingia kwenye Uislam,lakini nilichokuwa nawauliza siku zote walimu wangu waliokuwa wananifundisha Elimu ya Dini,kwa nini wasiwaubirie watu kama wanavyofanya wa upande ule,Sababu mafundisho ya Dini ya Kiisilamu ni ya kweli kabisa,Maana wako watu wengi waliozama kwenye ujinga wa Imani na bado wanaendele kuzamishwa na mafundisho ya uongo