Hili darsa la Swala ya Nabii swallallahu alaih wasallam litatufikisha mpaka kwenye namba 40 na kitu,kikubwa ni ufuatiliaji tu

Baadae inshallah
 
Abuu Huraira r.a amesimulia kuwa Nabii swallallahu alaih wasallam amesema " Hakika Allah amesamehe kwa umma wangu,fikra mbovu na matamanio ya nafsi zao,ikiwa hawa kuyatenda au kuyazungumza".


Inamaana kila mtu miongoni mwetu akiwemo Etugrul bey kuna wakati tunakuwa na fikra mbaya kuhusiana na mtu au jambo fulani,lkn maadamu itabakia mdani ya nafsi zetu basi tupo salama,lakini lau tukatamka kwenye ulimi,basi tutahukumiwa kwa maneno hayo

Vile vile lau tukawa na matamanio ya kuzini mathalani lkn maadamu hatujazungumza wala kutenda kitendo hicho basi tupo salama,huyo ndio Allah mwingi wa rehema mwenye kuremu



Abu Huraira r.a amesimulia kuwa Rasullullahi swallallahu alih wasallam amesema " Fanyeni wingi wa kushuhudia Laillaaha illa llahu ( Hakuna anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah) kabla kizuizi (kifo au maradhi) hakijakuja baina yenu na baina yake"


Uthman bin Affan r.a amesimulia.kuwa Rasulillahi swallallahu alaih wasallam amesema " Yule atakaye kufa naye anajua (na anaamini) kuwa hapana anayepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah ,ataingia Jannah"


Ali r.a amesimuli kuwa Nabii s.a.w amesema katika hadith Qudsi: "Kwa hakika Mimi ndiye Allah! Hakuna anayepaswa kuabudiwa kwa haki ila Mimi,Yule atakaye ukiri upweke Wangu,ataingia kwenye Ngome Yangu na atakayeingia kwenye ngome Yangu,amesalimika na Adhabu Yangu"
 
Asalaam alaikum ndugu zangu katika imani

Ndugu zangu miongoni mwa mambo ambayo Allah hayapendi kwa mja wake ni mtu kujiona ni bora kuliko wengine

Hakika sifa hii Allah haipendi kabisa,hii ni sifa ya Ibilisi laana ziwe juu yake,Ibilisi alijiona bora kwa Adam ndio maana alipoambiwa na Allah amsujudie alikataa

Alijiona yeye kaumbwa na Miale ya Moto iweje amsujudie Adam aliyeumbwa na Udongo

Haya nayo yamo miongoni mwetu,anayekaaa ushuani anajiona bora kuliko wa uswahilini

Mwenye kipato kizuri anajiona bora kuliko mwenye kipato kidogo

Mwenye elimu kubwa anajiona bora kuliko mwenye elimu ndogo

Hii tabia ni mbaya,muislamu hapambwi na tabia hizi,siku zote usijione wewe ni mbora kuliko wenzako,hata kama uko vizur kiasi gani penda kujishusha wallah utakuwa kipenzi cha Allah
 
Darsa inaendelea sehemu ya 17,kumbuka tunasoma Swalla Ya Rasullullahi



017-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Aamiyn - Imaam Kunyanyua Sauti Yake Anapoileta




AAMIYN, IMAAM KUNYANYUA SAUTI YAKE ANAPOILETA







Kisha alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anapomaliza kusoma Al-Faatihah husema:



‘Aamiyn’




kwa sauti na huku akiirefusha sauti yake[1]







Pia alikuwa akiwaamrisha wenye kumfuata Mamuumiyn waseme Aamiyn, kwa kusema: ((Imaam ataposema:




“Ghayril Magh-dhuubi ‘alayhim waladh dhwaaaaaalliyyyyyyn”




“Sio waliokasirikiwa wala waliopotea”




basi semeni: ‘Aamiyn’ [kwani Malaika na wao pia huwa wanasema: ‘Aamiyn’ na hakika Imaam anasema: 'Aamiyn']))




Katika usemi mwengine: ((Imaam atakaposema ‘Aamiyn’ basi na nyinyi semeni: ‘Aamiyn’ - kwani itakayeafiki ‘Aamiyn’ yake na ‘Aamiyn’ ya Malaika - [katika usemi mwengine] ((Anaposema Mmoja wenu katika Swalah ‘Aamiyn’ na Malaika mbinguni wakasema ‘Aamiyn’, zikaafikiana moja na nyingine, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia))[2]




Na Katika Hadiyth nyingine, ((Semeni: Aamiyn, Allaah Atakujibuni))[3]




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Mayahudi hawakuoneeni choyo kwa jambo lo lote lile zaidi kama wanavyoona choyo kwa kutoleana saalam na kuitikia Aamiyn [nyuma ya Imaam]))[4]


[1] Al-Bukhaairy katika Juz' Al-Qiraah na Abu Daawuud kwa isnaad Swahiyh.

[2] Ash-Shaykhaan na An-Nasaaiy na Ad-Daarimy. Maneno yaliyozidi yameripotiwa na wawili wa mwisho na ni dalili kuwa Hadiyth hii haiwezi kuthibitisha kuwa Imaam hasemi ‘Aamiyn’ kama ilivyoripotiwa na Maalik, hivyo Ibn Hajar anasema katika Fat-h Al-Baariy: "Inaonyesha dhahiri kwamba Imaam anasema ‘Aamiyn’ ". Ibn 'Abdil Barr anasema katika Tamhiyd (7/13), "Ni rai ya Waislamu wengi pamoja na Maalik kama watu wa Madiynah walivyosimulia kutoka kwake, kwani ni Swahiyh kutoka kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) kutokana na Hadiyth ya Abu Hurayrah (ambayo ni hii) na ile ya Waail Ibn Hujr (yaani ya nyuma yake)"




[3] Muslim na Abu Aawaanah.

[4] Al-Bukhaariy katika Al-Adaab Al-Mufrad, Ibn Maajah, Ibn Khuzaymah, Ahmad na Siraaj kwa isnaad mbili na zote ni Swahiyh.

