Ramadhan Special Thread
Utangulizi Wa Tarjama Ya Alhidaaya.com
000-Utangulizi Wa Tarjama Ya Alhidaaya.com



Utangulizi Wa Tarjama Ya Maana Ya Al-Qur-aan Al-‘Adhiwym



Alhidaaya.com





بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ







Himdi zote Anastahiki Allaah (سبحانه وتعالى) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba zake (رضي الله عنهم) na wote waliowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya Mwisho.



Qur-aan ni Maneno Matukufu ya Allaah Aliyoteremshiwa Nabiy wa mwisho Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) yenye kusadikisha yale yaliyokuja kabla yake katika Vitabu vilivyotangulia, na ni Maneno yasiyoweza kufikiwa na upotofu mbele yake wala nyuma yake kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):



لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ﴿٤٢﴾

“Hakitokifikia ubatili mbele yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.”[1]





Pia Qur-aan ni Kitabu cha mwisho chenye Risala (Ujumbe) kwa viumbe wote kutoka kwa Rabb wa walimwengu, kwa lengo la kuwaongoza viumbe kwenye njia iliyonyooka; na ni Mwongozo, Rahmah na Shifaa kwa Waumini.





Pia Qur-aan ni muujiza wa pekee, na wakati huo huo ni changamoto kwa viumbe wote. Hata kama viumbe vyote vitashirikiana ili vilete mfano wa Qur-aan basi havitoweza kuleta mfano wake; katika ufasaha wake, hukumu zake, ilimu zake, mwongozo wake na yote iliyoyaelezea.[2]





Qur-aan imekusanya yale yote yenye kuhitajiwa na viumbe; yawe ya dunia au ya Aakhirah yao, zikiwemo khabari za kabla yao na khabari za baada yao, na ni muamuzi na hakimu kwa Waumini wake, na ni Kitabu Alichohitimishia Allaah Sharia Zake.





Ni katika desturi Zake Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa kila Rasuli akitumwa huwa anapelekwa kwa lugha ya watu wake ili aweze kuwafikishia ujumbe. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:



وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ

“Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (Risala).”[3]





Ni jambo lenye kujulikana kuwa lugha ya Quraysh ambayo ni lugha ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), ilikuwa ni Kiarabu sanifu. Na kwa sababu hiyo, ujumbe uliokuja ndani ya Qur-aan ulikuja katika lugha ya Kiarabu, ambayo ndiyo lugha fasaha kuliko lugha zote.[4]





Usomaji wa Qur-aan katika lugha yake, kwa walengwa wake wengi wasiokuwa Waarabu ambao hawakuafikishwa kuisoma lugha ya Kiarabu na kuifahamu vizuri, haswa Qur-aan na taaluma zake, haukuweza kuwafikisha kufahamu misingi ya Dini yao, hivyo basi, ndio pakawa na haja na umuhimu mkubwa wa kuweko Tarjama itakayoweza kumsaidia Muislamu kuweza kufahamu anachosemeshwa na Rabb wake, ikiwa maamrisho apate kuyatekeleza, na ikiwa makatazo apate kuyaepuka.





Kadhaalika, kuna ilimu na fani nyingi ambazo zimefungamana na kushikamana na Qur-aan zenye kuweza kusaidia katika kufikia kufahamu Tafsiyr ya Aayah. Ni kama vile ilimu ya Uswuwl ya Tafsiyr pamoja na kutabahari (kubobea) katika fani zote zile ambazo hakuna njia ya kufahamika Tafsiyr wala kuwa sahihi isipokuwa kwayo, kama vile kufahamu sababu za kuteremka kwa Suwrah au Aayah (Asbaab An-Nuzuwl) pamoja na za mwanzo na za mwisho kuteremka. Pia Naasikh wa Mansuwkh (kinachofuta na kilichofutwa), ukusanyaji wake, mpangilio wa Aayah na Suwrah zake, visa vyake, mifano yake, kujibu tuhuma dhidi yake na kadhalika. Hivyo, Tafsiyr inayokubalika ni ile yenye kufuata Manhaj iliyoelezwa juu inayotegemea zaidi nukuu badala ya mawazo au rai ya Mfasiri.





Mkusanyiko wa hayo yote na mengineyo ndani ya sayansi hiyo unadhihirisha kuwa kunahitajika uangalifu mkubwa katika kukata shauri na kutoa hukumu kuhusu maana ya Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى). Ndio ikawa njia pekee sahihi na ya salama ya kufanikisha hilo, ni kwa kushikamana na kutegemea yale yaliyopokelewa na kuthibiti kutoka kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba (رضي الله عنهم) na wala si kutokana na rai.





La msingi na lililo muhimu katika kazi ya Tarjama ambalo ni sharti katika masharti ya anayefanya hiyo Tarjama ni kuwa awe mtu mwenye kushikamana na msingi madhubuti wa kufuata Manhaj ya Salaf[5] na wala si msingi wa kuzusha au ubunifu. Atakapokuwa ameshikamana na Manhaj sahihi ya Salaf, basi hivyo ndivyo kutampeleka na kumlazimisha kama ni sehemu ya ‘Aqiydah yake, kushikamana na zile Tarjama zenye kwenda sambamba na mafundisho ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), zenye kunukuu kauli za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), au kauli za Swahaba (رضي الله عنهم) au kauli za Taabi’iyn[6] na Atbaa’ Taabi’iyn.[7]





Kutokana na hali hii basi, Mufassiruna wa Qur-aan wameweka Manhaj maalumu ya Tafsiyr ya kufuatwa na kushikiliwa na ambayo kwayo kwa kuipitia vizuri, ndipo tutaweza kupata Tarjama iliyo sahihi.



1. Tafsiyr Ya Qur-aan Kwa Qur-aan





Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ndio njia ya kwanza inayopasa kufuatwa, kwani Qur-aan inajifasiri yenyewe kwa yenyewe. Utakuta pahala inaeleza jambo kwa kifupi na pahala pengine inalieleza jambo hilo hilo kwa ufafanuzi na kwa uchambuzi. Jambo inalolieleza kwa ujumla katika sehemu moja hulieleza kwa kuliwekea ima mipaka au kulihusisha kwa watu makhsusi katika sehemu nyingine. Hivyo, njia iliyo sahihi kabisa katika kufasiri Qur-aan, ni kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.[8]





Ibn Al-Qayyim (رحمه الله) amesema: “Kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan ni njia bora kabisa inayofikisha Risala (Ujumbe) na kuifafanua. Na si ajabu kwani Allaah (سبحانه وتعالى) ni Mjuzi wa malengo na makusudio Yake. Anafafanua Aayah Zake kwa Aayah nyinginezo. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ وَلِيَقُولُوا دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ﴿١٠٥﴾

“Na hivyo ndivyo Tunavyosarifu namna kwa namna Aayaat ili (makafiri) waseme: Umedurusu (kutoka kwa Watu wa Kitabu), na ili pia Tuibainishe kwa watu wenye kujua.”[9]





Ni jambo lisilopingika kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akifahamu kikamilifu kila kilichoelezwa ndani ya Qur-aan na ndio akawa wa kwanza kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan kama ilivyopokewa kuwa alifasiri baadhi ya Aayah kwa Aayah nyinginezo.[10]





Swahaba (رضي الله عنهم) walishuhudia na kumsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akifasiri Qur-aan kwa Qur-aan, hivyo nao kama ilivyo desturi yao, walimuiga katika hilo pia kama walivyokuwa wakimuiga katika mengineyo, na kwa kufahamu kuwa ni jukumu lao kufikisha kila walichochukua kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kuwafikishia wataokuja baada yao. Hivyo basi Swahaba (رضي الله عنهم) waliwafunza Taabi’iyn [Waislamu ambao hawakumuwahi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika uhai wake], kila walichopokea kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tena kwa muradi wake Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Taabi’iyn nao waliwafunza Atbaa’ Taabi’iyn (Waislamu ambao hawakuwawahi Swahaba katika uhai wao) kila walichopokea na kuchukua kutoka kwa waalimu wao ambao ni Swahaba (رضي الله عنهم). Kisha nao kwa upande wao walinukuu na kufikisha kwa waliokuja baada yao, tena kwa muradi ule ule walioupokea na kuuchukua kutoka kwa Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na katika waliyoyapokea ni aina hii ya kufasiri Qur-aan kwa Qur-aan.





Hivyo, haijuzu wala si sahihi kuiacha aina hii ya Tafsiyr na kuiendea nyingine ikiwa Aayah husika ina Aayah nyingine iliyoifasiri kama ilivyo katika mifano ifuatayo: Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



وَعِندَهُ مَفَاتِحُ الْغَيْبِ لَا يَعْلَمُهَا إِلَّا هُوَ ۚ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۚ وَمَا تَسْقُطُ مِن وَرَقَةٍ إِلَّا يَعْلَمُهَا وَلَا حَبَّة فِي ظُلُمَاتِ الْأَرْضِ وَلَا رَطْبٍ وَلَا يَابِسٍ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ ﴿٥٩﴾

“Na Kwake (Allaah) zipo funguo za ghaibu, hakuna azijuaye ila Yeye tu. Na Anajua yale yote yaliyomo barani na baharini. Na halianguki jani lolote ila Hulijua, wala punje katika viza vya ardhi, wala kinyevu na kikavu isipokuwa kimo katika Kitabu kinachobainisha wazi.”[11]



Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia na kuwawekea wazi kuwa funguo za ghaibu ni tano; kwa kuwasomea kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى) ifuatayo:



إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

“Hakika Allaah Ana ujuzi wa Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika matumbo ya uzazi. Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye Khabari za dhahiri na siri.”[12]





Mfano mwengine ni pale Allaah (سبحانه وتعالى) Anaposema:





الَّذِينَ آمَنُوا وَلَمْ يَلْبِسُوا إِيمَانَهُم بِظُلْمٍ أُولَـٰئِكَ لَهُمُ الْأَمْنُ وَهُم مُّهْتَدُونَ ﴿٨٢﴾

“Wale walioamini na hawakuchanganya imaan zao na dhulma, hao ndio watakaopata amani nao ndio waliohidika.”[13]





Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwabainishia Swahaba na kuwawekea wazi kuwa dhulma ni shirki kwa kuwasomea Aayah ifuatayo:



وَإِذْ قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ وَهُوَ يَعِظُهُ يَا بُنَيَّ لَا تُشْرِكْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ ﴿١٣﴾

“Na Luqmaan alipomwambia mwanawe huku akimuwaidhi: Ee mwanangu! Usimshirikishe Allaah, hakika shirki ni dhulma kubwa mno!”[14]





2. Kufasiri Qur-aan Kwa Sunnah[15] Za Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)



Sunnah inafasiri, inasherehesha na inabainisha Qur-aan kwa kudhihirisha yasiyokuwa dhahiri. Sunnah inaisherehesha Qur-aan kwa kuyachambua, kuyapambanua na kwa kuyaainisha yale ambayo Qur-aan imeyaelezea kwa ujumla. Sunnah inaweka mipaka kwa yale yasiyokuwa yamewekewa mipaka na Qur-aan. Sunnah inayachambua yaliyotolewa hukumu kwa pamoja, ikifafanua yaliyoachwa wazi hukumu zake. Yote hayo kwa kuwa katika Qur-aan, kuna yasiyoweza kufahamika isipokuwa kwa kupata ufafanuzi na kuwekwa wazi na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama vile uchambuzi wake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika namna za amri na makatazo, idadi za Rakaa za Swalaah, utekelezaji wa ‘Umrah na Hajj, viwango vya yale Aliyofaradhisha Allaah (سبحانه وتعالى) katika hukumu.[16]





Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alibainisha na kufafanua kwa kufasiri maana za Aayah za Qur-aan kwa Swahaba zake (رضي الله عنهم) kama inavyoashiria Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):



وَأَنزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ﴿٤٤﴾

“Na Tumekuteremshia Ukumbusho (Qur-aan) ili uwabainishie watu yaliyoteremshwa kwao huenda wakapata kutafakari.”[17]





Ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni kitu kisichoweza kuepukika, na ndio akaweka wazi kwa kusema kuwa hakupewa Qur-aan pekee, bali alipewa pamoja na Qur-aan kinachofanana nayo.[18]





Umahiri katika lugha ya Kiarabu pekee haukuwa wenye kutosheleza wala hautatosheleza katika kufahamu kusudio la Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) bila ya kutafuta msaada kutoka kwenye Sunnah. Kama ilivyokuwa hali kwa Swahaba (رضي الله عنهم) japokuwa walikuwa wenye ufasaha na umiliki kamili wa lugha ya Kiarabu, lakini walikuwa wakitatanishwa au wakati mwengine wakifahamu baadhi za Aayah kinyume na inavyotakiwa ifahamike, jambo lililowapelekea kurejea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutafuta ufafanuzi. Basi hufasiri Aayah au neno ambalo Swahaba (رضي الله عنهم) hawakuweza kuifahamu Tafsiyr yake au walipofahamu kinyume na inavyotakiwa ifahamike.





Kuna mifano mingi tu ya Aayah za Qur-aan ambapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amezifasiri na kuzifafanua.





Mfano neno la الْكَوْثَرَ



Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilifasiri nenoالْكَوْثَرَ katika Suwrah Al-Kawthar:

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

“Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar[19] (Mto katika Jannah).”



kuwa ni Mto katika Jannnah, maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya kufafanuliwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه) : ((إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ)) أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: ((هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ))

Amesimulia Anas (رضي الله عنه) : Kuhusu kauli yake Allaah:

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ

“Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar.”



Kuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Huo ni Mto katika Jannah.”[20]





Mfano mwengine ni neno زِيَادَةٌ



Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifasiri kwa kubainisha kuwa neno زِيَادَةٌ katika Aayah ya Suwrat Yuwnus,



لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ

“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).”[21]





Kuwa maana ya ziada ni kumuona Allaah (سبحانه وتعالى), maana ambayo haikufahamika isipokuwa kwa njia ya ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hadiyth ifuatayo:





عَنْ صُهَيْبٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ نُودُوا: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، إِنَّ لَكُمْ عِنْدَ اللَّهِ مَوْعِدًا لَمْ تَرَوْهُ، فَقَالُوا: وَمَا هُوَ؟ أَلَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا وَتُزَحْزِحْنَا عَنِ النَّارِ، وَتُدْخِلْنَا الْجَنَّةَ؟)) قَالَ: ((فَيُكْشَفُ الْحِجَابُ، فَيَنْظُرُونَ إِلَيْهِ، فَوَاللَّهِ مَا أَعْطَاهُمْ اللَّهُ شَيْئًا أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنْهُ)) ثُمَّ تَلاَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ))

Amesimulia Swuhayb (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Watakapoingia Watu wa Jannah katika Jannah (Pepo), wataitwa: Enyi Watu wa Jannah! Hakika nyinyi mna ahadi kwa Rabb wenu bado hamjaiona. Watauliza: Ni (ahadi) ipi hiyo? Kwani Hukuzing’arisha nyuso zetu, na Hukutuokoa na moto, na Hukutuingiza Jannah?” Akasema: “Litaondoshwa pazia, na watamtazama Allaah. Basi Wa-Allaahi, Hakuwahi Allaah kuwapa jambo walolipenda zaidi kuliko hilo (kumuona Allaah).” Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma Aayah hii:

لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ

“Kwa wale waliofanya ihsaan watapata (huko Jannah) jazaa nzuri kabisa na ziada (kumuona Allaah).”[22]





Hii inathibitisha kuwa ufafanuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni wenye umuhimu mkubwa katika kufasiri Qur-aan, kwani ni ufafanuzi wa aina yake pekee na wenye thamani isiyoweza kununulika wala kukadirika. Ndio ikawa Qur-aan inaihitaji Sunnah (Hadiyth), na ndio ikawa hakuna kitabu katika vitabu vya Hadiyth isipokuwa kutakuwepo mlango wa Tafsiyr Maathuwr.[23]





3. Kufasiri Qur-aan Kwa Kauli Za Swahaba (رضي الله عنهم)



Kauli (Tafsiyr) za Swahaba (رضي الله عنهم) ni chanzo cha tatu cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana kutoka vyanzo viwili vilivyotangulia, kama alivyosema Al-Haafidhw Ibn Kathiyr katika utangulizi wa Tafsiyr yake kuwa: “Tutakapokuwa hatukufanikiwa kupata Tafsiyr katika Qur-aan au Sunnah, tutarejea katika kauli za Swahaba (رضي الله عنهم) kwani wao waliifahamu Qur-aan vilivyo kwa ufasaha na sarufi zake, na kwa kuwa walishuhudia matukio yaliyosababisha kuteremshwa kwa Aayah au Suwrah husika. Hakuna aliyeyashuhudia isipokuwa wao, na pia kutokana na wao kuwa na ilimu sahihi na amali njema haswa haswa Wanachuoni miongoni mwao.”[24]





Swahaba (رضي الله عنهم) walijifunza Qur-aan na ilimu yake kwa kina kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).[25]





Hata hivyo, ufahamu wa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Qur-aan haukuwa wa daraja moja kwani miongoni mwao (رضي الله عنهم) wako waliojulikana kuwa ni wafasiri wa Qur-aan, kama vile Makhalifa wanne (رضي الله عنهم), Ibn Mas’uwd[26] ambaye alikuwa akijulikana miongoni mwa Swahaba kuwa ni mjuzi wao wa Qur-aan (kuisoma na kuifasiri). Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما),[27] pia Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) na wengineo ambao walikuwa na ufahamu uliokamilika kwa vile ulijengeka juu ya ilimu iliyo sahihi iliyopambika kwa amali njema. Hivyo, Tafsiyr zao zina thamani, uzito na umuhimu mkubwa mpaka ikawa Tafsiyr ya Swahaba inachukua hukumu ya Al-Marfuw[28] haswa inapojulikana kuwa Swahaba huyo hakuwahi kupokea Israaiyliyyaat[29] katika hilo.





