Tunaendelea na darsa letu la Swalaa ya Nabii swallallahu alaih wasallam



041-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kurefusha Kikao Baina Ya Sajdah Mbili, Adhkaar Na Kuinuka Kwa Kutegemea Mikono





KUREFUSHA KIKAO BAINA YA SAJDA MBILI



Pia, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikirefusha - hichi kikao baina ya sijida mbili- kiasi cha kukaribiana na urefu wa Sajdah yake([1]

), na mara nyingine, alibakia katika (kikao hiki) mpaka mtu akasema: "Amesahau".([2]

)










ADHKAAR BAINA YA SAJDAH MBILI




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) katika kikao hiki akisema:

1-












Allaahumma [Rabbi] ghfirliy, warhamniy, [wajburniy, [warfa’niy], wah-diniy [wa’aafiniy], war-zuqniy]

Ee Allaah! [Ee Mola Wangu!] Nisamehe, na Unirehemu, na [Uniunge], na [Uniinue], Na Uniongoze, [Na Unipe afya] na Uniruzuku([3]

). Na mara nyingine akisema:




2-








Rabbi ghfirliy ighfirliy

Ewe Mola wangu! Nisamehe, Nisamehe([4]

). Na alikuwa akizisoma zote hizo mbili katika Swalah ya usiku.([5]

)










SAJDAH YA PILI




Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akileta Takbiyr na Sajdah (kwa mara) ya pili([6]

). Pia alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo. Alimuambia baada ya kumuamrisha kutulia baina ya Sajdah mbili kama ilivyotangulia: ((…kisha sema 'Allaahu Akbar', na usujudu hadi viungo vyako vyote vitulie [na fanya hivyo katika Swalah yako yote]))([7]

). Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake pamoja na Takbiyr mara nyingine.([8]

)




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya katika Sajdah hii –Sajdah ya pili- (sawa sawa) kama aliyoyafanya katika Sajdah ya mwanzo.




Kisha, alinyanyua kichwa chake huku akileta Takbiyr([9]

), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo, akimuambia baada ya kumuamrisha kusujudu (kwa mara) ya pili kama ilivyotangulia: ((….kisha nyanyua kichwa chako na sema 'Allaahu Akbar'))([10]

). Akamuambia: (([…kisha fanya hivyo katika kila rakaa (na Sajdah], (kwani) utakapo fanya hivyo, basi Swalah yako itakamilika, na ukipunguza chochote kile katika hayo, basi Swalah yako itapungua)).([11]

) Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akinyanyua mikono yake([12]

) mara nyingine pamoja na Takbiyr.







KIKAO CHA KUPUMZIKA




Kisha, anakaa sawa sawa (juu ya mguu wake wa kushoto sawa sawa mpaka kila mfupa unarudi katika sehemu yake).([13]

)




KUTEGEMEZA MIKONO MIWILI KATIKA KUINUKA KWA AJILI YA RAKAA (INAYOFUATIA)



Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiinuka huku akiitegemea ardhi kuelekea kwenye rakaa ya pili (akijisaidia kwa (kukamata) ardhi)([14]

). Pia alikuwa akiifumba ngumi (yake)([15]

) katika Swalah akiitegemea kwa mikono yake anapoinuka.([16]

)













[1]

Al-Bukhaariy na Muslim.


[2]

Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Ibn Al-Qayyim amesema: "Sunnah hii imeachwa na watu baada ya zama za Maswahaba. Lakini anayefuata Sunnah na haangazi kwengine kunakoipinga, hana wasiwasi wa kupinga uongofu.”


[3]

Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na Al-Haakim, ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.


[4]

Ibn Maajah ikiwa na isnaad nzuri. Imaam Ahmad amechagua kuiomba na hii; Is-haaq bin Raahawayh amesema: "Akipenda aseme mara tatu au aseme 'Allaahumma-ghfir-liy', kwa sababu zote mbili zimeripotiwa kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) baina ya Sajdah mbili". (Masaail ya Imaam Ahmad na Is-haaq bin Raahawayh kama ilivyosimuliwa na Is-haaq Al-Marwaziy Uk.19).


[5]

Hii haikanushi kutekelezwa nyiradi hizi katika Swalah za Faradhi kwa sababu ya kuweko tofauti baina ya hizo na Swalah za Naafilah. Hii ni rai ya Ash-Shaafi'iy, Ahmad na Is-haaq ambao wameona kwamba hizi zimeruhusiwa katika Swalah zilizofaridhiwa na za Sunnah kama alivyoripoti At-Tirmidhiy. Imaam Atw-Twahaawiy pia amechukua rai hii katika Mushkil Al-Aathaar. Uchambuzi barabara unatilia nguvu hoja hii, kwani hakuna sehemu katika Swalah ambako hakuna dhikr, hivyo inafaa kuwa hali iwe hivi hapa.


[6]

Al-Bukhaariy na Muslim.


[7]

Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Ziada ni kutoka kwa Al-Bukhaariy na Muslim.


[8]

Abu 'Awaanah na Abu Daawuud ikiwa na sanad mbili Swahiyh. Kunyanyua mikono huku kumetiliwa nguvu na Ahmad, Maalik na Ash-Shaafi'iy katika usimulizi wao. Taz. Tanbihi ya nyuma katika Sujuud.


[9]

Al-Bukhaariy na Muslim.


[10]

Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali.


[11]

Ahmad na At-Tirmidhiy ambaye amekiri ni Swahiyh.


[12]

Taz. Tanbihi ya nne ya mwisho.


[13]

Al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Kikao hiki kinajulikana kwa Maulamaa wa Fiqh kama "Jalsah al-istiraahah" (kikao cha kupumzika). Ash-Shaafi'iy ametilia nguvu kama Ahmad katika Tahqiyq (111/1) na akapendekeza kwa nguvu, kama anavyojulikana kuwa ni mwenye kusisitiza kufuata Sunnah ambayo haina kipingamizi. Ibn Haaniy kasema katika Masaail ya Imaam Ahmad (Uk. 42): "Nilimuona Abu 'Abdillaah (yaani Imaam Ahmad) mara nyingine akiegemea mikono yake anaponyanyuka kwa ajili ya rakaa inayofuatia, na mara nyingine alikaa sawa sawa kisha akainuka". Ni pendekezo pia la Imaam Is-haaq bin Raahawayh aliyesema katika Masaail ya Al-Marwaziy (1/47/2). "Mfano umewekwa na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wa kujisaidia kwa mikono yake kuinuka ikiwa ni kwa mzee au kijana". Taz. Pia Al-Irwaa (2/82/3).


[14]

Al-Bukhaariy na Ash-Shaafi'iy.


[15]

Kama vile: "mtu anayekanda unga".


[16]

Abu Is-haaq Al-Harbiy kwa isnaad isiyo na makosa. Na maana yake inapatikana kwa Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Ama kuhusu Hadiyth: "Alikuwa akiinuka kama mshale bila ya kujisaidia kwa mikono yake", hii ni Hadiyth ‘mawdhwuu’ (Kutungwa) na usimulizi wote wenye maana kama hiyo ni Dhwa'iyf, sio Swahiyh na nimeelezea haya katika Silsilatul-Ahaadiyth Adh-Dwa'iyfah (562, 929, 968).
 
042-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Rakaa Ya Pili, Na Ulazima Wa Kusoma Al-Faatihah Katika Kila Rakaa



RAKAA YA PILI




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposimama katika rakaa ya pili, bila ya kunyamaza, huanza kwa kusoma 'AlhamduliLlaahi [Al-Faatihah 1:1] (bila ya kupumzika).([1])




Na hufanya katika rakaa hii kama alivyofanya katika ya kwanza, isipokuwa alikuwa akiifanya fupi ukiilinganisha na ya kwanza kama ilivyotangulia.






















ULAZIMA WA KUSOMA SURATUL-FAATIHAH KATIKA KILA RAKAA




Alimuamrisha (صلى الله عليه وآله وسلم) aliyeswali vibaya kusoma al-Faatihah katika kila rakaa wakati alipomwambia baada ya kumuamrisha aisome hiyo al-Faatihah katika rakaa ya mwanzo([2]): ((…kisha fanya hivyo katika Swalah yako yote)).([3]) [katika usimulizi mwengine] ((...katika kila rakaa))([4]). Na alisema: ((katika kila rakaa kuna kisomo)).([5])










[1] Muslim na Abu 'Awaanah. Kipumziko kilichokanushwa katika Hadiyth hii inaweza kuwa ni kipumziko cha kusoma du'aa ya kufungulia na hakijumuishi kipumziko cha kusoma isti'aadhah, au inaweza kumaanisha zaidi ya hivyo. Naona kwamba uwezekano wa kwanza unakinaisha zaidi. Kuna rai mbili baina ya Maulamaa kuhusu isti'aadhah na tunachukulia iliyo sahihi ni kuisema katika kila rakaa. Maelezo yametolewa katika Al-Aswl.

[2] Abu Daawuud na Ahmad ikiwa na isnaad iliyo na nguvu.

[3] Al-Bukhaariy na Muslim.

[4] Ahmad ikiwa na isnaad nzuri.

[5] Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake na Ahmad katika Masaail ya Ibn Haani (1/52). Jaabir bin 'Abdillaah (رضي الله عنه) amesema: "Atakayeswali rakaa bila ya kusoma Mama wa Qur-aan hakuswali, isipokuwa akiwa nyuma ya Imaam". Imesimuliwa na Maalik katika Al-Muwatwtwa.
 
043-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Tahiyyaatu (Tashahhud) Ya Kwanza



TAAHIYYAATU (TASHAHHUD) YA KWANZA




Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akikaa kwa tashahhud baada ya kumaliza rakaa ya pili. Swalah ikiwa ya rakaa mbili kama Alfajiri, hukaa "muftarishan"([1]) kama alivyokuwa akikaa baina ya Sajdah mbili. Na hivi hivi ndivyo anavyokaa katika tashahhud ya kwanza([2]) katika Swalah za rakaa tatu au nne.







Alimuamrisha hivyo aliyeswali vibaya kwa kumuambia: ((Utakapokaa katikati ya Swalah, jitulize, na utandaze paja lako la kushoto na lete tashahhud)).([3])







Abu Huraryah (رضي الله عنه) amesema: "Rafiki yangu (صلى الله عليه وآله وسلم) amenikataza kuchutama (iq'aa) mchutamo wa mbwa."([4]) [katika riwaaya nyingine] Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akikataza kuchutama kama Shaytwaan.([5])




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)anapokaa katika tashahhud huweka kiganja chake cha mkono wa kulia juu ya paja [katika usimulizi mwingine: goti] la kulia, na huweka kiganja chake cha kushoto katika paja [katika usimulizi mwengine: goti] la kushoto([6]). Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiweka kisugudi cha mkono wake wa kulia katika paja lake la kulia.([7])




Pia (صلى الله عليه وآله وسلم)alimkataza mtu aliyekaa katika Swalah hali ya kuwa anautegemea mkono wake wa kushoto akamwambia: ((Hakika hiyo ni Swalah ya Mayahudi))([8]). Na katika kauli nyingine: ((Usikae hivi, kwani hakika hiki ni kikao cha wale wanaoadhibiwa))([9]). Katika Hadiyth nyingine: ((Ni kitako cha wale walioghadhibikiwa [Na Allaah]))([10]).










[1] An-Nasaaiy(1/173) ikiwa na isnaad Swahiyh. "Muftarishan" ni kukalia tumbo la mguu wa kushoto na kuusimamisha unyayo wa mguu wa kulia kama ilivyotangulia.

[2] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[3] Abu Daawuud na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad nzuri.

[4] Atw-Twayaalisiy, Ahmad na Ibn Abi Shaybah. Kuhusu "iq'aa", Abu 'Ubaydah na wengineo wamesema: "Ni mtu anapogandamiza kikalio chake ardhini, akiweka muundi wake wima, na kuegemeza mikono yake ardhini kama mbwa anavyofanya". Hii ni tofauti na "iq'aa" baina ya Sajdah ambayo imekubaliwa katika Sunnah kama ilivyotangulia kabla.