TANBIHI:

‘Aamiyn’ ya Maamuumiyn nyuma ya Imaam inakuwa kwa sauti na inakuwa inaletwa pamoja na ‘Aamiyn’ ya Imaam, na wala hawamtangulii kama wafanyavyo waswaliji wengi, na wala hawaicheleweshi na ‘Aamiyn’ ya Imaam. Hii ndio iliyokuwa Raajih (na nguvu kwangu) kama nilivyoihakiki katika baadhi ya vitabu vyangu; miongoni mwake ni ‘Silsilat al-Ahaadityh Adh-Dhwa'iyfah’ (Namba. 952 Mjalada 2) ambayo imechapishwa kwa Fadhila Zake Allaah, na Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (1.205). Taz. Kiambatisho 6.
 
018-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kisomo Chake (صلى الله عليه وآله وسلم) Baada Ya Al-Faatihah




KISOMO CHAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) BAADA YA AL-FAATIHAH




Kisha, alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma Surah nyingine baada ya al-Faatihah, na alikuwa akikirefusha hicho kisomo mara nyingine, na mara nyingine akikifupisha kwa sababu ya safari, au kikohozi, au maradhi au kilio cha mtoto.




Kama alivyosema Anas Ibn Maalik (رضي الله عنه): "Alifupisha[1] Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) siku moja katika Swalah ya Alfajiri" (Na Katika Hadiyth nyingine, "Aliswali (صلى الله عليه وآله وسلم) Swalah ya Asubuhi akasoma Surah mbili zilizo fupi sana katika Qur-aan)". Pakaulizwa: "Ewe Mjumbe wa Allaah, kwa nini umefupisha?" Akasema: ((Nimesikia kilio cha mtoto hivyo nimehisi kwamba mama yake yu pamoja na sisi anaswali, kwa hiyo nikataka kumpa wasaa mama yake kwa ajili yake))[2]




Na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Hakika mimi huingia katika Swalah hali ya kuwa ninataka kuirefusha, ninaposikia kilio cha mtoto, hufupisha Swalah yangu kwa kuelewa machungu makubwa ya mama yake kwa kilio chake))[3]




"Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akianza kusoma kutoka mwanzo wa Surah, na aghlabu huimaliza"[4]




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Ipeni kila Surah sehemu yake katika Rukuu na Sujuud))[5]




Katika usemi mwengine: ((Kwa Kila Surah Raka’ah))[6]




Mara nyingine huigawa Surah katika Rakaa mbili[7] na mara nyingine huirudia yote nzima katika Raka’ah ya pili.[8]




Mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha katika Rakaah baina Surah mbili au zaidi.[9]




Mtu Mmoja katika Answaar alikuwa akiswalisha katika Msikiti wa Qubaa, na alikuwa kila anapoanza kuwasomea Surah[10] katika Swalah baada ya al-Faatihah, huanza kwa ‘Qul Huwa Llaahu Ahad’ [Suratul-Ikhlaasw: 112] hadi mwisho, kisha anasoma Surah nyingine pamoja nayo, na alikuwa akifanya hivyo katika kila Raka’ah. wenzake walimuuliza kwa kusema: "Unaanza na Surah hii, kisha huoni kama inakutosheleza mpaka unasoma nyingine, basi chagua moja; isome hiyo pekee au iache na uisome nyingine". Akasema: "Sitoiacha, ikiwa mtapenda mimi nikuswalisheni (niwe Imaam wenu) kwayo, nitaendelea, lakini ikiwa mtachukiwa, sitokuswalisheni tena", na walikuwa wakimuona kuwa yeye ni mbora miongoni mwao, na pia hawakuwa wanapendekezewa kuswalishwa na mwenginewe. Na pindi alipokuja Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamuelezea habari hiyo, Akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Ewe fulani, kipi kinachokuzuia kutekeleza wanayokuomba watu wako? Na Kipi kinachokupelekea kuwa lazima uisome Surah hii katika kila Raka’ah?)) Akasema: "Hakika Naipenda Surah hii" akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Mapenzi yako kwayo yatakuingiza Peponi))[11]










[1] Alifupisha Swalah kwa maana kuwa hakuirefusha, na katika Hadiyth hii na nyingine kama hii zinaonyesha kuruhusiwa watoto wadogo kuingia Misikitini. Ama Hadiyth iliyozagaa na kueleweka na wengi hadi kufikia kuwa inasemwa na kila mtu: "Watengeni mbali watoto wenu na Misikiti… "ni hadiyth dhwa'iyf na haiwezi kuwa ni dalili kabisa kwa mawafikiano yaliyopo. Na Miongoni mwa walisema kuwa ni dhwa'iyf ni: Ibn Al-Jawziy, Al-Mundhiriy, Al-Haythamiy, Ibn Hajar Al-'Asqalaaniy na Al-Buuswiyriy. Na akasema 'Abdul-Haqq Al-Ishbiyliy: "Haina asili"

[2] Ahmad kwa isnaad Swahiyh. Na Hadiyth nyingine imepokelewa na Ibn Abi Daawuud katika al-Maswaahif (4/14/2).

[3] Al-Bukhaariy Na Muslim

[4] Linathibitishwa hili na Hadiyth nyingi zilizotajwa mbele.

[5] Ibn Abi Shaybah (1/100/1), Ahmad na 'Abdul-Ghaniy Al-Maqdisiy katika Sunan (9/2) kwa isnaad Swahiyh.

[6] Ibn Naswr na At-Twahaawiy kwa isnaad Swahiyh. Maana ya Hadiyth kwangu ni: Jaaliyeni kwa kila Rakaa Surah kamili, ili Rakaa iwe na hadhi yake kamili kwa hiyo Surah! Amri hii ni pendekezo na sio lazima utekelezaji wake kutokana na dalili inayofuatia.

[7] Ahmad na Abu Ya'ala kutoka njia mbili. Pia tazama "kisomo katika Swalah ya Alfajiri'

[8] Kama alivyofanya katitka Swalah ya Alfajiri, kama itakavyofuatia.

[9] Maelezo yake na vyanzo vyake vitafuatia karibuni.

[10] Yaani miongoni mwa Surah baada ya al-Faatihah.

[11] Al-Bukhaairy ameipokea ta'liyqan (ni hadiyth inayoondoshwa mwanzo wa isnaad yake Msimulizi mmoja au zaidi kwa mfululizo); na At-Tirmidhiy ameipokea Mawswuulan (ni hadiyth inayoungana isnaad yake, iwe imemalizika kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) au kwa Swahaba), na At-Tirmidhiy akasema: ni Swahiyh.
 
