USIDHARAU JAMBO LOLOTE LA KHERI HATA KAMA NI DOGO KIASI GANI

Mtume swalla llahu alaih wassallam anasema usidharau jambo lolote la kheri hata ikiwa kumsalimia ndugu yako kwa tabasamu au kwa uso wa bashasha

Kwawaida tabasamu unaweza kulichukulia poa lkn mbele ya Allah linathawabu yake na litachangia kujazia mizani yako

Kutoa salamu iwe assalaam alalkum au salamu yoyote ile basi unapata thawabu kwa Allah,kwani salamu ni sababu ya kupendana, Mtume alisema je,niwaambie jambo ambalo mkilifanya mtapendana? Akasema toleaneni salamu au msalimiane

Ni hii ni kweli ,hata katika jamii yetu kama kuna ambaye huwa hapendi kusalimia watu hakika hawata mpenda lkn yule ambaye huwa anatoa salamu kwa watu hakika watampenda,basi usidharau hakika ni sehemu ya machumo yako

Ukiona udhia njiani,labda kuna miba au kuna jiti linawafanya watu wapite kwa shida,liondoe ni katika mambo mema ya kuyafanya na unapata thawabu

Ili mradi hakikisha hauchi jambo lolote la kheri ili upate ujira wako mbele ya Allah

Hakika kuna kheri nyingi ambazo zitatunufainisha ikiwa hatuta dharau jambo lolote la kheri

Tumche Allah
 
IBADA ZA ALLAH HAZINA UWAKILISHI KAMA WABUNGE

Ndugu zangu katika imani leo hii katika familia zetu tunafanya ibada za Allah kwa kuwakilishana kana kwamba ni wabunge wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Maana wabunge wanajulikana,tumewachagua baadhi yao kwenda kupigania maslahi yetu

Sasa katika familia zetu pia tumemteua ama ni baba au mama au mwanafamilia mmoja wapo kufanya ibada za Allah kwa niaba yetu,huu ni msiba mkubwa

Utakuta katika familia labda ni baba tu ndio anaswali,lkn mke na watoto wote hawa swali kabisa,au unakuta mke ana swali lkn baba na watoto hawana habari ya swala,au mtoto anaswali huku wazazi hawana habar na swala kabisa

Ndugu zangu katika ibada za Allah hakuna kuwakilishana,kila mtu ana wajibu mkubwa wa kufanya ibada kwa ajili ya nafsi yake,kwahiyo hatuna budi kuziokoa nafsi zetu zidi ya moto

Anasema Allah mtukufu:

66:6 - Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa anayo waamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa.

Hapa tunaona Allah anatoa tahadhari kwamba tujilinde na adhabu yake dhidi ya moto wa jahannamu,anasema tuhamasishe familia zetu na ndugu kufanya ibada ili kuepukana na moto

Na hapa baba wa familia una jukumu kubwa sana la kuhakikisha familia ina ifanya ibada,kwani Allah anasema "WANAUME NI WASIMAMIZI WA WANAWAKE"

Huyo mkeo ambae unamuonea aibu kumhamasisha katika kufanya ibada ya Allah,siku ya kiama atakuwa wa kwanza kukushika shati mbele ya Allah, atasema " ewe Allah hakika huyu mume wangu hakuniamasisha mimi au kunikazania mimi nifany ibada"

Naam wewe ni kiongozi wa familia hivyo hautakwepa lawama,kikubwa hamasisha sana na kumbusha sana ili wakikataa basi utakuwa na hoja juu yao,kwamba ulikumbusha lkn hawakukusikiliza

Pamoja na Nuhu kuwa Mtume na kipenzi cha Allah lkn mwanae aliangamia na gharika la maji, Nuhu alimwombea mwanae msamaha lkn Allah akamwambia yeye hakuwa mwanae kwakuwa hakuwa miongoni mwa watu wema

Ibrahim pamoja na kuwa kipenzi cha Allah lakini baba yake aliangamia kwa kuendelea kuwa mshirikina