[5] Muslim, Abu 'Awaanah na wengineo. Imetolewa katika Al-Irwaa (316).

[6] Muslim na Abu 'Awaanah.

[7]Abu Daawuud na An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Inayokusudiwa ni kwamba hakutenganisha viwiko vyake na ubavu wake kama alivyofafanua Ibn Al-Qayyim katika Zaad Al-Ma'aad.

[8]Al-Bayhaqiy na Al-Haakim ambaye amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Imetolewa pamoja inayofuatia katika Al-Irwaa (380).

[9] Ahmad na Abu Daawuud ikiwa na isnaad nzuri.

[10] 'Abdur-Razaaq; 'Abdul-Haqq amekiri ni Swahiyh katika Ahkaam yake (Namba 1284 katika utafiti wangu).
 
044-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kutikisa Kidole Kwenye Tashahhud



KUTIKISA KIDOLE KATIKA TASHAHHUD




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akitandaza kiganja chake cha mkono wa kushoto juu ya goti la mkono wa kushoto, na akikunja vidole vyake vya mkono wa kulia vyote, huku akiashiria kinachofuatia kidole cha gumba -kidole cha Shahada- upande wa Qiblah huku akikitupia jicho lake.[1]




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anapoashiria kwa kidole chake, huweka kidole cha gumba juu ya kidole cha kati([2]), na mara nyingine alikuwa akifanya duara kwa hivyo viwili.([3])




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) - anaponyanyua kidole chake - akikitikisa (huku) akiomba du'aa nacho([4]) akisema: ((Hakika kina nguvu zaidi kuliko chuma dhidi ya Shaytwaan)), akimaanisha kidole cha shahada.))([5])







Pia, Maswahaba wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) walikuwa wakikumbushana baina yao, yaani, kuhusu kuashiria kwa kidole wakati wa kuomba du'aa.([6])




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akifanya hivyo katika tashahhud zote mbili.([7])




Wakati mmoja, alimuona mtu akiomba du'aa kwa vidole vyake viwili akasema: ((Pwekesha (Kimoja, [kimoja])) na akaashiria kidole chake cha shahada.([8])
















[1] Muslim, Abu 'Awaanah na Ibn Khuzaymah. Al-Humaydiy (13/1) na Abu Ya'laa (275/2) wameongeza katika isnaad Swahiyh kutoka kwa Ibn 'Umar, ((Na hii ni kumdunga Shaytwaan, hakuna atakayesahau akifanya hivi)). Na Al-Humaydiy alinyosha kidole chake. Al-Humaydiy pia alisema kwamba Muslim bin Abi Maryam amesema: "Mtu alisimulia Hadiyth kwangu katika kanisa la Syria, aliona Surah za Mitume wakiwa katika taswira kama hiii", na Al-Humaydiy akanyosha kidole chake. Hii ni kauli ya ajabu lakini sanad yake hadi kwa 'huyo mtu' ni Swahiyh.

[2] Muslim na Abu 'Awaanah.

[3]Abu Daawuud, An-Nasaaiy, Ibn Al-Jaruud katika Al-Muntaqaa (208), Ibn Khuzaymah (1/86/1-2) na Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake (485) ikiwa na isnaad Swahiyh. Ibn Al-Mulaqqin amekiri ni Swahiyh (28/2), na inayo usimulizi madhubuti kutoka kwa Ibn 'Addiy (287/1).

[4] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni. Kuhusu 'kuomba du'aa nacho', Imaam Atw-Twahaawiy amesema: "Hii ni dalili kwamba ilikuwa ni mwisho wa Swalah". Hivyo kuna dalili kwamba Sunnah ni kuendelea kukielekeza na kukitikisa hadi katika Tasliym, kwani du'aa huwa hadi hapo. Hii ni rai ya Maalik na wengineo. Imaam Ahmad aliulizwa: "Je mtu akitikise kidole chake katika Swalah"? Akajibu: "Ndio, kwa nguvu" (Imetajwa na Ibn Haaniy katika Masaail yake Imaam Ahmad 1/80). Kutokana na hii, ni dhahiri kwamba kutikisa kidole ni Sunnah iliyothibiti ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) na ni desturi ya Ahmad na Maimamu wengineo wa Sunnah. Kwa hiyo wale wanaodhani kwamba hakuna maana na haipasi wala haihusu katika Swalah, wamche Allaah, kwani kwa sababu hii hawatikisi vidole vyao ingawa wanajua kuwa imethibiti katika Sunnah; na wanajitahidi kufasiri kwa njia isiyo mantiki na isiyolingana na ufasaha wa Kiarabu na kinyume cha ufahamu wa Imaam kuhusu hii.




Jambo la ajabu ni kwamba wengine watamtetea Imaam katika mas-ala mengine, japo kama rai yake inapingana na Sunnah, kwa hoja kwamba kudhihirisha makosa ya Imaam ina maana ni kufanya dhihaka na kumdharau. Kisha wanasahau hii na kukanusha Sunnah hii iliyothibiti na huku wakifanya istihzai kwa wanaoitekeleza. Ikiwa wanatambua au hawatambui, istihzai zao pia zinajumuisha wale Maimaam ambao kwa kawaida yao wanawatetea kwa yaliyo batili, na ambao wako sahihi katika Sunnah mara hii! Bali wanambeza Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) mwenyewe, kwani yeye ndiye aliyetuletea Sunnah hii. Kwa hiyo kuifanyia mzaha ni sawa na kumfanyia yeye ((...فَمَا جَزَاء مَن يَفْعَلُ ذَلِكَ مِنكُمْ إِلاَّ)) ((Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila….)) [Al-Baqarah: 85]




Ama kukiweka kidole chini baada ya kukielekeza, au kupunguza kutikisa na kukithibitisha (katika kusema 'Laa ilaaha [Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki…) na kukanusha (kusema 'illa-Allaahu ...' [isipokuwa Allaah']) vyote hivi hakuna asili katika Sunnah; bali ni kinyume na Sunnah, kama Hadiyth hii inavyothibitisha.




Juu ya hivyo, Hadiyth ambayo inasema hakutikisa kidole chake haina isnaad Swahiyh, kama nilivyoelezea katika Dhwa'iyf Abu Daawuud (175). Hata kama ingelikuwa ni Swahiyh, inakanusha na Hadiyth ya juu inathibitisha. Uthibitisho unapewa kipaumbele juu ya ukanushaji kama inavyojulikana kwa Maulamaa.




[5] Ahmad, Al-Bazzaar, Abu Ja'far, Al-Bukhtiriy katika Al-Amaail (60/1), 'Abdul-Ghaniy Al-Maqdisiy katika Sunan yake (12/2) ikiwa na isnaad nzuri, Ar-Ruuyaaniy katika musnad yake (249/2) na Al-Bayhaqiy.

[6] Ibn Abi Shaybah (2/123/2) ikiwa na isnaad nzuri.

[7] An-Nasaaiy na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[8] Ibn Abi Shaybah (12/40/1, 2/123/2) na An-Nasaaiy. Al-Haakim amekiri ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amekubali. Kuna usimulizi unaotilia nguvu kutoka kwa Ibn Abi Shaybah.
 
045-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Wajibu Wa Tashahhud Ya Kwanza Na Hukmu Ya Du'aa Ndani Yake Pamoja Na Matamshi Yake



WAJIBU WA TASHAHHUD YA KWANZA NA HUKUMU YA DU'AA NDANI YAKE




Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma At-Tahiyyaatu kila baada ya rakaa mbili([1]).




Na alikuwa kitu cha kwanza anachokisema anapokaa ni: ((At-Tahiyyaatu LiAllaah)).([2])




Na anapoisahau Tashahhud katika rakaa mbili za mwanzo, husujudu Sajdatus-Sahw-).([3])



Alikuwa akiiamrisha – Tashahhud - kwa kusema: ((Mtakapokaa katika kila rakaa mbili, semeni: 'At-Tahiyaatu …..na kila mmoja wenu ajichagulie du'aa anayoipenda zaidi amuombe Allaah (عزوجل) [kwayo]))([4]). Katika riwaaya nyingine: ((Semeni katika kila kikao 'At-Tahiyyaatu'))([5]), na alimuamrisha aliyeswali vibaya kufanya hivyo kama ilivyotajwa.




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم)akiwafundisha Tashahhud kama alivyokuwa akiwafundisha Surah katika Qur-aan([6]) na "Sunnah ni kuisema kimya kimya.([7])













MATAMSHI MBALI MBALI YA TASHAHHUD




Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم)aliwafundisha matamshi mbali mbali ya Tashahhud:




1- Tashahhud ya Ibn Mas'uud ambaye amesema: "Amenifundisha Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Tashahhud, viganja vyangu baina ya viganja vyake (صلى الله عليه وآله وسلم) kama anavyonifundisha Surah katika Qur-aan:











At-Tahiyyaatu LiAllaahi, Was-Swalawaatu, Wat-Twayyibaatu, As Salaamu ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warahmatu Allaahi Wabarakaatuh, As Salaamu ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-Hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Warasuuluhu.




Maamkuzi mema,([8]) na rehema([9]) na mazuri yote([10]), ni kwa Allaah, amani([11]), zishuke juu yako Ewe Mtume na Rehma za Allaah, na Baraka Zake ([12]), amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Allaah walio wema, (kwani mtu anaposema hivi, inajumuisha kila mja mwema mbinguni na ardhini) nashuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mjumbe Wake. [Na hali ya kuwa yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) yu pamoja nao (Hivi alivyokuwa na sisi, lakini) alipofariki tukawa tunasema:





As Salaamu ‘Alan-Nabiyyi

Amani ishuke juu ya Mtume).([13])






2- Tashahhud ya Ibn 'Abbaas, amesema: "Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitufundisha Tashahhud kama anavyotufundisha [Suraah katika] Qur-aan. Alikuwa akisema:





At-Tahiyyaatu Al-Mubarakaatu Aswalawaatu, At Twayyibaatu LiAllaahi, [As] Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warahmatu Allaahi Wabarakaatuh, [As] Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wa [Ash-hadu] Anna Muhammadan Rasuulu Allaah, [‘Abduhu Wa Rasuuluhu].

Maamkuzi mema, maneno ya Baraka, Swalah, mazuri yote ni ya Allaah, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Allaah na Baraka Zake. Amani ishuke juu yetu na waja wema wa Allaah, nashuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Allaah, na (nashuhudia) kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Allaah, [na katika riwaaya …mja wake na Mjumbe wake][14]






3- Tashahhud au Tahiyyaatu ya Ibn 'Umar ambaye ameripoti kwamba Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema katika Tashahhud:


At-Tahiyyaatu LiAllaahi [Wa] Sswalawaatu, [Wa] Ttwayyibaatu, As-Salaamu ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-Matu Allaahi – Wabarakaatuh -, As- Salaamu ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wah-dahu Laa Shariyka Lahuu, Ash-hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkuzi mema ni ya Allaah, (na) Swalah (na) mazuri, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Allaah - Ibn 'Umar amesema: "Nimeongezea([15]) …. na Baraka Zake – Amani ishuke juu yetu na waja wema wa Allaah, nashuhudia kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila ni Allaah – Ibn 'Umar amesema: "Nimeongozea([16]) - … Pekee Hana mshirika - na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na ni Mjumbe Wake.([17])






4- Tashahhud ya Abu Muusa Al-Ash'ariyy ambaye amesema kwamba, Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((… Mnapokaa, kauli ya mwanzo ya kila mmoja wenu iwe:


At-Tahiyyaatu At-Twayyibaatu As-Swalawaatu LiAllaahi, As-Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-Matu Allaahi Wabarakaatuh, As-Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-Hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wah-Dahu Laa Shariyka Lahuu Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkizi, mazuri, Swalah ni kwa ajili ya Allaah, amani ishuke juu yako ewe Mtume na Rehma za Alalh na Baraka Zake, amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema, nashuhudia kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, [Pekee Hana mshirika] na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mjumbe Wake.([18])

Matamshi saba ndio Taahiyyaatu.([19])




5- Tashahhud ya ‘Umar bin Al-Khatwtwaab ambaye alikuwa akiwafundisha watu Tashahhud huku akiwa juu ya Minbar akisema: "Semeni:


At-Tahiyyaatu LiAllaahi, Az-Zaakiyaatu LiAllaahi, At-Twayyibaatu [LiAllaahi], As-Swalawaatu LiAllaah, As-Salaamun ‘Alayka Ayyuha-Nnabiyyu Warah-matu Allaahi Wabarakaatuh, As-Salaamun ‘Alaynaa Wa’alaa ‘Ibaadi Allaahis Swaalihiyn, Ash-hadu Al-Laa Ilaha Il-La Allaah, Wa Ash-Hadu Anna Muhammadan ‘Abduhu Wa Rasuuluhu.