019-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kuchanganya Kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) Baina Ya Surah Zinazofanana Na Nyinginezo Katika Rakaa


KUCHANGANYA KWAKE (صلى الله عليه وآله وسلم) BAINA YA SURAH ZINAZOFANANA NA NYINGINEZO KATIKA RAKAA




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akiunganisha baina ya An-Nadhwaair([1]) miongoni mwa Surah za Mufasswal([2]), hivyo basi alikuwa akisoma jozi mojawapo za Surah zifuatazo katika Rakaa moja([3]):




Ar-Rahmaan (55: 78) ([4]) na An-Najm (53: 62).

Al-Qamar (54: 55) na Al-Haaqqah (69: 52).

At-Twuur (52: 49) na Adh-Dhaariyaat (51: 60).

Al-Waaqi'ah (56: 96) na Al-Qalam (68: 52).

Al-Ma'arij (70:44) na An-Naazi'aat (79:46).

Al-Mutwaffifiyn (83: 36) na 'Abasa (80: 42).

Al-Muddaththir (74: 56) na Al-Muzzammil (73: 20).

Ad-Dahr (76: 31) na Al-Qiyaamah (75: 40).

An-Nabaa (78: 40) na Al-Mursalaat (77: 50).

Ad-Dukhaan (44: 59) na At-Takwiyr (81: 29).




Mara nyingine alikuwa akiunganisha baina ya Surah kutoka Sab'at-Twiwaal (Surah Saba ndefu); kama al-Baqarah, an-Nisaa na aal-'Imraan katika Rakaa moja kwenye Swalah ya usiku kama itakavyokuja. Na alikuwa akisema:

((Swalah bora kabisa ni yenye kisimamo kirefu)).([5])




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma:




((أَلَيْسَ ذَلِكَ بِقَادِرٍ عَلَى أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَى))




Alaysa dhaalika biqaadirin ‘alaa-an Yuhyiyal Mawtaa




((Je! Huyo hakuwa ni Muweza wa kufufua wafu)). [Al-Qiyaamah 75: 40)




Husema:





Sub-haanak fabalaa

Utukufu ni Wako Ndio hapana shaka




Na anaposoma:

سَبِّحِ اسْمَ رَبِّكَ الْأَعْلَى




Sabb-hisma Rabbikal A’laa

((Litakase Jina la Mola wako Mlezi Aliye juu kabisa)). [Al-A'laa 87: 1)




Husema:


Sub-haana Rabbiyal A’laa

Ametakasika Mola wangu Aliye juu([6]).
















[1] "An-Nadhwaair": Ni Surah zilizofanana katika maana. Ni kama zile ambazo zote zina nasaha, maamrisho au visa.

[2] Mufasswal, hizi zimekubalika kuwa zinazomalizia Qur-aan mwisho, na mwanzo wake ni Surat Qaaf (Namba 50) kwa rai iliyo sahihi zaidi.

[3] Al-Bukhaary na Muslim.

[4] Namba ya mwanzo inamaanisha Surah, na ya pili ni idadi ya Aayah za hiyo Surah. Na namba zenye kumaanisha Surah, zimetuwekea wazi kuwa hakuwa

(صلى الله عليه وآله وسلم) akifuata katika kuunganisha baina ya Surah nyingi za An-Nadhwaair utaratibu wa Surah ulivyo katika Msahafu. Hivyo inaonyesha kuwa ni jambo lenye kuruhusiwa. Hali kama hiyo itaonekana katika Swalah ya Usiku, japokuwa ni bora zaidi kufuata mpangilio wa Qur-aan.

[5] Muslim na Atw-Twahaawiy.

[6] Abu Daawuud na al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh. Hadiyth hii ni ya kawaida, hivyo inajumuisha kisomo kwenye Swalah na nje ya Swalah, au Swalah hiyo iwe ni ya Sunnah au ya Faradhi. Ibn Abi Shaybah (2/132/2) amesimulia kutoka kwa Abu Muusa Al-Ash'ariyy na Al-Mughiyrah kwamba wao wawili walikuwa wakisema hivyo katika Swalah ya Faradhi. Na ameipokea kutoka kwa 'Umar na 'Aliy bila ya maelezo hayo.
 
Chemsha Bongo No. 1


Dhunun ni jina lingine la mtume gani?

Mtume gani aliomba dua maarufu-anlaa ilaaha ilaa anta subhanaka in kuntum minadhwalimini

Mtume gani aliomba mtoto kwa Allah,akapewa mtoto anaitwa Yahya


Ni mazingira au hali gani Muislamu atapaswa kutayamamu?

Nabii Mussa alifundishwa elimu ya ghaibu na mja wa Allaha,je anaitwa nani?


Ni mja gani wa Allah alitembea Mashariki na Magharubi ya dunia,kisha akaujenga ukuta ambao Yajuju na Majuju wakashindwa kuukwea?

Ni mitume watatu wamesifika kwa sifa ya Subira,je ni wapo hao?
 
020-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Ruhusa Ya Kusoma Al-Faatihah Pekee


RUHUSA YA KUSOMA AL-FAATIHAH PEKEE




Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) alikuwa akiswali 'Ishaa (ya mwisho) pamoja na Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha akirudi huwaswalisha wenzake. Usiku mmoja, aliporudi aliwaswalisha, na akaswali kijana mmoja katika watu wake [wa Banu Salamah aliyeitwa Sulaym], lakini (Swalah) ilipokuwa ndefu kwa yule kijana, [alijiondokea] na akaswali [pembezoni mwa Msikiti]. Kisha akatoka na kushika ungwe za ngamia wake na akajiondokea. Mu'aadh (رضي الله عنه) Alipomaliza kuswali alielezwa yaliyotokea, akasema: "Bila shaka ana baadhi ya unafiki! Nitamweleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya". Na yule kijana naye akasema: "Nami nitamweleza Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyofanya". Kulipopambazuka, walikuja kwa Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi Mu'aadh akamweleza yale aliyoyafanya yule kijana. Kijana akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Yeye hukaa na wewe muda mrefu, kisha anarudi na kuturefushia". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Je, wewe ni mfitini ewe Mu'aadh?!)). Na akasema kumwambia yule kijana([1]): ((Vipi unafanya unaposwali ewe mtoto wa ndugu yangu?)) Akamjibu: "Nasoma Kifungulio cha Kitabu, kisha namuomba Allaah Pepo, na najikinga Kwake kutokana na moto. Na hakika mimi sielewi dandanah([2]) yako wala dandanah ya Mu'aadh!" Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: ((Hakika Mimi na Mu'aadh tuko katika hayo hayo mambo mawili, au mfano wake)). Msimulizi alisema: "Yule Kijana akasema: "Lakini Mu'aadh ataelewa watakapokuja watu wakapewa habari kwamba adui wamefika". Msimulizi akasema: "(Hivyo) Adui wakaja na yule kijana akafa shahidi. Baada ya hapo, Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema kumwambia Mu'aadh: ((Amefanya nini yule aliyejadiliana nami na wewe?)). Akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Amemsadikisha Allaah, nami sikuwa mkweli, amekufa shahidi".([3])







[1] Asili ni 'Yule Kijana".