Mke wa nabii Luti aliangamia kule sodoma na gomora kwakuwa alikuwa akishirikiana na watu wenye tabia chafu


Kwahiyo hapa tunapata picha hauta pata nafasi ya kuokoka na adhabu ya Allah eti kwakuwa wewe ni mtoto wa Nabii au Mtume,au labda ni mtoto wa Sheikhe fulani mkubwa,au kwakuwa mumeo ni mchamungu au mkeo ni mcha mungu eti utapona kwa ucha mungu wake,hapana kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe

Ndugu zangu maisha ya hii dunia ni mafupi mno kuliko maisha ambayo yapo mbele yetu,je tuna jiandaa vipi kukabiliana na maisha hayo?

Tumche Allah
 
Majirani eti Sikukuu ya Idd inaweza kuwa lini nipange ratiba zangu...
Wewe jirani naona unapata taabu Sana katika mwezi huu Mtukufu na unaomba kwa udi na uvumba ili uishe haraka upate kuendelea na ratiba zako. Nina wasiwasi kama kweli umefunga yaelekea unashinda njaa tu.
 
TUMIA FAIDA YA MAMBO HAYA MATANO AU MANNE KABLA HAYAJA ONDOKA

Anasema Mtume rehma na amani ziwe juu yake:

Tumia vizur ujana wako kabla ya uzee wako,hakika ujana ndio kipindi kizuri sana kwa kijana kufanya sana ibada kwakuwa katika umri huu ana nguvu za kutosha,hivyo kumwemezesha kupambana na pilika pilika za ibada katika namna nzuri

Lakini bahati mbaya sana ujana ndio tunatumia kutofanya mambo ya ibada tukitarajia uzeeni ndio tufanya ibada za Allah,na tukibahatika kufikia umri huo nguvu za kufanya ibada hatuna tena

Tumia Uzima wako kabla ya maradhi yako,ndugu zangu hakika afya njema ni neema kubwa sana na ukitaka kulijua hilo ebu nenda katambee mahospitalini ndio utajua hakika afya kumbe ni neema kubwa sana,anasema Mtume kuna neema mbili watu wameghafirika nazo, nazo ni afya na faragha

Kuna kipindi huenda tukapata na mtihani wa maradhi na hivyo tukashindwa kufanya baadhi ya ibada kikamilifu,kwahiyo pale tunapokuwa na afya njema basi ebu tushikamanane na ibada

Tumia uhai wako kabla ya kifo chako,Jibril alimwambia Mtume Muhammad swalla llahu alaih wassallam ishi utakavyo ishi lkn tambua ipo siku utakufa na mpende utakaye mpenda lkn ipo siku utatengana nae

Kwahiyo uhai ni neema kubwa sana,ndio wakati wa kuchuma kwa wingi,ndio wakati wa kufanya aamali nyingi zaidi ili zije kutunufaisha huko mbele ya safari,maana tukisha kufa tu basi ujue mlango wa kufanya kheri unakuwa umefungwa isipokuwa kwa yule ambaye ameacha mtoto mwema ambaye atakuja kumuombea dua au akaacha elimu yenye manufaa hapa duniani au akaacha sadaka yenye kuendelea kama kujenga majumba ya ibada,kuchimba visima na mambo mengine ambayo watu watanufaika nayo yeye akiwa hayupo katika mgongo wa ardhi

Tumia wasaa wako kabla hujawa bize sana na kutingwa na shughuli nyingi,endapo una wasaa wa kufanya mambo mengi ya kiibada basi yafanye sana kabla ya kufika kipindi kutokana na shughuli sana ukashindwa kufanya baadhi ya mambo yenye kukupa manufaa kwa mola wako

Tumche Allah
 
Siku Kumi Za Mwisho Za Ramadhwaan

Shaykh Swaalih Ibn Fawzaan Al-Fawzaan

Imetarjumiwa na: Ummu Iyyaad

www.alhidaaya.com







عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ : "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ الْعَشْرُ أَحْيَا اللَّيْلَ وَأَيْقَظَ أَهْلَهُ وَجَدَّ وَشَدَّ الْمِئْزَرَ" رواه البخاري (2024) ومسلم (1174)

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa pindi zilipoinga kumi za mwisho, akikesha usiku na akiamsha ahli zake na akijitahidi na kukaza shuka yake." [Al-Bukhaariy, Muslim]



Hadiyth hii ni uthibitisho kuwa siku kumi za mwisho za Ramadhwaan zina fadhila mahsusi na adhimu kuliko siku nyenginezo ambazo Muislamu inampasa aongeze utiifu na kutekeleza ‘ibaadah kama kuswali, kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na kusoma Qur-aan.



‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amtuelezea hali ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inavyokuwa kama ni mfano bora kabisa kwa sifa nne zifuatazo:



1-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikesha katika ‘ibaadah.



Alikuwa halali usiku. Kwa hiyo yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikesha usiku mzima kufanya ‘ibaadah na akihuisha nafsi yake kwa kutumia usiku wake kukaa macho na kuacha kulala. Hii ni kwa vile kulala usingizi ni mauti madogo. Maana ya "akihuisha (akikesha usiku)" ni kwamba yeye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitumia wakati huo katika hali ya Qiyaam (kusimama kuswali usiku) na kufanya ‘ibaadah ambazo zinatendwa kwa ajili ya Allaah, Rabb wa walimwengu. Inatupasa tukumbuke kuwa siku kumi za mwisho za Ramadhwaan ni chache zilizokadariwa kwa idadi.



Ama kuhusu ilivyonukuliwa katika Hadiyth ya 'Abdullaah Ibn ‘Amr, imekatazwa kukesha usiku mzima katika Swalaah, hii inahusu mtu anayefanya hivyo kwa mfululizo wa siku zote za mwaka.





2-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiamsha ahli zake.



Ni wake zake waliotakasika ambao ni Mama wa Waumini, ili nao wanufaike katika ‘ibaadah hizo za kumdhukuru Allaah na ‘ibaadah nyenginezo katika siku hizo zenye baraka nyingi.





3-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya bidii.



Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijizuia na akijitahidi sana katika ‘ibaadah, akiongeza ‘amali njema zaidi kuliko alivyokuwa akifanya siku ishirini za mwanzo (wa Ramadhwaan). Akifanya hivi kwa sababu Laylatul-Qadr inatokea katika usiku mmoja wa siku hizo kumi.





4-Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikaza shuka yake.



Alikuwa akijihimiza na kufanya bidii kubwa katika ‘ibaadah nzito. Inasemekeana vile vile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akijitenga na wake zake. Hii ni kauli iliyo sahihi zaidi kwa vile inakubaliana na ilivyotajwa kabla katika Hadiyth ya Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akikunja kitanda chake na akijitenga na wake zake" [Latwaaif-ul-Ma'aarif, Uk. 219]



Vile vile Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya I'tikaaf katika siku za mwisho za Ramadhwaan na watu wenye kuwa katika hali ya I'itikaaf hujizuia kujamii na wake zao.



Kwa hiyo enyi ndugu Waislamu, jitahidini kujizoesha na kuwa katika sifa na khulka hizi. Na tekelezeni Swalaah za usiku pamoja na Imaam hata baada ya kuswali Taraawiyh ili jitihada zenu katika siku hizi kumi za mwisho zipindukie siku ishirini za mwanzo na ili mpate kufaulu kupata sifa ya "kuuhuisha usiku kwa ’ibaadah" kwa kuswali.



Na ni lazima muwe na subira katika utiifu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na ‘ibaadah za usiku kwani hakika Tahajjud ni ngumu lakini thawabu zake ni kubwa sana. Naapa kwa Allaah, ni fursa kubwa katika maisha ya Muislamu na vile vile ni faida kubwa kuitumia fursa hii kwa yule aliyejaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwani mwana Aadam hawezi kujua kama ataweza kuchuma tena thawabu nyingi kama hizi, ambazo zitamfaa katika maisha yake ya dunia na ya Aakhirah.