Maamkizi ni ya Allaah, kutakasika kote ni kwa Allaah, mazuri [ni kwa ajili ya] Allaah, Swalah ni kwa ajili ya Allaah, amani ishuke kwako ewe Mtume na Rahma za Allaah na Baraka Zake, amani ishuke kwetu na kwa waja wema wa Allaah, nashuhudia kwamba hapana apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad ni mja Wake na Mjumbe wake.([20])







[1] Muslim na Abu 'Awaanah.

[2] Al-Bayhaqiy amesimulia katika usimulizi kutoka kwa 'Aaishah ikiwa na isnaad nzuri kama ilivyohakikishwa na Ibn Al-Mulaqqin (28/2).

[3] Al-Bukhaariy na Muslim. Imetolewa katika Al-Irwaa Al-Ghaliyl (338).

[4] An-Nasaaiy, Ahmad na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Kabiyr (3/25/1) ikiwa na isnaad Swahiyh. Maana halisi ya Hadiyth ni dalili ya kuamrishwa du'aa katika kila Tashahhud hata isiyoungana na Tasliym. Na hii ni rai ya Ibn Hazm (رحمه الله ).

[5] An-Nasaaiy ikiwa na isnaad Swahiyh.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim.

[7]Abu Daawuud na Al-Haakim aliyekiri kuwa ni Swahiyh, na Adh-Dhahabiy amewafikiana.

[8] "At-Tahiyyaatu" yaani, maneno yote yanayoambatana na amani, ufalme na kudumu ni kwa ajili ya Allaah. (An-Nihaayah)

[9] "As-Swalawaatu" yaani, 'du'aa zote zinazotumika kumtukuza Allaah Ta'ala, kwani Yeye ni Mwenye kustahiki nazo, na hakuna apasaye kustahiki nazo isipokuwa Yeye. (An-Nihaayah)

[10] "At-Twayyibaatu" yaani, maneno mazuri na masafi yote yanayofaa kumsifu Allaah, na sio yale ambayo yasiyofanana na sifa Zake ambayo hutukuzwa kwazo wafalme. (Fat-hul-Baariy)

[11] Maana, kujikinga na Allaah na kutiwa nguvu Naye kwa vile As-Salaam (amani) ni Jina la Allaah khasa. Hivyo maamkizi yanamaanisha: Allaah Awe Muwakilishaji na Mlinzi wako. Kama inavyosemwa: 'Allaah Ma'ak' (Allaah Awe nawe) yaani Ulinzi Wake, msaada na ihsani.

[12] Ni neno linalotumika kwa mazuri yote yanayotoka kwa Allaah.

[13] Al-Bukhaariy, Muslim, Ibn Abi Shaybah (1/90/2) Siraaj na Abu Ya'laa katika Musnad yake (258/2). Imetolewa katika Al-Irwaa (321).




Kauli ya Ibn Mas'uud: "Tulisema: 'Amani ishuke juu ya Mjumbe', inabainisha kwamba Maswahaba (رضي الله عنهم) walikuwa wakisema: Amani ishuke juu yako ewe Mtume صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tashahhud alipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) yuhai, lakini alipofariki, waliacha hivyo na badala yake wakawa wakisema: 'Amani imshukie Mtume'. Bila shaka, hii ilikuwa ni kwa uidhinishaji wa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Hii imetiliwa nguvu kwa vile Mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها) alifundisha Tashahhud katika Swalah kwa: 'Amani ishuke juu ya Mtume' kama ilivyosimuliwa na Siraaj katika Musnad yake (9/1/2) na Mukhlisw katika Al-Fawaaid (11/54/1) ikiwa na isnaad mbili Swahiyh kutoka kwake.




Ibn Hajar amesema: 'Ziada hii inaonyesha dhahiri kwamba walikuwa wakisema: 'Amani ishuke kwako ewe Mtume' wakimuelekezea yeye wakati wa uhai wake, lakini alipofariki Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) waliacha kumuelekezea hivyo wakimtaja kama ni mtu wa nafsi ya tatu badala yake wakisema: 'Amani ishuke juu ya Mtume'". Amesema pia sehemu nyingine, 'As-Subkiy amesema katika Sharh Al-Minhaaj baada ya kutaja usimulizi kutoka kwa Abu 'Awaanah pekee, 'ikiwa usimulizi huu ni Swahiyh kutoka kwa Maswahaba, inathibitisha kwamba baada ya (kufariki) Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), sio lazima kumuelekezea Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) maamkizi ya amani, hivyo mtu aseme: 'Amani ishuke juu ya Mtume'. (Ibn Hajar anaendelea: "Hii ni Swahiyh bila ya shaka (kwa sababu imethibitishwa katika Swahiyh Al-Bukhaariy) na pia nimepata dalili ya kutilia nguvu". 'Abdur-Razzaaq amesema: "Ibn Jurayj ameniarifu: 'Atwaa amenijulisha kwamba Maswahaba walikuwa wakisema 'Amani ishuke kwako ewe Mtume' alipokuwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) yuhai, lakini baada ya kufariki walikuwa wakisema: 'Amani ishuke juu ya Mtume', na hii ni isnaad Swahiyh. Ama usimulizi wa Sa'iyd bin Manswuur kutoka kwa 'Ubaydah bin 'AbdiAllaah bin Mas'uud, ambaye ameripoti kutoka kwa baba yake kwamba Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amemfundisha Tashahhud kisha yeye (‘Abdullaah bin Mas'uud) akaisema (Tashahhud), Ibn 'Abbaas amesema: "Tulikuwa tukisema 'Amani ishuke juu yako ewe Mtume' alipokuwa yuhai pekee", ambayo Ibn Mas'uud amejibu akisema: "Hivi ndivyo tulivyofundishwa na hivi ndivyo tunavyofundisha". Inavyoelekea ni kwamba Ibn 'Abbaas amesema kuwa hili ni jambo la kujadiliana lakini Ibn Mas'uud hakulikubali. Lakini usimulizi wa Abu Ma'mar (yaani usimulizi katika Al-Bukhaariy) ndio ulio Swahiyh zaidi, kwa vile Abu 'Ubaydah hakusikia (Ahaadiyth) kutoka kwa baba yake, na juu ya hivyo, isnaad inayoelekea hadi kwa Abu 'Ubaydah ni dhaifu" (mwisho wa kunukuu kutoka kwa Ibn Hajar).




Maneno haya ya Ibn Hajar yamenukuliwa na Maulamaa wengi katika utafiti wao, mfano; Al-Qastwalaaniy, Az-Zarqaaniy, Al-Laknaawiy n.k. Wote wamechagua kutoa maneno yake bila ya kutoa tanbihi zaidi. Hoja hizi zimetajwa kikamilifu zaidi katika Al-Aswl.




[14] Muslim, Abu 'Awaanah, Ash-Shaafi'iy na An-Nasaaiy.

[15] Taz. Tanbihi inayofuatia.

[16] Ziada mbili hizi zimethibitika kuwa ni sehemu ya Tashahhud kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Ibn 'Umar hakuziongeza kwa upendekezo wa nafsi yake (hasha ameepukana na hayo); bali amejifunza hayo kutoka kwa Maswahaba ambao wameziripoti kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha ndio akaziongezea katika Tashahhud ambayo amesikia moja kwa moja kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم).

[17] Abu Daawuud na Ad-Daaraqutwniy ambaye amekiri ni Swahiyh.

[18] Muslim, Abu 'Awaanah, Abu Daawuud na Ibn Maajah.

[19] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.

[20] Maalik na Al-Bayhaqiy ikiwa na isnaad Swahiyh. Ingawa Hadiyth hii ni Mawquuf, lakini ina hukmu ya Marfuu' kwani inajulikana kuwa haisemwi tu kutokana na rai ya mtu, na lau kama ingelikuwa ni rai, basi kauli hii isingelikuwa ni dhikr bora miongoni mwa adhkaar nyingine kama alivyosema 'Ibn 'Abdil-Barr.




TANBIHI: Hakuna ziada ya 'wa maghfiratuhu…' (na maghfirah Yake) katika Tashahhud yoyote katika hizi, kwa hiyo isiwe desturi ya mtu kusema. Kwa ajili hiyo baadhi ya Masalaf wameikanusha kutokana na usimulizi ufuatao:




Atw-Twabaraaniy (3/56/1) ameripoti ikiwa na isnaad Swahiyh kutoka kwa Twalha bin Muswarrif ambaye amesema: "Rabiy' bin Khaytham ameongeza katika Tashahhud, '…wa Barakaatuhu, wa Maghfiratuhuu!' Hivyo 'Alqamah akasema: "Tumesita tulipofundishwa: 'amani ishuke juu yako ewe Mtume, na Rahma za Allaah na Baraka Zake". 'Alqamah alikuwa akifuata khaswa mfano wa Mwalimu wake ‘Abdullaahi bin Mas'uud (رضي الله عنه) ambaye kutoka kwake imeripotiwa kuwa ni Swahiyh. Alikuwa akimfundisha mtu Tashahhud, na alipofika katika neno: 'Nakiri kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah…', yule mtu alisema: "Pekee, Hana mshirika", na ‘Abdullaah akasema: "Yeye ni hivyo lakini tunakomea pale tulipofunzwa". [Imesi;;;/

muliwa na Atw-Twabaraaniy katika Mu'jam Al-Awswat Namba. 2848 ikiwa na isnaad Swahiyh].
 
Haki Za Mume Na Mke



Imekusanywa na: Ummu Iyyaad



Alhidaaya.com





Haki za mume na mke zimedhihirishwa katika Qur-aan na Sunnah. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ

Nao wake wana haki kama ambayo (ya waume zao) iliyo juu yao kwa mujibu wa shariy’ah. Na wanaume wana daraja zaidi juu yao. [Al-Baqara: 228]



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema katika Hijjah ya kuaga aliposimama kuwahutubia Swahaba:

((يآ أيُّهَا النَّاسُ إِنَّ لِنِسَائِكُمْ عَلَيْكُمْ حَقاً وَلَكُمْ عَلَيْهِنَّ حَقّ)) أبو داود

"Ee nyie watu, hakika nyinyi mna haki juu ya wake zenu na wake zenu wana haki juu yenu," [Abu Daawuud]



Zifuatazo ni haki zinazowahusu wote wawili; mke na mume katika kuamiliana:



1-Ukweli

Mke na mume wawe ni wakweli baina yao kwa kauli na vitendo. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آَمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ

Enyi mlioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah: 11]



2-Mapenzi, Huruma Na Utulivu.