Kilichojitokeza ni kuwa hakuna Tafsiyr iliyoandikwa katika wakati wao, kwani ilikuwa ni sehemu katika Hadiyth.





Mfano wa Tafsiyr ya neno لَامَسْتُمُ (mmewagusa) kuwa ni kujimai katika kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ

“au mmewagusa wanawake.”[30]



Ibn ‘Abbaas alilitafsiri kwa kusema kuwa: “Ni kujimai.”[31]





Mfano mwengine ni Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِى لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾

“Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) Njia ya Allaah bila ilimu, na huzichukulia (Aayaat) mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.”[32]





Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema kuhusu Aayah hii: “Naapa kwa Jina la Allaah! Hii inamaanisha ni muziki.”[33]



Mfano mwengine ni kuhusu Sa’yi baina ya majabali mawili ya Swafaa na Marwah kulikotajwa kwenye kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.”[34]





Baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) walifahamu kinyume na vile inavyotakiwa ifahamike Aayah hiyo. Mmojawao ni baba wa Hishaam bin ‘Urwah. Alimuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) ambaye alimfahamisha kwa kutumia Sababun-Nuzuwl (Sababu ya kuteremshwa) ili aweze kufahamu usahihi wa maana ya Aayah kama ilivyothibiti katika kauli ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) katika usimulizi ufuatao:



عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ: قُلْتُ لِعَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَنَا يَوْمَئِذٍ حَدِيثُ السِّنِّ: "أَرَأَيْتِ قَوْلَ اللَّهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا)) فَمَا أُرَى عَلَى أَحَدٍ شَيْئًا أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، فَقَالَتْ عَائِشَةُ: "كَلَّا، لَوْ كَانَتْ كَمَا تَقُولُ، كَانَتْ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ لَا يَطَّوَّفَ بِهِمَا، إِنَّمَا أُنْزِلَتْ هَذِهِ الْآيَةُ فِي الْأَنْصَارِ كَانُوا يُهِلُّونَ لِمَنَاةَ، وَكَانَتْ مَنَاةُ حَذْوَ قُدَيْدٍ، وَكَانُوا يَتَحَرَّجُونَ أَنْ يَطُوفُوا بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، فَلَمَّا جَاءَ الْإِسْلَامُ سَأَلُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَلِكَ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: ((إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَنْ يَطَّوَّفَ بِهِمَا))



Amesimulia Hishaam bin ‘Urwah kutoka kwa baba yake alisema: Nilimwambia ‘Aaishah (رضي الله عنها) mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na mimi wakati huo ni kijana mdogo: Unaionaje Kauli ya Allaah (تبارك وتعالى),



إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ

“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.”



Sioni kama kutakuwa na kitu juu ya yeyote ikiwa hatotufu baina yake. Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) akasema: Si hivyo! Ingelikuwa kama unavyosema basi ingekuwa (hivi): Hakutokuwa na dhambi juu yake kama hatotufu baina ya (vilima) viwili hivyo. Kwa hakika Aayah hii imeteremshwa kuhusiana na Answaar ambao walikuwa wakilitukuza Manaat (wakiliabudu sanamu hilo na wakilifanyia Hijjah na wakilitufu), lakini walikuwa hawatufu (Sa’yi baina ya Swafaa na Marwah) na lilikuwa hilo sanamu la Manaat likielekea (kijiji cha) Qadiyd, hivyo walikuwa wakiona tabu kulitufu. Ulipokuja Uislamu walimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hivyo (Sa’yi baina ya Swafaa na Marwah), ndio Allaah Akateremsha:



إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ فَمَنْ حَجَّ الْبَيْتَ أَوِ اعْتَمَرَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِ أَن يَطَّوَّفَ بِهِمَا ۚ وَمَن تَطَوَّعَ خَيْرًا فَإِنَّ اللَّـهَ شَاكِرٌ عَلِيمٌ ﴿١٥٨﴾

“Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah. Kwa hiyo yeyote anayehiji kwenye Nyumba hiyo au akatekeleza ‘Umrah, hakuna lawama kwake kutufu (vilima) viwili hivyo. Na atakayejitolea kufanya kheri, basi hakika Allaah Ni Mwenye Kupokea Shukurani, Mjuzi wa yote.[35]





4. Kufasiri Qur-aan Kwa Kauli Za Taabi’iyn





Kutakaposhindwa kupatikana Tafsiyr ya Aayah husika kwenye Qur-aan, au kwenye Sunnah, au kwenye kauli za Swahaba (رضي الله عنهم), ‘Ulamaa[36] hurejea kwenye kauli za Taabi’iyn, kwani kama walivyotajika baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) kwa Tafsiyr, wametajika pia baadhi ya Taabi’iyn[37] kwa Tafsiyr.





Taabi’iyn walitegemea katika Tafsiyr zao, ufahamu wao wa Qur-aan kutokana na yaliyokuja ndani ya Qur-aan yenyewe, na yale waliyoyapokea kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na yale Aliyowafungulia Allaah kupitia njia ya ijtihaad na utafiti wao katika Qur-aan na wala hawakuwa tayari kutumia rai zao.[38]





Kinachofahamika ni kuwa Tafsiyr zilizopokelewa kutokana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na pia kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم) hazikuwa za Qur-aan yote, bali zilikuwa ni zenye kuhusiana na baadhi ya Aayah za Qur-aan au baadhi ya maneno ya Aayah ambayo yalionekana kuwa ni miongoni mwa yale yenye kuhitaji ufafanuzi kwa wale waliokuwa katika zama hizo. Kutofahamika huku, huwa kunazidi kila pale wanapobaidika watu na zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Swahaba (رضي الله عنهم). Hivyo wale wenye kujishughulisha na fani ya Tafsiyr miongoni mwa Taabi’iyn, wakaongeza katika Tafsiyr kadiri ya kule kuongezeka kutofahamika, kisha baada yao wakaja wale waliokamilisha Tafsiyr ya Qur-aan huku wakitegemea juu ya yale waliyoyafahamu katika lugha na lahaja za Waarabu, na juu ya yale yaliyothibiti kuwa ni sahihi kwao katika matukio yaliyotokea wakati wa kuteremka Qur-aan.





Taabi’iyn wametunukiwa daraja ya kuwa miongoni mwa watu bora kabisa[39] kwa kuwa walichukua na kuchota ilimu zao kutoka vyanzo sahihi na vilivyoasisiwa kwa misingi sahihi.





Mfano wa Tafsiyr ya neno قَانِتُونَ katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



وَقَالُوا اتَّخَذَ اللَّـهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ بَل لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿١١٦﴾

“Na wakasema: Allaah Amejichukulia mwana. Utakasifu Ni Wake! Bali ni Vyake vilivyomo mbinguni na ardhini, vyote vinamtii.”[40]





Kuhusiana na neno قَانِتُونَ Mujaahid alilifasiri kwa kusema kuwa: “Ni kutii. Na kwamba utiifu wa kafiri hupatikana pale kivuli chake kinaposujudu wakati ambapo yeye mwenyewe (kafiri) ni mwenye kuchukia hilo.”[41]





Mfano mwengine ni kuhusiana na Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):



قَالَ أَنَا أُحْيِي وَأُمِيتُ ﴿٢٥٨﴾

“Akasema: Mimi (pia) nahuisha na kufisha.”[42]





Kuhusiana na ibara hii: “Mimi (pia) nahuisha na kufisha.” Qataadah amesema kuwa yule mfalme aliyemuhoji Nabiy Ibraahiym (عليه السلام) alimaanisha kuwa: Watu wawili waliostahiki kuuawa, wangeletwa mbele yake, na angeliamrisha mmoja wao auawe basi angeliuawa. Na angeliamrisha kuwa mtu wa pili asamehewe, basi angesamehewa. Hivi ndivyo ninavyoleta uhai na kifo.[43]





Hivyo Tafsiyr ya Taabi’iyn ni chanzo chengine cha kutafuta ufafanuzi pale inapokuwa haujapatikana ufafanuzi kutoka kwenye vyanzo vilivyotangulia. Hata hivyo baadhi ya Wanachuoni wanaonelea kuwa Tafsiyr za Taabi’iyn na wanafunzi wao hazitoki moja kwa moja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala si kama Tafsiyr za Swahaba (رضي الله عنهم), yote kwa kuwa Taabi’iyn na wanafunzi wao hawajamuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na wala hawakushuhudia Wahy pale zinapoteremshwa Aayah. Na vilevile si wote wanakubalika uaminifu wao, kwa kuwa wao si kama Swahaba (رضي الله عنهم) ambao uaminifu na uadilifu wao umeshuhudiwa na kuthibitishwa na Qur-aan. Ama wao Taabi’iyn na wanafunzi wao wamesifiwa kama ni ‘karne’ na si mmoja mmoja.





Hata hivyo, maelezo mazuri na ya salama ni yale ya Shu‘bah bin Al-Hajjaaj na wengineo ambayo ameyanukuu Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: “Kauli za Taabi’iyn katika furuw’ (matawi ya Sharia) si hoja, basi vipi zitakuwa hoja katika Tafsiyr. Kwa maana kuwa haziwi hoja juu ya wengineo wasiokuwa wao miongoni mwa wale waliowakhalifu, na hii ndio sahihi. Ama pale watakapokubaliana juu ya kitu, basi bila shaka yoyote ile ni hoja. Na endapo watakhitalifiana basi haitokuwa kauli ya baadhi yao hoja juu ya wengine. Na wala juu ya watakaokuja baada yao, bali kutafuatwa na kutazamwa lugha ya Qur-aan, au Sunnah, au kauli za Swahaba (رضي الله عنهم).“[44]





Hakuna shaka yoyote ile kwamba ujuzi wa lugha ya Kiarabu na matawi yake una mchango mkubwa na ni ufunguo katika kuifahamu Qur-aan na kuweza kupata Tafsiyr yenye kukubalika. Hivyo basi, ufahamu sahihi wa Tafsiyr ya Qur-aan, makusudio yake na yote yenye kufungamana nayo, unafungamana pia na ufahamu sahihi wa lugha ya Kiarabu na matawi yake.





Ilimu ya Tarjama ilibuniwa na kupelekea kuweko Tarjama nyingi sana katika kila zama na kila pahala na kwa lugha maarufu za walimwengu, jambo lililopelekea kumwezesha mlengwa kuweza kufahamu aliyolengewa kuyafahamu. Lakini, huenda Tarjama nyingi zikawa zimefanikiwa kumwezesha mlengwa kufahamu Maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kiasi fulani na kufahamu baadhi ya makusudio ya Aayaat katika upande wa Sharia. Ama kwenye upande wa ‘Aqiydah (Itikadi), baadhi ya Tarjama, hazikufanikiwa kumwezesha Muislamu kupata ufahamu wa wazi wa mas-ala muhimu ya ‘Aqiydah Sahihi kwa kuyatanabahisha na kuyafafanua kiwaziwazi baadhi ya mas-ala hayo ya ‘Aqiydah, mas-ala ambayo yana ufahamu usio sahihi katika itikadi za madhehebu mengineyo.





Hivyo basi, katika Tarjama hii[45], tumejitahidi kubainisha na kuyafafanua kwa dalili baadhi ya mas-ala yanayohusiana na ‘Aqiydah sahihi ili yamwezeshe mwenye kuzungumza Kiswahili afahamu pale alipotakiwa kufika kiitikadi; ‘Aqiydah iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na inayorandana na ‘Aqiydah ya Salaf Asw-Swaalih (Wema waliotangulia) miongoni mwa Swahaba, Taabi’iyn na Atbaa' Taabi’iyn na waliowafuata kwa wema.





Mifano ya baadhi ya mas-ala hayo ya ‘Aqiydah:




(i) Kuthibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) kama Aliyojithibitishia Mwenyewe (سبحانه وتعالى). Mifano: Wajihi Wake, rejea Al-Qaswasw (28:88), Al-Baqarah (2:115) na Ar-Rahmaan (55:27). Mkono au Mikono Yake, rejea Swaad (38:75), Al-Fat-h (48:10). Macho Yake, rejea Huwd (11:37), Al-Muuminuwn (23:27), Twaahaa (20:39). Kusikia na Kuona Kwake, rejea Twaahaa (20:46). Nafsi Yake, rejea Aal-‘Imraan (3:28), na Sifa nyenginezo bila ya Ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala Tamthiyl (kumithilisha, kufafanisha, kulinganisha), wala Takyiyf (kuainisha maana na kuziulizia namna yake au kuuliza ni vipi Sifa hiyo ipo, kuchunguza ni kwa “namna gani” zimefungamana au kuambatana na Allaah), wala Tahriyf (kubadilisha maana, kupotosha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutoa maana isiyo sahihi).





Na hakuna khofu wala shaka kuwa Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) zikithibitishwa kama zilivyotajwa katika Qur-aan, kwamba atashabihishwa Muumba na Viumbe Vyake! Hiyo si hoja muwafaka, kwani imaan thabiti ya Muislamu kuhusiana na Allaah (سبحانه وتعالى) ni kuwa: Hapana anayefanana Naye (Muumba) hata mmoja wala hakuna kitu chochote mfano Wake kama inavyothibitishwa na Allaah (سبحانه وتعالى) Mwenyewe.[46]





(ii) Kuthibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya Al-‘Uluww. Na kwamba Allaah Yuko juu ya Mbingu Zake saba, juu ya ‘Arsh Yake, na Ametenganishwa na viumbe Vyake, na viumbe Vyake vimetenganishwa Naye. Rejea Al-Mulk (67:16). Ama Anaposema Yuko na Waja Wake basi ‘Aqiydah sahihi ni kuamini kwamba Yuko na Waja Wake kwa Ujuzi Wake tu na si kwa Dhati Yake. Rejea Al-Mujaadalah (58:7).





(iii) Istawaa: Kuamini Kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Yuko juu Ya ‘Arsh Yake kama Alivyojijulisha Mwenyewe. Na kuweko huko juu ya ‘Arsh Yake, ni kulingana na Utukufu, Uadhama, Uajalali Wake na Ukamilifu Wake. Rejea Al-A’raaf (7:54) na Twaahaa (20:5).





(iv) Kuamini kwamba Qur-aan ni Kalaamu-Allaah (Maneno ya Allaah) na kwamba hayakuumbwa. Rejea At-Tawbah (9:6).





(v) Kuamini kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yuhai na Atateremka duniani kutoka mbinguni iwe ni alama mojawapo kubwa za Qiyaamah. Rejea An-Nisaa (4:159), Aal-‘Imraan (3:55) na rejea nyenginezo zilizotajwa humo.





(vi) Kuamini kwamba Waumini watamuona Allaah (سبحانه وتعالى) watakapokuwa Jannah (Peponi). Rejea Yuwnus (10:26) na Al-Qiyaamah (75:23).





(vii) Kuamini Kalaam (Kuongea): Kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Anaongea kama Alivyoongea na Nabiy Muwsaa (عليه السّلام). Rejea An-Nisaa (4:164), Al-A’raaf (7:143).





Kwa minajili hiyo, tukaona kuna umuhimu wa kuweko kwa Tarjama itakayokwenda sambamba na Manhaj ya Salaf haswa katika kuibalighisha na kuidhihirisha ile ‘Aqiydah iliyobalighishwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambayo iko wazi kwenye Qur-aan kwa atakaye kushikamana nayo.