[2] "Dandanah" ni mtu anaposema maneno kwa madaha na kusikiwa mvumo wa maneno yake lakini hayafahamiki. Ni karibu kidogo na kunong'ona. (An-Nihaayah)

[3] Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake (1634) na Al-Bayhaqiy kwa isnaad Swahiyh. Na pahala penye ushahidi kutokana na Hadiyth pako katika Abu Daawuud (Namba 758, Swahiyh Abu Daawuud) na asili ya kisa chenyewe kipo katika as-Swahiyhayn (Al-Bukhaary na Muslim). Nyongeza ya mwanzoni iko katika usimulizi wa Muslim. Ya pili iko katika Ahmad (5/74), na ya tatu na ya nne katika Al-Bukhaary. Pia mlango wa hizi, ni Hadiyth iliyotolewa na Ibn 'Abbaas kwamba Mjumbe wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Rakaa mbili ambazo hakusoma ndani yake isipokuwa Kifungulio cha Kitabu (Al-Faatihah) pekee". Imesimuliwa na Ahmad (1/282), Al-Haarith bin Abi Usaamah katika musnad yake (Uk. 38 kutoka zawaaiyd yake) na Al-Bayhaqiy (2/62) kwa isnaad dhwa'iyf. Nilikuwa nimesema kuwa Hadiyth hii ni nzuri katika chapa zilizopita, kisha ikanibainikia kuwa nilikuwa nimekwenda kombo, kwa sababu Hadiyth yenyewe inazunguka kwa Handhwalah Ad-Dawsiy ambaye anaeleweka kuwa ni dhaifu, na sielewi kwa nini sikuweza kugundua hili?! Huenda nilifikiri kuwa ni mtu mwengine. Hata hivyo, Sifa zote ni Zake Allaah Aliyeniongoza kuweza kufikia kutambua kosa langu, na ndio maana nikakimbilia kuisahihisha katika chapa. Kisha Allaah Akanisawazisha kwa kuniruzuku Hadiyth hii bora ya Mu'aadh ambayo inahusisha yaliyoashiriwa katika Hadiyth ya Ibn 'Abbaas. Sifa zote ni Zake Allaah Ambaye kwa Neema Zake yanatimia mema.
 
021-Sifa Ya Swalah Ya Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam): Kunyanyua Sauti Na Kusoma Kimya Katika Swalah Tano Na Swalah Nyinginezo



KUNYANYUA SAUTI NA KUSOMA (KISOMO CHA) KIMYA KIMYA KATIKA SWALAH TANO NA NYINGINEZO




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Asubuhi na katika Rakaa mbili za mwanzo za Swalah ya Magharibi na 'Ishaa, na akisoma kimya kimya katika Swalah za Adhuhuri, Alasiri na Rakaa ya tatu ya Swalah ya Magharibi na Rakaa mbili za mwisho za Swalah ya 'Ishaa.([1])




Walikuwa wakiweza kuelewa kuwa anasoma kimya kimya kutokana na mtikisiko wa ndevu zake([2]) na kwa kuwasikilizisha Aayah mara nyingine([3]).




Pia alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akitoa sauti katika Swalah ya Ijumaa na Swalah za 'Iyd mbili([4]), na Swalah ya kuomba mvua([5]), na Swalah ya kupatwa([6]) jua au mwezi.










KUNYANYUA SAUTI NA KUSOMA KIMYA KATIKA SWALAH YA USIKU([7])




Ama katika Swalah ya usiku, mara nyingine alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisoma kimya kimya na mara nyingine kwa sauti([8]), na alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) anaposoma hali ya kuwa yuko nyumbani kwake, humsikia kisomo chake aliyeko barazani mwake([9]).




Huenda mara moja moja akapandisha sauti yake zaidi ya hivyo hadi akaisikia aliyelala([10]). (Yaani nje ya baraza/uwa).




Na hivyo ndivyo alivyowaamrisha Abu Bakr na 'Umar (رضي الله عنهم) wakati alipokuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) ametoka nje usiku mmoja akatahamaki kumuona Abu Bakr (رضي الله عنه) anaswali huku akiishusha sauti yake chini. Na akampitia ‘Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) aliyekuwa akiswali kwa kunyanyua sauti yake juu. (Baadaye,) walipokutana pamoja kwa Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم). Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: ((Ewe Abu Bakr! Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kushusha sauti yako)). Akasema: "Nimemsikilizisha niliyekuwa nanong’ona Naye ewe Mjumbe wa Allaah". Akamwambia 'Umar: ((Nilikupitia na hali ukiwa unaswali kwa kupaza sauti yako)). Akasema: "Ewe Mjumbe wa Allaah! Nilikuwa naondosha usingizi na namkimbiza Shaytwaan". Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ewe Abu Bakr! Pandisha sauti yako kidogo. Na akasema kumwambia 'Umar: ((Ewe 'Umar! punguza sauti yako kidogo))([11]).




Alikuwa (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Mwenye kusoma Qur-aan kwa kunyanyua sauti, ni kama mfano wa mwenye kutoa sadaka kwa kuonekana na watu, na mwenye kusoma Qur-aan kimya kimya kwa kushusha sauti yake, ni kama mwenye kutoa sadaka kwa siri))([12]).







[1] Katika hili kuna Ijmaa ya Waislamu iliyopokewa na Khalaf kutoka kwa Salaf pamoja na Hadiyth Swahiyh ambazo zinathibitisha hayo kama alivyosema An-Nawawiy. Na zitafuatia baadhi yake. Tazama pia Al-Irwaa (345).

[2] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[3] Al-Bukhaariy na Muslim.