Kila mmoja amdhihirishie mwenziwe mapenzi, na wawe na huruma baina yao katika shida na matatizo mpaka iwe kila mmoja awe ni kutulizo cha mwenziwe wakati wa dhiki. Allaah (Subhanaahu wa Ta'aalaa) Anasema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَة ًإِنَّ فِي ذَلِكَ لَآ يَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Na katika Aayaat Zake ni kwamba Amekuumbieni kutokana na nafsi zenu (jinsi moja) wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na Rahmah. Hakika katika hayo bila shaka (kuna) Aayah kwa watu wanaotafakari.” [Ar-Ruwm 30: 21]



3-Amana, Uaminifu Na Kutumiza Ahadi:

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewasifu na kuwaahidi Jannah wanaotimiza amana na ahadi zao:

وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ ﴿٨﴾

Na ambao amana zao na ahadi zao wanazichunga. [Al-Muuminuwn: 8]



Kuweko uaminifu kutazuia dhana mbaya au kutiliana shaka:

فَإِنْ أَمِنَ بَعْضُكُم بَعْضًا فَلْيُؤَدِّ الَّذِي اؤْتُمِنَ أَمَانَتَهُ وَلْيَتَّقِ اللّهَ رَبَّهُ

Na ikiwa mmoja wenu amewekewa amana na mwengine, basi airudishe yule ambaye ameaminiwa amana ya mwenzake; na amche Allaah, Rabb wake; [Al-Baqarah: 283]



4-Tabia Njema

Wawe na tabia njema katika kauli na matendo ili iwepo heshima baina yao:

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

Na kaeni nao kwa wema. [An-Nisaa: 19]



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akausia:



"Nakuusieni kuwafanyia wema wanawake" [Al-Bukhaariy na Muslim]



5-Kuhifadhiana Siri

Haiwapasi wote kutoleana siri zao au kutoa aibu zao nje:



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Watu watakaokuwa katika hali mbaya kabisa mbele ya Allaah Siku ya Qiyaamah ni mwanamme anaekwenda kwa mke wake na mke kwenda kwa mume wake kisha (mmojawao) akapita kutoa siri yake". [Muslim]



Haki hizo zitakapotimizwa kwa mume na mke, itakuwa ni kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَلاَ تَنسَوُاْ الْفَضْلَ بَيْنَكُمْ إِنَّ اللّهَ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

Na wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Allaah kwa myatendayo ni Baswiyr (Mwenye kuona). [Al-Baqarah: 237]



Haki Za Mke Kutoka Kwa Mume:

1-Ni wajibu wa mume kumlisha mkewe kumvisha na kumtimizia mahitaji yake.



2-Mume ana haki kumfunza adabu mke anapohisi mke anamuasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا

Na wale (wanawake) ambao mnakhofu uasi wao, basi waonyeni na (wakiendelea uasi) wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni. Wakikutiini, basi msitafute dhidi yao njia (ya kuwaudhi bure). Hakika Allaah ni ‘Aliyyan Kabiyraa (Mwenye Uluwa – Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa). [An-Nisaa: 34]



Aayah hiyo inataka maelezo kidogo kwani baadhi wa wanaume wameifahamu sivyo kuhusu: ((wahameni katika malazi (vitanda) na (mwishowe wakishikilia uasi) wapigeni)).

Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) na wengineo wamesema: "Aayah imemaanisha kupiga mpigo usio mkali" (yaani mpigo hafifu) Al-Hasan Al-Baswriy kasema: "Ina maana mpigo usio wa nguvu".



Wanavyuoni wamefafanua kuhusu kauli hiyo ifautavyo:



i) Kwanza mume amnasihi mkewe bila ya kumshutumu au kumuonea au kumtia aibu kwa watu. Mke atakapomtii mumewe, itosheleze kuwa matatizo yamekwisha.



ii) Atakapoendelea mke kutokumtii mume wake, basi mume ajitenge naye kitandani, yaani asiwe analala nae kwa muda wala asiseme nae mpaka mke ahisi vibaya na atambue kuwa mumewe amamekasirikia. Pindi mke akikubali makosa yake, yaishe matatizo na warudiane katika hali yao ya kawaida.



iii) Ikiwa bado mke hana utiifu, hapo mume anaweza kufuata amri hiyo ya kipigo. Lakini sio kumpiga kwa nguvu bali kama alivyosema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:

عن جابر (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم: أنه قال في حجة الوداع: ((واتَّقُوا اللهَ في النِّساءِ، فإنهن عندكم عَوَانٌ، ولكم عليهن ألا يُوطِئْنَ فُرُشكم أحدا تكرهونه، فإن فَعَلْن فاضربوهن ضَرْبا غير مُبَرِّح، ولهن رزْقُهنَّ وكِسْوتهن بالمعروف))

Kutoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika Hijja ya kuaga: "Mcheni Allaah kuhusu wanawake kwani wao ni wasaidizi wenu. Mnayo haki juu yao kuwa wasimuruhusu mtu msiyempenda kukanyaga zulia lenu. (kuingia katika nyumba) Lakini wakifanya hivyo, mnaruhusiwa kuwatia adabu ndogo. Wao wana haki kwenu kwamba muwatimizie matumizi yao na nguo kwa njia ya kuridhisha".[Muslim]



3-Ni wajib wa mume kumpatia mafunzo ya Dini mke wake ikiwa mke hakujaaliwa kupata elimu ya Dini yake. Mume amfundishe mwenyewe, na pindi asipoweza, amruhusu mke kuhudhuria darasa kwa sababu ni muhimu kwake apate kujifunza yanayopasa kama ‘Aqiydah na Tawhiyd na ajiepushe na shirki. Pia ajifunze Fiqhi na yote yanayohusiana na Dini yake, aweze kutekeleza ibaada zake sawasawa na pia apate kuitakasa nafsi yake na aweze kujiepusha na maasi na aweze kulea watoto wake. Kwa ujumla aihami familia yake na Moto wa Jahannam. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaamrisha hivyo:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ عَلَيْهَا مَلَائِكَةٌ غِلَاظٌ شِدَادٌ لَّا يَعْصُونَ اللَّـهَ مَا أَمَرَهُمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ﴿٦﴾

Enyi walioamini! Jikingeni nafsi zenu na ahli zenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe; juu yake wako Malaika washupavu hawana huruma, shadidi, hawamuasi Allaah kwa yale Anayowaamrisha na wanafanya yale wanayoamrishwa. [At-Tahriym: 6]



4-Ni wajibu wa mume kumrekebisha mkewe anapokosea kufuata Shariy’ah za Dini; mfano mke asipotimiza hijaab. Vile vile asimwachie kuchanganyika na wanaume isipokuwa ambao kaharimishwa nao kuolewa.



5-Ni wajibu wa mume kumhifadhi mke kwa kila njia. Mume awe ndio mlinzi na msimamizi wa mambo yake na ndiye mwenye majukumu ya kumhudumia:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. [An-Nisaa: 34]

Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema: "Mwanamme ni mchunga (msimamizi) wa nyumbani kwake na ataulizwa kuhusu uchungaji (usimamizi) wake" [Al-Bukhaariy na Muslim]



6-Ikiwa mume ana mke zaidi ya mmoja, inampasa afanye uadilifu baina ya hao wake. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anakataza kutokufanya uadillifu:



وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ ۖ فَلَا تَمِيلُوا كُلَّ الْمَيْلِ فَتَذَرُوهَا كَالْمُعَلَّقَةِ ۚ

Na wala hamtoweza kuadilisha baina ya wake japokuwa mkipania. Basi msimili muelemeo wote (kwa mke mmoja) mkamuacha (mwengine) kama kining’inio. [An-Nisaa: 129]



Na Anasema:

فَإِنْ خِف ْتُمْ أَلاَّ تَعْدِلُواْ فَوَاحِدَةً أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ذَلِكَ أَدْنَى أَلاَّ تَعُولُواْ

Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu au ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. [An-Nisaa: 3]



Juu ya hivyo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ameusia wanawake watendewe mema:



"Mbora wenu ni yule aliye mbora kwa familia yake na mimi ni mbora kabisa kwa familia yangu." At-Twabaraaniy



Haki Za Mume Kutoka Kwa Mke:



1-Mke amtii mumewe na atambue kwamba ni amri ilotiliwa nguvu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kwa kuwa amesema:

لَوْ كُنْتُ آمِراً أَحَداً أَنْ يَسْجُدَ لأِحَدٍ لأَمَرْتُ الْمَرْأَةَ أَنْ تَسْجُدَ لِزَوْجِهَا مِنْ عِظَمِ حَقَّهِ عَلَيْهاَ

"Ningeliweza kumuamrisha mtu amsujudie binaadamu mwenzake, ningeliamrisha mwanamke amsujudie mume wake kwa jinsi haki ya mume ilivyo tukufu kwa mke wake" Tuhfat Al-Ahwadhi 4.323 kutoka Tafsiyr ya Ibn Kathiyr



2-Mke inampasa kumuitikia mumewe anapomhitaji kujimai naye. Kutomtimizia haja yake bila ya sababu inayokubalika katika Shariy’ah ya Dini ni kulaaniwa na Malaika kwa dalili:

((إذا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأتَهُ إِلىَ فِرَاشِهِ فَأَبَتْ عَلَيْه لَعَنَتْهَا الْمَلائِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ))

"Mume atakapomwita mkewe kitandani na mke akikataa, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi". [Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy]



3-Haimpasi mke kutoa swadaqah yoyote bila ya idhini ya mumewe; amekataza Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

((لاَ تُنْفِقُ الْمَرْأَةُ شَيْئًا مِنْ بَيْتِهَا إِلا بِإِذْنِ زَوْجِهَا)) قالوا: "يا رسول الله! وَلا الطَّعَامَ؟ قال: ((ذَاكَ أَفْضَلُ أَمْوَالِنَا)) صحيح ابن ماجه - حديث حسن الألباني

"Mwanamke asitoe kitu chochote kutoka nyumbani kwake ila kwa idhini ya mumewe". Wakasema: "Hata chakula ee Rasuli wa Allaah"? Akasema: "Hicho ni mali bora yetu". Hadiyth Imepokelewa na Ibn Maajah na Shaykh Al-Albaaniy kasema ni ‘Hasan’.



Lakini mke anayo haki kutoa swadaqah katika kipato chake mwenyewe. Pia mke anaweza kutoa swadaqah ikiwa anatambua kuwa hatoghadhibikiwa na mumewe:

عن همام (رضي الله عنه) قال: سمعت أبا هريرة (رضي الله عنه) عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((إِذَا أَنْفَقَتِ الْمَرْأَةُ مِنْ كَسْبِ زَوْجِهَا عَنْ غَيْرِ أَمْرِهِ فَلَهُ نِصْفُ أَجْرِهِ)) - البخاري

Kutoka kwa Hamaam (Radhwiyya Allaahu ‘anhu) amesema: “Nimemsikia Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke akitoa swadaqah kutoka katika kipato cha mumewe bila ya amri yake basi na yeye atapata thawabu nusu yake". [Al-Bukhaariy]



4-Haimpasi mke kutoka nyumbani kwake bila ya idhini ya mumewe (hata kwenda kwa wazazi wake ila kwa makubaliaono).



5-Haimpasi mwanamke kumfanyia ujeuri, ufedhuli au usafihi mumewe. Atakapokuwa ni kinyume cha hivyo akamtii mumewe basi amepewa fadhila kubwa ya kuingia Jannah (Peponi):

عن عبد الرحمن ابن عوف (رضي الله عنه) قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((إِذَا صَلَّتْ الْمَرْأَةُ خَمْسَهَا، وَصَامَتْ شَهْرَهَا، وَحَفِظَتْ فَرْجَهَا، وَأَطَاعَتْ زَوْجَهَا, قِيلَ لَهَا: ادْخُلِي مِنْ أَيِّ أَبْوَابِ الْجَنَّةِ شِئْتِ)) صحيح الترغيب

Kutoka kwa Abdur-Rahmaan bin 'Awf (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwanamke atakaposwali Swalaah zake tano, akafunga Swawm mwezi wake (wa Ramadhwaan), akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataambiwa ingia Jannah (Peponi) kupitia mlango wowote autakao." Swahiyh at-Targhiyb



Hizo ni baadhi ya haki tulizojaaliwa kuzinukuu, tukitaraji kwamba pindi zikitimzwa, basi ndoa itaendelea kudumua katika usalama na amani.
 
Hikma Ya Ruhusa Ya Ukewenza



Alhidaaya.com



Kuna sababu nyingi za kibinafsi, kimaadili, kiuchumi na kijamii zinazoonesha kuwa wakati mwengine kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilobudi.



