Ertugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 12,785
- 24,951
Ukumbusho mzuri sanaNdugu zangu katika imani matendo ya kiibada ambayo yanapokelewa na Allah ni yale ambayo yamefanywa tu kwa kutaka radhi zake
Je swaumu yako umeifunga kwa kuwa hapo nyumbani wote wamefunga ndio maana umefunga au umefunga kwa ajili ya Allah?
Je umefunga kwakuwa wafanyakazi wenzako wote wamefunga ndio maana nawe umefunga kwa kukwepa aibu?
Je umefunga kwakuwa mume kafunga nawe umefunga au kwakuwa mke kafunga ndio nawe kwa aibu umefunga?
Ndugu yangu katika imani ikiwa umefunga kwa ajili ya watu au mazingira uliyopo basi tambua hakika unashinda na njaa tu,hutalipwa na Allah
Hakika Allah hukubali tu matendo yanayofanywa kwa ajili yake tu
Takasa nia yako kwa kila ibada iwe ni kutoa sadaka,swala,funga au amali nyingine yoyote ile hakikisha ni kwa ajili ya kupata radhi za Allah tu
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Ukumbumsho mzuri Allah akulipe, nakukubali sana maalim wewe na kaka adriz Allah awahifadhiWenzetu maswahaba walipokuwa wanaagana baada ya mazungumzo yao,walikuwa wanapeana nasaha kwa kusomeana suratil al asir ndio kisha wanaagana
Sura hii inazungumzia kwamba hakika wanadamu wote haijalishi waislamu au wasio waislamu,kuanzia baba yetu Adamu mpaka Mtume wa mwisho Muhammad swalla lahhu alaihy wa salaam, wote wapo katika hasara
Isipokuwa wale waliomwamini Allah kwa maana Mungu mmoja, kisha wakafanya mambo mema kwa maana matendo mema,kisha wakahusiana kuhusu mambo ya haki,kwa maana haki ya kumjua Allah, kukijua kitabu cha Allah na kujua mafundisho sahihi ya mtume Muhammad
Kisha wakahusiana juu ya kusubiri,hakika subira ni ibada kubwa sana,maana uwe na subira ya kuacha maovu uliyoyazoea na uwe na subira na kudumu kufanya mambo mema,maana hakika kudumu kufanya ibada za Allah ni mtihani mkubwa sana
Hawa ndio ambao hawapo katika hasara yani wamesamilika
Je sisi tupo upande upi? Tujitathimini na kufanya yale yenye kutupa mwisho mwema
Allahu akbar ukumbusho huu umenipa hamasa zaidiSiku ya jana nikiwa pale mloganzila nimempeleka mzee wangu katika clinic yake,katika korido za pale hospitalini nikamsikia muislamu mwenzangu anaongea na simu huku akisema " tutamuoshea hapa hapa na kumswalia kabisa huku huku"
Naam huyo ni ndugu yetu katika imani ameondoka jana katika mgongo wa ardhi,na huenda yeye na wengine kama yeye waliazima kumaliza mfungo salama lkn hakika umri wao wa kuishi duniani umefikia mwisho
Je mimi na wewe ambao tupo hai hadi leo tunajitahidi vipi kuchuma zaidi ndani ya mwezi huu,je tutafanikiwa kumaliza salama mfungo au nasi huenda ikatufika safar ya kwenda kwa mola wetu?
Tutumie kila dakika na sekunde ya uhai wetu katika mwezi huu kuchuma thawabu nyingi zaidi kwani huenda,tusiimalize ramadhani hii au ama tusikutane na ramadhani nyengine
Tumche Allah sana
Jazakallahu kher ukhty,amiini na atuhifadhi sisi soteUkumbumsho mzuri Allah akulipe, nakukubali sana maalim wewe na kaka adriz Allah awahifadhi
Kuomba msamaha "Toba na Istighfar" ni muhimu mno ndio maana katika mambo ya kufanya mtu wakati wa kuomba dua na mtu akitaka Dua yake ikubalike kwa wepesi basi kabla ya kuomba Dua atangulize na Istighfar kwanza kwani madhambi ni kiwazo Cha mambo mengi na chanzo Cha mabalaa.Mtume Muhammad rehma na amani ziwe juu yake,anasema akitaka mtu daftar lake la matendo limfurahishe siku ya kiama au siku ya hesabu basi apende sana kuomba msamaha kwa kusema astaghfirullah mara kwa mara
Na ndio maana dua bora sana kudumu nayo na ambayo pia ni dhikri nzur kuifanya mwezi huu wa ramadhani ni "Allahuma innaka afuwun tuhibulah afwa fafuana"
Ewe mola wangu hakika wewe ni msamehevu na unapenda kusamehe basi nisamehe
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Aamiyn, wewe pia na waumini wote Jf .Ukumbumsho mzuri Allah akulipe, nakukubali sana maalim wewe na kaka adriz Allah awahifadhi