[4] Tazama kisomo (sehemu ya TILAAWAH) chake (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Swalah ya Ijumaa na Swalah za 'Iyd mbili.

[5] Al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[6] Al-Bukhaariy na Muslim.

[7] 'Abdul-Haqq alisema katika Tahajjud (90/1):

"Ama Swalah za Sunnah za mchana, hakikusihi chochote Swahiyh kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) chenye kuonyesha (kuhusu) kuswali kimya au kwa sauti katika Swalah hizo, Na kinachoelekea (inavyoelekea) zaidi ni kwamba alikuwa akisoma kimya kimya katika hizo Swalah. Imeripotiwa kutoka kwake (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba mara moja (wakati wa mchana,) alimpitia 'Abdullaah Ibn Hudhaafa ambaye alikuwa akiswali mchana na kusoma kwa sauti, akamwambia: Ewe 'Abdullaah, Amesikia (mwache) Allaah (Asikie), na wala usitusikilizishe (sio) sisi)). Lakini Hadiyth hii haina nguvu"

[8] Muslim na Al-Bukhaariy katika Af'aal Al-'Ibaad.

[9] Abu Daawuud na At-Tirmidhiy katika Shamaail ikiwa na isnaad nzuri. Hadiyth ina maana kwamba yeye (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa yu katikati baina ya ukimya na kupaza sauti.

[10] An-Nasaaiy na At-Tirmidhiy katika Shamaail na Al-Bayhaqiy katika Dalaail ikiwa na isnaad nzuri.

[11] Abu Daawuud na Al-Haakim ambaye amesema kuwa ni Swahiyh na Adh-Dhahabiy amekubaliana naye.

[12] Kifungu kile kile kilichotajwa hapo mbeleni.
 
Maswali na Majibu




Maswali: Zinaa-Liwati
SWALI:



Assalam wallakum, nina swali linanikosesha raha. Sijawahi kuolewa, nimezaa. Baba mtoto anataka kunioa kwani kumekiri makosa. Je inawezekana?



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu kutaka kuolewa na mwanamme aliyekuzalisha bila ya ndoa.

Kwanza, tunataka kukujulisha kuwa swali kama hili limeshaulizwa mara nyingi na majibu yapo tele ndani ya Alhidaaya; ulikuwa unatakiwa kutafuta kwanza kabla ya kuuliza na kupoteza muda wako wa kusubiri muda mrefu hadi zamu yako ya kujibiwa ifike na pia kutupa sisi kazi ya kujibu maswali yanayofanana ambayo tayari majibu yapo kwenye tovuti.



Pili, kabla ya kukujibu kuhusu kuwezekana kuolewa na mwanamme huyo ni kukufahamisha kuwa kitendo ulichofanya ni katika madhambi makubwa. Kwa hiyo, inatakiwa nyote wawili muombe msamaha kutoka kwa Allaah Aliyetukuka kwa kutimiza masharti yafuatayo:



1. Kujiondoa katika maasiya.

2. Kujuta kufanya maasiya hayo.

3. Kuweka azma ya nguvu kuwa hutarudia tena kosa hilo.



Baada ya nyinyi kuomba msamaha kwa kutimiza masharti hayo na kupita kipindi ambacho kitaonyesha na kudhihirisha manadiliko kwenu ya kitabia ba naadili, basi mnaweza kuoana kwa sharti kuwa yule mtoto hatoitwa kwa ubini wa mume wako ambaye kibayolojia ni baba yake lakini kishari’ah si baba yake. Mtoto huyo hataweza kumrithi baba huyo wala baba kumrithi mtoto huyo.

Kwa muhtasari ni kuwa hakuna makatazo ya nyinyi kuweza kuoana.

Ingia katika viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu suala hilo:

Ndoa Ya Waliozini Kwa Mtazamo Wa Ahlus Sunnah Wal Jama'ah

Ndoa Ya Wazinifu




Ndoa Baada Ya Kutubu Zinaa




Watoto Baada Ya Ndoa Ya Uzinifu




Wazinifu Waliotubu Wanaweza Kufunga Ndoa Na Waliotakasika




Ndoa Ya Waliofanya Zinaa




Nini Hukmu Ya Watoto Wa Nje Ya Ndoa?




Ndoa Inafaa Baada Ya Kumchezea Mwanamke?




Avunje Ndoa kwa sababu Walizini Kabla ya Ndoa?




Wamezini Kisha Wakaoana Bila Kufanya Tawbah Kwa Kuwa Walikuwa Hawajui, Nini Hukmu Ya Ndoa Yao?





Avunje Ndoa kwa sababu Walizini Kabla ya Ndoa?






Na Allaah Anajua zaidi
 
Mume Hapendi Kustarehe Na Mimi: Nyongeza Katika Majibu ya Swali La Kwanza
Maswali: Maingiliano



Mume Wangu Hapendi Kustarehe Na Mimi: Nyongeza Katika Majibu ya Swali La Kwanza



Alhidaaya.com







SWALI:



Assalamu alykum.



Nimefurahi sana kwa jawabu zenu tatizo hili limeanza zamani tangu bada ya kuoana.



Mume Hapendi Kustarehe Na Mimi Anastarehe Nje Na Wanawake Nje





1)tatizo hilo tangu baada ya kuaona

2)ndio tumepata watoto lkn kwakudra ya Allah Mwenyewe

3) tumeoana kijamaa

4) yeye mwenyewe ndio alonitaka na mwenyewe nimemkubali.

5) hatukuwahi kupendana kimapenzi wala kukatana kimapenzi.

6) tokea awali ndio hivi hivi.

7) naishi mm na mume wangu tu lkn namshukuru Allah katupa watoto pia mume wangu hali miraa wala hatizami film za ngono pia sikuwahi kumuona na habri hizo za kujichua. na hao wanawake sina uhakika kama anfanya nao wla vipi lkn nishawahi kuona msg number za cmna pia kachat na mwanamke na kumstarehesha kwa maneno kwa hiyo mm In Shaa Allaah nimo kusubiri na ntasubiri lkn nimechoka kifkra sijui kakusudia nini ikiwa mm hawezi kustarehe na mimi lkn huku anpenda wanawake.





JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani kwa dada yetu kwa nyongeza hizo. Lakini ibara nyingine zimekatwa katwa au hazieleweki ili kuweza kutoa nasaha za kina na za kutosheleza.