Kabla ya kulieleza jambo hili ni vyema tukaelewa nini maana hasa ya ndoa (Nikaah) katika Uislam. Ndoa ni mkataba ('Aqd) wa hiari kati ya mume na mke wa kuishi pamoja kwa wema na upendo kufuatana na masharti na taratibu zilizowekwa na sheria ya Kiislam.



Kwani umuhimu wa ndoa kwa mtazamo wa Uislam ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii. Kama Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Alivyosema katika kitabu Chake kitukufu cha Qur-aan Suwrah Al-Nuwr, Aayah ya 32:

وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٢﴾

Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah Atawatajirisha katika fadhila Zake. Na Allaah Mwenye Wasaa, Mjuzi wa yote. [An-Nuwr: 32]



Tafsiri yake ni kwamba:

Na waozesheni wajane miongoni mwenu (waungwana) na walio wema katika watumwa wema (wanaume) na wajakazi wenu.



Pia vile vile Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema katika Suwrah An-Nisaa, Aayah ya 3:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ

Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne. Lakini mkikhofu kuwa hamtoweza kufanya uadilifu, basi mmoja tu. [An-Nisaa: 3]



Tafsiri:

Oeni walio wazuri miongoni mwa wanawake wawili, watatu na wanne, ikiwa munaogopea uadilifu kwa wanawake hao basi oeni mmoja.



Hii inadhihirisha kuwa tendo la ndoa lina umuhimu mkubwa katika jamii, ambazo zimetubainishia kuwa ndoa ni ngao ya kujikinga na kitendo kichafu cha zinaa.



Allaah Amehalalisha ndoa na kuitilia mkazo kwa wale wenye uwezo kama tunavyojifunza katika Aayah zifuatazo:

وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَاءَ ذَٰلِكُمْ أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم مُّحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ ۚ

Na mmehalalishiwa wengineo wasiokuwa hao, mtafute (kuwaoa) kwa mali zenu mkijistahi pasi na kuzini. [An- Nisaa:24]



Pia katika Suwrah ya [Al-Maaidah: 5]

الْيَوْمَ أُحِلَّ لَكُمُ الطَّيِّبَاتُ ۖ وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ ۖ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الْمُؤْمِنَاتِ وَالْمُحْصَنَاتُ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ إِذَا آتَيْتُمُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ مُحْصِنِينَ غَيْرَ مُسَافِحِينَ وَلَا مُتَّخِذِي أَخْدَانٍ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٥﴾

Leo mmehalalishiwa vizuri. Na chakula cha wale waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na wanawake walioimarisha sitara (wasiozini) miongoni mwa Waumini wanawake na wanawake walioimarisha sitara miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu; mtakapowapa mahari yao mkijistahi bila ya kuwa maasherati wala kuchukua hawara. Na yeyote atakayekanusha iymaan; basi kwa yakini imeporomoka ‘amali yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika. [Al-Maaidah: 5]



Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kwamba:

"Enyi vijana na atakaeweza kati yenu gharama za ndoa (mahari) na aoe."



Pia katika hadithi nyengine amesema:



'Abdullaah bin Mas'uud (Radhwiya Allaahu 'anhu) ameeleza kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema “Enyi kongamano la vijana na aoe yule alie na uwezo miongoni mwenu, hakika kunainamisha macho (na matamanio) na kuhifadhi tupu (humzuilia mtu na zinaa)na asiyeweza kuoa na afunge, Hakika funga hukata matamanio. [Al-Bukhaary na Muslim].



Pia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"Mmoja wenu atakapomuona mwanamke kisha akamtamani, hana budi kumuendea mkewe kwani ana kile alichonacho huyo mwanamke aliyemtamani." [At-Tirmidhy]



Ndoa ni Sunnah lakini itakuwa wajibu kwa mwenye kuweza na akawa anayo matamanio na anaogopa kutumbukia katika zinaa.



Katika suala la kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilo budi, kwa kuangalia mifano kadhaa kama vile:



a) Kama mke ni tasa

Mfikirie mwanamme ambae amehakikisha kuwa mkewe ni tasa na bado ana hamu ya kupata mtoto atakayekuwa mrithi wake. Katika hali hii mwanamme huyu atafanya mojawapo katika haya yafuatayo:



i. Atakaa na kusononeka kwa kukosa mtoto katika maisha yake yote au

ii. Atamuacha huyo mwanamke asiyezaa ili aoe mwengine anayezaa au

iii. Atatembea na mwanamke mwengine nje ya ndoa ili ampatie watoto, japo kisheria si watoto wake au

iv. Ataendelea kukaa na mkewe kwa mapenzi na furaha kisha aoe mke mwengine atakaemzalia watoto ambao watakuwa wake kisheria.



Utakuta uchaguzi wa kuoa mke wa pili ndio ulio bora kabisa. Wengi katika jamii ya Kiislam wameoa mke wa pili kwa sababu hii.



b) Kama mke ana maradhi ya kudumu

Mfikirie tena mwanamme ambaye mkewe ana ugonjwa wa kudumu kwa kiasi kwamba hana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama mke bila ya shaka mwanamme huyu atafanya mojawapo kati ya yafuatayo:



i. Atajizuia na matamanio yake ya kimwili kwa muda wote wa maisha yake uliobakia au

ii. Anaweza kumtaliki, mkewe mgonjwa wakati ambapo anahitajia uangalizi, huruma na mapenzi ya hali ya juu kutoka kwake, ili aoe mke mwengine atakayetosheleza mahitaji yake au

iii. Anaweza kubakia na mkewe mgonjwa na kufanya uzinifu na wanawake wengine nje au

iv. Ataoa mke wa pili atakayemsaidia kumuhudumia mkewe mgonjwa



Hebu tuzijadili hizi hatua tatu (3) kwa mtazamo wa mafundisho ya Uislam



Hatua ya kwanza: Inakwenda kinyume na umbile la mwanaadamu. Allaah Analifahamu fika umbile la mwanaadamu ya haja yake ya kutosheleza matamanio ya jimai na Ameweka utaratibu mzuri wa sheria ya ndoa wa kutosheleza mahitajio haya ya kimaumbile.



Hatua ya pili: Ni kinyume kabisa na ubinaadamu, kumuacha mke kwa sababu amekuwa mgonjwa badala ya kumuhudumia kwa upendo na huruma ni kinyume kabisa na utu. Utaona kuwa hatua ambayo inamuwezesha mume huyu aendelee kumtunza mkewe kwa huruma na wakati huo huo aweze kutosheleza mahitajio yake ya kimaumbile kwa utaratibu mzuri wa heshima ni kuoa mke wa pili



c) Wanawake Wajane

Wajane ni wanawake waliofiwa na waume zao, hakuna jamii isiyokuwa na wajane na idadi yao huongezeka zaidi wakati wa vita ambapo wanaume wengi huuliwa vitani. Je, wanawake hao warudishwe kwa wazazi au walezi wao au kukaa hivyo hivyo bila ya kukidhi matashi yao ya kimaumbile mpaka wazeeke, au waachiwe wawe malaya na kuitokomeza jamii kutokana na matatizo mbali mbali yanayosababishwa na zinaa? Kwa vyovyote vile, njia pekee ya kuwahifadhi wanawake na watoto wao ni hii ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja hadi wanne, kwa kufuata masharti yaliyowekwa.



d) Wanawake Wakiwa Wengi Katika Jamii

Inatokezea katika jamii nyingi wanawake kuwa wengi zaidi kuliko wanaume. Katika jamii hizi, kama tutaweka sheria ya mume mmoja – mke mmoja kama wanavyodai watetezi wa usawa wa wanawake. Wanawake watakaokosa wa kuwaoa watakwenda wapi? Watafanyaje ili kukidhi matashi yao ya kimaumbile?



Je, kama watazuiliwa mpaka wazeeke huoni hii itawaathiri kimwili, na kifikra na kuwafanya wasiwe watu wenye manufaa katika jamii? Nani watakaotoa hifadhi kwa wanawake hawa kiuchumi na kimaadili? Ilivyo katika maadili ya kibinaadamu, kila mwanamke wa kawaida anahitajia kuwa na mwanamme anayempenda na kumuhurumia, hivyo wanawake hawa watakapokosa waume wa ndoa watafanya kila hila za kuwashawishi wanaume kwa kuwawekea mitego mbali mbali kama vile kujipitisha mbele yao wakiwa wamejipodoa na kujiremba, kutembea mbele yao uchi, kuzurura kwenye majumba ya sinema n.k. ambayo itawanasa na kuwatumbukiza katika zinaa.



e) Kuhifadhi jamii na zinaa

Matamanio ya jamii ni katika maumbile na hayaepukiki katika Uislam. Ndoa ni jambo lililokokotezwa sana kutokana na umuhimu wake katika kujenga na kuendeleza jamii. Ndoa kwa mtazamo wa Uislam inatarajiwa:



1. Kuhifadhi jamii na zinaa;

2. Kuendeleza kizazi cha mwanaadamu kwa utaratibu mzuri;

3. Kujenga mapenzi, huruma na ushirikiano katika familia;

4. Kukuza udugu na ushirikiano katika jamii.



Kwa hivyo kuoa mke zaidi ya mmoja ni jambo lisilo budi kwa mwanaadamu kama tulivyoeleza katika mada yetu hii ya ndoa.



Wa Allaahu A'alam





Du’aa Ya Mada Husika

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu, na kheri ya maumbile Uliyomuumba nayo, na najilinda Kwako na shari yake na shari ya maumbile Uliyomuumba nayo.
 
Du’aa Ya Mada Husika

Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu, na kheri ya maumbile Uliyomuumba nayo, na najilinda Kwako na shari yake na shari ya maumbile Uliyomuumba nayo.

Hiyo dua bwana harusi ukienda kumuona mkeo basi unamshika kichwani na kuomba dua hiyo,uislamu haujaacha kitu ndugu,mapema unajilinda kwa Allah na shari ya mwanamke huyo na kuomba vile vile kheri ya mwanamke huyo

Nami nilifanya hivyo pia
 
Jinsi Ya Kumfurahisha Mkeo

Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid

Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman.

www.alhidaaya.com







Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta, Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni :

Namna ya kumfurahisha Mkeo
Namna ya kumfurahisha Mumeo
Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona katika somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia haki na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali katika kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika zaidi katika majukumu ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au matendo ya Maswahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni tafsiri ya kitabu cha kwanza.

Tafsiri hii ya Kiingereza imemilikiwa na MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta (Canada), na ya Kiswahili inamilikiwa na www.alhidaaya.com.



Usisite kuituma kwa wengine au kuitoa kopi kwa njia nyoyote, ilimradi tu hutofanya mabadiliko yoyote, au kuongeza, au kupunguza bila ya ruhusa.

Ifuatayo ni sehemu ya KWANZA ya ufupisho wa kitabu “ How to make your wife happy” na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid.



1- Mapokezi mazuri

Baada ya kurudi kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisheni:

Anza kwa maamkizi mazuri
Anza kwa Assalaamu 'Alaykum na tabasamu.
Salaam ni Sunnah na ni duaa kwake (mkeo) pia.
Mpe mkono na ziache habari mbaya mpaka baadae.






2- Maneno mazuri na makaribisho ya kufurahisha

Chagua maneno mema na jiepushe na maneno mabaya.
Shughulika nae unaposema au anaposema yeye
·Sema kwa ufasaha na rejea maneno inapohitajika mpaka afahamu/aelewe.
Mwite kwa majina mazuri anayoyapenda, mfano Mpenzi wangu, honey (asali, tamtam), (habibty), swaaliha (mwanamke mwema), n.k






3- Urafiki na maliwazo

Tumia muda kuzungumza nae
Mfikishie habari njema
Kumbuka kumbukumbu zenu nzuri za kuwa pamoja.






4- Michezo na burudani

Mfanyie mzaha na jiweke katika hali ya furaha
Chezeni na mshindane katika michezo na mambo mengine.
Mchukue kuangalia aina za burudani zilizo halali.
Jiepushe na mambo ya haram katika kuchagua aina ya burdani.






