Ramadhan Special Thread

Hakika katika swala jepesi kabisa ni swala tano, kwasababu ni kitendo ambacho hakichukui zaidi ya dakika 10, lakini swaumu ni ngumu sana , kutokana na kushinda njaa masaa zaidi ya 13, na ni nguzo ya nne katika nguzo za uislam , lakini waislam wanaiheshimu kuliko hata swala, Allah awajalie wale wote ambao hawaswali swala 5 waweze kuswali daima.


Nawatakia ramadhani Mubarak waislam wote.
 
Usiwe ni mwenye kutaraji akhera bila ya matendo mazuri, unasema katika dunia maneno ya watu wema na unatenda matendo ya watu waovu, ukipewa hutosheki na ukinyimwa hukinai, unashindwa kushukuru kwa ulichopewa , na unataka uongezwe kwa ulichokikosa, unakataza lakini wewe hukataziki, unaamrisha lakini wewe hufanyi, unapenda watu wema lakini hufanyi matendo yao. (Imam Ally a.s katika Nahjulbalagh hikma no 150)
 
*FATAAWA* *ZA* *SWAUMU* 2⃣



Iwapo kumepambazuka asubuhi na Mtu alikuwa katika hali ya janaba, hili halitoharibu saumu yake. Yeye Mume/ Mke anaruhusiwa kuchelewesha kutekeleza ghusl(kuoga) ima ilitokana na Janaaba au imetokana na heidh au nifaas, mpaka baada ya jua kuchomoza, lakini ni bora kuharakisha kutekeleza ghusl ili mtu aweze kuswali.




Na Iwapo mwenye kufunga amelala na katika usingizi wake akaota ndoto na kutoka na manii, hili haliharibu saumu yake kulingana na maafikiano ya wanavyuoni (Ijmaa’), kwahivyo na amalize saumu yake. Kuchelewesha kuoga ghusl hakuharibu saumu ya mtu, lakini na aharakishe kutekeleza ghusl ili apate kuswali na ili Malaika wapate kumkurubia.


*imeandaliwa* *na* *Brother* *Abdillah* *Bin* *Abdallah*

_Whatsap_: *+255756549117*


_Kutoka_ _Group_; *QUR'AN* *NA* *SUNNAH*

 
Ma shaa Allah Allah akulipe kwa tanbeeh hio ni wajibu wetu kuifanyia kaz

Lakini pia nami nichukue Fursa hii kuwajuza juu ya Uzi Maalum kwa ajili ya Mafunzo ndani ya Mwezi wa Ramadhan huko tutajifunza Mengi juu ya Funga zetu na tutayajua yale yatopelekea kuharibika kwa Funga
Tembeleeni uzu huu


MASWALI MAJIBU NA MAFUNZO YAHUSUYO RAMADHAN

https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/MASWALI-MAJIBU-NA-MAFUNZO-YAHUSUYO-RAMADHAN.1257501/
MashaAllah!
Ila mkuu naona itakuwa vyema uwasiliane na mods ili huo uzi uunganishwe hapa uwe pamoja na huu nafkiri itakuwa bora zaidi, uzi ullioanzisha na huu lengo ni moja.
 
d7d887bf5fd6c62b136ca9ffeb4ae642.jpg
d7d887bf5fd6c62b136ca9ffeb4ae642.jpg
 
HOTUBA YA MTUME (SAW) KUHUSU RAMADHANI

Makala haya kwa ihsani ya : Amiraly M. H. Datoo.
Amenakili Sheikh As-Sadduq r.a. kutoka kwa Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. kutokea kwa Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kutokea kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kutokea kwa Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. kutokea Al Imam Zaynul 'Aabediin a.s. kutokea kwa Al Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kutokea Imam Amir Al-Muuminiin Al Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kutokea kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.:


Ya ayyuha-Naas (Enyi watu)! Kwa hakika Mwezi wa Allah swt umewafikieni pamoja na baraka, rehema na misamaha yake, kwani ni mwezi ulio bora kwa Allah swt, usiku na mchana wake ni bora kuliko usiku na mchana wowote mwingine, saa zake ndizo bora kabisa kuliko saa zote na ni mwezi ambamo Allah swt anakualikeni na kuwafanyeni katika watu waliokarimiwa, pumzi zenu katika Mwezi huu ni Tasbihi, na usingizi wenu humo ni ‘ibada, na ‘amali zenu humo zinakubaliwa na Dua’a zenu humo zinajibiwa na hivyo mumwombe Allah swt kwa nia safi na iliyo kweli na moyo msafi ili awajaalieni tawfiqi ya kufunga saumu na usomaji wa Qur’ani Tukufu katika mwezi huu mtukufu. Kwa hakika yeyote atakayekosa msamaha wa Allah swt katika mwezi huu ulio Adhimu basi atakuwa ni mtu asiyebahatika.

Mkumbukeni njaa na kiu cha Siku ya Qiyamah mkiwa katika hali ya njaa na kiu katika mwezi huu mtukufu, na vile vile, mutoe sadaqa zenu kwa ajili ya mafukara na masikini miongoni mwenu, muwaheshimu walio wakubwa wenu, na kuwahurumia walio wadogo miongoni mwenu na muwajaze kwa huruma zenu.