Hata hivyo, sisi hapa tunasema yafuatayo baada ya maelezo hayo:





1-Ikiwa tatizo hilo lilikuwa kuanzia muoane inaonyesha ana tatizo. Kwa hiyo, ni vyema uzungumze naye mumeo, kijamaa na kama mke wake ili muweze kwenda kuonana na daktari aliyebobea katika magonjwa ya kiume. Kwa kufanya hivyo, inawezekana ikapatikana dawa ya kuweza kumsaidia kuweza kustarehe nawe.





2-Huenda ikawa amesikia sifa zako au kwa sababu ya ujamaa alipendekewa akuoe kupitia kwa mzazi wake lakini yeye hakuwa na mapenzi nawe. Kwa kuwaridhisha wazazi wake alifanya hivyo ndivyo hahisi kabisa kustarehe nawe.





3-Inawezekana kuwa kwa kuwasiliana na mwanamke au wanawake wengine akawa anaona aoe mwingine au anaona kwa kufanya hivyo utataka talaka ili isionekane yeye ndio hakutaki. Kwa hiyo, akapata fursa ya kumuoa amtakae kwa ridhaa yake bila kuelekezwa na mtu mwingine.





4-Tatizo kama hilo huwa bila shaka linashosha kifikra, kiakili, kifiziolojia na ikiwa shida hiyo haitatatuliwa mapema huenda ikakufishika sehemu mbaya sana.





Kwa tatizo lilivyo tunaona unaweza kufanya yafuatayo:





a-Ukae na mumeo kama wanandoa na mzungumze kiutu uzima hilo tatizo kwa uwazi na bila kuficha. Ikiwa kila mmoja atakuwa wazi kwa mwenziwe huenda suluhisho ikapatikana kwa usahali kabisa





b-Ikiwa hatua hiyo ya kwanza haikuzaa natija yoyote, bila shaka itakuwa muhimu sana kwa wazazi wa kila upande waje katika mkutano wa kutaka upatanishi na tatizo hilo sugu baina yenu. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi kuwa lau kila upande utakuja katika kikao hicho kwa niyya nzuri, ikhlaasw na kutaka upatano basi suluhisho la kudumu litapatikana. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِّنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِّنْ أَهْلِهَا إِن يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّـهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرًا ﴿٣٥﴾

Na mkikhofu mafarikiano baina yao wawili, basi pelekeni mwamuzi kutoka watu wa mume na mwamuzi kutoka watu mke. Wakitaka sulhu Allaah Atawawafikisha baina yao. Hakika Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [An-Nisaa: 35]



Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa suluhu Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah kwa yale myatendayo ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika [An-Nisaa: 128]





c-Ikiwa hakuna suluhisho lolote basi itabidi mutengane na jambo hilo litakuwa bora kwa kila mmoja. Kufanya hivyo, itampatia fursa kila mmoja kuweza kupata mwendani mwengine ambaye ataweza kuridhiana naye kwa kiasi kikubwa zaidi. Hili litafanyika tu ikiwa njia nyingine hazikufaulu.





Tunakuombea Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akuwafikie na kukuondolea tatizo hilo kwa wakati muafaka kabisa.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Maswali: Zinaa-Liwati





SWALI



(Nimeona nakala ilitumwa katika moja ya sites za Kiswahili

muandikaji katika kujibu nakala za mwengine alitoa hoja kuwa,
Mtume SAW alipokuja kuwaleta watu katika haki na kuacha machafu, hajawaamrisha wale walioowana kabla ya Uislam waowane kwa mara ya pili, na pia aliuliza kama kuna hadithi au Aya ambayo jambo kama hili lilitokezea wakati wa Mtume SAW nae Mtume akawaambia watu wavunje ndoa yao kwasababu walizini kabla ya hapo, na hoja nyingi alizitoa muandikaji kwa

kusema jee kwa wakati wa leo watu kama watasilimu hali ya wao walioana kabla jee waozeshwe tena? na alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa katika Aya MZINIFU HAOI ISIPOKUWA KWA MZINIFU MWENZIWE NA HILO NI HARAMU, alisema hii inaonyesha kuwa kama mtu alikuwa mzinifu asipewe mtoto alikuwa msafi (asiekuwa mzinifu) kumuoa, na wala wale wasiozini
wanaume wasioe wazinifu wanawake, sasa hapa tunaomba tuwekwe sawa maana katika hiyo hiyo Aya inaishia kusema na jambo hilo ni haramu. Sasa hawa watu kama wameamua kutubia na kurudi kwa Mola wao kihaki lilah na wakaoana patakua uharamu wowote? Tafadhali msione dhiki kujibu masuali yetu ndio kutaka kujua kwa usahihi. Na naomba Mnapotujibu katika
maelezo mengi na mkiishia muweke japo mstaari mmoja kuwa hili jambo ni linafaa au halifai kisheria.





JIBU:

Kwa mafunzo sahihi kwa mujibu wa itikadi ya Salafus Swaalih (wema waliopita) ambayo ndio Itikadi ya Ahlus Sunnah wal Jama'ah, wanamzingatia mwenye kufanya madhambi makubwa kama ni mwasi au fasiki. Na vile vile wenye kufa hali ya kuwa anatenda madhambi makubwa, basi mtu huyo yupo katika mapendeleo ya Mwenyeezi Mungu. Akitaka Atamsamehe kwa ukarimu Wake na Akitaka Atamwadhibu kwa uadilifu Wake mpaka atakasike na makosa ya uasi wake kisha atahamia peponi. Ama itikadi ya wengine kama Makhaawarij, wao humwiita mwenye kufanya madhambi makubwa kafiri wakidai kwamba huu ni ukafiri wa neema au ukafiri wa unafiki, si ukafiri wa dini, na pia wanasema kwamba mwenye kufanya maasia, basi huyo ni mtu wa motoni milele.