5- Msaada katika kazi za nyumbani

Fanya kile ambayo wewe mwenyewe unaweza/ unapenda kukifanya ili kumsaidia, hasa anapokuwa mgonjwa au amechoka.
La muhimu kuliko yote ni kumuonyesha wazi kuwa unathamini/unashukuru jitihada zake katika kazi.






6- Kushauriana (Shuura)

Hususan katika masuala ya familia
Kumpa hisia kuwa maoni yake ni muhimu kwako.
Kuyazingatia maoni yake kwa makini
Kuwa tayari kubadilisha maoni yako kwa maoni yake iwapo yatakuwa ni bora zaidi.
Mpe shukurani kwa msaada wake wa maoni.






7- Kutembelea wengine

Chagua watu wenye malezi mema wa kufanya mahusiano nao. Kuna malipo makubwa katika kuwatembelea jamaa na watu wacha Mungu. (Sio kuwatembelea kwa kupoteza wakati)
Kuwa muangalifu kuhakikisha tabia za Kiislamu wakati mnapowatembelea watu.
Usimlazimishe kuwatembelea wale ambao yeye hajisikii raha kuwa nao.






8- Muongozo wakati wa kusafiri

Muage vizuri na kumpa ushauri mwema
Mtake akuombee dua
Watake jamaa wacha Mungu na marafiki kuiangalia familia wakati wa kutokuwepo kwako.
Mpe pesa za kutosha kwa mahitaji anayoweza kuhitajia
Jaribu kuwa na mawasiliano nae ama kwa simu, e-mail (barua pepe), barua, n.k.
Rejea haraka iwezekanavyo.
Mchukulie zawadi
Jiepushe na kurejea nyakati zisizotarajiwa au nyakati za usiku.
Mchukue (safarini) ikiwezekana.






9- Msaada wa kifedha

Unatakiwa kuwa mtumizi kwa mujibu wa uwezo wake wa kifedha. Usiwe
bahili na pesa zake (wala usiwe mfujaji).
Unapata malipo kwa matumizi yote unayotumia kwa ajili ya kumkirimu (mkeo) hata kwa kipande kidogo cha mkate ambacho unamlisha kwa mkono wako (hadiyth).
Unahimizwa sana kumpa kabla yeye hajakuomba.






10- Kunukia vizuri na kujipamba mwili

Kufuata Sunnah ya kunyoa nywele za utupuni na kwapani.
Daima uwe msafi na nadhifu.
Jitie manukato kwa ajili yake (mkeo)






11- Jimai (Tendo la ndoa)

Unawajibika kulifanya mara kwa mara iwapo huna dharura (ugonjwa,n.k)
Uanze kwa “BismiLlaah” na du'aa zilizo sahihi.
Umuingilie katika sehemu iliyo sahihi tu (sio sehemu ya nyuma)
Uanze kwa vitangulizi (vya jimai) ikiwa ni pamoja na maneno ya mapenzi.
Uendelee mpaka umtosheleze hamu yake.
Mpumzike na mfanyiane mzaha mnapomaliza
Epukana na jimai wakati wa damu ya mwezi kwa sababu kufanya hivyo ni haraam
Fanya chochote unachoweza kuepuka kuharibu kiwango chake cha haya alicho nacho (haya na staha) mfano kuvua nguo pamoja badili ya kumtaka avue yeye mwanzo huku ukiwa unamuangalia.
Epuka wakati wa jimai mkao ambao unaweza kumuumiza mfano kumgandamiza katika kifua inayopelekea kumzuilia pumzi, hususan iwapo wewe ni mzito.
Chagua muda muwafaka kwa jimai na uwe unamjali kwani wakati mwengine anaweza kuwa ni mgonjwa au amechoka.






12- Kudhibiti Siri

Jiepushe na kutoa habari za siri mfano wa siri za chumbani, matatizo yake binafsi na masuala mengine ya kibinafsi.






13- Kumuongoza katika kumtii Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)

Muamshe katika sehemu ya tatu ya mwisho ya usiku kusali “Qiyaam-ul-Layl” (Swalah za ziada za usiku zenye sujuud na ruku’u za muda mrefu).
Mfundishe kile unachokijua katika Qur-aan na tafsiri zake.
Mfundishe “Dhikr” (njia za kumtaja Allaah kama alivyofundisha Mtume) za asubuhi na jioni.
Muhimize kutumia pesa kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama vile kutoa sadaka.
Mchukue katika safari ya Hijja na 'Umrah wakati unapokuwa na uwezo.






14- Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake

Mchukue katika matembezi kwa familia na jamaa, hususan wazazi wake.
Waalike kumtembelea na wakaribishe.
Wapatie zawadi kunapokuwa na jambo maalum (kama sikukuu)
Wasaidie wanapokuwa na haja kwa msaada wa fedha, nguvu, n.k.
Endeleza uhusiano mzuri na familia yake baada ya kifo chake iwapo atakufa mwanzo. Pia kwa hali kama hii mume anahimizwa kufuata Sunnah na kutoa kile ambacho yeye (mke) alizoea kutoa wakati wa uhai wake kuwapa rafiki ya jamaa zake.






15- Mafunzo ya Kiislam na kumshauri kwa kumrekebisha Hii ni pamoja na:

Misingi ya Uislam.
Haki na wajibu wake.
Kusoma na kuandika.
Kumhimiza kuhudhuria darsa na halaqah (darsa duara za Msikitini na majumbani).
Hukumu za Kiislam zinazowahusu wanawake.
Kumnunulia vitabu vya Kiislam na kaseti kwa ajili ya maktaba ya nyumbani.






16- Wivu unaokubalika

Hakikisha kuwa anavaa hijaab kamili anapotoka nyumbani.
Usimruhusu kuchanganyika ovyo na wanaume wasio- Mahram.
Jiepushe na wivu uliozidi mno. Mfano wake ni kama:
Kulichambua kila neno na sentensi asemayo na kuyajaza maneno yake kwa maana ambazo hakuzikusudia.
Kumzuia kutoka nje ya nyumba hata kama kuna sababu zinazokubalika.
Kumzuilia kujibu simu, n.k.






17- Subira na Upole

Matatizo yanatarajiwa katika kila ndoa kwa hivyo hili ni jambo la kawaida, Lililo kosa ni majibizano ya kupindukia na kuyakuza matatizo mpaka yakapelekea kuvunjika kwa ndoa.
Hasira lazima zionyeshwe pale anapochupa mipaka ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), kwa kuchelewesha Swalah, kusengenya, kuangalia yasiyofaa katika TV, n.k.
Kumsamehe makosa anayokukosea wewe (Angalia sehemu ya 18).
Ni namna gani unaweza kumrekebisha makosa yake?
Kwanza, mpe ushauri kwa njia ya mzunguko na ya moja kwa moja mara kwa mara
Kisha kwa kumpa mgongo katika kitanda kumuonyesha hisia zako). Tanabahi kuwa hii haihusishi kuhamia chumba kingine, kuhamia nyumba nyingine, au kutomsemesha
Utatuzi wa mwisho ni kumpiga kidogo (kwa namna ilivyoruhusiwa) Katika hali hii, mume ni lazima aangalie yafuatayo
Ni lazima ujue kuwa Sunnah ni kuepukakumpiga kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumpiga mwanamke wala mtumwa
Ni lazima ufanye hivyo katika hali ya juu kabisa ya kutotii, mfano mara kwa mara kukataa tendo la jimai bila ya sababu, mara kwa mara kutosali kwa wakati wake, kuondoka nyumbani kwa muda mrefu bila ya ruhusa na kukataa kusema pahala alipokuwepo, n.k
Usifanye hivyo mpaka awe umeshampa mgomo na kulijadili hilo suala pamoja nae kama ilivyoelezwa katika Qur-aan
Usimpige pigo la nguvu la kumuumiza au kumpiga usoni au katika sehemu zilizo nyepesi kuathirika katika mwili wake.
Jiepushe na kumdhalilisha kama kumpiga kwa kiatu, n.k.






18- Kusamehe na makaripio yanayofaa

Mhukumu kwa makosa makubwa tu
Msamehe makosa aliyokukosea wewe bali mhukumu kwa makosa ya haki za Allaah, mfano kuchelewesha Swalah, n.k
Kumbuka mazuri yote anayomfanyia kila wakati anapofanya makosa
Kumbuka kuwa kila mwanaadamu hukosea na umuwazie dharura mfano huenda amechoka, ana huzuni, yumo katika siku zake za mwezi au imani/mafungamano yake katika Uislam bado yamo katika kukua
Jiepushe na kumgombeza kwa mapishi mabaya kwani Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakuwahi kumlaumu yeyote katika wake zake kwa jambo hili. Iwapo amekipenda chakula, hula na iwapo hakukupenda hukiwacha na hatoi maoni yoyote.
Kabla ya kumuwekea wazi kuwa amefanya makosa, jaribu njia nyingine za mzunguko ambazo ni za hekima kuliko kumlaumu wazi wazi
Epukana na kutumia jeuri au maneno yanayoumiza hisia zake
Inapokuwa kuna ulazima wa kujadili tatizo subiri mpaka mnapokuwa faragha
Subiri mpaka hasira zipungue kidogo, hii inasaidia kuweza kudhibiti maneno
 
Jinsi Ya Kumfurahisha Mumeo

Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid

Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman

Alhidaaya.com







Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta, Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni :

Namna ya kumfurahisha Mkeo
Namna ya kumfurahisha Mumeo
Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona katika somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia haki na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali katika kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika zaidi katika majukumu ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au matendo ya Swahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni tafsiri ya kitabu cha kwanza.

Tafsiri hii ya Kiingereza imemilikiwa na MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta (Canada), na ya Kiswahili inamilikiwa na Alhidaaya.com.



Usisite kuituma kwa wengine au kuitoa kopi kwa njia nyoyote, ilimradi tu hutofanya mabadiliko yoyote, au kuongeza, au kupunguza bila ya ruhusa.

Ifuatayo ni sehemu ya KWANZA ya ufupisho wa kitabu “ How to make your wife happy” na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid.





1- Mapokezi mazuri

Baada ya kurejea kutoka kazini, skuli, safarini, au popote pale palipowatenganisha, anza kwa maamkizi mazuri.
Mpokee kwa uso mchangamfu
Jipambe na ujitie manukato (Perfume)
Anza na habari nzuri na chelewesha habari yoyote mbaya mpaka atapokwisha pumzika
Mpokee kwa maneno ya mapenzi na hamu/shauku
Fanya jitihada kubwa katika mapishi mazuri na kitayarishe kwa wakati.


2- Ipambe na ilainishe sauti

Ni kwa ajili ya mumeo peke yake, isitumike mbele ya wanaume wasio mahram (wanaume wanaoweza kukuoa iwapo utakuwa huna mume)


3- Harufu nzuri na kujipamba mwili

Ushughulikie vyema mwili wako na afya yako.
Vaa nguo za kuvutia na jitie manukato.
Koga mara kwa mara, na baada ya siku za hedhi, safisha madoa madoa yote ya damu na ondosha harufu mbaya.
Jiepushe kuonekana na mumeo ukiwa na nguo chafu au ukiwa ovyo.
Jiepushe na mapambo yaliyokatazwa, mfano wa tattoo.(kuchorwa mwili kwa kitu cha moto kwa ajili ya pambo.)
Tumia aina ya manukano, rangi, na nguo ambazo mumeo anazipenda.
Badilisha mtindo wa nywele, manukato n.k. mara kwa mara.
Hata hivyo usifanye israfu katika vitu hivi, na bila shaka fanya hivyo mbele ya mahram zako na wanawake wenzako tu.


4- Jimai (Tendo la ndoa)

Harakisha kufanya jimai pale mumeo anapokuwa na hamu ya tendo hilo.
Weka mwili wako safi na wenye kunukia kadri iwezekanavyo pamoja na kujisafisha maji maji yanayotoka wakati wa jimai.
Semeshaneni maneno ya mapenzi na mumeo.
Mwachie mumeo atosheleze kabisa hamu yake.
Chagua wakati muwafaka na muda mzuri wa kumchangamsha mumeo, na kumtia hamu ya kufanya jimai, mfano baada ya kurudi safari, mwisho wa wiki, n.k.