Mzihifadhi ndimi zenu na muyaweke macho yenu chini kwa yale yote yasiyoruhusiwa kutazamwa na wala msiyasikie yale yote yasiyoruhusiwa kusikilizwa, muwawie vyema mayatima ili wanapokuwa watoto wenu mayatima, nao pia watendewe mema na mumwombe Allah swt msamaha wa madhambi yenu, na mnyoosheeni Allah swt mikono yenu kwake kwa ajili ya Dua’a katika nyakati za Sala kwani ndiyo iliyo saa bora kabisa ambamo Allah swt huwatazama wanaomwabudu kwa Rehema na hujibu anapoombwa na huitikia anapoitwa.

Ya ayyuha-Naas (Enyi watu)! Kwa hakika nafsi zenu zinategemea amali zenu na muzikomboe kwa istighfar zenu, migongo yenu imelemewa kwa uzito wa madhambi yenu na hivyo mupunguze uzito wenu kwa kurefusha sujuda zenu na mujue kuwa Allah swt ametamka kwa kula kiapo cha Ukuu Wake kwa kutowaadhibu wanaosali na wanaosujudu na kutowatishia moto Siku ya Qiyamah, ambamo watu watakuwa wamesimama mbele ya Mola wao.

Ya ayyuha-Naas (Enyi watu)! Miongoni mwenu atakayemfuturisha aliyefunga saumu katika funga za Mwezi huu Mtukufu basi ni sawa na kupata thawabu za kumpatia uhuru mtumwa mmoja na kupatiwa msamaha wa madhambi yaliyopita.”

Masahaba walisema: “Ewe Mtume Mtukufu s.a.w.w.! Si wote tulio na uwezo huo.” Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alijibu: “Jiepusheni na moto wa Jahannam hata kwa kulisha kipande cha tende au hata kwa kunywisha maji. Kwa hakika Allah swt hupendezewa na hulipa mema kwa atendaye hivyo hata kama hatakuwa na zaidi. ”

Ya ayyuha-Naas (Enyi watu)! Yeyote atakayezirekebisha tabia zake basi Allah swt atamfanyia wepesi upitishio wake siku ya Qiyamah juu ya Siraat ambapo miguu ya wengineo ikitetemeka, na yeyote yule atakayewafanyisha kazi kidogo wamfanyakazi wake siku hizi za funga, basi Allah swt pia atamfanyia wepesi hisabu yake Siku ya Qiyamah, na yeyote yule atakayeziepusha shari zake kwa watu, basi Allah swt atamwepusha na ghadhabu Zake, na yeyote atakayewakirimu mayatima basi Allah swt atamkirimu Siku ya Qiyamah na yeyote atakayewatendea mema ndugu na jamaa zake basi Allah swt atamjaalia Rehema Zake Siku ya Qiyamah.

Na yeyote atakayevunja uhusiano wake pamoja na jamaa na ndugu zake, basi Allah swt pia atauvunja uhusiano wake pamoja mtu huyo. Na atakayesali Sala za Sunnah katika mwezi huu Mtukufu, basi Allah swt atamwepusha na moto wa Jahannam na yeyote yule atakayetimiza Sala zake zilizo Wajib basi atalipwa usawa wa Sala sabini kuliko miezi mingine, na huyo atakuwa na uzito wa mizani kuliko watu wengine watakao kuwa na uzito hafifu wa mizani katika Siku hiyo, na yeyote yule atakayesoma hata Ayah moja ya Qur’ani Tukufu katika Mwezi huu Mtukufu, basi atapata thawabu za kuhitimu Qur’ani kamili, zaidi kuliko miezi mingine.

Ya ayyuha-Naas (Enyi watu)! Kwa hakika milango ya Jannat (Peponi) ipo wazi katika mwezi huu Mtukufu, hivyo mwombeni Allah swt kuwa milango hiyo isifungwe kwa ajili yenu, na vile vile milango ya Jahannam (Motoni) ipo imefungwa katika mwezi huu Mtukufu, hivyo mwombeni Allah swt kuwa milango hiyo isifunguliwe kwa ajili yenu. Na Mashetani wamefungwa kwa minyororo katika mwezi huu Mtukufu, na hivyo mumwombe Allah swt kuwa hao Mashetani wasiwasaliti ………!”

Ndugu msomaji, unaombwa kuwasomea Surah al-Fatihah na Sura al-Ikhlaas (Qul-Huwallahu Ahad …) mara tatu kwa ajili ya thawabu za marehemu wote
 
Mashaallah, leo katika msikiti wangu wakitaa ulijaa hadi safu zamwisho, wakati tulikuwa tunaswali swafu mbili hadi tatu. Nawaombea kwa Allah awajalie waendelee na ibada hawa ndugu zetu hata baada ya ramadhani.


Ramadhani Mubarak.
Inshallah
 
Mashaallah, yaani tungekuwa tunafanya ibada waislam siku zote kama mwezi wa ramadhani, tungekuwa mbali sana kiuchumi, kidini na kimaendeleo, Allah wafanyie umma wako wepesi wawezi kuzinduka.

Ramadhan kareem.
Swadakta mkuu
Umesema kweli ushahidi wa hadithi ya Mtume (saw) pia upo
''kama waumini wangeamini vile haswa inavyotakiwa waamini,basi Allah (sw) angewaruzuku kama ndege ambao hutoka ndani ya viota vyao asubuhi hali ya kuwa wana njaa na hurudi jioni wameshiba''
ugumu wa maisha na mabalaa yanayotupata maishani, bila shaka, mara nyingi husababishwa na maasi,maovu na kumsahau kwetu Mungu (s.w)
 
Back
Top Bottom