Kwa hiyo Muislamu aliyetubu kikweli kutokana na kitendo cha zinaa, akafuata shuruti za Tawbah ikawa Tawbatun-Nasuuha na akazidisha na kuendelea kufanya vitendo vyema badili yake, basi alama ya zinaa huondoka, yaani haitwi tena mzinifu, bali husamehewa kama yule aliyefanya matendo ya shirki, kuua ambayo ni maasi yenye madhambi makubwa kama ilivyo zinaa. Mwenyeezi Mungu Anasema:

}}وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ وَمَن يَفْعَلْ ذَلِكَ يَلْقَ أَثَامًا{{



}}يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا{{



}}إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُوْلَئِكَ يُبَدِّلُ اللَّهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا{{

{{ Wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye fanya hayo atapata madhara}}

{{azidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka}}

{{Isipokuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}}

Al-Furqaan: 68-70

Hadithi hii hapa chini pia inathibitisha kusamehewa huko kwa vitendo kama hivyo:

((عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ نَاسًا مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا ، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَقَالُوا : إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ ، لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً ، فَنَزَلت:



}}والذينَ لا يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلا بِالْحَقِّ وَلا يَزْنُونَ {{ وَنَزَلَتْ : }} قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ{{ ))


روى البخاري (4436) ومسلم (174)




((Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye kasema; baadhi ya watu Mushrikiin ambao waliua sana na kutenda zinaa kwa wingi walikuja kwa Mtume صلى

الله عليه وآله وسلم na kumwambia; Unayotuitia (katika Uislamu) ni mazuri, lakini tujulishe tu kama kuna kafara ya yale maovu tuliyoyafanya; hapo zikateremshwa aya hizi:

{{Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini} Al-Furqaan: 68

Na ikateremka:

{{Sema: Enyi waja wangu walio jidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zote. Hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu}})) Az-Zumar: 53 (Al-Bukhari na Muslim)

Kisha baada ya kutubu anatakiwa Muislamu ajistiri kwa kuficha siri yake ya mambo aliyofanya maovu kabla, na sio kujifehedhesha kwa kuyatangaza maovu hayo na kujisifu nayo, kama livyotuambia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika hadithi hii :

(( اجتنبوا هذه القاذورة التي نهى الله عز وجل عنها ، فمن ألم فليستتر بستر الله عزوجل)) رواه البيهقي وصححه الألباني في السلسلة الصحيحة 663



((Jiepusheni na uchafu huu alioukataa Allaah عزوجل, na atakaye tenda dhambi ya aina hiyo, basi ajisitiri kwa stara ya Allaah ((عزوجل

[Al-Bayhaaqiy na Amesahihisha Saykh Al-Albaaniy katika Silsilatus Swahiyhah: 663.]



Kwa hivyo suali lako kuhusu Aaya katika Suratun-Nuur

}}الزَّانِي لَا يَنكِحُ إلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ{{

{{Mwanamume mzinifu hamwoi ila mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina. Na mwanamke mzinifu haolewi ila na mwanamume mzinifu au mshirikina. Na hayo yameharimishwa kwa Waumini.}} An Nuur:3

inakusudiwa wale ambao bado wanaendelea katika katika kitendo hicho cha zinaa. Ama waliotubu kikweli wanaweza kuoa na kuolewa na waliotakasika.

Kama ulivyotaka tujibu kwa kifupi mwisho, ni kwamba "Baada ya kutubia Tawbah ya kweli ndoa itasihi na inafaa ndoa na waliotakasika"




Wa Allaahu A'alam
 
Maswali na Majibu



Maswali: Zinaa-Liwati


SWALI:



masheikh wangu mimi nnasuala langu ambalo linanitia wasiwasi. kwa ufupi niliposa mwanamke na nilimtolea mahari wakati tunasubiri kufunga ndoa, tulifanya maskosa ya zinaa (tulizini), lakini kabla ya kufunga ndoa kama mwezi au zaidi hatukufanya kitendo hicho, huyo mwanamke alikuwa mbali na mimi. baadae siku ile iliyopangwa tukafunga ndoa na sasa ni muda wa miaka mingi.

Suala langu jee hii ndoa ni halali? Kwani nimeona kwenye website yenu (alhidaaya ) kuwa lazima mnatakiwa mjute kwanza kabla ya kuowana. mimi nilokuwa nnajuwa kuwa kama mmezini basi mnaweza kuowa (na ndivyo nilivyo fanya).

jee kujuta huko ni vipi? Maana mimi nilikuwa siyajuwi hayo, nnachojuwa kuwa tulikuwa na nia ya kuowana, basi tumetimiza ile ahadi yetu, japokuwa tulifanya makosa (inshaalah ALLAAH atatusamehe), tulifanya haramu na kuigeuza iwe katika uhalali.

Wasiwasi wangu nini nifanye? Kwani naogopa kuwa bado nimo katika zinaa hata ibada zangu zikawa hazikubaliki na pia tumebahatika kupata mtoto hivi karibuni tuu, jee mtoto huyu ni wa halali au laa. Ningependelea kupata jawabu kwenu ili nijuwe nini nnafanya.

Sina cha kukulipeni lakini ALLAAH ndie atakupeni funguleni kwa kutusaidia sisi kutatuwa matatizo yetu. Ameen

Wasaalamu alykum







JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Tunashukuru kwa swali lako na kutaka kwako kupata ufumbuzi wa masuala hayo mazito. Ni ajabu kuwa mwanadamu katika maumbile yake ya papatiko anakuwa ni mwenye kujiingiza katika maangamivu. Ni ajabu kuona mtu anazini na mchumba wake na hali anajua atamuoa na hivyo inasikitisha kuona mwanaadam alivyo na uchu wa maasi na kukosa subira kwa jambo ambalo baada ya muda mfupi litakuwa halali kwake kishari'ah.



Na yaliyotokea ni natija ya Muislamu kukosa subira ambayo tumehimizwa sana tuwe nayo.




Tawbah ni lazima kwa kila dhambi analofanya Muislamu, naye Allaah Aliyetukuka Amechukua dhamana ya kusamehe madhambi yote kama tunavyokuta katika Aayah mbalimbali za Qur-aan.




Ama masharti ya tawbah ni haya yafuatayo:

1. Kujiondoa katika maasiya.

2. Kujuta kwa kufanya maasiya.

3. Kuazimia kutorudia tena katika hayo maasiya.


Yaonyesha kutoka katika maelezo yako kuwa mlitengana na mchumba wako au mlijiondoa katika maasi baada ya matendo hayo ya zinaa, ikiwa kutengana huko ni kwa Niyah ya kutubu kutokana na matendo hayo, basi ulishatimiza sharti moja. Sharti ambalo limebakia ni kujuta kwenu na kwa sababu hukuwa na elimu juu ya hilo Allaah Aliyetukuka Anasamehe kwa madhambi yaliyofanywa katika hali ya ujinga. Anasema Aliyetukuka:

“Hakika tawbah inayokubaliwa na Allaah ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Allaah Huwakubalia tawbah yao, na Allaah ni Mjuzi na ni Mwenye hikima” (4: 17).




