*
KUFUNGA RAMADHANI BILA KUSWALI SWALA TANO
*
HAKUNA 'Amaal yoyote inayopokelewa kwa Allaah ikiwa mtu hafanyi ibada ya Swala, iwe Funga, Zakah, Hajj au Sadaka au chochote kile katika ibada
Kuacha kusali unaingia katika Kufru
Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:
*"Kati ya mwanadamu na kuingia kwake kwenye shirki na kufru ni kuacha Kuswali".*
[Imaam Muslim
]
ALLAAH Aliyetukuka Amesema katika Qur-aan:
*"Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi yaliyo tawanyika".*
[Suratil Furqaan : 23
]
Imekuja Hadiyth kutoka kwa Imaam Bukhaary kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:
*"Mwenye kuacha sala ya 'Asr matendo yake yameharibika".*
[Imaam Bukhaary
]
Maana yake matendo ya mtu huyo hayapokelewi na Allaah.
Mtu asiyeswali Allaah hapokei vitendo vyake na matendo yake mema hayamsaidii chochote ikiwa hatimizi Swala Tano.
Katika swala la kuacha Swala kuna watu wa aina mbili ;
Kuacha kabisa siku zote Yaani *"Taariq Swalaa"* maarufu
Na kuacha sala baadhi ya vipindi, nyakati na siku.
*
KAULI ZA WANAZUONI*
1. Wa mwanzo ambaye haswali kabisa kaacha hakuna anachofanya katika Swala huyu kaingia katika KUFRU/UKAFIRI kwa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam)
2. Na huyu wa pili anayeacha baadhi ya Swala na nyakati, siku ambayo ameacha Swala zake matendo ya siku hiyo hayapokelewi.
Ibn Qayyim Al jawziyyah (Allaah Amrehem) alisema:
_"Wale wanaoacha Swala baadhi ya masiku, matendo yao masiku hayo hayakubaliki, hakuna jambo linalopokelewa kwa Allaah ikiwa mtu kaacha Swalaa"_
[Kitab Al salaa ukurasa wa 65
]
KUACHA KUSWALI NA MTU ANAFUNGA anajishindisha NJAA MCHANA wa RAMADHANI
Sheiykh Swaaleh Al 'Uthaymeen (Allaah Amrehem) alisema:
_"Ikiwa mtu anafunga na hali ya kuwa haswali, Funga haipokelewi na haikubaliki kwani mwenye kuacha kuswali ni kaafir na murtadi kwani ALLAAH (Aliyetukuka) Anasema:_
*"Basi wakitubu na wakashika Swala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini"....*
[Suratul Tawbah : 11
]
Pia Mtume (Swalla Allaahu 'aleyhi wasalam) alisema:
*"Tofauti yetu na wao (mushrik) ni kuacha swala na atakaewachau sala ni kaafir".*
[Imaam Tirmidh
] na imesahihishwa na Sheikh Albaani (Allaah Amrehem).
[FATAWA AL SWIYAAM ukurasa 87
]
*UZINDUSHI
*
Tunaishi na jamii ya watu ambao wao wanajua Swawm (Funga) maana yake ni kuacha kula na kinywa mchana tu, KUWSALI HAKUMUUSU na tunao majumbani au hata wewe unaesoma ujumbe huu kama una tabia hii iache na badilika, fahamu kuwa Funga yako haipokelewi bila ya kuswali.
Kwa kifupi hakuna kinachopokelewa mbele ya Allaah ikiwa mja hafanyi ibada ya swala hili lieleweke vizuri.
Allaah Alete hidaaya mioyoni mwao na mioyoni mwetu.
Allaahumma Aamiyn!!
Na ALLAAH Anajua zaidi.