Pia, tumeona ni vyema na ndio sahihi ndani ya kazi hii pia, kulithibitisha Jina la ‘Allaah’ badala ya kulifasiri kwa kuligeuza na kutumia neno ‘Mwenyezi Mungu’, kama linavyotumika katika karibu Tarjama zote za lugha ya Kiswahili, kwani Allaah ni Pekee na mungu inatumika kwa miungu wengi hata kama itaunganishwa na ‘mwenyezi.’ Ni imaan yetu kuwa kulithibitisha jina Lake ‘Allaah’ kama lilivyothibiti, ni kumuadhimisha Yeye Allaah (سبحانه وتعالى) na kulipa haki Jina Lake Tukufu kwani hakuna mwenye Majina kama Yake Allaah (سبحانه وتعالى). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):



رَّبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا فَاعْبُدْهُ وَاصْطَبِرْ لِعِبَادَتِهِ ۚ هَلْ تَعْلَمُ لَهُ سَمِيًّا ﴿٦٥﴾

“Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi mwabudu Yeye tu na dumisha subira katika Ibaada Yake. Je, unamjua yeyote anayefanana Naye (Allaah)?” [Maryam (19:65)][47]





Na kubwa na la muhimu zaidi ni kuwa kuna thawabu kwa kuwa ndivyo lilivyothibiti. Hivyo, tutalitumia na kulithibitisha Jina la ‘Allaah’ pote katika Tarjama hii kama lilivyothibitishwa na Qur-aan na Sunnah za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa lengo la kuwarejesha Waumini katika kutumia Majina ya Allaah kama yalivyothibiti.





Hali kadhaalika, tumethibitisha Sifa ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya ‘Rabb’ kwa kuibakisha kama ilivyo katika asli yake bila kuipa maana, kwa sababu neno ‘Rabb’ linatumika Kiswahili kama ‘Rabi’ na linafahamika. Ama kulipa maana ya ‘Mola’ tumeona ni maana finyu isiyokidhi taarifu kamili ya ‘Rabb’ kwa sababu ‘Ar-Rabb’ ina maana nyingi na pana. Inaweza kumaanisha: Mfalme, Bwana, Mlezi, Mwendeshaji, Mpangaji, Mola, Msimamiaji, Mwenye Kuneemesha, Mwenye Kuruzuku n.k. Hivyo, tumeonelea litumike kwenye Tarjama hii hivyo hivyo lilivyo.





Pia, tumejaribu sana kutumia misamiati ya lugha ya Kiswahili, ambayo inalingana sawasawa katika maana na misamiati ya lugha ya Kiarabu, ili iwafikiane na makusudio ya neno la asili la Kiarabu. Na misamiati mingineyo ambayo hayafahamiki kiwepesi katika jamii, tumeyawekea ufafanuzi katika Faharasa. Na baadhi ya misamiati hiyo, inapatikana katika Kamusi za Kiswahili zifuatazo: (i) Kamusi Ya Kiswahili Sanifu (ii) Kamusi Ya Maana Na Matumizi (iii) Kamusi Ya Visawe.





Vilevile, tumeweka baadhi ya faida au tanbihi ili nazo zimpanulie ufahamu msomaji na kumuongezea ilimu ya ufahamu wa Qur-aan.





Pia katika kila Suwrah, tumetanguliza Tangulizi za Suwrah; humo tumetaja Maqaaswid As-Suwrah[48] (Makusudio ya Suwrah), maudhui za Suwrah kwa mukhtasari, fadhila za Suwrah na faida nyenginezo.





Pia tumeambatanisha katika faharasa, kurasa zenye maana ya Majina Mazuri Kabisa ya Allaah na Sifa Zake Kamilifu, ili zimfaidishe msomaji na kumuongezea ilimu.





Msomaji akipendelea kupata faida ya ziyada zifuatazo: (i) Sababu Za Kuteremshwa (Asbaabun-Nuzuwl) Suwrah au Aayah za Qur-aan (ii) Kinachofuta Na Kinachofutwa (An-Naasikh Wal-Mansuwkh) ambayo ni ujuzi wa kujua Aayah zilizofutwa hukmu zake na ambazo zikateremshwa Aayah nyenginezo badala yake (iii) Aayah Na Mafunzo (iv) Tafsiyr Al-Muyassar iliyofasiriwa kwa Kiswahili, basi atembelee Tovuti ya Alhidaaya.com ambako masomo hayo yameorodheshwa kwa bayana. Njia ya kuzifikia ni ifuatavyo:



Maudhui Za Qur-aan > Tangulizi Za Suwrah



Maudhui Za Qur-aan > Tafsiyr Al-Muyassar (Kiswahili)



Maudhui Za Qur-aan > Tafseer As-Sa’di (Kiarabu)



Maudhui Za Qur-aan > Tafseer As-Sa’di (Kiingereza)



Maudhui Za Qur-aan > Asbaabun-Nuzuwl (Sababu Za Kuteremshwa) Aayah Au Suwrah.



Maudhui Za Qur-aan > An-Naasikh Wal-Mansuwkh (Kinachofuta Na Kinachofutwa)



Maudhui Za Qur-aan > Aayah Na Mafunzo.





Basi hizo hazitamzidishia faida pekee, bali atazidisha ilimu yake ya ufahamu wa Qur-aan kwa kina, na atapata ladha, raghba (utashi), ilhamu na mapenzi ya Qur-aan.





Tumetegemea zaidi katika kuikamilisha kazi hii Tafsiyr zifuatazo:





تفسير القرآن العظيم للإمام الحافظ ابن كثير

Tafsiyr Al-Qur-aan Al-‘Adhwiym ya Al-Haafidhw ‘Imaad Ad-Diyn Abi Al-Fidaa Ismaa’iyl bin Kathiyr. Au umaarufu wake تفسير ابن كثير Tafsiyr Ibn Kathiyr.





تيسير الكريم الرحمن في تفسير كلام المنان

Taysiyr Al-Kariym Ar-Rahmaan Fiy Tafsiyr Kalaam Al-Manaan ya Al-‘Allaamah Ash-Shaykh ‘Abdur-Rahmaan bin Naaswir As-Sa’diy. Au umaarufu wake kama تفسير السعدي Tafsiyr As-Sa’diy.





التفسير الميسر - نخبة من العلماء

At-Tafsiyr Al-Muyassar – Nukhbat Minal ‘Ulamaa





Na Tarjama ya Kiingereza:



Interpretation of The Meanings of The Noble Quran in The English Language (A Summarized Version of At-Tabari, Al-Qurtubi and Ibn Kathir with Comments from Sahih Al-Bukhari) Dr. Muhammad Taqi-ud-Diyn Al-Hilaaliy, Dr Muhammad Muhsin Khan.





Mwisho tunamshukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kutuwafikisha kuweza kuikamilisha kazi hii tukufu, kazi ambayo ni jukumu kubwa mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى) wala hatusemi kuwa Tarjama hii itakuwa haina kasoro, kwani hakuna mkamilifu isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى).





Tunawaomba ndugu zetu watuarifu kwa kosa lolote lile watakaloligundua au kasoro yoyote ile watakayoiona kwa kuwasiliana nasi kupitiwa webmaster@alhidaaya.com.





Tunamuomba Allaah (سبحانه وتعالى) Atughufurie kwa makosa yetu na Aijaalie kazi hii iwe ni kwa ajili ya kuzipata Radhi Zake Pekee na Atutakabalie.





Na Allaah Ni Mjuzi Zaidi



الحمد لله رب العالمين وصلى الله على محمد وعلى آله واصحابه وسلم





Imeandaliwa Na: Alhidaaya.com






[1] Fusw-Swilat (41:42).



[2] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الْإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَىٰ أَن يَأْتُوا بِمِثْلِ هَـٰذَا الْقُرْآنِ لَا يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ﴿٨٨﴾

“Sema: Ikiwa watajumuika wanaadamu na majini ili walete mfano wa hii Qur-aan, hawatoweza kuleta mfano wake na japokuwa watasaidiana wao kwa wao.” [Al-Israa (17:88)]



[3] Ibraahiym (14:4).



[4] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّهُمْ يَقُولُونَ إِنَّمَا يُعَلِّمُهُ بَشَرٌ ۗ لِّسَانُ الَّذِي يُلْحِدُونَ إِلَيْهِ أَعْجَمِيٌّ وَهَـٰذَا لِسَانٌ عَرَبِيٌّ مُّبِينٌ ﴿١٠٣﴾

“Na kwa yakini Tunajua kwamba wao wanasema: Hakika hapana isipokuwa mtu anamfundisha (Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم Qur-aan). Lugha wanayomnasibishia nayo ni ya kigeni, na hii ni lugha ya Kiarabu bayana.” [An-Nahl (16:103)]



[5] Salaf:



Maana yake kilugha ni kilichopita, kilichotangulia.

Na wanaokusudiwa kuwa ni Salafus-Swaalih ni Wema Waliotangulia. Nao ni Waumini wa karne ya kwanza ambao ni Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Muhaajirina na Answaar kama Anavyosema Allaah (عزّ وجلّ):



وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِى تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿١٠٠﴾

“Na wale waliotangulia awali (katika Uislamu) miongoni mwa Muhajirina na Answaar na wale waliowafuata kwa ihsaan, Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Na Amewaandalia Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo abadi. Huko ndiko kufuzu kukubwa kabisa.” [At-Tawbah (9:100)] Rejea pia Al-Hashr (59:8-10).



Kisha wale waliokuja baada yao na wakajifunza kwao miongoni mwa Taabi’iyn na Atbaa’ At-Taabi’iyn, halafu pia waliokuja baada yao katika karne iliyo bora kabisa aliyosema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ): “Wabora wenu zaidi ni wa karne yangu, kisha wale wanaowafuatia (Taabi’iyna), kisha wale wanaowafuatia hao (Atbaa’ Taabi’iyn).” [Al-Bukhaari - Yamenukuliwa kutoka Manhaj As-Salaf Asw-Swaalih Wa Haajatul-Ummati Ilayhi, Tovuti Rasmi ya Ma’aaliy Shaykh Ad-Duktuwr Swaalih Bin Fawzaan Bin ‘Abdillaah Al-Fawzaan]



Kisha wengineo ambao wamewafuata hao wote katika Manhaj ya Salaf kwa kufuata mafundisho ya Kitabu na Sunnah, kuyalingania kwa watu, na kuyafanyia kazi mpaka Siku ya Qiyaamah. Na kwa mwenendo huu, wanakuwa ni Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah.”



[6] Taabi’iyn: Ni Waislamu waliokuja baada ya zama za Unabii na hawakuwahi kukutana na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ), bali walikutana na Swahaba wake wakasuhubiana nao. Miongoni mwa hao ni: Hasan Al-Baswriy, Qtaadah, ‘Urwah bin Az-Zubayr, Sa’iyd bin Al-Musayyib, Mujaahid bin Jabar, Sa’iyd bin Jubayr, Naafi’ (Mtumwa aliyeachwa huru na Ibn ‘Umar رَضِيَ اللهُ عَنهُمَا), na ‘Ikrimah (Mtumwa aliyeachwa huru na Ibn ‘Abbaas رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا).



[7] Atbaa' Taabi’iyn: Ni Waislamu ambao hawakuwahi kukutana na Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ), bali walikutana na Taabi’iyn na wakasuhubiana nao. Miongoni mwa hao ni: Maalik, Abu Haniyfah (ingawa baadhi ya Wanachuoni wanasema ni Taabiy' kwa sababu alikutana na Swahaba wa mwisho mwisho), Ash-Shaafi’iy, Ahmad bin Hanbal, Sufyaan Ath-Thawriy, Sufyaan bin ‘Uyaynah, Ibn ‘Abiy Laylaa, Rabiy’ah, Abu ‘Abdirrahmaan Al-Awzaa’iy, Ibn Hurmuz, Al-Hasan Ibn Swaalih, ‘Abdullaah Ibn al-Hasan, na Ibn Shubrumah.



Kisha baada ya hao wakaja Taabiy' Atbaa' Taabi'iyn, na katika hao ni Imaam wa Hadiyth ambao ni: Al-Bukhaariy, Muslim Abu Daawuwd At-Tirmidhiy An-Nasaay, Ibn Maajah.



[8] Tazama Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr - Ibn Taymiyyah.



[9] Al-An’aam (6:105).



[10] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

إِنَّ عَلَيْنَا جَمْعَهُ وَقُرْآنَهُ ﴿١٧﴾ فَإِذَا قَرَأْنَاهُ فَاتَّبِعْ قُرْآنَهُ ﴿١٨﴾ ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾

“Hakika ni juu Yetu Kuikusanya na Kukuwezesha kuisoma kwake. Basi Tunapoisoma (kupitia Jibriyl), fuata kusomwa kwake. Kisha ni juu Yetu Kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah (75:17-19)]



[11] Al-An’aam (6:59).



[12] Luqmaan (31:34).



[13] Al-An‘aam (6:82).



[14] Luqmaan (31:13).



[15] Sunnah:



Ni kila kilichonasibishwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au yale aliyoyakubali au sifa za kimaumbile au tabia au mwenendo.



[16]Hakika kila kile alichohukumu kwacho Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika yale aliyoyaelewa (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Qur-aan kama alivyosema Imaam Ash-Shaafi’y. Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr. Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:



إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ لِتَحْكُمَ بَيْنَ النَّاسِ بِمَا أَرَاكَ اللَّـهُ ۚ وَلَا تَكُن لِّلْخَائِنِينَ خَصِيمًا ﴿١٠٥﴾

“Hakika Sisi Tumekuteremshia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa Aliyokuonyesha Allaah. Wala usiwe mtetezi kwa makhaini.” [An Nisaa (4:105)]



Pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:



وَمَا أَنزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ إِلَّا لِتُبَيِّنَ لَهُمُ الَّذِي اخْتَلَفُوا فِيهِ ۙ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٦٤﴾

“Na Hatukukuteremshia Kitabu (Qur-aan) isipokuwa uwabainishie yale waliyokhitilafiana, na pia ni Mwongozo na Rahmah kwa watu wanaoamini.” [An Nahl (16:64)]



[17] An-Nahl (16:44). Kadhalika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا بَيَانَهُ ﴿١٩﴾

“Kisha ni juu Yetu kuibainisha (kwako).” [Al-Qiyaamah (75:19)] inawarudi kwa uwazi kabisa wale wenye kudai kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakubainisha maana ya Majina na Sifa za Allaah, na kwa kauli yao hii, ima wanakusudia kuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa hajui maana ya Majina na Sifa za Allaah, au Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alificha kile alichokifahamu. Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.



[18] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:



أَلَا إِنِّي أُوتِيتُ الْقُرْآنَ وَمِثْلَهُ، أَلَا يُوشِكُ رَجُلٌ يَنْثَنِي شَبْعَانًا عَلَى أَرِيكَتِهِ يَقُولُ: "عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَلَال فَأَحِلُّوهُ وَمَا وَجَدْتُمْ فِيهِ مِنْ حَرَامٍ فَحَرِّمُوهُ... رواه أبو داود والترمذي والحاكم وصححه وأحمد بسند صحيح

“Tanabahi! Hakika nimepewa Qur-aan na inayofanana nayo (Sunnah) Tanabahi! Utafika wakati mtu aliyeshiba mno ataegemea kwenye kochi na kusema: “Shikamaneni na Qur-aan, mtakayokuta humo ya halali halalisheni, na mtakayokuta ya haramu haramisheni.” [Imepokewa na Abu Daawuwd, na At-Tirmidhiy, na Al-Haakim na ameisahihisha Ahmad kwa isnaad Swahiyh]



[19] Al-Kawthar (108:1).



[20] Al-Bukhaariy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, At-Tirmidhiy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan.



[21] Yuwnus (10:26).



[22] Ahmad katika Musnad, Kumi waliobashiriwa Jannah, Ukamilisho wa Musnad ya Kuufiyyiyn; na At-Tirmidhiy, katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, na Riwaaya nyenginezo.



[23]Ni Tafsiyr yenye kutegemea yaliyo sahihi katika yaliyopokelewa kulingana na mpangilio huu: Tafsiyr ya Qur-aan kwa Qur-aan, Tafsiyr ya Qur-aan kwa Sunnah, Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Swahaba (رضي الله عنهم), Tafsiyr ya Qur-aan kwa kauli za Taabi’iyn kwa kuwa wao walichukua Tafsiyr zao kutokana na Swahaba (رضي الله عنهم). Vitabu vinavyotajika katika fani hii ya Tafsiyr ni kama:



i. Jaami’ul Bayaan Fiy Tafsiyril Qur-aan ya Ibn Jariyr Atw-Twabariy.

ii. Tafsiyrul Qur-aanil ‘Adhwiym ya Ibn Kathiyr.

iii. Fat-hul Qadiyr ya Ash-Shawkaaniy.



[24] Utangulizi wa Tafsiyr Ibn Kathiyr; vyanzo vya Tafsiyr.