Salafus-Swaalih (Wema waliotangulia) wa Ummah huu walikuwa wakijitahidi katika ‘ibaadah za masiku haya kwa kuzirefusha Swalaah za usiku. As-Swaa'ib bin Yaziyd amesema, "'Umar bin Al-Khattwaab alimuamrisha Ubay bin Ka'ab na Tamiym Ad-Daariy kuimamisha watu katika Swalaah kwa Raka'ah kumi na moja. Imaam alikuwa akisoma Aayah mia moja hadi ilibidi tuegemee mkongojo kwa sababu ya kisimamo kirefu, na tulikuwa hatupumziki hadi inapoanza kuingia Alfajiri". [Al-Muwattwa, Mjalada 1, Uk. 154]



'Abdulllaah Bin Abiy Bakr amesema "Nimemsikia baba yangu akisema, wakati wa Ramadhwaan, tulikuwa tukichelewa kumaliza Swalaah za usiku hata tukiwahimiza watumishi kutuwekea suhuwur (daku) kwa kuogopa Alfajiri isitufikie" [Muwattwa ya Imaam Maalik, Mjalada 1, Ukurasa 156]



Nafsi ya Muumini inapambana na jitihada mbili katika Ramadhwaan; Jitihada ya mchana kwa swiyaam na jitihada ya usiku kwa Qiyaam. Kwa hiyo yeyote atakayejumuisha jitihada mbili hizi na akatimiza haki zake, basi yeye atakuwa miongoni mwa wenye subira kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿١٠﴾

Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]



Siku kumi hizi ni za mwisho katika mwezi mtukufu huu, na ‘amali za Muislamu zinazohesabika zaidi ni zile za mwisho, kwa sababu huenda akafaulu kukutana na usiku wa Laylatul-Qadr wakati akiwa amesimama katika Swalaah ikawa ni fursa nzuri ya kufutiwa madhambi yake yote na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).



Ni wajibu wa kila mtu kuamsha na kuhimiza na kushurutisha familia yake kutekeleza ‘ibaadah khasa nyakati hizi tukufu, kwani hakuna atakayedharau kufanya hivi ila yule aliyenyimwa fadhila hizi. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wakati wengine wako katika ‘ibaadah khasa za masiku haya kumi, wengine wanatumia wakati wao katika vikao vya maasi. Hakika hii ni khasara kubwa.



Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atuhifadhi na Atuhidi.



Kwa hiyo Muislamu atakayejishughulisha na ‘ibaadah katika siku kumi hizi za mwisho atakuwa amejiingiza katika milango ya kuchuma mema yaliyobakia katika mwezi huu mtukufu. Ni khasara kwa mtu aliyeanza mwezi wa Ramadhwaan kusimama kwa nguvu kuswali, kusoma Qur-aan na dhikru-Allaah kisha siku za mwisho akawa na mzito na mvivu katika kufanya ‘ibaadah na hali hizi siku za mwisho ndio siku muhimu na zenye uzito wa thawabu za kusimama kuswali na kadhaalika kuliko zote. Hivyo kila mmoja inampasa aongeze bidii zaidi na kujitahidi kwa kadiri awezavyo kuongeza ‘ibaadah katika kumalizia mwezi mtukufu huu. Na kukumbuka kuwa ‘amali za mtu zinahesabika zile za mwisho.



Du’aa ya Laylatul-Qadr:



Katika siku hizi kumi za mwisho ni vizuri sana kuisoma du'aa hii kila mara khasa katika usiku wa Laylatul-Qadr kama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo:



عَنْ عَائِشَةَ , أَنَّهَا قَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ أَرَأَيْتَ إِنْ وَافَقْتُ لَيْلَةَ الْقَدْرِ مَا أَدْعُو؟ , قَالَ : ((تَقُولِينَ : اللَّهُمَّ إِنَّكَ عَفُوٌّ تُحِبُّ الْعَفْوَ فَاعْفُ عَنِّي)) ابن ماجه و صححه الألباني

Imepekelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) amesema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je nitakapojaaliwa kufikia Laylatul-Qadr niombe nini?" Akasema, ((Sema: Allaahumma Innaka 'Afuwwun Tuhibbul-'Afwa fa'fu 'anniy - Ee Allaah Hakika Wewe Ndiye Mwenye Kusamehe Unapenda Kusamehe basi Nisamehe)) [Ibn Maajah na kaisahihisha
 
ZAKAA TULFITIR

Kwa uchache kabisa ni zaka ambayo hutolewa baada ya kumaliza mfungo wa Ramadhani,na lengo kubwa ni kuitakasa funga ya mja wa Allah,pamoja na kuwa wezesha waislamu wengine wasio jiweza kupata sadaka hii ili nao wapate nafasi ya kuifurahia sikukuu ya eid

Inasemwa katika hadith funga ya mja huwa kati kati ya mbingu na ardhi,na mara baada ya kutolewa zaka hiyo ndio hupelekwa kwa Allah,lkn kwa wewe ambaye ikakukuta mwishoni wa ramadhani na huna cha kutoa basi Allah hakika anajua hali yako naye ni mjuzi wa mambo ya siri na dhahiri na katu Allah hamdhulumu mja wake,ila kama uwezo unao na ukafanya ubakhiri hayo ni makosa makubwa

Wanaotolewa zakaa tulfitir ni watu wote wa nyumbani kwako ambao wako chini ya usimamizi wako kama wewe ni baba,hata kichanga kilichozaliwa siku ya eid unakitolea zakaa tul fitir

Na kipimo ni kibaba cha Mtume swallallahu alaih wassallam ambcho ni sawa na kilo mbili na nusu,kwahiyo kwa kila mtu ndani ya familia yako unamtolea kilo mbili na nusu,utapiga mar idadi ya nyie wote na kutoa jumla yake

Na hutolewa kwa chakula kinacho pendwa zaidi kwa mji huo,mathalani kwa wabongo huwa sikukuu tunapenda zaidi kutumia mchele kwa maana kupika wali au pilau au biriani

Kwahiyo nunua mchele na uwape wenye uhitaji,lkn inashauriwa badala ya kutoa mchele kama mchele unaweza badala yake kutoa fedha ili mhusika mwenyewe ajikadirie mahitaji yake,au ukitoa mchele basi toa na fedha kidogo kwa hesabu ya hiyo zaka yako,maana sawa utampa mchele je atapikia na nini? Atahitaji mkaa,mafuta nakadhalika

Na ni vizur anza kutoa kwa ndugu zako kwanza kama hawana uwezo huo hilo ndio jambo zuri zaidi,sadaka nzur huanzia kwa watu wa karibu,lau kuwa hujui watu wenye uhitahi utawapata wapi,basi nenda msikiti wa karibu kakabidhi zaka yako nao wanawajua wahitaji

Na lau kuwa hukuwa na uwezo wa kutoa zakaa tulfitir lkn ukapokea zakaa ambayo ni kubwa basi nawe waeza pia kuitoa kwa watu wengine,kikubwa uwe na mlo wa kula siku hiyo eid na jioni yake,kisha cha ziada toa nawe zakaa tulfitir,lengo kubwa ni ndugu zetu nao kufurahia siku ya eid

Wallah sita sahau mwaka fulani uchumi ulikuwa mbaya mpaka mwisho wa usiku wa ramadhani sijui kesho ntakula nini sikukuu,mashallah mara pap kwenye simu muamala ukaingia kutoka kwa mdogo wangu na kuleta tabasamu katika familia yangu

Nawe waeza leta tabasamu kwa watu wengine pia nao wakafurahia sikukuu ya eid

Unaweza kuitoa siku tatu kabla ya eid lkn inashauriwa ni vizur zaidi kutoa jioni ya kuamkia sikukuu ya eid au waeza toa asubuhi ya eid lkn kabla ya kuswaliwa swala ya eid,kwani ukitoa baada ya swala ya eid inakuwa sadaka ya kawaida hivyo utakosa fadhila za zakaa tulfitir

Allah atufanyie wepesi kuiendea a'amali hii

Tumche Allah
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…