5- Kutosheka na kile ulichojaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

Usiwe mnyonge kwa kuwa mumeo ni maskini au na aina ya kazi anayofanya.
Uwaangalie masikini, wagonjwa, na vilema na kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa yote yale uliyopewa.
Ni lazima ukumbuke kuwa utajiri wa kweli upo katika Iman na uchaji Allaah.


6- Kutoshughulishwa na mambo ya kidunia

Usiichukulie dunia hii kuwa ya matumaini na kushughulishwa nayo.
Usimdai mumeo vitu vingi visivyo na ulazima.
Kutosheka na kuishi maisha ya kawaida hakuna maana ya kutofurahia/kutotumia kilicho kizuri na kilichoruhusiwa (halali), bali kunamaanisha mtu kuangalia akhera yake na kutumia kile ambacho Allaah Amempa kwa ajili ya kupata Pepo (Jannah).
Muhimize mumeo kupunguza matumizi na kubakisha fedha kwa ajili ya kutoa sadaka na kuwalisha masikini na wasiojiweza


7- Shukurani

Kutokana na hadiyth ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wengi wa watu wa motoni ni wanawake kwa sababu hawana shukurani na kutoridhia wema wanaofanyiwa.
Matokeo ya kuwa na shukurani ni kuwa mumeo atakupenda zaidi na atafanya awezalo kukufurahisha kwa njia nyingi.
Matokeo ya kutokuwa na shukurani ni kuwa mumeo atavunjika moyo na ataanza kujiuliza: Kwa nini nilazimike kumfanyia wema hali ya kuwa hana shukurani?


8- Kujitolea na Twaa

Hususan nyakati za maharibiko/matatizo makubwa katika mwili wa mumeo au katika kazi yake, mfano ajali au kufilisika.
Kumpa msaada kwa kufanya kazi, msaada wa fedha, na vitu vyengine iwapo utahitajika.


9- Kumtii

Kumtii katika yote anayokuamrisha, isipokuwa katika yale yaliyoharamishwa.
Katika Uislam, mume ndie kiongozi wa familia, na mke ni msaidizi na mshauri wake.


10- Kumliwaza anapokasirika

Kwanza kabisa, jaribu kujiepusha na kile ambacho una uhakika kuwa kitamkasirisha.
Bali iwapo imetokezea kuwa huwezi, basi jaribu kuepusha ugomvi kwa njia zifuatazo:
Iwapo wewe ndiye uliyekosea, basi mtake radhi (muombe msamaha)
Iwapo yeye ndiye aliyekosea basi:
Endelea kunyamaza badala ya kubishana au
Samehe haki yako au
Subiri hadi zitakapokwisha hasira zake na mlijadili suala hilo kwa amani
Iwapo amekasirishwa na mambo nje ya nyumba basi:
Endelea kunyamaza kimya hadi hasira zake zitapokwisha
Mpe udhuru (wa hasira zake), mfano kuchoka, matatizo kazini, kuna mtu amemuudhi.
Usimuulize masuala mengi na kushikilia kujua nini kimetokezea, mfano (kumwambia)
Ni lazima unieleze nini kimetokezea.
Ni lazima nijue nini kimekukasirisha namna hiyo.
Unanificha kitu, na mimi nina haki ya kujua.


11- Muongozo (na majukumu) anapokuwa hayupo:

Jilinde na mahusiano yoyote yaliyokatazwa.
Zidhibiti siri za familia, hususan jimai (tendo la ndoa) na mambo ambayo mumeo hapendi watu wengine wayajue.
Ishughulikie nyumba na watoto.
Ishughulikie mali yake na vitu vyake.
Usitoke nje ya nyumba yako bila ya ruhusa yake na bila ya hijaab iliyo kamili.
Usikaribishe watu ambao mumeo hapendi kuja kwao.
Usimruhusu mwanamme yeyote asie Mahram wako kuwa nawe faragha pahala popote.
Kuwa mwema kwa wazazi wake na jamaa zake akiwa hayupo.


12- Kuonyesha heshima kwa familia yake na rafiki zake

Ni lazima uwakaribishe wageni wake na ujaribu kuwafurahisha, hususan wazazi wake.
Ni lazima uepuke matatizo kati yako na jamaa zake kwa kadri iwezekanavyo.
Ni lazima uepuke kumuweka pahala ambapo inambidi achague kati ya mama yake na mkewe.
Onyesha urafiki (makaribisho mazuri) kwa wageni wake kwa kuwatayarishia pahala pazuri pa kuketi, chakula kizuri, kuwakaribisha vizuri wake zao, n.k.
Muhimize kuwatembelea jamaa zake na uwaalike nyumbani kwako.
Wapigie simu wazazi na dada zake, watumie barua, na wanunulie zawadi, wasaidie wakati wanapoharibikiwa, n.k.


13- Wivu wenye kukubalika

Wivu ni aina ya mapenzi ya mke kwa mumewe bali ni lazima ubakie katika mipaka ya Uislam, mfano kutowatukana na kuwasengenya wengine, kuwavunjia heshima zao, n.k.
Usifuate au kuanzisha tuhuma zisizo na msingi


14- Subira na kumpa moyo

Kuwa na subira mnapokabiliwa na umasikini na hali ngumu (kimaisha na kifamilia).
Wakati mnapokabiliwa na majanga na maharibiko ambayo yanaweza kutokea kwako, kwa mumeo, kwa watoto wako, jamaa au mali, mfano magonjwa, ajali, kifo, n.k.
Wakati mnapokabiliwa na matatizo katika Da’wah (kufungwa jela, kukamatwa, n.k.), kuwa na subira na mhimize katika kubaki katika njia ya Allaah na kumkumbusha kuhusu Pepo (Jannah).
Anapokufanyia uovu, mlipe uovu wake kwa kumfanyia wema.


15- Msaidie katika kumtii Allaah, Da'awah (Ulinganiaji) na Jihaad

Shirikiana na mumeo na mkumbushe ibada mbali mbali za faradhi na za Sunnah.
Muhimize kusali usiku.
Sikiliza na soma Qur-aan peke yako na ukiwa pamoja na mumeo.
Mkumbuke (mtaje) Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) sana, hasa hasa baada ya Alfajiri na kabla ya Magharibi.
Pangeni pamoja shughuli za Da’wah kwa wanawake na watoto.
Jifunze hukumu za Kiislam na adabu za Kiislam kwa wanawake.
Msaidie mumeo katika shughuli zake kwa kumhimiza, kumpa ushauri mwema, kumliwaza machungu yake, n.k.
Samehe baadhi ya haki zako na samehe sehemu ya muda wako wa kuwa pamoja na mumeo kwa ajili ya Da’wah.
Mhimize kwenda Jihad anapohitajika na mkumbushe kuwa wewe na watoto mtakuwa katika hifadhi ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).


16. Utunzaji mzuri wa Nyumba

Iweke nyumba safi, weka mapambo na iweke katika mpangilio mzuri.
Badilisha mpangilio wa nyumba mara kwa mara ili kuzuia kupoteza hamu nayo na kuchoshwa nayo.
Tayarisha chakula kizuri na chenye afya.
Jifunze ujuzi wowote wa muhimu kuhusu uangalizi wa nyumba, mfano kushona, n.k.
Jifunze namna ya kuwalea vyema watoto na kwa njia ya Kiislam.


17- Kuhifadhi/Kutunza fedha na familia

Usitumie fedha zake, hata kwa sadaka bila ya ruhusa yake labda uwe na uhakika kuwa atakubaliana na matumizi hayo.
Ilinde nyumba yake, gari, n.k. anapokuwa hayupo.
Waweke watoto katika hali nzuri, nguo safi, n.k. Zingatia lishe yao, afya, elimu, tabia, n.k wafunze Uislam na wahadithie visa vya Rusuli ('Alayhimus-salaam) na Swahaba (Radhwiya Allaahu 'anhum).
 
Manufaa Na Matatizo Katika Ndoa
Mume Na Mke


Mume Na Mke



Imefasiriwa Na: Ummu Ahmad



Alhidaaya.com





Manufaa Katika Ndoa



1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu.



2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) na Nabiy Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu.



Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi:



"Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu." [Ahmad]



3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa:



"Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake." [Riyadhus-Swaalihiyn]



Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:



4. Kinga kutokana na Shaytwaan katika mambo yanayopelekea au yanokaribisha tendo la zinaa.



5. Utulivu wa akili na moyo na kuwa na urafiki ambao hupelekea mapenzi na huruma baina ya mume na mke.



6. Kunganisha kwa Familia za pande mbili za ukeni na uumeni.



7. Kusaidiana katika kazi za nyumba (sio kumuachia mke kazi zote za ndani ya nyumba). Hii ni tabia ambayo ingalipo kwa baadhi ya akina baba. Kwa vile tabia hii imekuzwa na utamaduni wetu wa tunakotoka, kinyume kabisa na maamrisho ya dini yetu ya Kiislamu yanavyotuagiza.



8. Kuelimishana majukumu ya kifamilia. Pia kuweka bidii na kuwa tayari kuihami na kuitunza familia. Na vile vile kuishughulikia na kuitimizia mahitaji yake yakiwa ama ya (kimwili, kimavazi, kisiha, kimawazo na kiroho) na kustahamiliana pale panapotokea kutoelewana.





Matatizo Katika Ndoa



Wakati huo huo kuna matatizo yanayopatikana katika ndoa ambayo inabidi tuzingatie na kujichunga ili tuepukane na matatizo hayo. Nayo ni kama yafuatayo:



a. Kushindwa kuchuma pato la halali, ambapo itapelekea kutafuta njia ambazo si za halali za kimapato ili kuweza kutimiza mahitaji ya familia. Haimfalii mke kumlazimisha mumewe ampatie mambo yaliyo nje ya uwezo wa mume. Na tuwaige wanawake wema waliopita, ambao kila waume zao wakitoka kwenda kwenye shughuli zao za kutafuta riziki, wakiwausia kuwa wasirejee na chochote cha haramu. Wakiwanasihi waume zao kuwa ni bora wastahamili kwa njaa ya hapa duniani kwani adhabu ya kesho Aakhirah sio ya kustahamilika.



b. Kushindwa kutimiza majukumu ya ndoa, na hasa kutimiza haki za mke au kutoweza kustahamili kwenye wakati mgumu wa kimaisha. Na tuwe makini katika suala hili kwani kuna ile dhana ya kuwa ndoa ni jambo la kujionyesha tu kuwa fulani kaoa au kaolewa.



"Kila mmoja kati yenu ni mchungaji, na kila mmoja kati yenu atapaswa kuulizwa ya juu ya kile anachokichunga. Mume ni mchungaji wa familia yake, naye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga. Na mke ni mchungaji wa nyumba ya mumewe, naye pia atapaswa kuulizwa juu ya anachokichunga. Hivyo basi, kila mmoja kati yenu ni mchungaji ambaye atapaswa kuulizwa juu ya anaowachunga" [Al-Bukhaariy na Muslim]



c. Kuacha kushughulikia mambo muhimu ya kidini, kwa mfano kutumia muda mwingi katika mambo ya anasa za kidunia kama vile kuangalia Televisheni, kwenda kwenye shehere za kuzaliwa mtoto au kwa kutimiza umri fulani wa mtoto (birthday party), badala ya kutumia muda huo kwa kutengeneza maisha ya Aakhirah ambayo ndio ya milele. Kama tunavyotanabahishwa kwenye Quraan Tukufu:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ عَن ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ﴿٩﴾

Enyi walioamini! Zisikupurukusheni mali zenu na wala watoto wenu mkaacha kumdhukuru Allaah. Na yeyote atakayefanya hivyo basi hao ndio waliokhasirika. [Al-Munaafiquun 63: 9]



Mwandishi wa mada hii amemalizia kwa kusema kuwa:

Dinaar (pesa) unayoitumia katika njia za Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa), dinaar unayoitumia kumuachia huru mtumwa, dinaar unayoitumia katika kutoa sadaka kwa mtu anayehitaji sadaka hiyo, basi hakuna Dinaar iliyo bora kati ya dinaar hizo ila ile unayoitumia kwa ajili ya familia yako.