[25]Amesema Abuu ‘Abdir-Rahmaan As-Sulamy: “Wametuhadithia wale waliokuwa wakitusomesha Qur-aan kama ‘Uthmaan bin ‘Affaan (رضي الله عنه) na ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) na wengineo kuwa wao walikuwa pale wanapojifunza kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Aayah kumi huwa hawaongezi nyingine mpaka pale watakapojifunza (na kutekeleza) yale yaliyomo ya ilimu na amali katika hizo Aayah kumi walizojifunza, basi wakasema: Tulijifunza Qur-aan na ilimu na amali kwa pamoja, na kwa sababu hiyo ndio walikuwa wakichukua muda kati kuhifadhi Suwrah.” Taz. Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.



[26]Aliyepokelewa akisema: “Naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakuna katika Kitabu cha Allaah Suwrah isipokuwa mimi najua ilivyoteremka, na hakuna Aayah isipokuwa najua imeteremshwa kwa ajili gani (sababu) na lau ningelimjua yeyote kuwa yeye ni mjuzi zaidi yangu kwa Kitabu cha Allaah, na ngamia anaweza kufika kwake, basi ningepanda kwenda kwake.” [Imepokelewa na Muslim, katika Kitabu cha Fadhila za Swahaba, mlango wa fadhila za ‘Abdullaah bin Mas’uwd na mama yake (رضي الله عنهما)]



[27]Ibn ‘Abbaas aliyetambulikana kama ni ‘Tur-jumanil Qur-aan’ na aliyeombewa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

((اللَّهُمَّ عَلِّمْهُ الْحِكْمَةَ وَتَأْوِيلَ الْكِتَابِ))

“Ee Allaah, Mfunze Hikmah na Ta-awiyl (ufasiri, utambuzi) wa Kitabu (Qur-aan).” [Imepokelewa na At-Tirmidhiyy, katika Kitabu cha Ad-Da’waat, milango ya Manaaqiyb; na Sunan Ibn Maajah, katika Kitabu cha Ibn Maajah, milango ya fadhila za Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)]



[28]Ni kila kilichotegemezwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kauli au kitendo au kuthibitisha jambo au sifa katika tabia zake au umbo lake.



[29] Israaiyliyyaat: Ni khabari, visa, simulizi zitokazo kwa Mayahudi katika Vitabu vya Tafsiyr, Taariykh n.k.



[30]An-Nisaa (4:43).



[31]Tafsiyr Ibn Kathiyr.



[32] Luqmaan (31:6). Tanbih: Kinachoruhusiwa ni dufu na sio ala nyenginezo za muziki.



[33] Atw-Twabariy (20:127).



[34] Al-Baqarah (2:158).



[35] Al-Baqarah (2:158).



[36] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl at-Tafsiyr.



[37] Kama vile Mujaahid, Sa’iyd bin Jubayr, ‘Ikrimah, Twaawuws, ‘Atwaa, Zayd bin Aslam, Abul ‘Aaliyah na Muhammad bin Ka’b, ‘Alqamah bin Qays, Masruwq, ‘Aamir Ash-Sha’biy na Hasan Al-Baswriy na Qataadah.



[38] Imaam At-Tirmidhiy amesema: “Ama yale yaliyopokelewa kutokana na Mujaahid na Qataadah na wengineo miongoni mwa Ahlul-‘Ilmi kwamba walifasiri Qur-aan, basi hakuna haja ya kuwadhania kuwa walifasiri Qur-aan bila ya ilimu –kwa rai zao- au kutokana na nafsi zao, na kumekwishapokewa kutokana na wao yale tuliyoyasema yenye kuthibitisha kwamba wao hawakuifasiri Qur-aan kutokana na nafsi zao bila ya ilimu kama ilivyothibiti kutokana na Al-Hassan bin Al-Mahdiy Al-Baswriyy amesema: Ametupa khabari ‘Abdur-Razzaaq kutokana na Ma’mar kutoka kwa Qataadah amesema: “Katika Qur-aan hakuna Aayah yoyote ile isipokuwa nimesikia kitu kuhusiana nayo.” [At-Tirmidhiyy katika Kitabu cha Tafsiyr ya Qur-aan, mlango wa katika yale yaliyokuja kwa yule anayefasiri Qur-aan kwa rai yake]



[39] Kutoka kwa Ibn Mas’uwd(رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

((خَيْرُ النَّاسِ قَرْنِي، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ)) صحيح البخاري ومسلم

“Watu bora kabisa ni karne yangu, kisha wanaowafuatia, kisha wanaowafuatia.” [Imepokelewa na Al-Bukhaariy, katika Kitabu Al-Manaaqib, mlango wa Fadhila za Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Muslim Kitabu cha Fadhila za Swahaba, mlango wa Fadhila za Swahaba (رضي الله عنهم)]



[40] Al-Baqarah (2:116).



[41] Tafsiyr Ibn Kathiyr.



[42] Al-Baqarah (2:258).



[43] Tafsiyr Ibn Kathiyr.



[44] Tazama Ibn Taymiyyah, Sharh Kitaab Muqaddimah fiy Uswuwl At-Tafsiyr.



[45] Tarjama Hii Ziko Mbili: Ya Mtandaoni Na Iliyochapishwa:



(i) Tarjama Iliyoko Mtandaoni Alhidaaya.com:



Tarjama hii imetoa maelezo na fafanuzi kwa baadhi ya Aayah kwa faida ya msomaji. Maelezo hayo yanahusiana na mas-ala ya ‘Aqiydah kama Al-Istiwaa (Uwepo wa Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya ‘Arsh). Pia kuthibitisha Sifa Zake kama Alivyojithibitishia Mwenyewe na kadhalika. Vile vile, imefafanua baadhi ya maneno ya Kiarabu au ya Kiswahili ambayo hayafahamiki kiwepesi katika jamii. Isitoshe, pametajwa ndani yake rejea za Aayah zilizo katika Suwrah tofauti ambazo zinagusia maudhui moja, ili msomaji aweze kuzipata kirahisi pale zilipo, na kulifahamu suala kwa ujumla wake. Na hatimaye, zimetajwa rejea za mtandaoni Alhidaaya.com za maudhui kwenye makala na vitabu vya maudhui husika, zikiwemo rejea za Asbaabun-Nuzuwl (Sababu Za Kuteremshwa) Aayah au Suwrah., ambazo zitampa msomaji uelewa kamili na mzuri wa Aayah au Suwrah husika ili msomaji ajinufaishe zaidi na aweze kuongeza ilimu yake.



(ii) Tarjama Iliyochapishwa:



Tarjama hii iliyochapishwa kwenye karatasi haikuwekewa maelezo au fafanuzi kuhusu baadhi ya Aayaat. Sababu, ni kuzipa nafasi hati ziwe kubwa za wazi zinazosomeka kirahisi, na pia upatikane mjeledi mmoja tu wa Tarjama ili msomaji aweze kuutumia kiwepesi.



[46] Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ ﴿١١﴾

“Hakuna chochote kinachofanana Naye, Naye Ni Mwenye Kusikia yote, Mwenye Kuona yote.” [Ash-Shuwraa (42:11)]



[47] Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Hakuna yeyote anayeitwa Ar-Rahmaan isipokuwa Allaah (تبارك وتعالى) na Jina Lake linatukuzwa [Tafsiyr Ibn Kathiyr]



[48] Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym Nukhbah Min Al-‘Ulamaa – Markaz Tafsiyr Lid-Diraasaat Al-Qur-aaniyyah. Na Maqaaswid nyenginezo.



مركز تفسير للدراسات القرآنية
 
Naam ndugu yangu katika imani naona umesoma hapo utangulizi murua kabisa kutoka kwa alhidaaya.com kuhusiana na Tarjama ambayo tutaisoma hapa

Bilashaka umepata faida kujua watu wa karne bora kabisa aliyosema Nabii swalla aallahu alaihy wa aliih wa sallam ambao Maswahaba,Tabiiny na atba tabiiny


Vile vile umejua mtiririko mzima wa elimu ulipoanzia mpaka umetufikia sisi

Kaa tayar kuisoma Tarjama/tafsir ya qur'an tuongeze elimu zaidi

Endelea kufuatilia uzi elimu ipo jamii forums
 
Adhana Ya Alfajri Huwa Ngapi? Na Ni Ipi Huongezwa الصَّلاةُ خَيْرٌ مِنَ النَّوم ?
Maswali: Vitendo-Kauli
SWALI:


Assalaam aleikum warahmatulahi taala wa barakatuhu.

Shukran kwa kazi nzuri. Nauliza juu ya adhana ya Alfajri. Adhana ya Afajir huwa ni ngapi? Ni adhana ipi ya kuweka Assalaatul khairu minna naum? Nijibu tafadhali.


JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.


Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Adhana zinazotolewa kwa Swalaah ya Alfajiri.


Adhana hizo kuanzia wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ni mbili. Ya kwanza ilikuwa inatolewa kabla ya kuingia Alfajiri kwa muda ili watu wapate kujitayarisha kwa ajili ya Swalaah hiyo. Ya pili ni ile iliyokuwa ikitolewa kuwajulisha watu kuwa wakati wa Swalah umeshaingia au kuwapasha habari wenye kutaka kufunga kuwa wakati umekwisha na hawawezi kula wala kunywa tena.




Adhana ya kwanza ndio ya kuwatayarisha na kuwaamsha watu ili wawe tayari kwa ajili ya Swalah. Hivyo, kulingana na Hadiyth kadhaa imekuja kuwa maneno ya nyongeza yanayosemwa, “Asw-Swalaatu Khayrum-minan-nawm" (Swalaah ni bora kuliko usingizi) ni katika Adhana ya kwanza lakini kutokana na ufafanuzi wa Wanachuoni katika ufahamu sahihi wa Hadiyth hizo, ni kuwa, wao wanafafanua hizo Hadiyth kuwa makusudio ya Adhana ya kwanza ni ile ambayo Swalah imefika wakati wake na baada ya hapo inafuatiwa na Adhana ya pili ambayo ni Iqaamah kama inavyojulikana kwenye Hadiyth nyinginezo kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anaposema "Katika kila baina ya Adhana mbili kuna Swalah" akikusudia Adhana na Iqaamah. Hivyo hapo Wanachuoni wanaeleza makusudio ya Adhana ya kwanza ni hiyo ambayo hujulikana kama ni Adhana ya pili ambayo hufuatiwa na Iqaamah.

Na hivyo ndivyo walivyoeleza Wanachuoni wa Fataawa al-Lajnah ad-Daa’imah lil-Buhooth al-‘Ilmiyyah wal-Iftaa, 6/63



Kwa hivyo, kauli yenye nguvu kwenye suala hili, ni kuwa Maneno hayo " As-Swalaatu khayrum-minan nawm ni kwenye hii inayojulikana na watu kuwa ni Adhaana ya pili.









Na Allaah najua zaidi
 
Maswali: Vitendo-Kauli
Adhkaar Katika Rukuu Na Sujuwd



www.alhidaaya.com






SWALI:



Assalaam alaykum alaykum alhidaaya, kwanza samahani kwa kuuliza maswali kwani siruhusiki kwa majibu ya maelezo lkn sheikh nakuomba unitowe wasiwasi kama utapata muda ili nijuwe vipi ibada yangu naitekeleza sahihi ama na hasa mwezi huu mtukufu isije ikawa nafanya ibada kumbe nakwenda kinyume.



Moja, ni kuhusu adhkar za rukuu na sujudu nimeona ktk hiswnul muslim wameandika kwa namba, je mie natakiwa nizisome zote kama za sujudu au nichague moja halikadhalika na rukuu.





JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Adhkaar za Sunnah katika Swalaah zinapatikana katika Kitabu cha Hiswnul-Muslim, pamoja na za kurukuu na kusujudu nazo ni katika viungo vifuatavyo:



Nazo zinapatikana katika viungo vifuatavyo. Bonyeza usome na usikilize Adhkhaar hizo:



017-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Wakati Wa Kurukuu



018-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuinuka Kutoka Kenye Rukuu



019-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Wakati Wa Kusujudu



020-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Kikao Kati Ya Sijdah Mbili



Ukiweza kuzihifadhi zote zitakusaidia katika kisimamo cha kuswali usiku ambacho kinapaswa kuwa kirefu katika kila hali.



Na Allaah Anajua zaidi
 
017-Hiswnul-Muslim: Du’aa Za Wakati Wa Kurukuu
Hiswnul-Muslim

017-Du’aa Za Wakati Wa Kurukuu

www.alhidaaya.com





Bonyeza Hapa Usikilize







[33]

سُبْـحانَ رَبِّـيَ الْعَظـيم



Subhaana Rabbiyal ’Adhwiym



Ametakasika Rabb wangu aliye Mtukufu[1] (mara 3)





[34]

سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ رَبَّـنا وَبِحَـمْدِك، اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي



Subhaanaka Allaahumma Rabbanaa wabihamdika, Allaahummaghfir liy



Utakasifu ni Wako Ee Allaah Rabb wetu na Himdi ni Zako Ee Allaah, nighufurie[2]





[35]

سُبـّوحٌ قُـدّْوس، رَبُّ الملائِكَـةِ وَالـرُّوح



Subbuwhun Qudduwsun Rabbul-Malaaikati war-Ruwh



Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Rabb wa Malaika na Jibiriyl[3].





[36]

اللّهُـمَّ لَكَ رَكَـعْتُ، وَبِكَ آمَـنْت، ولَكَ أَسْلَـمْت، خَشَـعَ لَكَ سَمْـعي، وَبَصَـري، وَمُخِّـي، وَعَظْمـي، وَعَصَـبي، وَما استَقَـلَّ بِهِ قَدَمي



Allaahumma Laka raka’-tu, wabika aamantu, walaka aslamtu. Khasha’a Laka sam-’iy, wabaswariy, wamukh-khiy, wa ’adhwmiy, wa ‘aswabiy, wamas-taqalla bihi qadamiy



Ee Allaah Kwako nimerukuu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimejisalimisha, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, na uwoni wangu, na ubongo wangu, na mfupa wangu, na hisia zangu, na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu[4].





[37]

سُبْـحانَ ذي الْجَبَـروت، والمَلَـكوت، وَالكِبْـرِياء، وَالْعَظَـمَه



Subhaana dhil-Jabaruwti wal-malakuwti, wal-kibriyaai, wal-‘adhwamah



Ametakasika Mwenye Ujabari (Utawala, Utukufu), na Ufalme, na Ukubwa, na Uadhama [5].






[1]Hadiyth ya Hudhayfah bin Al-Yamaan (رضي الله عنه) - Ahlus-Sunan: Abu Daawuwd [871], At-Tirmidhiy [262], An-Nasaaiy (1/190), ibn Maajah [888], Ahmad (394, 382/5) na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (1/83)



[2]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy (1/99), Muslim (1/350)



[3]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - Muslim (1/353), Abu Daawuwd (1/230)



[4]Hadiyth ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (رضي الله عنه) - Muslim (1/534) na Maimamu wane wa Hadiyth isipokuwa ibn Maajah. Isipokuwa kauli ya “Wamastaqalla bihi qadamiy” haikupokelewa na Muslim wala Maimamu wanne, bali ametamka Ibn Hibbaan. Angalia: Swahiyh ibn Hibbaan [1901] na Swahiyh Ibn Khuzaymah [607]



[5]Hadiyth ya ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (1/230), An-Nasaaiy (2/191), Ahmad (6/24) na isnadi yake ni Hasan.
 
018-Du’aa Ya Kuinuka Kutoka Kenye Rukuu

www.alhidaaya.com





Bonyeza Hapa Usikilize







[38]

سَمِـعَ اللهُ لِمَـنْ حَمِـدَه



Sami’a Allaahu liman hamidah



Allaah Amemsikia mwenye kumsifu[1]







[39]

رَبَّنـا وَلَكَ الحَمْـدُ حَمْـداً كَثـيراً طَيِّـباً مُـبارَكاً فيه



Rabbanaa walakal-hamdu, hamdan kathiyran twayyiban mubaarakan fiyhi



Ee Rabb wetu, ni Zako Himdi, Himdi nyingi, nzuri, zenye Baraka[2]







[40]



مِلْءَ السَّمـواتِ وَمِلْءَ الأَرْض، وَما بَيْـنَهُمـا، وَمِلْءَ ما شِئْـتَ مِنْ شَيءٍ بَعْـدْ، أَهـلَ الثَّـناءِ وَالمَجـدْ، أَحَـقُّ ما قالَ العَبْـد، وَكُلُّـنا لَكَ عَـبدٌ، اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد



Mil-as-samawaatil wamil-al-ardhwi wamaa baynahumaa, wamil-a maa Shi-ita min shay-in ba’du. Ahlath-thanaa-i walmajdi. Ahaqqu maa qaalal-‘abdu, wakullunaa Laka ‘abdun. Allaahumma laa maani’a limaa A’-twayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu



Zimejaa mbingu na zimejaa ardhi na vilivyomo ndani yake (Himdi Zako), na zimejaa (Himdi Zako) kwa Ulichokitaka baada yake, Wewe ni Mstahiki wa Sifa na Utukufu, ni kweli aliyoyasema mja (Wako), na sote (sisi) ni waja Wako, Ee Allaah, hakuna mwenye kukizuia Ulichokitoa, wala mwenye kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.[3].