Kwa kuwa sasa umejua uwajibu wa jambo hilo inafaa ujute sana ndani ya moyo kwa kufanya matendo hayo machafu huko nyuma, na kisha jitahidi sana utende yaliyo mema pamoja na kuleta istighfaar kwa wingi.



Ikiwa ndoa yenyewe baada ya zinaa ilitekeleza masharti ya ndoa kama ifuatavyo ndoa yenyewe itakuwa ni sawa:

1. Kukubali kwa msichana anayeolewa.

2. Bwana harusi kukubali kwa ndoa hiyo.

3. Bibi harusi kupewa mahari yake.

4. Kuwepo kwa mashahidi wawili waadilifu.

5. Kuwepo na kupatikana idhini ya walii.




Endelea kuomba msamaha na kufanya mema wala usitie wasiwasi kwa yaliyopita yafaa kwa sasa uganje yajayo. Uhalali wa mtoto inategemea je, mimba yenyewe iliingia kabla ya kumuoa baada ya kitendo cha zinaa au baada yake. Ikiwa iliingia kabla basi mtoto hatokuwa wako kishari'ah, na hatoweza kukurithi wala wewe kumrithi lakini ikiwa mimba ilipatikana baada ya Nikaah ya halali, basi mtoto huyo atakuwa wa halali.




Na ikiwa mlikuwa tu mumeacha maasi yale kwa muda kwa ajili ya kusubiri kuoana bila ya Niyah wala maazimio ya kutubia na kujutia yale makosa mliyoyafanya, basi Maulamaa wanaonelea ikiwa mko ndani ya ndoa yenu hivi sasa, ni bora na kwa usalama zaidi kufanya ndoa mpya ambayo atakuwepo walii na mashahidi wawili. Vilevile wanaonelea kuwa ikiwa mtu atashindwa kabisa kueleza sababu ya hiyo ndoa mpya kwa watu na hao wahusika wa kuisimamia ndoa hiyo kwa kuogopa madhara zaidi na mengineyo yanayoweza kuleta matatizo, basi wanaweza kuendelea na ndoa yao na huku wakizidisha sana istighfaar na kutenda mambo mema kwa wingi.


Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atusamehe sote katika madhambi tuliyoyafanya kwa kujua au kutojua.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Naam elimu kubwa inapatikana,kwa wale walio fanya makosa basi mjirekebishe ama kuoana tena akiwemo walii na mashahidi wawili au mkiona mtaleta sintofahamu kwa mujibu wa Maulamaa basi mfanye istighfar kwa wingi na mzidishe mema

Haya kwa wale ambao mmo kwenye janga la zinaa,muache,mtubie na mfunge ndoa

Tumche Allah
 
Maswali: Zinaa-Liwati


SWALI:

NINA SWALI MAWILI ,

1.ISLAM INASEMA NINI KWA WATOTO WA KUZALIWA INJE YA NDOWA? NASEMA KWA UZINIFU (OUTSIDE OF MARIAGE BEFORE AND AFTER)









JIBU







Sifa zote njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Ahli zake, Sahaba zake (Radhiya Allaahu ‘Anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Katika Uislamu kitendo hicho cha zinaa ambacho kimefanywa na mwanaume na mwanamke ndio makosa na waliofanya wanafaa waadhibiwe hapa duniani ili wasafishwe kwa kosa lao hilo hadharani. Na Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Ametuagizia Tusikaribie kabisa zinaa (17: 32). Lakini tufahamu ya kwamba yule mtoto anayezaliwa hana hatia yoyote. Allah (Subhaanahu Wa Ta’ala) Anasema:

“Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Naye Atakuambieni mliyo kuwa mkitofautiana” (6: 164).

Na Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) amesema: ((Kila kinachozaliwa kinazaliwa katika Uislamu .....)) l-Bukhaariy).

Na haifai kwa Muislamu kumuita mtoto aliyezaliwa kwa jina la mwana-haramu kwa sababu mtoto mwenyewe si wa haramu bali kitendo chenyewe ndicho haramu. Na ieleweke kuwa mtoto huyu hataitwa kwa jina la huyu mwanaume aliyezini na mamake kwa sababu kisheria si mtoto wake wala hawa wawili hawarithiani kabisa. Mtoto huyu hatamrithi huyo mwanaume na huyo baba hatamrithi mtoto huyo. Lakini mtoto anaweza kumrithi mama yake na mama kumrithi mtoto wake.



Tanbihi kwa kila mmoja wetu ajichunge sana ili asiingie katika madhambi haya ya zinaa. Na ndio sheria ikafanya ndoa kuwa rahisi na ikaweka adhabu kali kwa wenye kuzini.



Na Allaah Anajua zaidi.
 
Kuna kipindi zilitokea nyuzi hapa jukwaani hasa kwa wasio waislamu,na kutoa mapovu mtoto hana kosa kwanini anaadhibiwa?

Hapa mtoto hana makosa,ila mzazi ndio anaadhibiwa kwa kosa kuzaa nje ya ndoa,just imagine mtoto ni wako kibailogia lkn humpi jina la ubini wako,hakika ni moja ya adhabu kubwa

Umenyang'anywa haki ya kurithiana na mwanao,hiyo ni adhabu pia

Haya yamefanywa ili jamii isifanye makosa haya,kwahiyo ambao hamjaingia kwenye haya makosa muwe makini sana

Na kingine masikini kama baba ana mtoto wa kike wa nje ya ndoa anashindwa kumuozesha huu nao ni mtihani mwingine

........................

Kuna ndugu yangu mmoja naye alizaa nje baadae akamuoa huyo mwanamke,nikampa somo,akaniambia sasa bro si nimeshamuoa huyo.mwanamke na mtoto nimempa jina langu,je kuna ubaya?

Nikamwambia kinachoangaliwa je,mtoto alipatika kipindi gani? Kama nje ya ndoa,basi ndoa haifanyi kosa kuwa jambo sahihi,bado mtoto atakuwa ni wa nje ya ndoa


Ndio maana ni muhimu sana kupenda kusoma soma ili tujue mambo ya msingi ambayo yanatuathiri katika maisha yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…