Msemo huu una maana ya kwamba hakuna jambo muhimu katika mafundisho ya kijamii ya Kiislamu kama lile la kuzishughulikia familia zetu kwa mali na hali, ili kuweza kupata umma mwema na bora duniani na Aakhirah.



Mwishoni tunamuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'aalaa) Atupe wake, waume na watoto watakaotupa kitulizo cha macho na nyoyo zetu, na Atufanye tuwe viongozi wazuri wa familia zetu. Ee Allaah Mpe Bwana Wetu Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Baraka na Amani na Familia yake pamoja pia na Swahaba wake. "Aamiyn"
 
Muenzi Mke Wako



Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy



Imefasiriwa na Iliyaasa



Alhidaaya.com





Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako mpenzi.



Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.



Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona ni macho yake. Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu wake mzima.



Kielezo bora kabisa ambacho mimi binafsi nishawahi kusoma kinafafanua ukaribu wa wanandoa juu ya wao kwa wao na kielezo hicho kipo katika aya ya Qur-aan ambayo inasema:



هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ

Wao ni vazi kwenu na nyinyi ni vazi kwao. .[Al-Baqarah: 187].



Na Kweli, wanandoa ni kama vazi juu ya wao kwa wao kwa sababu wanapeana ulinzi, liwazo, kinga (stara), msaada (tegemeo), na mapambo ambayo vazi linampa mtu. Hebu jaribu kufikiri msafara wakati wa siku za baridi kwenda sehemu kama vile Alaska bila ya kuwa na nguo! Wanandoa wetu wanatupa kiwango kile kile cha faraja (liwazo), ulinzi, na msaada katika msafara wa maisha yetu katika dunia hii kama vile nguo itakavyofanya katika msafara wa Alaska.



Mahusiano baina ya wanandoa ni ya kustaajabisha kabisa katika mahusiano yote ya kibinaadamu: Idadi ya mapenzi na mahaba, undani na ukaribu, huruma na imani, amani na utulivu ambao unajaza nyoyo za wanandoa ni jambo lisiloelezeka kwa wepesi. Ufafanuzi pekee wa mantiki ambao unaweza kuelezeka juu ya haya mastaajabu makubwa katika hisia zote za kibinaadamu ni kwamba: Ni kitendo cha Allah Subhanahu wa Ta'aalaa:

وَاللَّـهُ جَعَلَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا

Na Allaah Amekufanyieni wake katika jinsi yenu; [An-Nahl: 72]



Rabb wetu tu Allaah Subhanahu wa Ta'aalaa katika katika Utawala Wake usio na upeo wa huruma Yake isiyo na mipaka na Hekima Yake adhimu Anaweza kujenga na kuzididimiza katika akili hizi hisia za kustaajabisha na za kubarikiwa katika nyoyo za wanandoa. Kwa kweli Allah Subhanahu wa Ta'aalaa Anawakumbusha wale ambao wanatafuta ishara Zake katika ulimwengu huu kwamba hisia hizi katika moyo wa wanandoa ni katika ishara Zake ambazo zinatakiwa zimuongoze mwanaadamu katika kuwepo Kwake kama Alivyosema katika Qur-aan,



وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾

Na katika Aayaat (ishara, dalili) Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao; na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rahmah. Hakika pana katika hayo, bila shaka Aayah (ishara, zingatio nk) kwa watu wanaotafakari. [Ar-Ruwm: 21]



Lakini Allaah Subhanahu Wa Ta’aalaa Anajua kwamba moyo wa binaadamu sio kitu ambacho kiko tuli, wakati mwengine huwa dhaifu na wakati mwengine huwa na nguvu. Hisia zinaweza kubadilika na hubadilika pindi wakati unavyosogea. Mapenzi yanaweza kufifia na kupayuka mbalini. Mshikamano wa ndoa unaweza kuwa dhaifu kama haujahudumiwa vizuri. Furaha katika ndoa haiwezi kudharauliwa; furaha ya kuendelea inahitaji utowaji wa daima kutoka pande zote. Ili mti wa mapenzi ya ndoa ubaki hai na kuendelea kuishi, udongo lazima udumishwe, uhifadhiwe, umwagiwe maji na ulelewe.



Kumbuka kwamba Nabiy wetu Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipata nafasi ya kwenda kwenye majangwa na kushindana mbio na mke wake Bibi 'Aaishah. Bibi 'Aaishah alimshinda Nabiy lakini baadae aliponenepa, Nabiy alimshinda Bibi 'Aaishah. Kumbuka kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimchukua mkewe kwenda kuwatazama vijana wa Ki-Ethiopia wakicheza michezo ya utamaduni wao. Maonyesho ya hisia yanahitajika kuweza kuufanya mshikamano wa ndoa usifanye kutu na kuoza. Kumbuka kwamba utapata thawabu kutoka kwa Allaah (Subhanahu wa Ta'aalaa) kwa hisia zozote unazomuonyesha mkeo kama Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyosema:



"Mmoja wenu atapata thawabu kwa chochote ambacho atafanya ili kutafuta radhi za Allaah hata kwa tonge analomlisha mkewe"



Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kuweka chakula kwenye mdomo wa mkeo, kumfungulia mlango wa gari, na hali kadhalika. Kumbuka kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anasogeza goti lake kwa mkewe amkanyage kuweza kumpanda ngamia.



Jaribu kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja. Kuuimarisha uhusiano kati yenu na Allaah (Subhanahu wa Ta'aalaa) ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Allah (Subhanahu wa Ta'aalaa) daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.



Kumbuka kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwapa habari nzuri (aliwabashiria) wanandoa wanaoamka usiku kuswali pamoja. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anamsisitiza mwanandoa anayeamka mwanzo amuamshe mwenzake, japo kummwagia maji katika uso wake.



Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongea nae, mchekee, tafuta ushauri wake, muulize juu ya mawazo yake, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:



"Wabora katika nyinyi ni wale ambao ni wabora kwa wake zao".



Mwishowe, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenziwe mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. amilia yake, anaowapenda yeye uwapende pia. Usiwe kama mwenzangu mmoja ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia wazi mkewe "Mimi siwapendi wazazi wako". Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, “Na wako pia siwapendi”.



Mapenzi yasiishe na pia tunaamini kuna maisha baada ya mauti ambapo wale ambao walifanya wema katika dunia hii wataungana na wanandoa wenzio wataungana na watoto wao. Allaah Subhaanahu wa Ta'aalaa anasema katika Qur-aan Tukufu:

ادْخُلُوا الْجَنَّةَ أَنتُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ تُحْبَرُونَ﴿٧٠﴾

Ingieni Jannah nyinyi na wake zenu mfurahishwe. [Az-Zukhruf: 70]



Pia Na mfano bora katika mintarafu hii itakuwa ni Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye mapenzi yake kwa Bibi Khadiyjah, mkewe aliyeishi naye kwa miaka 25 yalisogea mpaka kwa wale aliowapenda Khadiyjah; mapenzi yake haya yaliendelea hata baada ya kufa Bibi Khadiyjah. Ilikuwa miaka mingi baada ya kifo cha Bibi Khadiyjah na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hakumsahau na kila panapochinjwa mbuzi katika nyumba yake basi hutuma kifurushi kwa familia ya Bibi Khadiyjah na marafiki zake na kila akihisi kuwa mgeni anayegonga mlango ni Dada ya Khadiyjah aitwaye Hala, Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiomba huku akisema, "Ee Allaah Jaalia awe ni Hala."
 
01-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Kwa nini Allaah Katuumba?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com





01-Kwa nini Allaah Katuumba?



Allaah Ametuumba ili tumuabudu na tusimshirikishe Naye kwa chochote.

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu. [Adh-Dhaariyaat: 56]



((حَقُّ اَللَّهِ عَلَى الْعِبَادِ أَنْيَعْبُدُوهُ، وَلاَ يُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا))متّفق عَلَيهِ

((Haki ya Allaah kwa waja wake ni kwamba wamwabudu na wasimshirikishe na chochote)). [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com





02-Vipi tumuabudu Allaah?



Tumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa ikhlaasw kama Alivyotuamrisha Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)



وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini [Al-Bayyinah: 5]



((مَن عمِلَ عمَلاً لَيْسَ عَلَيهِ أمْرُنا فَهُوَ رَدٌّ)) رواه مسلم .

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa katika jambo letu kitarudishwa)) [Muslim]



Yaani: Hakitapokelewa.
 
03-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Tumuabudu Allaah kwa kumuogopa na kutumaini?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com







03- Je, Tumuabudu Allaah kwa kumuogopa na kutumaini?



Naam! Tumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa kumukhofu na kuwa na matumaini

وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا ۚ

Na muombeni kwa khofu na matumaini. [Al-A’raaf: 56]



Yaani: Kukhofu moto na kutumaini Jannah.



((أسألُ اللهَ الجنّة وأعوذ بِهِ مِن النّار)) صحيح رواه أبو داود .

((Namuomba Allaah Jannah na najikinga Kwake kutokana na moto)) [Swahiyh ameipokea Abuu Daawuwd]
 
04-Nini Ihsaan katika ‘ibaadah?



Maana ya Ihsaan katika i’baadah ni kujichunga kuwa makini katika ‘ibaadah kwa ajili Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Pekee.

إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا ﴿١﴾

Hakika Allaah daima Amekuwa juu yenu Mwenye kuchunga [An-Nisaa: 1]

الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ ﴿٢١٨﴾

Ambaye Anakuona wakati unaposimama. [Ash-Shu’araa: 218]



((الإحسانُ أَنْ تعبُدَ اللهَ كأنّك تراه فإن لَمْ تكن تراهُ فإنَّه يراك)) رواه مسلم

((Ihsaan ni kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama vile unamuona, na kama humuoni basi Yeye Anakuona)). [Muslim]
 
05-Kwanini Allaah Ametuma Rusuli?



Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amewatuma Rusuli ili walinganie watu kumwabudu na kuepukana na kumshirikisha.



وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ

Na kwa yakini Tulituma katika kila ummah Rasuli (alinganie) kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na twaghuti. [An-Nahl: 36]



((الأنبياء إخوةٌ ودينُهُم واحد)) متّفق عَلَيهِ

أَيْ كلُّ الرسل دعوا إِلَى التّوحيد

((Manabiy ni ndugu na Dini yao ni moja)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Yaani: Rusuli wote wamelingania Tawhiyd
 
06-Nini Tawhiyd ya Ilaah?



Tawhiyd ya Ilaah ni kumfanyia ‘ibaadah Pekee Yeye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kama du’aa, kuchinja, kuweka nadhiri na kadhaalika.

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ

Basi jua kwamba laa ilaaha illa-Allaah, hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah [Muhammad: 19]

Yaani: Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah.



((فَلْيَكُنْ أَوَّلَ مَا تَدْعُوهُمْ إِلَيْهِ شَهَادَةَ أَنلاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ)) متّفق عليه

أَيْ إِلَى أَنْ يوحّدوا الله

((Basi liwe jambo la kwanza la kuwalingania wao Kwake ni "Shahaadah kwamba hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]



Yaani; Wampwekeshe
 
07-Nini maana ya Laa Ilaaha illa Allaah.



Maana ya laa ilaaha illa-Allaah ni: Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ

Hivyo ni kwa kuwa Allaah Ndiye wa Haki na kwamba wale wanaowaomba badala Yake, ni batili; [Luqmaan: 30]



((من قَالَ لآ إله إِلاَّ الله وكَفَرَ بِمَا يُعبدُ مِن دون الله حَرُمَ مالُه ودمُه)) مسلم

((Atakayesema 'Laa ilaaha illa Allaah na akakanusha wanaoabudiwa wasio Allaah italindwa (itakuwa haramu mtu kuchukua) mali yake na damu yake (uhai wake)) [Muslim]
 
Naam ndugu zangu katika imani tutaendelea baadae kupata elimu

Inshaallah....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…