[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/282)



[2]Hadiyth ya Rifaa’ah bin Raafi’ Az-Zurqiyy (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (2/284)



[3]Hadiyth ya Abu Sa’iy Al-Khudriyy (رضي الله عنه) - Muslim (1/346)
 
019-Du’aa Za Wakati Wa Kusujudu

www.alhidaaya.com





Bonyeza Hapa Usikilize





[41]

سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى



Subhaana Rabbiyal a’-laa



Ametakasika Rabb wangu Aliye juu[1] (mara 3)







[42]

سُبْـحانَكَ اللّهُـمَّ رَبَّـنا وَبِحَـمْدِكَ، اللّهُـمَّ اغْفِرْ لي



Subhaanaka Allaahumma Rabbanaa wabihamdika, Allaahummagh-firliy



Utakasifu ni Wako Ee Allaah, Rabb wetu, na Himdi ni Zako, Ee Allaah nighufurie [2]





[43]

سُبـّوحٌ قُـدّْوس، رَبُّ الملائِكَـةِ وَالـرُّوح



Subbuwhun Qudduwsun, Rabbul-Malaaikati war-Ruwh



Mwingi wa kutakaswa, Mtakatifu, Rabb wa Malaika na Roho[3]





[44]



اللّهُـمَّ لَكَ سَـجَدْتُ وَبِـكَ آمَنْـتُ، وَلَكَ أَسْلَـمْتُ، سَجَـدَ وَجْهِـيُ لِلَّـذي خَلَقَـهُ وَصَـوَّرَهُ وَشَقَّ سَمْـعَـهُ وَبَصَـرَهُ، تَبـارَكَ اللهُ أَحْسـنُ الخـالِقيـن


Allaahumma Laka sajjadtu, wabika aamantu, walaka aslamtu. Sajada wajhiya liLLadhiy khalaqahu, wa swaw-warahu, wa shaqqa sam-’ahu wa baswarahu, Tabaaraka-Allaahu Ahsanul-Khaaliqiyn



Ee Allaah Kwako nimesujudu, na Wewe nimekuamini, na Kwako nimesilimu, umesujudu uso wangu kumsujudia Aliyeuumba na Akautia sura na Akaupasua usikizi wake na uwoni wake, Amebarikika Allaah Mbora wa waumbaji [4]







[45]

سُبْـحانَ ذي الْجَبَـروت، والمَلَـكوت، وَالكِبْـرِياء، وَالْعَظَـمَه



Subhaana dhil-Jabaruwti wal-malakuwti, wal-kibriyaai, wal-‘adhwamah



Ametakasika Mwenye Ujabari (Utawala, Utukufu), na Ufalme, na Ukubwa, na Uadhama [5].





[46]

اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي ذَنْـبي كُلَّـه، دِقَّـهُ وَجِلَّـه، وَأَوَّلَـهُ وَآخِـرَه وَعَلانِيَتَـهُ وَسِـرَّه



Allaahummagh-firliy dhambiy kullahu diqqahu wajillahu wa awwalahu wa aakhirahu wa ’alaaniyatahu, wasirrahu



Ee Allaah nighufurie dhambi zangu zote, ndogo na kubwa, za mwanzo na za mwisho, za dhahiri na za siri[6]







[47]



اللّهُـمَّ إِنِّـي أَعـوذُ بِرِضـاكَ مِنْ سَخَطِـك، وَبِمعـافاتِـكَ مِنْ عُقوبَـتِك، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْـك، لا أُحْصـي ثَنـاءً عَلَـيْك، أَنْـتَ كَمـا أَثْنَـيْتَ عَلـى نَفْسـِك



Allaahumma inniy a’uwdhu biridhwaaka min sakhatwika, wabimu’aafaatika min ’uquwbatika, wa a’uwdhu Bika Minka, laa uhswiy thanaa-an ’Alayka, Anta kamaa athnayta ’alaa Nafsika



Ee Allaah hakika mimi najikinga kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako, na kwa msamaha Wako kutokana na adhabu Yako, na najikinga Kwako unihifadhi na Wewe, mimi siwezi kuzidhibiti sifa Zako, Wewe ni kama ulivyojisifu Mwenyewe[7].






[1]Hadiyth ya Hudhayfah bin Al-Yamaan (رضي الله عنه) - Ahlus-Sunan: Abu Daawuwd [871], At-Tirmdhiy [262], An-Nasaaiy (1/190) Ibn Maajah [888], Ahmad [394, 382] na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (1/83)



[2]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) imetangulia namba 34 juu - Al-Bukhaariy (1/99), Muslim (1/350).



[3]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) imetangulia juu namba 35 -Muslim (1/353), Abu Daawud (1/230)



[4]Hadiyth ya ‘Aliy bin Twaalib (رضي الله عنه) - Muslim (1/534) na wengineo.



[5]Hadiyth ya ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (1/230), An-Nasaaiy (2/191), Ahmad (6/24) na isnadi yake ni Hasan.

Abu Daawuwd (1/230), Ahmad (6/24), An-Nasaaiy (2/191) na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/166) (Pia imetangulia katika Du’aa Namba 37)



[6]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (1/350)



[7]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - Muslim (1/352)
 
020-Du’aa Za Kikao Kati Ya Sijdah Mbili

www.alhidaaya.com





Bonyeza Hapa Usikilize





[48]

رَبِّ اغْفِـرْ لي، رَبِّ اغْفِـرْ لي



Rabbighfir-liy, Rabbighfir-liy



Rabb nighufurie, Rabb nighufurie[1]







[49]

اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي، وَارْحَمْـني، وَاهْدِنـي، وَاجْبُرْنـي، وَعافِنـي وَارْزُقْنـي وَارْفَعْـني



Allaahummaghfir-liy, warhamniy, wahdiniy, wajburniy, wa ’aafiniy, warzuqniy, warfa’-niy



Ee Allaah nighufurie, na unirehemu, na uniongoze, na uniungie, na unipe afya, na uniruzuku na uniinue[2]






[1]Hadiyth ya Hudhayfah bin Al-Yamaan (رضي الله عنه) Abu Daawuwd (1/231) na angalia: Swahiyh Ibn Maajah (1/148)



[2]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) - Aswhaab As-Sunan isipokuwa An-Nasaaiy; Abu Daawuwd [850], At-Tirmdihiy [284], Ibn Maajah [898], na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (1/90) na Swahiyh ibn Maajah (1/148)
 
Adhkaar Za Baada Ya Swalah Tasbiyh, Tahmiyd Na Takbiyr Mara 33
Maswali: Vitendo-Kauli


SWALI:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullahi Taalah Wa Barakatuh,
kuna mtu ameuliza swali lifutalo nami nimeona niwatumie nyinyi mlijibu. Inajulikana kuwa baada ya salah unasema
SUBHANNA LLAHU 33TIMES,
ALHAMDULLILLAHI 33TIMES NA
ALLAHU AKBAR 33 TIMES
so suala lake yeye,JEEE INAJUZU AKAWA ASOMA HIZO ZOTE BADALA YA 33 AKAWA ANASOMA 100 TIMES each one,yaani SUBAHHANNALLAH 100 times,ALHAMDULILLAHI 100 NA ALLAH AKBAR 100 kwa kila salah zake za fardhi na sunnah? well ktk maongezi yake nikamuuliza kwa nn anasema asome 100 times?akanambia anaona kama akisoma 100 times she loosing nothing after all anasema shughuli zote hizo kama atakuwa anasoma 100timess each itam-cost abt 20min while she can spends 5hrs-8hrs a day kuangalia tv na mambo mengine so anahizi kwa nini asipoteze 20min kwa kila salah kuongea,kumsifu,na kumpwekesha allah?











JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Jibu ni kwamba, ingawa ni kitendo chema kumdhukuru Allaah kwa wingi, lakini tunapaswa kufahamu kuwa vitendo vya ibaada ni tawqifiy - kwa maana vitekelezwe kama tunavyopata mafunzo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam).


Mafunzo hayo ya kumdhukuru Allaah kwa idadi ya 33 kila baada ya Swalah yamo katika dalili ya mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam). Haikutajwa kuwa hapo baada ya Swalah tumdhukuru zaidi ya hivyo katika kutaja hizo tasbiyh, (Subhaana Allah) tahmiyd (AlhamduliLlaah) na takbiyr (Allaahu Akbar). Hivyo basi kufanya kinyume na idadi hiyo itakuwa ni kuyageuza mafunzo ya tuliyoletewa na mbora wa viumbe na tukaweka ufundi wetu na mwisho kuingia katika kupingana na tuliyofunzwa, na kwa maana nyingine ni kumfanya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa alihi wa sallam) kuwa hakuwa akijua umuhimu wa kuzifanya ziwe mara mia kama ndugu yetu anavyoona. Pia bila ya shaka kuna hikma ya kuwekewa idadi kadha ya adhkaar ambayo hatuwezi kujua sisi ila Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Aliyempa wahyi (ufunuo) Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwani yeye hasemi kwa matamanio yake:



((وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَى)) (( إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَى))

((Wala hatamki kwa matamanio)) ((Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa)) [An-Najm: 3-4]

Mfano, tumepata mafunzo ya kujua faida ya kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa adhkaar kama hizo mara 33 kabla ya kulala katika usimulizi ufuatao:

وعن أبي هريرة رضي الله عنه أن فاطمة رضي الله تعالى عنها أتت النبي صلى الله عليه وسلم تسأله خادماً وشكت العمل، فقال صلى الله عليه وسلم: ((ألا أدلك على ما هو خير لك من خادم، تسبحين ثلاثاً وثلاثين: وتحمدين ثلاثاً وثلاثين، وتكبرّين أربعاً وثلاثين، حين تأخذين مضجعك)) أخرجه مسلم .

Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Faatwimah (Radhiya Allaahu 'anha) alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kumuomba mtumishi akilalamika kazi [za nyumba]. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Je nikupe lililo bora kuliko mtumishi? Ufanye tasbiyh mara thelathini na tatu, tahmiyd mara thelathini na tatu, takbiyr mara thelathini na nne unapokwenda kulala)) [Muslim]

Baada ya kutekeleza hayo, 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu) mume wa Faatwimah alikiri maajabu na faida kubwa walizoziona ya mabadiliko ya maisha yao hata akasema kwamba hawakuwa wakiacha abadan kuleta hizo adhkaar walipokuwa wakilala.

Kwa hiyo hatuwezi sisi kujua ya hikma au mambo ya ghayb ila ni wajib wetu kusema sami'naa wa atwaa'naa (tumesikia na kutii)

Muislamu anaweza kumdhukuru Allaah (Subhaana wa Ta'ala) wakati wote apendao masaa 24 kwa siku bila hata ya kupoteza dakika moja, kwa sababu kumdhukuru Allaah hakuna kikwazo wala hakuna mipaka, sio kama ibada nyinginezo. Ndimi zetu zinatakiwa daima zishughulishwe na adhkaar. Kwa hivyo basi afanye hivyo wakati mwengine wowote hata anapokuwa anafanya kazi zake kama za nyumba n.k.


Ama kwenda kinyume na yale tuliyofundishwa ni jambo lisilofaa na la hatari.

Anachotakiwa baada ya Swalah azisome hizo idadi kama zilivyotajwa yaani 33 - kisha atakapomaliza anaweza kubakia hapo na kuleta Adkhaar nyinginezo ima kwa idadi kama ziko kwenye dalili au kuleta bila ya idadi maalumu.

La muhimu pia ni kwamba idadi yoyote atakayoleta katika adhkaar, anaweza kuleta bila ya kuweka idadi maalumu ikawa ndio ada yake kila siku au kila wakati fulani. Anaweza tu kuleta idadi maalumu ikiwa ipo dalili. Tutambue kwamba mafunzo yetu yote yanapasa yatokane na dalili.

Kitabu cha Hiswnul Muslim kifuatacho kina dalili za idadi ya aina za dhikri kama hizo zilizotajwa.

Tunatumai kwamba mafunzo haya yatatekelezwa ili kupata thawabu zake bila ya upungufu kwa kufuata mafunzo ya Sunnah.

Na Allaah Anajua zaidi.

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)



025-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Baada Ya Kutoa Salaam Ya Kumaliza Swalaah



130-Hiswnul-Muslim: Fadhila Za Tasbiyh, Tahmiyd, Tahliyl Na Takbiyr





Na Allah Anajua zaidi
 
Adkhaar Za Swalah Je, Inafaa Zisomwe Pia Katika Swalah Za Sunnah?
Maswali: Vitendo-Kauli








SWALI:



Assalaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh baada ya maamkizi hayo mema shukran zangu ziende kwa Mola wetu aliyetuumba Subhaana Wataala na pia alhidaaya. Sheikh nina maswali mengi kuhusu swala itakuwa vizuri kama utapata muda kunielimisha.



Baada ya swala ya fardhi kuna adhkaar ambazo Mtume wetu SWALA LLAH ALAYHI WASALLAM ametufundisha tuzisome JE swala za sunna nisome adhkaar zipi



JIBU:









Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kusoma Adhkaar baada ya Swalah za Sunnah.

Hatujapata katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alikuwa analeta Adhkaar kama zile za baada ya Swalah ya Faradhi kwenye Swalah za Sunnah.



Ile tuliyopata ni du’aa aliyokuwa akileta baada ya Swalah ya Sunnah kabla ya Alfajiri. Hii ni kutokana na mapokezi ya Ibn as-Sunniy kuwa ‘Aamir bin Usaamah kutoka kwa baba yake kuwa aliswali rakaa mbili za Alfajiri na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) yuko karibu naye aliswali rakaa mbili nyepesi kisha akamsikia anasema naye amekaa: “Allaahumma Rabba Jibriyl wa Israafiyl wa Miyka’iyl wa Muhammad an-Nabiyy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), A‘udhu bika minan Naar”. Alikariri mara tatu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Akiswali Pekee Swalah Za Jahriyyah (Za Kusomwa Kwa Sauti), Ni Lazima Atoe Sauti?
Maswali: Vitendo-Kauli


SWALI:



Nashkuru sana kwa kupata nafasi kama hii yakuweza kusoma na kuskiza mawaidha na manufaa mengi kutoka kwa hii website.mungu awajazi kheri na awajaalie muzidi kutupa faida,amin



Swali langu ni kuwa kama twasali swala ya maghrib au ishaa,je nilazima tusome suatul faatiha na sura nyengine kwasauti hata kama naswali pekeyangu?




JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Inafahamika kwa kila mmoja wetu kuwa Ibadah ya Swalah inatakiwa tufuate muongozo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hii ni kwa mujibu wa maneno yake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

"Swalini kama mulivyoniona nikiswali" (al-Bukhaariy).



Kwa ajili hiyo hata kama Muislamu anaswali peke yake yake Swalah ya kutoa sauti kama Alfajiri, Maghrib au 'Ishaa inafaa atoe sauti. Wanachuoni wanasema kuwa kutoa sauti katika Swalah za sauti ni katika Sunnah iliyokokotezwa (iliyohimizwa) sana hivyo haifai kwa Muislamu kuacha kufuata kwa makusudi.



Na Allaah Anajua zaidi
 
UJUMBE WA LEO:

Imepokewa kutoka kwa Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna kitu chochote kilicho kizito zaidi katika mizani ya Muumini Siku ya Qiyaamah kuliko tabia nzuri. Na hakika Allaah anamchukia mwenye kutoa maneno machafu na ya kishenzi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh].
 
Tarjama Ya Maana Ya AL-QUR-AAN AL-'ADHWIYM (Alhidaaya) /001 - Al-Faatihah
001 - Al-Faatihah





الْفَأتِحَة

001-Al-Faatihah



001-Al-Faatihah: Utangulizi Wa Suwrah



Alhidaaya.com









بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿١﴾

1. Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu)[1].





الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٢﴾

2. AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki) Allaah Rabb wa walimwengu.





الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ ﴿٣﴾

3. Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu.



مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ ﴿٤﴾

4. Mfalme wa Siku ya Malipo.





إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ ﴿٥﴾

5. Wewe Pekee tunakuabudu na Wewe Pekee tunakuomba msaada.[2]



اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ ﴿٦﴾

6. Tuongoze njia iliyonyooka.[3]





صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ ﴿٧﴾

7. Njia ya wale Uliowaneemesha, si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.[4]


[1] Tofauti Ya Jina Na Sifa Ya Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu).



Ar-Rahmaan: Sifa ya Jina hili ni pana zaidi na ni Sifa yenye kuenea zaidi kuliko Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu). Sifa hii inakusanya maana zote za Rehma, huruma n.k. Allaah Ndiye Mwenye Rehma iliyokusanya kila kitu, iliyoenea kwa viumbe Vyake vyote duniani; wanaadamu, majini, Waumini, makafiri, wanyama, mimea na kadhaalika. Hakuna yeyote au chochote katika kuwepo kwake ila Rehma Yake imemuenea. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ﴿٥﴾

Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Yuko juu ya ‘Arshi. [Twaahaa (20:50]



Na Sifa ya Majina mawili ya Ar-Rahmaan na Ar-Rahiym yanatokana na herufi tatu za asili, hivyo basi asili yake ni maana moja, isipokuwa tu kama ilivyobainishwa katika Sifa ya Rahmaan kuwa ni Rehma inayowafikia viumbe wote. Ama Rahiym ni Sifa khaswa kwa ajili ya Waumini pekee kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا ﴿٤٣﴾

Naye daima Ni Mwenye Kurehemu Waumini. [Al-Ahzaab: (33:43)]





[2] Isti’aanah (Kuomba Msaada):



Rejea makala ifuatayo kupata faida:



18-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aanah (Kuomba Msaada) Kwa Asiyekuwa Allaah



Rejea pia Al-Anfaal (8:9), Al-Qaswasw (28:15) kupata maana ya Istighaathah (Kuomba Uokozi).



[3] Maana Ya Swiraatw Al-Mustaqiym (Njia Iliyonyooka):



Hadiyth Ya Kwanza:

Amesimulia An-Nawaas bin Sam’aan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Allaah (تعالى) Amepiga mfano Swiraatw (njia) iliyonyooka, imezungukwa pande zote na kuta mbili na kila ukuta una milango iliyo wazi na imefunikwa na mapazia. Na katika lango la Swiraatw kuna mlinganiaji akiita: “Enyi watu! Ingieni nyote katika swiraatw na msipite pembeni.” Na juu ya Swiraatw, kuna mlinganiaji mwengine anamuonya mtu yeyote anayetaka kufungua hiyo milango akiwaambia: Ole wenu! Msiufungue! Kwani mkifungua mtapita ndani! Kwani Asw-Swiraatw ni Uislaam, na kuta mbili ni mipaka Aliyoiweka Allaah. Na milango iliyofunguliwa ni yaliyoharamishwa na Allaah. Na huyo mlinganiaji juu ya lango la Swiraatw ni Kitabu cha Allaah, na mlinganiaji juu ya Swiraatw ni Maonyo ya Allaah yaliyo ndani ya kila nafsi ya Muislamu.” [Ahmad, ameisahihisha Al-Albaaniy; Swahiyh Al-Jaami’ (3887)]



Hadiyth Ya Pili:

Amesimulia Jaabir (رضي الله عنه): Tulikuwa tumekaa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akachora mstari mbele yake, kisha akachora mistari miwili kuliani, na mistari miwili kushotoni, kisha akaweka mkono wake katika njia ya katikati akasema: “Hii Njia ya Allaah.” Kisha akasoma:



وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ

Na kwamba hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake. [Al-An’aam (6:153)]

[Ahmad, Swahiyh Ibn Maajah (11)]



Rejea pia (Aal-‘Imraan (3:103) (3:105), Al-An’aam (6:153).



[4] Nani Walioghadhibikiwa Na Waliopotea:



Amesimulia ‘Adiy bin Haatim (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Walioghadhibikiwa ni Mayahudi, na waliopotea ni Manaswara.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Ghariyb na taz. Silsilah Asw-Swahiyhah (363)]
 
002-Al-Baqarah: Utangulizi Wa Suwrah



Alhidaaya.com





Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.



Idadi Ya Aayah: 286



Jina La Suwrah Al-Baqarah:



Suwrah imeitwa Al-Baqarah (Ng’ombe), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila za Suwrah. Na pia kwa kutajwa kwake katika Aayah namba (67).



Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:



1-Kulithibitisha jambo la ukhalifa (urithisaji wa kutawala) katika ardhi, kwa kuusimamisha Uislamu, na watu wote kunyenyekea kwa Allaah (سبحانه وتعالى), na kuchukua tahadhari juu ya hali iliyowatokea Bani Israaiyl. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]



2-Kuelezea baadhi ya sifa za wanafiki.



3-Kuelezea baadhi ya sifa za Mayahudi katika itikadi zao, na katika kuasi amri za Allaah na Rasuli wao, na mengineyo waliyoyafanyia inadi.



4-Kubainisha umuhmu wa ‘Aqiydah na kubainisha misingi yake.



5-Kubainisha dalili zenye kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah na Uwezo Wake wa kila kitu, na hoja za wazi kabisa za kuthibitisha kufufuliwa.



6-Kubainisha baadhi ya Sharia za Kiislamu katika ibaada mbalimbali, maswala ya ndoa, na miamala ya kifedha, au adhabu kutokana na makosa mbalimbali, yasiyokuwa hayo.



Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:



1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya namba (2:1). Kisha ikathibitisha kwamba Qur-aan haina shaka ndani yake, na kwamba ni mwongozo, na kuwasifu Waumini wanaomkhofu Rabb wao kwa ghaibu, na wanaosimamisha Swalaah na kutoa Zakaah. Pia wanaoamini yote Aliyoyateremsha Allaah, na wanoamini Siku ya Mwisho, kisha wakabashiriwa kuwa hao ndio waliohidiwa na waliofaulu.



2-Imebainisha aina za watu, ambao ni Waumini, makafiri na wanafiki na zimetajwa baadhi ya kufru na uasi wao.



3-Wameusiwa watu wote kumuabudu Rabb wao, na zikatajwa dalili zinazothibitisha kuwa Anaestahiki kuabudiwa ni Allaah Pekee, na kuwapa tahadhari watakaoabudu ghairi ya Allaah. Kisha Waumini wamebashiriwa Jannaat za kudumu walizoandaliwa na Allaah (سبحانه وتعالى).



4-Imetajwa majadiliano kati ya Allaah (سبحانه وتعالى) na Malaika kuhusu Kumuumba Nabiy Aadam (عليه السّلام), na Aadam kupewa ukhalifa hapa ardhini, na jinsi Ibliys alivyokataa amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kumsujudia Aadam na kumshawishi kwake Aadam akamtelezesha, na tawbah ya Aadam (عليه السّلام).



5-Imetajwa sehemu ya kisa cha Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na kufadhilishwa kwa wana wa Israaiyl katika hali kadhaa, kama kuokolewa na mateso ya Firawni, kuwekewa kivuli, kuteremshiwa al-manna na as-salwaa na kadhaalika. Na imetajwa baadhi ya maasi yao, na inda zao za kutaka kumuona Allaah waziwazi. Imetajwa pia shirki zao za kumwabudu ndama, na zikatajwa baadhi ya adhabu zao.



6-Kimetajwa kisa cha Al-Baqarah (Ng’ombe) na imebainishwa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa kuhuisha na kufisha.



7-Wamebashiriwa adhabu watu wa Kitabu kutokana na kubadilisha Maneno ya Allaah kwa kutaka manufaa ya dunia, na kukanusha Kitabu cha Allaah kwa kujitenga nacho na kumkanusha Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم).



8-Wamebashiriwa adhabu wana wa Israaiyl kwa kuvunja kwao baadhi ya ahadi na fungamano kadhaa walizofungamana na Allaah, na kuamini kwao sehemu ya Kitabu na kukanusha mengineyo. Pia uasi wao wa kuwakanusha na kuwaua baadhi ya Rusuli. Pia kuasi kwao katika mambo kadhaa, na kukhiari kwao uhai wa dunia.



9-Allaah (سبحانه وتعالى) Amemwambia Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم), awaambie waliomfanyia uadui Jibriyl (عليه السّلام), watambue kwamba yeye ndiye aliyeiteremsha Qur-aan kwake (صلى الله عليه وآله وسلم). Hivyo basi, kumfanyia kwao uadui Allaah na Rusuli Wake, na Malaika Wake khasa Malaika wawili Jibriyl na Miykaaiyl, kwamba wao ni maadui wa Allaah. Na Allaah (سبحانه وتعالى) Akamliwaza Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuthibitisha kuwa Qur-aan ni ya haki na imetoka Kwake.



10-Imetolewa tahadharisho la kuwafuata mashaytwaan wanaofundisha watu uchawi (2:102), na la kufuata twaghuti (2:256-257).



11-Allaah (سبحانه وتعالى) Amefichua chuki na uhasidi wa waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara), kuchukia kheri na Fadhila za Allaah Alizomteremshia Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwamba wanatamani Waislamu wawe makafiri kama wao.



12-Radd kwa makafiri kumsingizia Allaah kuwa kajichukulia mwana, ilhali Allaah Ametakasika na hayo!



13-Imetanabahishwa kwamba watu waliopewa Kitabu hawataridhia mpaka Waislamu wafuate mila zao, na wameonywa Waislamu kutokuwafuata au kufuata matamanio yao, bali wameamrishwa wathibitike katika Dini ya haki.



14-Imetajwa Allaah kumtahini Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa maneno. Na kuhusu ujenzi wa Al-Ka’bah alipojenga Nabiy Ibraahiym na mwanawe Ismaa’iyl, na du’aa walizoziomba kuwaombea vizazi vyao, na kumuomba Allaah Awapelekee Rasuli atakayewasomea Aayah Zake, na kuwafunza Hikma na kuwatakasa.



15-Imetajwa wasia wa Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kwa wanawe, kisha Ya’quwb (عليه السّلام) kuwausia watoto wake watahadhari na wathibitike katika Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) hadi kufariki kwao.



16-Waislamu wamefaridhishwa Swibghah (Dini) ya Allaah yenye kuwaongoza katika ‘Aqiydah sahihi na mwenendo mzuri upasao wa Kiislamu. Rejea faida katika Aayah namba (138).



17-Suwrah hii imetaja faradhi zote za Muislamu (Shahaada, Swalaah, Zakaah, Swawm na Hajj). Hizi zimetajwa katika sehemu mbalimbali za Suwrah, kuanzia mwanzo wake na kwengineko. Pia, Suwrah imedhihirisha Sharia nyingi upande wa ibaada, yanayohusiana na Swalaah kama umuhimu wa kusimamisha Swalaah, na Qiblah cha Waislamu. Swawm na kuteremshwa Qur-aan ndani ya Ramadhwaan. Pia baadhi ya hukmu za Hajj.



18-Imedhihirishwa miamala, kadhaa kama mas-ala ya kisasi, uharamu wa riba kisha baada ya haramisho la riba ikafuatia Aayah ya mwisho kabisa kuteremshwa katika Qur-aan. (2:281). Pia miamala ya deni na Aayah ya deni ikawa ni Aayah ndefu zaidi kuliko Aayah zote katika Qur-aan. Pia miamala ya rehani na mengineyo. Na katika upande wa familia, mambo ya ndoa, talaka, hedhi, eda, mama kumnyonyesha mwanawe, viapo (vya kujitenga na wake zao) na hukmu nyenginezo.



19-Suwrah imeweka wazi matukio ya kuhuisha wafu ambayo yanadhihirisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) wa Kufufua wafu. Miongoni mwa hayo, ni kisa cha aliyeuwawa katika Bani Israaiyl na kuhusiana na Al-Baqarah (ng’ombe). Kisa cha wale waliokufa kwa radi. Kisa cha wale waliotoka katika majumba yao wakiwa maelfu kwa maelfu ilihali wanaogopa kufa Allaah (سبحانه وتعالى) Akawafisha kisha Akawafufua. Kisa cha yule aliyepita kwenye kijiji kikiwa magofu matupu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akamfisha miaka mia kisha Akamfufua (2:259). Na kisa cha Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na ndege waliokatwa vipande vipande na jinsi Allaah (سبحانه وتعالى) Alivyowafufua ndege hao kwa Kuunga vipande hivyo na mbele ya macho yake (2:260).



20-Wametahadharishwa watu kutokumfuata shaytwaan anayeelekeza katika uasi na machafu.



21-Wamebashiriwa Waja wa Allaah (سبحانه وتعالى) ambao wamejaaliwa hikma kwa kunena na kutenda yaliyo haki, kwamba hao wamejaaliwa kheri nyingi mno.



22-Imeelezea pia kisa cha Twaalutw na Jaalutw wakiwa pamoja na watukufu katika Bani Israaiyl baada ya Nabiy Muwsaa (عليه السّلام) na ikadhihirisha Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwapa ushindi waja wake wema kama Nabiy Daawuwd (عليه السّلام) katika kisa hicho cha Twaalutw na Jaalutw.



23-Imetajwa Aayah tukufu kabisa ambayo ni Aayatul-Kursiy. Na wakatahadharishwa Waislamu kutokumfuata twaghuti wasije kutoka katika nuru wakaingia vizani.



24-Imeelezea kisa cha mfalme Nimruwdh aliyehojiana na Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) kuhusu Rabb wake, akaangamizwa kwa kutakabari kwake kujifanya yeye ndiye mwenye uwezo wa kuhuisha na kufisha.


25-Imetajwa utoaji wa swadaqa kwa wingi na fadhila zake, na Allaah Akapiga mfano wa asiyetoa swadaqa na khasara zake. Na Waumini wameamrishwa kutoa vilivyo vizuri badala ya kutoa vilivyoharibika katika rizki za Allaah Alizomjaalia mtu. Na pia wamesifiwa wanaojizuia kuomba omba.



26-Imetaja uharamisho wa riba na ikatajwa Aayah ya mwisho kuteremshwa ambayo ni Aayah namba (281).



27-Imetajwa Aayah ndefu kabisa katika Qur-aan, nayo ni Aayah ya deni, Aayah namba (282).



28-Suwrah imekhitimishwa kwa kutajwa Aayah mbili ambazo zina fadhila adimu kama ilivyothibiti katika Hadiyth za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).



Fadhila za Suwrah:



Hadiyth mbalimbali zimethibiti, miongoni mwazo ni:



1-Atakayesoma Usiku Aayah Mbili Za Mwisho Zinamtosheleza:



حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا الأَعْمَشُ، قَالَ حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ، عَنْ عَلْقَمَةَ، وَعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الأَنْصَارِيِّ، قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم ‏ "‏ الآيَتَانِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ مَنْ قَرَأَ بِهِمَا فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ ‏"‏‏.‏



Amesimulia Abuu Mas‘uwd Al-Answaariyy: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Atakayesoma usiku Aayah mbili za mwisho wa Suwratul-Baqarah zitamtosheleza.” Yaani: zinamtosheleza kumkinga na kila baya na kila lenye kumdhuru. [Al-Bukhaariy na Muslim]



2-Shaytwaan Haingii Nyumba Inayosomwa Suwrah Al-Baqarah:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ لاَ تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ وَإِنَّ الْبَيْتَ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ الْبَقَرَةُ لاَ يَدْخُلُهُ الشَّيْطَانُ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ ‏



Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Msifanye nyumba zenu makaburi. Kwa hakika shaytwaan haingii nyumba ambayo husomwa humo Suwratul-Baqarah.” [At-Tirmidhiy Hadiyth Hasan Swahiyh] Na katika Riwaayah ya Muslim, Hadiyth (780): “Shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa ndani yake Suwratul-Baqarah.”



عن سَهْل بن سعد قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وآله وسلم : إِنَّ لِكُلِّ شَيْءٍ سَنَامًا، وَإِنَّ سَنَامَ القُرْآنِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ، مَنْ قَرَأَهَا فِي بَيْتِهِ لَيْلًا لَمْ يَدْخُلِ الشَّيْطَانُ بَيْتَهُ ثَلَاثَ لَيَالٍ، وَمَنْ قَرَأَهَا نَهَارًا لَمْ يَدْخُلِ الشَّيْطَانُ بَيْتَهُ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ



Amesimulia Sahl bin Sa’d (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kila kitu kina kinara, na Al-Baqarah ndio kinara cha Qur-aan. Atakayesoma Al-Baqarah usiku nyumbani kwake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba yake nyusiku tatu. Na atakayesoma mchana ndani ya nyumba yake, shaytwaan hatoingia ndani ya nyumba hiyo kwa siku tatu.” [Atw-Twabaraaniy (6/163), Ibn Hibbaan (2/78) na Ibn Mardawayh, Swahiyh At-Targhiyb (2/314)]



3-Suwrah Al-Baqarah Ni Taa Mbili Zitakazomuombea Mtu Siku Ya Qiyaamah, Na Kushikamana Nayo Ni Baraka, Kuicha Ni Majuto, Na Wachawi Hawaiwezi:



عن ابي أُمَامَةَ الْبَاهِلِيُّ قَالَ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ ‏ "‏ اقْرَءُوا الْقُرْآنَ فَإِنَّهُ يَأْتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ شَفِيعًا لأَصْحَابِهِ اقْرَءُوا الزَّهْرَاوَيْنِ الْبَقَرَةَ وَسُورَةَ آلِ عِمْرَانَ فَإِنَّهُمَا تَأْتِيَانِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ كَأَنَّهُمَا غَمَامَتَانِ أَوْ كَأَنَّهُمَا غَيَايَتَانِ أَوْ كَأَنَّهُمَا فِرْقَانِ مِنْ طَيْرٍ صَوَافَّ تُحَاجَّانِ عَنْ أَصْحَابِهِمَا اقْرَءُوا سُورَةَ الْبَقَرَةِ فَإِنَّ أَخْذَهَا بَرَكَةٌ وَتَرْكَهَا حَسْرَةٌ وَلاَ تَسْتَطِيعُهَا الْبَطَلَةُ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ مُعَاوِيَةُ بَلَغَنِي أَنَّ الْبَطَلَةَ السَّحَرَةُ ‏.‏

Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan kwani zitakuja Siku ya Qiyaamah kama kwamba ni maumbile ya mawingu, au sehemu mbili za mawingu, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka. Zitawatetea watu wake (walioshikamana nazo) siku hiyo. Someni Suwratul-Baqarah, kwani kushikamana nayo ni baraka, na kuiacha kwake ni majuto, na wachawi hawawezi kuihifadhi kwa moyo.” [Muslim (804)]



Rejea pia Utangulizi wa Suwrah Aal-‘Imraan kupata fadhila nyenginezo zinazohusiana na Suwrah hii ya Al-Baqarah.



Faida:




Suwrah hii ni Suwrah ndefu kabisa kuliko Suwrah zote za Qur-aan. Ndani yake kuna hukmu za faradhi kadhaa kama Swalaah, Swiyaam za Ramadhwaan, Hajj, na hukmu nyenginezo ambazo Waislamu wanazihitaji katika maisha yao ya kijamii ya kila siku.



Pia zimetajwa maudhui mbalimbali, pamoja visa kadhaa, vikiwemo visa vyenye kudalilisha miujiza ya Allaah na Uwezo Wake wa kuhuisha na kufisha. Kisa kimojawapi ni kisa cha Al-Baqarah (Ng’ombe), ambacho ni kuhusu mtu aliyemuua mwenzie zama za Nabiy Muwsaa (عليه السّلام), ikawa hakujulikana nani aliyemuua mtu huyo. Basi Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaamrisha wana wa Israaiyl wamchinje ng’ombe, kisha wampige maiti huyo kwa kipande cha sehemu ya ng’ombe. Kisha Allaah (سبحانه وتعالى) Akumhuisha mtu huyo, nae akawa hai na akataja mtu aliyemuua. Na hii ni ushahidi wa Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى) kuwa ni Muweza wa kufufua wafu baada ya kufa kwao na Muweza wa kila kitu. Rejea Aayah (67-73).



Na katika kutofautisha na Suwrah nyenginezo, ni kuweko ndani yake Aayatul-Kursiyy ambayo ni Aayah Tukufu kabisa ya Qur-aan. Pia Aayah mbili za mwisho wa Suwrah, ambazo amepewa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) pekee katika Manabii, alipokuwa mbingu ya saba katika Safari ya Al-Israa na Al-Mi’raaj.
 
003-Aal-Imraan: Utangulizi Wa Suwrah



Alhidaaya.com







Imeteremka: Madiynah kwa itifaki ya ‘Ulamaa.



Idadi Za Aayah: 200



Jina La Suwrah:



Imeitwa Aal-‘Imraan (Familia Ya ‘Imraan), na yanayodalilisha ni kutajwa kwake katika Hadiyth zilizonukuliwa katika Fadhila za Suwrah, na pia kutajwa kwake katika Aayah namba (35).



Miongoni Mwa Makusudio Ya Suwrah:



1-Uthibitisho kwamba Dini ya Kiislamu ndio ya Dini ya haki. Radd (kujibu kwa kukanusha) kwa shubuhaat (tuhuma) za Watu wa Kitabu (Mayahudi na Naswara). Kuwathibitisha Waumini. [Al-Mukhtaswar Fiy Tafsiyr Al-Qur-aan Al-Kariym]



2-Kuthibitisha Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kwamba Allaah ni Mmoja, na kusimamisha dalili na hoja juu ya hilo



3-Kubainisha ‘Al-Walaa na Al-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah), na tahadhari juu ya kumtawalisha asiye kuwa Muumini.



4-Kuchambua hali za Ahlul-Kitaab na baadhi ya itikadi zao na maasi yao.



5-Kuupa umuhimu upande wa malezi, na maelekezo kwa Waumini.



Miongoni Mwa Maudhui Ya Suwrah:



1-Suwrah imefunguliwa kwa herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Al-Baqarah (2:1). Kisha imethibitishwa kwamba Allaah ni Mmoja, na imeithibitishwa aina tatu za Tawhiyd: (i) Tawhiyd Al-Uluwhiyyah (Kumpwekesha Allaah katika ibaada). (ii) Tawhiyd Ar-Rubuwbiyyah (Kumpwekesha Allaah katika Uola Wake). (iii) Tawhiyd Asmaa Wasw-Swifaat (Kumpwekesha Allaah katika Majina Yake Mazuri Na Sifa Zake Kamilifu)



2-Imebainishwa watu walivyogawanyika kuhusu kuzifahamu Aayah zenye maana za wazi, na zisizokuwa wazi maana zake.



3-Wametahadharishwa makafiri wanaompinga Allaah na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba: Ufalme, nguvu, vyeo, watoto, mali, havitawasaidia mbele ya Adhabu ya Allaah, na kwamba mwisho wao ni khasara ya wazi Duniani na Aakhiirah. Na Allaah Akawapigia mifano ya Makafiri waliotangulia na wataokuja baada yao, na jinsi utavyokuwa mwisho wao.



4-Kumetajwa kutokea kwa Vita vitukufu vya Badr na Uhud. Na katika vita vya Uhud, kuna maelezo ya matukio ya vita hivi na mafunzo waliyopata Waumini walipoenda kinyume na matakwa ya Rasuli wao (صلى الله عليه وآله وسلم) katika mbinu za kupigana kwenye vita hivyo vya Uhud ikasababisha kushindwa kwa Waislamu. Vita hivyo vilibainisha na kuwafichua wazi Waumini wakweli na wanafiki.



5-Vimetajwa vitu vinavyopendwa zaidi na nafsi ya mwanaadam, na kutanabahishwa kwamba hivyo vyote ni vitu vya starehe fupi ya kilimwengu na pambo lake lenye kutoweka. Lakini kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kuna marejeo mazuri na thawabu adhimu ambazo Allaah Amewaandalia wenye taqwa, nayo ni Jannah yenye uhai wa starehe na neema za kudumu milele.



6-Imethibitishwa umuhimu wa Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى) na ndani yake imetaja mara nne Kalimah ya Tawhiyd ya Allaah (سبحانه وتعالى):

لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ

Na imeeleza pia Amri ya Allaah kwa Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) awalinganie kwenye neno la sawasawa, ambalo ni neno la Tawhiyd.



7-Suwrah inaongoza katika hidaaya, kwani inawalingania watu wote kwenye Dini moja ya Uislamu na inawaambia kuhusu malipo watakayopewa watu wema na adhabu watakazopewa makafiri na kwamba Allaah (عزّ وجلّ) Haridhii dini yeyote ile isipokuwa Dini ya Kiislamu.



8-Suwrah imetaja kuhusu mke wa ‘Imraan, Bi Hannah na kumzaa kwake Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Imeelezewa kisha cha Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) na kuzaliwa kwa Yahyaa. Pia kuzaliwa kwa ‘Iysaa (عليهم السّلام). Rejea Aayah (36).



9-Kuna uchambuzi wa hali za Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu; Mayahudi na Manaswaara), na kuufedhehesha uovu na upotevu wao, ukiwemo kumpinga Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) na yaliyowatokea ambayo ni kutofautiana katika Dini zao, na maovu waliyoyafanya, ya kuzikadhibisha Aayaat za Allaah, na kuwauwa Manabii Wake, na wale wanaolingania haki. Na pia kule kugoma kwao kuhukumiwa na Kitabu cha Allaah.



10-Suwrah inawajadili Watu wa Kitabu kwa dalili, ushahidi na hoja za waziwazi kabisa za kuthibitisha kuwa Dini ya Kiislamu ndio Dini ya haki iliyokuja kukhitimisha Dini za Manabii wote waliotangulia. Basi Suwrah inakanusha upinzani wao dhidi ya Tawhiyd ya Allaah na ukanushaji wao wa Dini ya mwisho ya Kiislamu.



11-Suwrah imeeleza majadiliano yao juu ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) na kuwabainishia haki kwenye jambo lake (Ibraahiym), na kutaja sifa zao nyingi ambazo walikuwa nazo (Ahlul-Kitaab), kama vile walivyokuwa wakitaka kuwapoteza Waislam, na kule kuzipinga kwao Aayaat za Allaah, na kule kuchanganya kwao haki na baatwil, na kuingiza maneno yao kwenye Kitabu chao, kwa lengo la kuwarubuni na kuwadanganya Waumini, na yasiyokuwa hayo.



12-Imebainishwa kuwa Ahlul-Kitaab wa awali waliomwamini Allaah na kumwamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hawako sawa, na kwamba wako kati yao wanasoma Aayaat za Allaah (سبحانه وتعالى) usiku na mchana, na wanaamini Siku ya mwisho, wanaamrisha mema na kukataza mabaya.



13-Suwrah imetoa tanbihi juu ya ‘Aqiydah ya Al-Walaa Wal-Baraa (kupendana na kuchukiana kwa ajili ya Allaah), na kulisisitiza hilo, na tahadhari juu ya kuwapenda wasiokuwa Waumini.



14-Imebainishwa kuwa mapenzi ya Allaah yana alama na dalili zake, ikiwemo kumfuata Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumpenda Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumtii.



15-Imeeleza pia khabari za Manabii na kwamba daraja zao ni za juu, na kwamba Allaah (سبحانه وتعالى) Aliwachagua.



16-Imetajwa pia adabu nyingi za malezi, wasia wa kumcha Allaah (سبحانه وتعالى), kushikamana na Dini ya Allaah, kuacha kutengana na kukhtalifiana, na kuwaamrisha Waumini walinganie kheri, na kuwahimiza kutoa mali zao kwa njia ya Allaah.



17-Imetajwa baadhi ya Hukmu za Kisharia kama vile Jihaad, kuzuia watu kula riba, na adhabu za wanaozuia Zakaah.


18-Waumini wamefunzwa subra na wameshajiishwa kuhusu subra katika hali za neema na hali za misiba ya nafsi na mali na dhiki nyenginezo.



19-Imetajwa kuhusu Shuhadaa na fadhila zao. Hali kadhaalika imetajwa malipo watakayopata Waumini nayo ni Jannah na mapokezi mazuri humo kutoka kwa Rabb wao.



20-Imetajwa ukosefu wa adabu wa Mayahudi na dhulma yao kubwa iliyovuka mipaka kwa kumsingizia na kumpachika Allaah (سبحانه وتعالى) sifa ya ufakiri, ilhali Yeye Ni Al-Ghaniyy (Tajiri na Mkwasi Hahitaji lolote), na Allaah (سبحانه وتعالى) Akawaradd kwa hilo na kuwaadhidi adhabu waonje adhabu kali.



21-Wamesifiwa Waumini wenye kutafakari Uumbaji wa Allaah na wenye kumdhukuru Allaah (سبحانه وتعالى) kila nyakati na katika kila hali, na Kumpwekesha Allaah (سبحانه وتعالى) katika kumuomba duaa, na zikatajwa fadhila zao na malipo yao mazuri kabisa ya kuingizwa Jannah.



22-Suwrah imekhitimishwa kwa kuwataka Waumini wavute subira na ribaatw (wabakie imara) na wamche Allaah ili wapate kufaulu. Rejea katika faida ya Aayah ya mwisho kupata fadhila za ribaatw.



Fadhila za Suwrah:



1-Ni Taa Mbili Zitakazokuja Siku Ya Qiyaamah Kuwa Ni Shafaa’ah (Kiombezi) Kwa Wanaoisoma Na Kutekeleza Amri Zake:



عن أبي أُمامةَ الباهليِّ رضِي اللهُ عنه، قال: سمعتُ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يقول : اقْرَؤوا القُرْآنَ؛ فإنَّه يأتي يَومَ القيامةِ شفيعًا لأصحابه، اقرَؤوا الزَّهْرَاوَيْنِ: البقرةَ وسورةَ آلِ عِمْرانَ.

Amesimulia Abuu Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Someni Qur-aan kwani itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa ni shafaa’ah (kiombezi) kwa watu wake wanaoisoma na kutekeleza (amri zake). Someni taa mbili: Al-Baqarah na Aal-‘Imraan. [Muslim]



1-Itakuwa Kama Mawingu Mawili Na Itawatetea Wanaoisoma Na Kutekeleza Amri Zake:



Amesimulia An-Nawwaas bin Sam-‘aan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Siku ya kufufuliwa, Qur-aan na watu waliokuwa wakiisoma na kutekeleza mafunzo yake, wataletwa mbele wakitangulizwa na Suwratul-Baqarah na Aal-‘Imraan.” Akasema An-Nawwaas: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa mifano mitatu kwa Suwrah mbili hizi na sikusahau mifano hiyo tokea wakati huo. Alisema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): “Zitakuja kama mawingu mawili au vivuli viwili vyeusi kati yake kuna nuru, au makundi mawili ya ndege waliotandaza mbawa zao wakiruka, zitawatetea watu wake (wanaoshikamana nazo).” [Muslim]



Rejea pia Al-Baqarah kupata fadhila inayohusiana na Suwrah hii ya Aal-‘Imraan.



Faida:



Aal-‘Imraan ni baba yake Maryam mama wa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام). Rejea Aayah (35-37). Mama yake ni ndugu wa Nabiy Zakariyyah (عليه السّلام): Familia ya ‘Imraan ni miongoni mwa familia Alizozifadhilisha Allaah (سبحانه وتعالى) juu ya walimwengu. Rejea Aayah namba (33-34). Na kisa chao kimetajwa kwenye Aayah namba (35-37).



Aayah za mwisho wa Suwrah hii [Aal-‘Imraan: (190-200]) ni Aayah ambazo ameteremshiwa Nabiy Allaah (سبحانه وتعالى) usiku mmoja zikamliza mno. Nazo ni Sunnah za kuzisoma pindi mtu anapoamka kwa ajili ya Tahajjud (kuamka usiku kuswali).
 
Nitasitisha hii Tarjama,naona ni bora mjisomee wenyewe kwenye App au katika Misahafu ya Tafsiri
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب احتمال الأذى

076-Mlango Wa Kuvumilia Maudhi



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾

Na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. [Aal-'Imraan: 134]



وَلَمَن صَبَرَ وَغَفَرَ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ﴿٤٣﴾

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [Ash-Shuwraa: 43]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ رَجُلاً ، قَالَ : يَا رسول الله ، إنّ لي قَرَابةً أصِلُهم وَيَقْطَعُونِي ، وَأُحْسِنُ إلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إلَيَّ ، وَأحْلُمُ عَنهم وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ ! فَقَالَ : (( لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ ، فَكأنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ ، وَلاَ يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ تَعَالَى ظَهيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mimi nina jamaa wa karibu nawaunga, wao wananikata. Nawafanyia wema wao wananitendea uovu, nawafanyia upole wao wananifanyia ujinga." Akasema: "Ukiwa kama uanvyosema basi ni kama unawalisha jivu la moto. Msaada wa Allaah hautaacha kuwa pamoja nawe maadamu utadumu juu ya hilo." [Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب الغضب إِذَا انتهكت حرمات الشّرع والانتصار لدين الله تعالى

077-Mlango Wa Kuwa na Hasira Wakati Inapokiukwa Hukumu ya Sheria na Kuinusuru Dini ya Allaah Ta'aalaa



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّـهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ ۗ ﴿٣٠﴾

Na yeyote anayeadhimisha vitukufu vya Allaah basi hivyo ni khayr kwake mbele ya Rabb wake. [Al-Hajj: 30]



إِن تَنصُرُوا اللَّـهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ﴿٧﴾

Mkisaidia kunusuru Dini ya Allaah, (Allaah) Atakunusuruni na Ataithibitisha miguu yenu. [Muhammad: 7]





Hadiyth – 1

وعن أَبي مسعود عقبة بن عمرو البدري رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : إنِّي لأَتَأخَّرُ عَن صَلاةِ الصُّبْحِ مِنْ أَجْلِ فلانٍ مِمَّا يُطِيلُ بِنَا ! فَمَا رَأيْتُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم غَضِبَ في مَوْعِظَةٍ قَطُّ أشَدَّ مِمَّا غَضِبَ يَوْمَئذٍ ؛ فَقَالَ : (( يَا أَيُّهَا النَّاسُ ، إنَّ مِنْكُمْ مُنَفِّرِينَ ، فَأيُّكُمْ أمَّ النَّاسَ فَلْيُوجِزْ ؛ فَإنَّ مِنْ وَرَائِهِ الكَبِيرَ وَالصَّغِيرَ وَذَا الحَاجَةِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Mas'uwd 'Uqbah bin 'Amru Al-Badriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Mimi ninachelewa Swalaah ya Asubuhi kwa ajili ya fulani anarefusha kisomo." Sijaona Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameghadhibika katika mawaidha yoyote kama alivyokasirika siku hiyo. Akasema: "Enyi watu! Hakika miongoni mwenu kuna wenye kufukuza, Anaposwalisha mmoja wenu afupishe, kwani nyuma yake kuna wazee, na watoto wadogo, na wenye haja zao (shughuli zao)." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].





Hadiyth – 2

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَدِمَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ سَفرٍ ، وَقَدْ سَتَرْتُ سَهْوَةً لِي بِقِرَامٍ فِيهِ تَمَاثيلُ، فَلَمَّا رَآهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم هتكَهُ وَتَلَوَّنَ وَجهُهُ ، وقال : (( يَا عائِشَةُ ، أشَدُّ النَّاسِ عَذَاباً عِنْدَ اللهِ يَوْمَ القيَامَةِ الَّذِينَ يُضَاهُونَ بخَلْقِ اللهِ ! )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Alikuja Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka safari wakati ambao nilikuwa nimeangika pazia nyembamba iliyokuwa na sura (picha) nje ya chumba changu. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoiona hiyo pazia aliiharibu na sura zake zikabadilika, na hapo akasema: "Ee 'Aaishah! Watu watakao pata adhabu kali kutoka kwa Allaah Siku ya Qiyaamah ni wale ambao watakaokuwa wakitengeneza sura kwa mfano wa viumbe vya Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim].





Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : أن قرَيشاً أهَمَّهُمْ شَأنُ المَرأَةِ المخزومِيَّةِ الَّتي سَرَقَتْ ، فقالوا : مَنْ يُكَلِّمُ فِيهَا رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فقالوا : مَنْ يَجْتَرِئ عَلَيْهِ إِلاَّ أُسَامَةُ بنُ زَيْدٍ حِبُّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ؟ فَكَلَّمَهُ أُسَامَةُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أتَشْفَعُ في حَدٍّ مِنْ حُدُودِ الله تَعَالَى ؟! )) ثُمَّ قامَ فَاخْتَطَبَ ، ثُمَّ قَالَ : (( إنَّمَا أهْلَك مَنْ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الشَّرِيفُ تَرَكُوهُ ، وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ أقامُوا عَلَيْهِ الحَدَّ ، وَايْمُ الله ، لَوْ أَنَّ فَاطمَةَ بِنْتَ مُحمّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعتُ يَدَهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Makureshi walishughulishwa na kesi ya mwanamke wa Makhzuum aliyeiba, wakasema: "Hakuna anayeweza kuzungumza naye ila usamah bin Zayd kipenzi cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya jambo hilo?" wakasema: "Hakuna anayeweza kuzungumza naye ila Usamah bin Zayd kipenzi cha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)?" Usamah akazungumza naye, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Unamuombea msamaha kwa Hadd (adhabu) miongoni mwa adhabu za Allaah? Kisha akasimama akahutubia akasema: "Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu, walikuwa anapoiba kati yao mtukufu wanamwacha, na anapoiba kati yao dhaifu wanamuadhibu. Naapa kwa Allaah! Lau Faatimah bint Muhammad angeiba basi ningekata mkono wake." [Al-Bukhaariy na Muslim].





Hadiyth – 4

وعن أنس رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم رَأى نُخَامَةً في القبلَةِ ، فَشَقَّ ذَلِكَ عَلَيْهِ حَتَّى رُؤِيَ في وَجْهِهِ ؛ فَقَامَ فَحَكَّهُ بِيَدِهِ ، فَقَالَ : (( إن أحدَكُمْ إِذَا قَامَ فِي صَلاَتِهِ فَإنَّهُ يُنَاجِي رَبَّهُ ، وَإنَّ رَبَّهُ بَيْنَهُ وَبيْنَ القِبلْةِ ، فَلاَ يَبْزُقَنَّ أحَدُكُمْ قِبَلَ الْقِبْلَةِ ، وَلَكِنْ عَنْ يَسَارِهِ ، أَوْ تَحْتَ قَدَمِهِ )) ثُمَّ أخَذَ طَرَفَ رِدَائِهِ فَبَصَقَ فِيهِ ، ثُمَّ رَدَّ بَعْضَهُ عَلَى بَعْضٍ ، فَقَالَ : (( أَوْ يَفْعَلُ هكذا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliona kohozi kwenye Qiblah, Jambo hilo lilimkera mpaka likaonekana katika uso wake akasimama akalikwangua kwa mkono wake, Akasema: "Hakika mmoja wenu anaposimama katika Swalaah yake anazungumza na Rabb wake, na Rabb wake yuko baina yake na Qiblah. Hivyo, asiteme mmoja wenu sehemu ya Qiblah , lakini ateme kushotoni mwake au chini ya unyao wake." Kisha akashika ncha ya shuka yake juu ya nyingine akasema: "Au anaweza kufanya hivi." [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn





باب أمر وُلاة الأمور بالرفق برعاياهم ونصيحتهم والشفقة عليهم والنهي عن غشهم والتشديد عليهم وإهمال مصالحهم والغفلة عنهم وعن حوائجهم

078-Mlango Wa Jukumu la Viongozi Kuamiliana na Watu kwa Upole, Kuwanasihi, Kuwahurumia, Kukatazwa Kuwadanganya, Kuwawekea Vikwazo Bila Kuangalia Maslahi yao, Kughafilika Nao na Kutowatimizia Haja zao



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

وَاخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢١٥﴾

Na inamisha ubawa wako kwa anayekufuata miongoni mwa Waumini. [Ash-Shu'araa: 215]



إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ وَإِيتَاءِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَيَنْهَىٰ عَنِ الْفَحْشَاءِ وَالْمُنكَرِ وَالْبَغْيِ ۚ يَعِظُكُمْ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ﴿٩٠﴾

Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan na kuwapa (msaada) jamaa wa karibu; na Anakataza machafu na munkari na ukandamizaji. Anakuwaidhini ili huenda mkapata kukumbuka. [An-Nahl: 90]





Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( كُلُّكُمْ رَاعٍ ، وَكُلُّكُمْ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتهِ : الإمَامُ رَاعٍ وَمَسؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ في أهلِهِ وَمَسؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، وَالمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ في بَيْتِ زَوْجِهَا وَمَسْؤُولَةٌ عَنْ رَعِيَّتِهَا ، وَالخَادِمُ رَاعٍ في مال سيِّدِهِ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ ، وَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَمَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swaalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila mmoja ana majukumu (na ataulizwa) kwa wale walioko chini yake. Amiri ni mchunga na mwanamume ni mchunga kwa watu wake wa nyumbani na mke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake. Hivyo, kila mmoja wenu ni mchunga, na ataulizwa juu ya alichokichunga." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad].





Hadiyth – 2

وعن أَبي يعلى مَعْقِل بن يَسارٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَا مِنْ عَبْدٍ يَستَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً ، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ ، إِلاَّ حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الجَنَّة )) متفقٌ عليه .

وفي رواية : (( فَلَمْ يَحُطْهَا بِنُصْحِهِ لَمْ يَجِدْ رَائِحَةَ الجَنَّة )) .

وفي رواية لمسلم : (( مَا مِنْ أميرٍ يلي أمور المُسْلِمينَ ، ثُمَّ لا يَجْهَدُ لَهُمْ وَيَنْصَحُ لَهُمْ ، إِلاَّ لَمْ يَدْخُلْ مَعَهُمُ الْجَنَّةَ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ya'laa Ma'qil bin Yasaar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna mja yeyote Allaah anampa uchungu wa raia wake, akafa siku anayokufa ameghushi raiawake, isipokuwa Allaah anamharimishia Pepo." [Al-Bukhaariy na Muslim].

Katika riwaayah nyingine: "Hakuwatizama kwa nasaha zake hatapata harufu ya Pepo."

Katika riwaayah ya Muslim: "Hakuna Amiri anasimamia mambo ya Waislamu, kisha hakuwafanyia juhudi na hakuwanasihi, Isipokuwa hataingia pamoja nao Peponi."





Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول في بيتي هَذَا : (( اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ ، فاشْقُقْ عَلَيْهِ ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ ، فَارفُقْ بِهِ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema katika nyumba yangu hii: "Ee Rabb wangu! Mwenye kusimamia chochote katika Ummah wangu, akawafanyia uzito. Mfanyie uzito. Na mwenye kusimamia chochote katika Ummah wangu, akawahurumia, Nawe mhurumie." [Muslim].





Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( كَانَتْ بَنُو إسرَائِيلَ تَسُوسُهُم الأَنبِيَاء ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبيٌّ ، وَإنَّهُ لاَ نَبِيَّ بَعْدِي ، وَسَيكُونُ بَعْدِي خُلفَاءُ فَيَكثرُونَ )) ، قالوا : يَا رسول الله ، فَمَا تَأْمُرُنَا ؟ قَالَ : (( أَوْفُوا بِبَيْعَةِ الأَوَّل فَالأَوَّل ، ثُمَّ أعْطُوهُمْ حَقَّهُمْ ، وَاسْأَلُوا الله الَّذِي لَكُمْ ، فَإنَّ اللهَ سَائِلُهُمْ عَمَّا اسْتَرْعَاهُمْ )) متفقٌ عليه .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Uongozi miongoni mwa Bani Israaiyl ulikuwa ukitekelezwa na Manabiy. Kila anapofariki Nabiy, Nabiy mwengine alikuwa akichukua mahali pake. Na hakika hakuna Nabiy baada yangu na kutakuwa baada yangu Makhalifa ambao watakuwa wengi." Wakasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Unatuamuru tufanye nini?" Akasema: "Kuweni watiifu kwao mmoja baada ya mwengine, kisha wapatieni haki yao na muombeni Allaah kwa mambo yenu. Hakika Allaah atawauliza kwa kile walicho chunga." [Al-Bukhaariy na Muslim].





Hadiyth – 5

وعن عائِذ بن عمرو رضي الله عنه : أَنَّهُ دَخَلَ عَلَى عُبَيْد اللهِ بن زيادٍ ، فَقَالَ لَهُ : أيْ بُنَيَّ ، إنِّي سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( إنَّ شَرَّ الرِّعَاءِ الحُطَمَةُ )) فإيَاكَ أن تَكُونَ مِنْهُمْ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaidh bin 'Amru (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba alimtembelea 'Ubaydullaah bin Ziyaad na kumwambia: "Ee mtoto wangu, hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Hakika viongozi wabaya kabisa ni wale wakali (kwa raia zao). Hivyo, kuwa na tahadhari usiwe miongoni mwao." [Al-Bukhaariy na Muslim]





Hadiyth – 6

وعن أَبي مريم الأزدِيِّ رضي الله عنه : أنّه قَالَ لِمعاوية رضي الله عنه : سَمِعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ وَلاَّهُ اللهُ شَيْئاً مِنْ أُمُورِ المُسْلِمِينَ ، فَاحْتَجَبَ دُونَ حَاجَتِهِمْ وَخَلَّتِهِمْ وَفَقْرِهِمْ ، احْتَجَبَ اللهُ دُونَ حَاجَتِهِ وَخَلَّتِهِ وَفَقْرِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ )) فجعل معاوية رجلاً عَلَى حوائج النَّاسِ . رواه أَبُو داود والترمذي .

Imepokewa kutoka kwa Abu Maryam Al-Azdiy (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba alimwambia Mu'aawiyah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote ambaye Allaah atamchagua kuwaongoza Waislamu katika mambo yao na akashindwa kutatua shida zao na kuwaondoshea ufakiri wao, Allaah hatamtizama haja zake (wala hatamjibu dua yake) na kumuondoshea hali yake na ufakiri wake Siku ya Qiyaamah." Hivyo, Mu;aawiyah alimchagua mtu kuangalia haja za watu." [Abuu Daawuud na at-Tirmidhiy]
 
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn



باب الوالي العادل

079-Mlango Wa Kiongozi Muadilifu



Alhidaaya.com



قَالَ الله تَعَالَى:

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ ﴿٩٠﴾

Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan. [An-Nahl: 90]

وَأَقْسِطُوا ۖ إِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ﴿٩﴾

Hakika Allaah Anapenda wanaotimiza haki. [Al-Hujuraat: 9]





Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ الله في ظِلِّهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إِلاَّ ظِلُّهُ : إِمَامٌ عادِلٌ ، وَشَابٌ نَشَأ في عِبادة الله تَعَالَى ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ في المَسَاجِدِ ، وَرَجُلانِ تَحَابَّا في اللهِ اجتَمَعَا عَلَيْهِ ، وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأةٌ ذاتُ مَنْصِبٍ وجَمالٍ ، فَقَالَ : إنّي أخافُ اللهَ ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "(Watu) saba Allaah atawafunika chini ya kivuli Chake siku isio na kivuli isipokuwa kivuli Chake: Imamu muadilifu, na kijana ameinukia katika kumuabudu Allaah, na mtu moyo wake umefungamana na Misikiti, na watu wawili wamependana kwa ajili ya Allaah, wamejumuika juu yake na kufarikiana juu yake, na mtu ameitwa na mwanamke mwenye hadhi na uzuri, akasema: 'Mimi namwogopa Allaah', na mtu ametoa swadaqah akaificha hadi kushoto kwake kusijue kilichotoa kulia kwake, na mtu ambaye amemtaja Allaah peke yake na macho yake yakabubujika machozi." [Al-Bukaariy na muslim].





Hadiyth – 2

وعن عبدِ اللهِ بن عَمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ المُقْسِطِينَ عِنْدَ اللهِ عَلَى مَنَابِرَ مِنْ نُورٍ : الَّذِينَ يَعْدِلُونَ في حُكْمِهِمْ وأَهْلِيْهِم وَمَا وَلُوْا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika waadilifu watakuwa juu ya mimbari za nuru mbele ya Allaah: Ambao wanafanya uadilifu katika hukumu zao na familia zao, na waliyotawalishwa." [Muslim]





Hadiyth – 3

وعن عوفِ بن مَالِكٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( خِيَارُ أئِمَّتِكُمُ الَّذِينَ تُحِبُّونَهُمْ وَيُحِبُّونَكُمْ ، وَتُصَلُّونَ عَلَيْهِمْ وَيُصَلُّونَ عَلَيْكُمْ . وشِرَارُ أئِمَّتِكُم الَّذِينَ تُبْغِضُونَهُمْ وَيُبْغِضُونَكُمْ ، وَتَلعَنُونَهُمْ وَيَلْعَنُونَكُمْ ! )) ، قَالَ : قُلْنَا : يَا رسول اللهِ ، أفَلاَ نُنَابِذُهُم ؟ قَالَ : (( لاَ ، مَا أقَامُوا فِيْكُمُ الصَّلاَةَ . لاَ ، مَا أقَامُوا فِيكُمُ الصَّلاَةَ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Awf bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Wabora wa viongozi wenu ni ambao mnawapenda na wao wanawapenda, na mnawaombea na wao wanawaombea. Na waovu wa viongozi wenu ni mnaowachukia na wao wanawachukia, na ambao mnawalaani na wao wanawalaani." Akasema: "Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! "Tujitenge nao?" Akasema: "La! Madamu wamesimamisha Swalaah kati yanu. La! Madamu wamesimamisha Swallaah kati yenu." [Muslim].





Hadiyth – 4

وعن عِياضِ بن حِمارٍ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( أهلُ الجَنَّةِ ثَلاَثَةٌ : ذُو سُلطانٍ مُقْسِطٌ مُوَفَّقٌ ، وَرَجُلٌ رَحيمٌ رَقِيقُ القَلْبِ لكُلِّ ذي قُرْبَى ومُسْلِمٍ ، وعَفِيفٌ مُتَعَفِّفٌ ذو عِيالٍ )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Iyaadh bin Himaar (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Mimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Watu wa Peponi ni aina tatu: Kiongozi muadilifu mwenye kutoa swadaqah kwa uwezo wake; na mtu mwenye kuwarehemu na mwenye moyo laini kwa kila jamaa yake na kwa kila Muislamu; na mtoharifu anyejizuilia na uchafu (asiezini) mwenye familia." [Muslim].
 
Back
Top Bottom